Tuesday, April 27, 2021

Premier Betting yakubali kujenga viwanja vya mpira wa kikapu nchini

MAKUBALIANO hayo yalifikiwa katika kikao kilichowakutanisha Ndg. Sami Matar Mkurugenzi wa kampuni ya Premier Betting , James Mbalwe Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania - GBT) na Phares Magesa, Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF.) 

Viwanja hivyo vitajengwa na kampuni ya Premier Betting kupitia mradi wa Premier Projects ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii (CSR.) 

Kwa kuanzia kampuni hiyo ya Premier Betting itajenga uwanja wa kikapu Dar es Salaam itafuatia mikoa mengine yote nchini itafikiwa kwa awamu, utekelezaji wa mradi huu inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa. 

Rais wa TBF ameishukuru kampuni ya Premier Betting kwa kukubali ombi la TBF kusaidia ujenzi wa viwanja nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji  wa moja ya melengo muhimu ya mpango kazi wa TBF katika kuinua mchezo wa kikapu nchini.

Magesa amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa GBT kwa kusimamia na kuhakikisha Premier Betting inafikia makubaliano na TBF na amewataka kutekeleza mradi huu haraka.

Ndg. Magesa alisema tayari wameshawasiliana na Mamlaka husika za Jiji la Dar es Salaam ili kupatiwa eneo ambako uwanja huo unatarajiwa kujengwa na pia ameziomba Halmashauri zote nchini kutenga maeneo ya viwanja vya michezo ili kila mkoa utakapofikiwa basi eneo la kujenga liwe tayari.

 

Miili ya Watu Wawili na Kichwa Kimoja Vyakutwa Hifadhi ya Ruaha





Miili ya watu wawili na kichwa cha mtu mmoja vimekutwa kwenye eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Wilayani Mbarali mkoani Mbeya huku vikiwa vimeharibika huku chanzo cha vifo hivyo kikiwa hakijulikani.

 

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Urlich Matei akizungumza na chombo kimoja cha habari mapema hii leo, amethibitisha kukutwa kwa miili na kichwa hicho jana Jumatatu April 26, 2021 na kueleza kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.

 

Kamanda Matei amesema kuwa kwa sasa bado polisi wanandelea na ufuatiliaji wa tukio hilo ili kujua sababu ya vifo hivyo kama ni kutokana na maji ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo au mauaji.

Wabongo waiwashia moto NIGERIA baada ya kuandika kuwa IDRISS ni MKENYA, povu zito lashuka

 


Wabongo waiwashia moto NIGERIA baada ya kuandika kuwa IDRISS ni MKENYA, povu zito lashuka

VIDEO:

Tamko la Azam kuhusu Prince Dube kutua Simba

 


Uongozi wa Klabu ya Azam Fc umesisitiza kwamba mshambuliaji wao Prince Dube hatoondoka klabuni hapo kama ambavyo imearifiwa na mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa huenda atajiunga na wekundu wa msimbazi Simba mwishoni mwa msimu huu.

 


Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa wana lambalamba hao Abdulkarim Amim ''Popat'' ikiwa ni siku chache baada ya Prince Dube kuifungia bao pekee na la ushindi Azam Fc dhidi ya Yanga lililomfanya awe kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu Tanzania bara akiwa amefikisha mabao 12 akimpiku Medie Kagere wa Simba mwenye mabao 11.


Popat amesema ''Kwa ufupi Prince Dube yupo sana Azam, na hauzwi kwa gharama yotyote hapa nchini Tanzania, iwapo ataondoka basi itakuwa ni nje ya nchi'' alisema Mtendaji Mkuu huyo wa Azam.


Kwa upande wa Dube alipoulizwa na East Africa Radio iwapo angependa kujiunga na Simba iwapo itatokea nyota huyo alikataa kuzungumza chochote.


''Mimi ni mchezaji wa Azam, na ninaheshimu Mkataba wangu na wao hivyo sipo tayari kusema lolote juu ya hilo''alisema Dube.


