Tuesday, August 28, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA MAJESHI NCHINI


Birdman Ajishusha Amuomba Msamaha Lil Wayne Mbele ya Maelfu ya Mashabiki

 Birdman Ajishusha Amuomba Msamaha Lil Wayne Mbele ya Maelfu ya Mashabiki
UGOMVI wa kifamilia kati ya wasanii Birdman na Lil Wayne umemalizika Jumamosi iliyopita kwenye tamasha la  Lil Weezyana Fest lililofanyika huko New Orleans, Marekani, ambapo Birdman aliomba msamaha mbele ya maelfu ya mashabiki waliokusanyika katika dimba la  Champions Square.

Tukio hilo linafuatia watu hao wawili kumaliza bifu lao ambapo Wayne alimfungulia mashitaka Birdman kwa kumdai Dola mil. 51 (Sh. bil. 117) ili ajiondoe katika mkataba wake mwaka 2015.

Hilo lilimalizika kwa siri mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Chinese firms eye pharmaceutical industry

Investors from five Chinese companies are expected in the country next month for negotiations with the government with a view to investing in the pharmaceutical sector.
Source

PICHA: Rais Uhuru Kenyatta Alivyokutana na Trump Ikulu ya Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na mwezake wa Kenya Uhuru Kenyatta mjini Washington na kuzungumzia masuala mbalimbali, zaidi wakiangazia biashara na usalama.

Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya Marekani, wakati wa ziara hiyo mataifa hayo mawili yalikubaliana na kutangaza mikataba ya jumla ya $900 milioni.

Rais Kenyatta ni kiongozi wa tatu kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara kukaribishwa Ikulu ya White House na kufanya mazungumzo na Rais Trump.

"Tumekuwa na ushirikiano mzuri na wa kipekee na Marekani katika masuala ya usalama na ulinzi, hasa katika harakati za kukabiliana na ugaidi. Muhimu zaidi tuko hapa kuboresha ufungamano wetu katika biashara na uekezaji, " kasema Rais Kenyatta.

Rais Trump alisema Kenya na Marekani zitaendelea kushirikiana kuimarisha ufungamano wao katika biashara, uekezaji na usalama.

"Tunafanya shughuli nyingi za utalii, biashara na ulinzi. Na kwa wakati huu tunajibidiisha kuboresha usalama," alisema Rais Trump. " Tunafurahia sana kuwa nawe hapa."

Miongoni mwa mengine, Bw Trump alifurahia pendekezo lililowasilishwa na kampuni ya ujenzi kutoka Marekani Bechtel Corporation kutaka kupewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kisasa ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.

Mataifa yote mawili yalikubaliana na kuendelea na mashauriano zaidi ili kuafikiana kuhusu ufadhili wa ujenzi huo.

Viongozi hao wawili walijadiliana pia kuhusu safari za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi New York zitakazoanza mwezi Oktoba mwaka huu na kukubaliana kwamba safari hizo za ndege zitaimarisha zaidi utalii na biashara kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Marekani ndiyo chanzo kikuu cha watalii wanaozuru Kenya na taifa hilo la Afrika Mashariki linatarajia kutumia fursa ya safari za moja kwa moja za ndege za Kenya Airways kati ya mataifa hayo mawili ambazo zitaanza Oktoba 28 kuimarisha idadi ya watalii wanaofika kenya.

Viongozi hao wawili kwa pamoja wamejadili njia za pamoja za kupambana na ugaidi na ushirikiano wa kibiashara. Mpango wa upanuzi wa barabara inayohusisha miji mikubwa ya Kenya, Mombasa na Nairobi pia ilijadiliwa.

