Monday, April 27, 2020

Ukiyazingatia haya utaishi na watu vizuri


Nimezipenda hizi nasaha. Naamini na nyinyi wenzangu hamtakosa japo machache ya kujifunza unayopaswa kuyazingatia ili kuishi na watu vizuri kama ifutavyo:-

1. Epuka hasira za ovyo na kila mtu, kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo).

2. Usiwatendee wengine ubaya ukadhani kuwa utakuwa salama (ubaya hulipwa kwa ubaya, ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea kama sio kuwarejea watu wa kizazi chako)

3. Usichukue maamuzi kabla ya kutafiti ukweli (pengine wapo wanadamu wanaopenda kuonekana wao wema kwa kuumiza wengine). Mtuhumu mtu lakini mpe muda wa kumsikiliza, usimshambulie mtu kwa maneno makali bila kuujua ukweli, ukijua ukweli nafsi inaweza kukusuta.

4. Mchukulie kila mwanadamu ni mkosaji (tambua kuwa hata wewe unawakosea sana wengine na wanakuvumilia. Hivyo usiwe mwepesi wa kuwaadhibu wenzio kwa ubaya).

5. Usipande mbegu ya chuki na ubaya katika jamii unayoishi ukadhani itakuacha salama (chuki hukua kama mti utambaao, ukiipanda ndani ya jamii yako, haitatoka kwako na inaweza kutafuna kizazi chako ukajutia.

6. Tambua kuwa yule unayeishi nae ni mwanadamu kama wewe, mpe heshima na mwonyeshee upendo hata kama huoni anafanana nawe. Maisha ni duara huenda ulikuwa kama yeye au atakuja kuwa kama wewe baadae.

7. Usiwe muongeaji ovyo ovyo na usiye na subira. Kuongea sana kunapoteza busara.

8. Jiepushe na maisha ya kusukumwa na wengine kufanya jambo usilojua manufaa yake. Jifunze kujitegemea kiakili. Sio kila unayemdhania rafiki moyoni mwake yupo pamoja nawe, na ukashirikiana nae, wengi wa marafiki zetu hututumia sana kuliko tunavyoweza kuwatumia wao.

9. Usipende sana kugombana na watu kwa njia ya maongezi yanayodumu kama vile, ujumbe wa maandishi, mawasiliano ya simu au ujumbe wa maneno (SMS). Kumbuka kuwa maneno yanaishi kuliko ugomvi au uadui, ipo siku yatakurudi na utajiona mpumbavu na kukosa pa kujificha. Jifunze kusubiri.

10. Usifumbue mdomo wako kutamka ubaya au kunyanyua kidole chako kuandika ubaya juu ya mwenzio bila kujiuliza mara mbili moyoni mwako hatima ya unachokitoa kwa mwingine.

11. Jishushe na jifunze kusikiliza wengine wakati wa mazungumzo ili uweze kujifunza kabla ya kukurupuka kujibu, usikivu ni kipimo cha busara, mtu anayekurupuka kujibu jibu kila anachosikia hawezi kuwa kiongozi, Mume au Mke mwema kwani mara nyingi atapotoka tu.

12. Usitunze hasira nyingi moyoni kwani hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Jitahidi pia kuepuka kuwa na hasira mara kwa mara na zisizo na maana. Elewa kuwa hasira zisizo maana hukupunguzia maisha na kukupa maumivu wewe mwenyewe kuliko yule uliyemfanyia hasira, utakufa kwa magonjwa kabla ya wakati ufaao.

13. Thamani yako inategenezwa na watu wengine, wewe kama ni mtoto, mheshimu sana mzazi wako na kama umeoa au kuolewa, heshimu wazazi na familia ya mke au mumeo kwa kuwa bila wao, usingekuwa hivyo ulivyo leo unajivunia ndoa njema, kwa kuwa yupo mtu alimzaa huyo mwenzio. Mheshimu kwa lolote liwe jema au baya, utalipwa kwa wakati ufaao.

14. Usijibizane na mtu usiyemjua au ambaye hawezi kukupunguzia kitu katika maisha yako. Tambua kuwa unapunguza sehemu kubwa ya maisha yako kwa kutafuta magomvi na mtu wa mbali nawe.