Nyota huyo raia wa Zimbabwe amekuwa na mwenendo mzuri ikiwa ndio msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu Tanzania bara, kiasi cha kuwa kivutia kwa vigogo wa soka nchini 

VIDEO: Olakira Ft zuchu- SERE

 VIDEO: Olakira Ft zuchu-  SERE



Viatu vya Kanye West vyauzwa kwa $1.8m

Viatu ambavyo mtindo wake ulibuniwa na kuvaliwa na mwanamuziki Kanye West vimeuzwa kwa $1.8m (£1.3m) katika mnada ikiwa ni bei ya juu zaidi kuwahi kununuliwa .

Viatu hivyo aina ya Nike Air Yeezy 1vilivunja rekodi iliowekwa na viatu vya Nike Air Jordan 1s vilivyouzwa kwa $615,000 mwaka uliopita.

Mauzo hayo pia yanamaanisha kwamba ndio viatu vya kwanza aina ya sneakers kuuzwa kwa bei ya juu ya $1m," lilisema jumba la minada la Sotheby siku ya Jumatatu.

Kanye West kwa mara ya kwanza alivalia viatu hivyo katika tamasha la Grammy mwaka 2008 .Viatu hiyo ni saizi 12 au 11 ya Uingereza.

Vilinunuliwa na RARES, mtandao wa kuwekeza viatu visivyo vya kawaida.

Wanachama wake wanaweza kununua hisa katika viatu sawa na jinsi wawekezaji hununua hisa katika kampuni.

Viliuzwa na aliyevichukua viatu hivyo Ryam Chang katika mauzo ya faragha, ikimaanisha kwamba mnunuzi na bei yake haiwezi kuchapishwa hadi mnunuzi atakapokubali kujitokeza.

''Mauzo hayo yanaadhimisha bei ya juu kuwahi kuchapishwa hadharani '',ulisema mnada huo katika taarifa yake.

 

Wapiganaji wa upinzani na serekali ya Somalia wajiweka hali ya tayari




Wapiganaji wa upinzani wakiwa na silaha kali walijiweka katika hali ya utayari katika sehemu mbalimbali za mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, Jumatatu. Hali hii imetokea ikiwa ni siku moja baada ya kuzuka kwa mapigano dhidi ya vikosi vya serekali kupinga hatua ya kuongezewa muda kwa rais, katika nchi ambayo imekumbwa na ghasia kwa miaka mingi. Wapiganaji hao waliweka vizuizi katika barabara huku watu wenye silaha pamoja na magari yakiwa na bunduki za risasi za rashasha waliwekwa katika ngome za upinzani baada ya mapigano yaliyo sababisha vifo vya watu watatu. Shuhuda mmoja aliyetambulika kwa jina la Abdullahi Mire, na kuzungumza na shirika la habari la AFP, amesema kwamba vikosi vyote vya wapiganaji wa serekali na upinzani wote wamejiweka tayari katika barabara muhimu za mji.

WAZIRI KALEMANI ARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)

 

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,akizungumza wakati akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato,akizungumza na Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa umeme vijijini (Rea) Mhandisi Advera Mwijage,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki baada ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kufunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Medard Kalemani,amesema kuwa, Serikali imeridhishwa na utendaji kazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati imekuwa ikijivunia utendaji kazi wao.

Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha kutathimini utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini kilichowashirikisha REA na TANESCO.

Dkt. Kalema amewataka REA kulinda hadhi yao kwa kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ambayo hayajafikishiwa huduma ya nishati ya umeme.

"Ndugu zangu mafanikio ya nchi hii yanategemea REA na TANESCO, vigezo vilivyofanya tuingie kwenye uchumi wa kati umeme umechangia kwa kiasi kikubwa sana" amesema Dkt. Kalemani.

Dkt.Kalemani amesema kuwa Serikali imeweka malengo na mipango yake kuhakikisha wananchi kila Kijiji wanapata nishati bora ya umeme hivyo muhakikishe vijiji vyote vinapata nishati ya umeme.