A

Source

TV ORIGINAL NA ZENYE WARRANTY HIZI HAPA UNAPEWA NA OFFA UNASUBIRI NINI

Msimu Huu Wa Kombe La Dunia Jipatie Flat Screen Tv Mpya Kumbuka Ukinunua Tv Kutoka Kwetu Tunakupa Offa Ya Wall Bracket Na Kufungiwa Tv Ukutani Bure Kabisa Kama Huhitaji Kufungiwa Ukutani Hatukuachi Hivi Hivi Tunakupa Offa Ya Tv Guard Bure Pia Usisahau Kuwa Tunakuletea Mpaka Kwako / Ofisini Usafiri Bure Call / WhatsApp 0716366999 / 0762022066 Tunapatikana Mwenge Lufungila
BEI ZA TV ZA STAR X
Star-x Inch 24'  330,000
Star-x inch 32' 465,000
Star-x inch 43'  780,000
Star-x Inch 43' smart Tv 850,000
Star-x 50' inch smart Tv 1,150,000
Star x 55' curved 4k smart  1,600,000
BEI ZA HISENSE LED Tv 
Inch 32 550,000 
Inch 39 900,000
Inch 43 1,150,000
Inch 50 1,450,000
Inch 55 1,700,000
Inch 58  2,120,000

HISENSE FULL HD SMART TV
Inch 32'' 800,000
Inch 43'' 1,200,000
Inch 49'' 1,400,000
Inch 50'' 1650,000

 HISENSE TV SMART 4K ULTRA
Inch 50 1,750,000
Inch 55 2,150,000
Inch 58 2,900,000
Inch 65 3,550,000

HISENSE CURVED TV
Inch 55 Curved TV 3,900,000


BEI ZA TV ZA  LG 
LG LED TV 
Inch 24 380,000
Inch 32 (lj520) 550,000
Inch 43 (lh510) 900,000
Inch 43 (lh543) 920,000
Inch 49 (lj510)1,350,000
Inch 55 (lh545) 2,100,000

LG SMART TV
Inch 32 670,000
Inch 43 1,100,000
Inch 49 1,500,000
Inch 55 2,000,000

LG Smart 4k 
Inch 43 (uj602) 1,300,000
Inch 49 (uj602) 1,750,000
Inch 55 (55uj651v) 2,350,000
Inch 65 (65UJ651V) 3,600,000

BEI ZA TV ZA TCL

TCL SMART TV
Tcl 32" (32S6200S) smart tv 550,000
Tcl 43". (43d2930) Smart tv 950,000
Tcl 48".(48d2730)  Smart tv 1,150,000
Tcl 48 Curved Smart Tv 1,350,000
Tcl 49" 1,350,000
Tcl.55". (55d2940)  Smart tv 1,600,000
Tcl 55". (55p1000) Smart 4k 1,700,000
Tcl. 55". (C55C1CUS) Smart curved 4k 2,000,000
Tcl. 65" (65P1100) Smart tv 3,000,000

BEI ZA TV ZA SAMSUNG
Inch 32 (j4003)  550,000
Inch 40 (k5000)  900,000
Inch 43 (k5002)  1,050,000
Inch 49 (m5000)  1,350,000

Samsung Smart Tvs
inch 32 700,000
Inch 40 (k5300)  1,050,000
Inch 43 (k5300)  1,400,000
Inch 49 (j5200)  1,500,000
Inch 55 (m6000)  2,150,000 

Samsung Curved Smart Tv 
Inch 55 (m6500)  2,350,000
Inch 55 (MU7350) 2,400,000
INCH 65 (KU7350) 4,000,000




BEI ZA TV ZA BOSS
BOSS LED TV ( SIO SMART )
LED 24" @360,000
LED 32" @500,000
LED 39" @750,000

BOSS SMART TV
LED 43=850,000
LED 49=1,000,000
LED 55=1,250,000
LED 65=2,250,000

EVOLI INCH 32'' 440,000


PHILIPS INCH 32 480,000


Pinetech Inch 32" 525,000 ( Ina Protector Ngumu Sana )
Pinetech inch 43'' 850,000


Tunapatikana Mwenge Lufungila Kwa Mkazi wa Dar Tunakuletea Mpaka kwako Wa Mikoani Tunatuma Ukihitaji Tupigie 0716366999 / 0762022066 Pia Unaweza Kulipia kidogo kidogo Ukimaliza Unachukua Tu Mzigo Wako

JINSI WAZIRI MPANGO ALIVYOMSHUKIA MAKONDA KAMA MWEWE SAKATA LA MAKONTENA...ATAKA VIONGOZI WA SERIKALI WACHUJE MANENO


Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango (kushoto) akielezwa jambo na Ofisa Forodha Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa Bandari ya Dar es Salaam, Stephano Mathias (kulia) kuhusu samani zilizopo kwenye moja ya makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipofanya ziara ya kukagua jana. Picha na Wizara ya Fedha 


Na Julius Mnganga, Mwananchi 

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amemshukia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu sakata la mnada wa makontena 20 yaliyopo bandarini.