15. Kumbuka asili yako, kumbuka upo hapo kwa kuwa kuna mahali ulitoka, maisha yanabadilika, usidharau pale ulipokuwa zamani kwa kuwa ndipo palipokufanya leo uwe hapo.



16.Subiri, sikiliza, elekeza, vumilia. Elewa sio kila mtu ana uelewa kama wako. Jitahidi kuwa mvumilivu katika kila jambo, usiinuke kuwafokea au kuwakaripia wengine kwa jambo ambalo pengine nao wanahitaji muda kueleweshwa ili walifanye vyema. Kumbuka sana, kuna wakati nawe ulikuwa huelewi kabisa lakini wapo wenzio walikuvumilia, wakakuelekeza njia njema, kufokea wengine mara kwa mara sio njia njema ya kuwafundisha bali ni kuwaweka mbali nawe.

Sunday, April 26, 2020

Hivi kuna Ukweli Kwamba Wanawake Walioajiriwa Hujitongozesha kwa Mabosi?

Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi.

Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake.

Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.

Katika mahojiano na jarida moja nchini Marekani mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Jarida hilo halikufanya mahojiani ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

Wanawake wenye watoto ambao walihojiwa kwenye tafiti hizo walisema kwamba ajira zinawasumbua na wamefikiria kuwa ni ngumu kujigawa kazini na nyumbani kishughuli.

Tafiti hizo hata hivyo hazikulenga katika kuonyesha kwamba wanawake ni dhaifu bali huenda zimelenga katika kuonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojitongozesha kwa mabosi ni ndogo kuliko inavyotazamwa au kuaminika na pia kuonyesha kwamba bado wanawake walioajiriwa wako kwenye nafasi kubwa zaidi kushiriki mapenzi kuliko wale walioko majumbani. Ni juu ya wanawake ambao wanadhani ni halali kuuza thamani zao kwa ajili ya kazi kubadili mwenendo huo..
Source

Kanisa la Mlima wa Moto watangaza wiki ya maombelezo

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Sabasaba Jijini Dodoma, Slivanus Komba ametangaza maombi ya Maombolezo ya siku saba ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Dk. Getrud Rwakatale.

Mchungaji Komba ambaye pia ni Askofu wa Kanda ya Kati na  Nyanda za Juu kusini amesema lengo la maombolezo hayo ni kumuenzi kwa vitendo kutokana na mema na maonyo alikuwa akiyatenda mbeba maono wa Kanisa hilo na aliyekuwa askofu mkuu wa Kanisa la Mlima wa Moto Tanzania, Marehemu Mch. Rwakatale.

Askofu Komba alisema pamoja na kutangaza maombolezo ya siku saba ya Kanisa hilo pia litaendelea na maombolezo ya siku 40 ambayo yametangazwa kitaifa na Kanisa hilo ambayo yatakuwa ya kitaifa.

Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kuwa kibiblia hakuna kioongozi yeyoye wa kidini ambaye anaweza kufanya maombolezo kwa ajili ya kumshawishi Mungu kubadilisha mawazo ya mtu aliyekufa kumpeleka peponi au motini kulingana na kile ambacho alikitenda akiwa hai.

Alisema wakati wa uhai wa Mch. Dk. Rwakatale alikuwa ni mstari wa mbele katika kuhakikisha kazi ya Mungu inasonga mbele licha ya kuwa alikuwa mfanyabiashara mkubwa na mwanasiasa.

Katika ibada hiyo ambayo ilikuwa ya tofauti ambayo ilighubikwa na majonzi vilio kwa washirika wa kanisa hilo, Askofu Komba aliwataka waumini wote kuhakikisha wanahudhuria Ibada zote za siku bila kukosa ikiwa ni sehemu ya maombolezo.

Katika hatua nyingine, Askofu Komba amekemea baadhi ya uzushi juu ya wanaopakaza kuhusu mrithi wa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo.