''Maeneo ambayo REA imekuwa na mafanikio ni kufikisha umeme katika vijiji 10,300 sawa na asilimia 87, kati ya vijiji 12,268 hapa nchini na lengo letu ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata Nishati ya umeme''amesema Dkt.Kalemani

Naye , Naibu Waziri wa Nishati Wakili, Stephen Byabato,aliwapongeza REA kwa kufanya kazi nzuri ya usambazaji umeme nchini na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA), Mhandisi Advera Mwijage, amesema kuwa watahakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wanayafanyia kazi ili wananchi wote wanufaike na nishati hiyo ya umeme.

WAZIRI AWESO AKAGUA MRADI WA MAJI MWAKITOLYO SHINYANGA... ATOA SIKU 10 UKAMILIKE "SITAKI KUZINGULIWA"


Waziri wa Maji Jumaa Aweso, (katikati mwenye shati la bluu) akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, ametembelea ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, na kutoa siku 10 mradi huo uwe umekamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Aweso amefanya ziara hiyo Jumatatu Aprili 26,2021 , akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

Amesema kati ya miradi ya maji 177 ambayo ni kero hapa nchini, mmoja wapo ni mradi huo wa Mwakitolyo hivyo kuagiza hadi ifikapo Mei 5 mwaka huu ndani ya siku 10 zijazo, uwe tayari umeshakamilika.

"Mradi huu wa maji Mwakitolyo nina historia nao, ni kati ya miradi ya maji kichefuchefu hapa chini, hivyo naagiza hadi ifikapo Mei 5 uwe tayari umeshakamilika, sitaki kuzinguliwa na Rais, nadhani siku ile Bungeni mlisikia Rais alivyosema, na kiu yake kubwa ni wananchi wapate maji," amesema Aweso.

"Pia ma-Meneja Wakala wa maji vijijini Ruwasa, naagiza mfanye kazi kwa kishirikiana na wakuu wa mikoa ,wilaya, na Madiwani, ili kuhakikisha mnafanya kazi zenu kwa ufanisi na kuhudumia wananchi maji safi na salama," ameongeza.

Katika hatua nyingine Aweso amesema, Wakandarasi wasio na uwezo hawana nafasi kupewa kazi za ujenzi wa miradi ya maji kwenye wizara hiyo, pamoja na Wahandisi wa maji ambao ni wazembe watawajibishwa, huku akiahidi kutoa Sh. milioni 100 kwa ajili ya kujenga Tenki lingine la maji lenye lita Laki Tano kwenye mradi huo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kujenga mradi huo wa maji Mwakitolyo, na kuahidi kuusimamia ili ukamilika kwa siku hizo 10 ambazo zimetolewa na kutoa huduma ya maji safi na salma kwa wananchi.

Aidha ameongeza kuwa, wao kama Serikali mkoani Shinyanga wapo vizuri kwenye usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maji, ambapo wiki ya madhimisho ya maji walizindua miradi mingi ya maji ukiwamo wa Ihapa, Salawe, Mwamashele na Mwawaza huku miradi mingine wataendelea kuizindua ukiwemo wa Masengwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa, ambao ndiyo watekelezaji wa mradi huo wa maji Mwakitolyo kwa kushirikiana na (RUWASA), alimhakikishia Waziri Aweso kuwa mradi huo utakamilika ndani ya siku hizo 10, ambapo ujenzi wake ulianza mwaka 2020  na utagharimu Sh. bilioni 2.3.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji safi na salama Mwakitolyo wilayani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwenye ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mbonekom akielezea mradi huo wa maji namna utakavyosaidia wananchi wa Mwakitolyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) ,Mhandisi Joshua Mgeyekwa (wa pili kushoto), akielezea namna watakavyo kamilisha mradi huo wa maji Mwakitolyo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiendelea kukagua ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo.
Ukaguzi ukiendelea.
Mtambo ukiendelea na shughuli ya kufukia mabomba ya maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (mwenye shati la bluu katikati) akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...