Makontena hayo yenye samani za ndani kama viti, meza na mbao za kuandikia yenye umiliki wa Makonda yanadaiwa kodi inayokadiriwa kuwa Sh1.2 bilioni.
Jumamosi iliyopita, makontena hayo yalikosa wanunuzi katika mnada kutokana na watu wengi kushindwa kufikia bei iliyotajwa.
Baada ya makontena hayo kutouzika, juzi Jumapili Makonda alitoa onyo kuwa mtu atakayenunua makontena hayo atamlaani yeye na uzao wake.
Huenda kauli hiyo ya Makonda ndiyo iliyomfanya Waziri Mpango jana kufanya ziara ya kushtukiza katika Bandari Kavu ya Dar es Salaam (DICD), kukagua makontena hayo na akatumia mwanya huo kutoa onyo kwa viongozi serikalini.
Baada ya kuyakagua makontena hayo jana alasiri, Waziri Mpango aliwataka viongozi serikalini kuchunga maneno yao na akawaomba wanaotaka kununua samani hizo wasiogope.
Dk Mpango alisema wanachokifanya ni kusimamia sheria za nchi ambazo hazichagui sura wala cheo cha mtu.
"Niliapa kutekeleza sheria za nchi na sheria za kodi. Katika usimamizi wa sheria hizi, kamishna zisimamie bila kuyumba. Piga mnada mara ya kwanza, ya pili na ya tatu kadri sheria inavyokuruhusu. Sheria inasema mzigo ulioagizwa kutoka nje hauna msamaha wa kodi. Hivyo, mchakato ulioanza kuutekeleza endeleeni nao," alisema Dk Mpango akimuelekeza kamishna wa Forodha, Ben Usaji.
Dk Mpango alisema, "Niwaombe viongozi wenzangu serikalini tuchuje maneno. Nawaomba Watanzania, anayetaka kuja kununua samani hizi asiogope, aje kununua. Haipendezi kusikia eti mtu atakayenunua samani hizi atapata laana, tena ya Mungu. Kwa nini tunahusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii? Nawaomba Watanzania anayetaka kuja kununua samani hizi aje, hakuna cha laana wala nini."
"Kamishna piga mnada mara ya kwanza, ya pili, ya tatu kadri sheria inavyokuruhusu. Hata mimi ningekuwa na hela ningekuja kununua tuone hiyo laana inatoka wapi," alisema Waziri Mpango.
Kuhusu kauli ya Makonda kuwa samani hizo ni kwa ajili ya ofisi za walimu, Dk Mpango alisema Serikali inathamini mchango wao na inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha inaboresha mazingira yao ya kazi.
"Tuliapa kusimamia sheria. Sheria za kodi mimi ndiye mwenye dhamana hivyo niulizeni ni wajibu. Si sahihi hata kidogo kuingilia utaratibu ambao umebainishwa kisheria. Kamishna endelea kupiga mnada mpaka kieleweke," alisema.
Waziri Mpango alisema sheria haitoi msamaha kwa samani kutoka nje na kila anayeziagiza anapaswa kufahamu hilo.
"Nimejizuia sana kujibizana kwenye mitandao, hii si hulka yangu lakini haya ndiyo maelekezo ya Serikali," alisema Mpango.
Historia ya makontena
Sakata la makontena hayo lilianza baada ya tangazo la TRA lililochapishwa kwenye gazeti la Serikali la Daily News Mei 12, likiwataka wamiliki wa mali zilizokaa bandarini kwa zaidi ya siku 90 kujitokeza kuzilipia.
Tangazo hilo lilionyesha kuwa TRA inakusudia kufanya mnada wa wazi Juni kwa mizigo iliyokaa bandarini kwa muda mrefu bila kukombolewa, ikiwamo ya Paul Makonda.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa na Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Ben Asubisye, wamiliki walitakiwa kuitoa mizigo hiyo ndani ya siku 30 kuanzia siku ilipotangazwa.
Tangazo hilo lililokuwa na orodha ya makontena zaidi ya 800, jina la Paul Makonda lilijitokeza mara 20 akiwa mpokeaji wa makontena 20 yaliyopo katika bandari kavu ya DICD yakiwa na samani.
Ingawa hakukuwa na uthibitisho kuwa Makonda ndiye mwenye makontena hayo wakati huo, Februari 16 mkuu huyo wa mkoa alikaririwa katika mtandao wa gazeti la Serikali la HabariLeo kuwa alipokea makontena 20 yenye samani zitakazotumika katika ofisi za walimu zinazoendelea kujengwa. Mzigo huo ulikuwa sehemu ya shehena ya makontena 36.
Samani hizo za ofisini zilizokuwa na thamani ya Sh2 bilioni, zilitolewa na Watanzania wanaoishi Marekani wanaojulikana kama Six Region Diaspora Council.
Kauli za Makonda