"Pamoja na kuwa Mimi siyo msemaji wa Kanisa hili wapo wasemaji lakini nipende kusema kuwa kwa sasa tupo katika kipindi kigumu cha kuondokewa na Kiongozi wetu mbeba maono.

"Nashangaa kwa mtu yeyote ambaye anawaza kurithi sisi hatupo kwa ajili ya kurithi, tunawaza kufanya kazi ya Mungu na kwa sasa Kanisa lipo ya Baraza la wazee.

"Kwa mtu ambaye anawaza kurithi hana nia njema na huduma ya kuifanya kazi ya Mungu bali maamuzi yote yatatolewa na Baraza la wazee wa kanisa baada ya siku 40," alisema Askofu Komba.

Wenye Virusi vya Corona Nchini Kenya Wafika 355....Ni Baada ya Wengine 12 Kuongezeka

Watu wengine 12 wamepatikana na virusi vya corona nchini  Kenya ndani ya masaa 24 yaliyopita.

Sasa idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya imefikia 355 tangu kisa cha kwanza kiripotiwe Machi 13 mwaka huu. 

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili, Aprili 26, na katibu msimamizi katika Wizara ya Afya Rashid Aman. 

Aman amesema  kuwa hakuna kifo zaidi kimeripotiwa kutokana na virusi hivyo na idadi ya waliofariki imesalia watu 14.

Watu 8 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 106


Maimartha: Wema Sepetu Alipokuwa na Diamond Walimsema ‘Unatembeaje na Mtu MCHAFU’ Alikaa kimya, Alimvalisha na Kumpa PROMO...


Maimartha: Wema Sepetu Alipokuwa na Diamond walimsema 'Unatembeaje na Mtu MCHAFU' Alikaa kimya, Alimvalisha na Kumpa PROMO...

Sikiliza Hapa chini:

Ulaya yataka usitishaji wa mapigano Libya

Mawaziri wa Mambo ya nchi za kigeni wa Ujerumani, Ufaransa, Italia pamoja na Umoja wa Ulaya wametoa tamko la pamoja linaloelezea wasiwasi wao kuhusiana na ongezeko la mapigano nchini Libya.

Katika taarifa ya pamoja, wamezitaka pande hasimu nchini Libya kurejea kwenye meza ya mazungumzo na kutafuta makubaliano ya uhakika ya usitishaji mapigano.

Viongozi hao wametilia mkazo umuhimu wa kuwepo utulivu wa uhakika katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na wakati Libya inaendelea kukabiliana na mlipuko wa viruis vya corona.

 Hivi karibuni mapigano yameongezeka kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli licha ya kutiwa saini mkataba wa kusitisha mapigano mnamo mwezi Januari.

Waziri Bashungwa Amewaagiza TEMDO Kutengeneza Mashine Za Kukamua Miwa Na Kuchakata Zao La Mkonge.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ametoa rai kwa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) kuhakikisha wanawasaidia wajasiliamali wadogo  na wa kati kubuni  mashine za kutengeneza sukari pamoja na kuchakata katani ili kufungua fursa ya ajira na ongezeko la viwanda nchini.

Mhe. Bashungwa aliyasema hayo mkoani Arusha alipokuwa akizindua mashine 14 za kisasa zinazoendeshwa kwa mfumo wa kompyuta yaani CNC zikiwa na  thamani ya shilingi milioni 600 zilizotolewa kwa fedha za Maendeleo za Serikali na za ufadhili wa shirika la kimataifa la UNIDO.

Akizungumza na watumishi wa taasisi hiyo Mhe. Bashungwa aliwataka TEMDO kuongeza kasi ya kubuni mtambo mdogo wa kuchakata miwa ili kupata sukari ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa wa bidhaa hiyo sokoni.

Aliongeza kwa kusema wafanyabiashara wanapandisha bei ya bidhaa hususani sukari sokoni, lakini endapo TEMDO itatengezeza mashine za kutengeneza sukari kwa wajasiriamali wadogo  itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kusaidia upatikanaji wa sukari nchini.

Aidha amewataka pia kuongeza kasi ya kubuni mashine  ndogo ndogo za kuchakata zao la mkonge kwa kiwango cha upatikanaji wa nyuzi ili kuwasaidia wajasiliamli wadogo kutengeneza nyuzi wao wenyewe ili waweze kuziuza na  kujiongezea kipato badala ya hali ilivyo hivi sasa ambapo wakulima wanategemea wazalishaji wakubwa kununua bidhaa hiyo kwa kiasi kikubwa ambapo mkulima amekuwa hanufaiki.

Sambamba na hilo Mhe. Bashungwa alikabidhi barakoa zenye thamani ya Tsh.500,000 zilizotolewa na TEMDO  kwa mkoa wa Arusha ikiwa ni sehemu ya kuungana na Serikali kupambana na ugonjwa wa Korona kwa watoa huduma ya afya.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Prof. Fredrick Kahimba aliishukuru serikali kwa kuwawezesha kupata mashine hizo ambazo zitawezesha kuunda mitambo na mashine mbalimbali kwa urahisi zaidi kuliko awali.

Aliongeza kuwa "taasisi ya TEMDO imeendeleza shughuli mbalimbali zinazochangia maendeleo ya Viwanda Tanzania na kuwawezesha wakulima na wajasiliamali wadogo, wa kati na wakubwa kujipatia teknologia ya kuogeza uzalishaji mali.

Pia alimuomba Waziri Bashungwa kusaidia kuharakishwa uundwaji wa bodi mpya ya Wakurugenzi ya taasisi kwa kuwa liyokuwepo imemaliza muda wake.

Kwa upande wake bi Restuta Mrosso ambaye ni mnufaika wa utaalamu unaotolewa na TEMDO aliishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia ujuzi  wajasiriamali kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwasaidia kupata nembo ya Ubora (TBS).



Saturday, April 25, 2020

Zijue tabia za watu wenye wivu


Mara mtu apatapo mafanikio mambo mengi hutokea au hubadilika. Moja kati ya mambo ambayo hutokea ni mabadiliko kwa watu wanao mzunguka mtu huyo. Wengine humpenda, wengine humheshimu, wengine humchukia au hata kumwonea wivu.

Wivu umekuwa ukitesa na kurudisha maendeleo ya watu nyuma hasa wale ambao ndio huwa na wivu huo mioyoni mwao.

Kwa kuwa wivu hauwaathiri wale walio nao pekee, ni vyema nawe ukafahamu tabia za watu wenye wivu ili uwaepuke wasije wakakuathiri kwa kukurudisha nyuma katika hatua zako za maendeleo.

1. Hawastaajabishwi na mafanikio ya wengine
Moja kati ya tabia kubwa ya watu wenye wivu ni kutostaajabishwa na mafanikio ya wengine. Wao hata wasikie jambo zuri au kubwa kiasi gani la mtu mwingine wao hujifanya kuliona kama la kawaida tu.

Unaweza kusikia hata wakisema kauli kama vile "mbona hayo mambo ya kawaida", "mbona wapo wengi waliofikia hapo", "mambo ya kupita hayo, cha muhimu uzima bwana", "mafanikio ya watu hayanihusu bwana", n.k. Watu wenye tabia kama hii ni wakuepukwa maishani kwani wivu umewatawala.

2. Huhusianisha mafanikio na bahati
Watu wenye wivu huamini kuwa hakuna mtu mwingine anayestahili au mwenye uwezo wa kufanikiwa. Wao hujiona kuwa wao ndiyo wenye tiketi ya mafanikio na endapo basi yatatokea kwa watu wengine itakuwa ni kwa bahati tu.

Unaweza kusikia wakisema kauli kama vile, "hiyo kazi kaipata kwa bahati tu bwana", "amepata dili kweli", n.k.

3. Wanapenda kuiga na kushindana
Kwa kawaida watu wanaopenda kuiga na kushindana ni wale wasiokuwa na malengo wala maono yoyote. Watu hawa wao huangalia wanayoyafanya au wanavyoishi watu wengine na kuiga.