Akizungumza na Mwananchi kwa simu juzi, Makonda alisema alishiriki ibada mjini Ngara mkoani Kagera kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa kuwa anaamini Mungu alimpa kwa ajili ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwananchi lilikuwa limempigia simu Makonda baada ya kuthibitisha kuwa ni makontena yake ili kujua jitihada anazochukua kuhakikisha hayauzwi na badala yake yanatolewa kwa walimu kama yalivyokusudiwa.
"Leo (juzi) nimekwenda katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Anglikana mjini Ngara, nimefanya ibada maalumu kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa kuwa naamini Mungu alinipa kwa ajili ya walimu wa mkoa wangu," alisema Makonda.
Alisema kupatikana kwa samani hizo ni jitihada zake binafsi za kuboresha mazingira ya kufanyia kazi walimu ikiwa ni kumuunga mkono Rais John Magufuli aliyeamua kutoa elimu bure kwa Watanzania na hasa watoto wa masikini.
"Rais alitambua umuhimu wa elimu ndiyo maana kama msaidizi wake sikuona sababu ya kukaa kimya wakati mazingira ya walimu si rafiki na kusubiri kuwalaumu pale watoto wanapofeli bila kufanyia kazi changamoto zao," alisema Makonda.
"Baada ya kuona jitihada za Rais katika sekta ya elimu, kwa kutoa elimu bure nami nikawaza kama msaidizi wake, nafanya nini kuunga mkono kazi nzuri anayoifanya Rais."
"Ndipo Mungu aliweka wazo lake ndani ya moyo wangu juu ya ujenzi wa ofisi za walimu kama sehemu ya kuboresha mazingira yao. Kwa utukufu wake Mungu, akaandaa watu wa kuchangia tena kutoka nje na ndani ya nchi," alisema Makonda.
Akitumia maneno ya vitabu vitakatifu, Makonda alisema utukufu wa Mungu umejidhihirisha kwa Watanzania kuchangia, wakiwemo askari wa Jeshi la Kujenga Taifa waliojitolea kujenga majengo; benki kwa kununua saruji; baadhi ya viwanda kutoa mabati na nondo na wengine kujitolea masinki, mabomba na taa.
Wasemavyo wadau
Akizungumzia uamuzi wa TRA na kilichosemwa na Makonda, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Benson Bana alisema ifike wakati kila mtu au taasisi ifuate sheria zilizopo.
"Nawapongeza TRA kwa kusimamia sheria. Hili ni fundisho kwa watu wanaotaka kukiuka sheria zilizopo. Zipo hata taasisi za dini," alisema Dk Bana.
Alisema kilichozungumzwa na Makonda ni msimamo unaotokana na imani yake kama ambavyo mtu mwingine yeyote angeweza kulalamika baada ya mali yake kushikiliwa lakini Serikali haina imani.
Dk Bana alilitaka Bunge kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko ya sheria ili kuwapa nafuu wanaochangia maendeleo ya Taifa.
"Nadhani Makonda alikuwa haelewi sheria zilizopo vinginevyo angewaomba waliomchangia fedha za kuondolea mzigo huo bandarini. Sheria ni msumeno ingawa zinapaswa kuwa rafiki kwa baadhi ya mambo kama mchango huu," alisema.
Mwanaharakati wa haki wa binadamu, Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema haipendezi kwa Mkristo kwenda kanisani kufanya ibada inayokiuka sheria za nchi.
Alisema kama Makonda anaona TRA wamekiuka sheria basi anapaswa kufuata utaratibu wa kawaida kudai haki yake. Alisema anaweza kwenda mahakamani kama TRA hawatamuelewa.
Alisema Makonda anapaswa kuwa mfano na hasa kwa vijana wanaompenda kwa kuonyesha utii wa sheria za nchi badala ya kulalamika.
Dk Kijo-Bisimba alisema kuna watu wengi vijijini ambao kwa kukiuka sheria mali zao huwa na sifa za kupigwa mnada, lakini wakiwa na sababu za msingi huwa wanajieleza kupata msamaha, hivyo Makonda anapaswa kuwatia moyo.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Profesa Haji Semboja alisema kabla ya uongozi, Makonda ni mtu kama walivyo wengine wenye umri mdogo wanaofanya mambo ambayo hayawezi kufanywa na wazee.
"Kwa vijana mambo mengi yanawezekana. Hii ingeshangaza kama haya yangesemwa na mzee kama mimi. Makonda hawezi kuongea kama Semboja," alisema.
Alisema kutokana na vijana wengi kushika nafasi za juu, ulimwengu unashuhudia aina tofauti ya utekelezaji wa majukumu na hata mawasiliano baina ya wenye madaraka na wananchi wanaowatumikia.
"Tunaona yanayofanywa na Rais (Donald) Trump wa Marekani. Kila siku anajaribu kuwasiliana na wananchi kwa namna tofauti. Hata hapa nyumbani tunao viongozi wengi vijana ambao wanafanya vitu ambavyo visingefanywa na wazee," alisema.