Watu hawa, wengi wao huwa na wivu ndiyo maana hutaka yale yanayotokea kwa wengine yatokee na kwao. Utashangaa kuwaona mara unapofanya hiki nao wameshaiga, unapopanga hiki nao wameshaiga, unapoeleza umefanikisha hiki nao wanaeleza walivyokifanikisha tena hata kwa namna ambayo inaonekana inakuzidi.

Watu wa aina hii ni wenye wivu na watakunyonya nguvu ikiwa utashiriki kwenye mashindano yao.

4. Hupenda kuleta taarifa mbaya
Kuna watu ambao kila mara wao ni kuleta taarifa mbaya hasa juu ya jitihada zako za kimaendeleo au dhidi ya malengo yako.

Unaweza kusikia watu hawa wakisema kauli kama vile, "Aaa! yule jamaa mwenye biashara kama yako amefilisika", "Inavyoonekana biashara kama hii yako huko tunakoenda haitakuwa na dili", "ufugaji haulipi", "biashara hazilipi", "hakuna maana kuwekeza kwenye kilimo kwa sababu ni pata potea", n.k.

Tabia hii ni ya watu wenye wivu wakitaka tu kukurudisha nyuma ili ukate tamaa na uwe na hofu ya kutimiza malengo yako.

Sanjari na hilo, watu wenye wivu hupenda kuzungumzia zaidi kushindwa kuliko kushinda. Wao watakueleza zaidi jinsi utakavyoshindwa kwenye kila unalolifanya kuliko utakavyofanikiwa.

5. Hufurahia wengine wanaposhindwa
Ukiona mtu anayefurahia kushindwa au kuanguka kwa mwingine basi ujue kiwango chake cha wivu ni kikubwa sana. Watu wasio na wivu husikitika pale wengine wanapoanguka; pia huwatia moyo ili wainuke tena na si kufurahia.

Kwa kuwa watu wenye wivu huwa hawapendi kuona meli ya mtu mwingine baharini, basi wao hufurahia sana mara wengine waangukapo au wapatapo matatizo.

6. Hawajumuiki pamoja kusherehekea mafanikio
Mtu mwenye wivu hapendi kuona mwingine akifanikiwa kumzidi yeye; hivyo itakuwa ni vigumu sana kwake kushiriki katika tukio lolote ambalo ni lakusheherekea mafanikio ya mtu mwingine.

Watu hawa huishia kutoa udhuru na vijisababu ambavyo vitawafanya wasihudhurie kwenye tukio hilo.

7. Hukusema vibaya kwa wengine
Je umeshaona watu ambao mkiwa pamoja wanakuwa marafiki wakubwa sana lakini ukiwapa tu kisogo wanakuwa nyoka wenye sumu kali? Kama jibu ni ndiyo, basi hawa ni moja kati ya watu wenye wivu.

Kiuhalisia tunao marafiki, ndugu, wafanyakazi wenzetu au hata majirani wengi wa aina hii.

Huja kwako kwa uso wa urafiki na wema lakini wakiondoka tu wanaanza kukusema vibaya ili kuharibu mahusiano yako na watu au kukwamisha kile unachokifanya.

8. Hupenda kujikweza na kujionyesha
Watu wenye wivu hukosa unyenyekevu; wao hupenda kuonyesha kuwa wako juu ya kila mtu na hupenda kutambulika kwa kila mtu.

Wakati wewe ukifikiri kuwa mafanikio ni kitu cha kuwa mnyenyekevu, wao huona ni kitu cha kujitangaza; wakati wewe ukieleza mafanikio yako halisi wao hueleza makubwa zaidi hasa ya uwongo ili tu waonekane bora zaidi.

9. Hutoa ushauri mbaya
Kwa kuwa watu wenye wivu hawapendi watu wengine wafanikiwe, basi wao huwapa wengine ushauri ambao utawakwamisha.

Kwa mfano mtu mwenye wivu anaweza kuona ukiingia kwenye mahusiano na mtu mbaya; lakini akakutia moyo kwa sababu anajua utaangamia.

Pia, mtu mweye wivu naweza kukupa wazo ili ulitekeleze na kukudanganya kuwa ni wazo zuri huku akijua kuwa wazo hilo litakukwamisha ndani ya muda mfupi.

10. Hukupa sifa za uwongo
Kuna msemo usemao "Sifa zinaua"; watu wenye wivu hujifanya wanakukubali na hivyo hukupa sifa za uwongo ili zikuangamize.

Unaweza kulibaini hili kwa kutazama matendo yao kwani utawaona wakikusifia lakini ukiwapa kisogo nao wanaanza kukudharau na kukukejeli kwa wengine.

Ili kulinda malengo yako hakikisha huendeshi maisha yako kwa kutegemea sifa za watu wengine, kwani zinaweza kuwa ni za wenye wivu tu zenye lengo la kukuangusha.



Zilizoelezwa hapa ni tabia 10 za watu wenye wivu ambazo unapaswa kuzifahamu ili uweze kuwaepuka maishani mwako. Bila shaka umeona wazi jinsi tulivyozungukwa na watu wengi wenye wivu na wanavyoweza kuathiri  maisha yetu ya kila siku.

Jamal Khashoggi alizungumza nini wakati wa uhai wake?

Wanaharakati wa vyombo vya habari vya kijamii wameposti mahojiano ya runinga ya mwandishi wa Saudia marehem Jamal Khashoggi ambapo alizungumza juu ya umuhimu wa mwanaharakati wa haki za binadamu na msomi mashuhuri "mtaalam wa katiba" wa Saudia,Abdullah al-Hamid, ambaye amefariki akiwa gerezani.

Vyanzo vya haki za binadamu na wanaharakati vimethibitisha kifo cha al-Hamid, mwenye umri wa miaka 69, katika moja ya magereza ya Saudi Arabia,ambapo inadaiwa matibabu yake yalipuuzwa na viongozi.

Mamlaka hayakuweza kufikia kwa ajili ya kutoa maoni ya haraka lakini Riyadh imekanusha tuhuma za upuuzaji huduma za matibabu kwa wafungwa katika magereza yake na kukataa malalamiko yanayotolewa ndani na nje ya nchi.

Katika mahojiano hayo, Khashoggi alisema kwamba harakati za utawala wa kikatiba ziliibuka katika ufalme hata kabla ya maasi ya Kiarabu ya kijeshi yaliyoanza mnamo 2011.

Alisema takwimu kubwa za harakati zinazoongozwa na al-Hamid zilifungwa, pamoja na kuwekwa vikwazo vingi vya kusafiri.

Khashoggi, aiyekuwa mwandishi wa habari wa Saudia na mwandishi wa "The Washington Post", ambaye aliuawa Oktoba 2, 2018, ndani ya ubalozi wa Saudia huko Istanbul, alisema harakati hiyo "ilikuwa yenye nguvu, na ni wakati wasaudia kuligundua hilo."

Wakati wa mahojiano, Khashoggi aliwasihi Waaarabu wa Saudi Arabia kusoma kitabu kilichoandikwa na al-Hamid juu ya "uvumbuzi wa kikatiba."

"Jambo zuri juu ya harakati hii ni uvumbuzi wake, sio wazo kutoka magharibi. Ni maandiko halisi ya kiisamu ya Saudia yaliyoandikwa na raia msafi wa Saudia" alisema Khashoggi.

Alisisitiza kuwa al-Hamid alikuwa "mtu mwenye elimu dhabiti na asiye na sheria kali za Kiislamu."

Al-Hamid, aliyeanzisha Chama cha Haki za Kiraia za Saudia na Kisiasa, moja ya vikundi mashuhuri nchini kutetea mabadiliko ya serikali, alikamatwa na viongozi mnamo Machi 2013 na kuhukumiwa miaka 11 jela.

Jumuiya ya Haki za Binadamu ya Saudia, shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi nje ya ufalme, inadai viongozi walikuwa hawajamshutumu al-Hamid na uhalifu wowote kabla ya kufungwa.

Shirika hilo lilisema katika taarifa ya awali kwamba afya ya Al-Hamid ilikuwa imezorota kwa zaidi ya miezi mitatu, huku viongozi wakiwa "hawakubali kuachiliwa kwake licha ya umri wake."
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...