Picha : RAIS KENYATTA AKUTANA NA TRUMP IKULU YA MAREKANI

Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na mwezake wa Kenya Uhuru Kenyatta mjini Washington na kuzungumzia masuala mbalimbali, zaidi wakiangazia biashara na usalama.

Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu ya Marekani, wakati wa ziara hiyo mataifa hayo mawili yalikubaliana na kutangaza mikataba ya jumla ya $900 milioni.

Rais Kenyatta ni kiongozi wa tatu kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara kukaribishwa Ikulu ya White House na kufanya mazungumzo na Rais Trump.

"Tumekuwa na ushirikiano mzuri na wa kipekee na Marekani katika masuala ya usalama na ulinzi, hasa katika harakati za kukabiliana na ugaidi. Muhimu zaidi tuko hapa kuboresha ufungamano wetu katika biashara na uekezaji, " alisema Rais Kenyatta.

Rais Trump alisema Kenya na Marekani zitaendelea kushirikiana kuimarisha ufungamano wao katika biashara, uekezaji na usalama.

"Tunafanya shughuli nyingi za utalii, biashara na ulinzi. Na kwa wakati huu tunajibidiisha kuboresha usalama," alisema Rais Trump. " Tunafurahia sana kuwa nawe hapa."

Miongoni mwa mengine, Bw Trump alifurahia pendekezo lililowasilishwa na kampuni ya ujenzi kutoka Marekani Bechtel Corporation kutaka kupewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kisasa ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.

Mataifa yote mawili yalikubaliana na kuendelea na mashauriano zaidi ili kuafikiana kuhusu ufadhili wa ujenzi huo.

Viongozi hao wawili walijadiliana pia kuhusu safari za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi New York zitakazoanza mwezi Oktoba mwaka huu na kukubaliana kwamba safari hizo za ndege zitaimarisha zaidi utalii na biashara kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Marekani ndiyo chanzo kikuu cha watalii wanaozuru Kenya na taifa hilo la Afrika Mashariki linatarajia kutumia fursa ya safari za moja kwa moja za ndege za Kenya Airways kati ya mataifa hayo mawili ambazo zitaanza Oktoba 28 kuimarisha idadi ya watalii wanaofika kenya.

Viongozi hao wawili kwa pamoja wamejadili njia za pamoja za kupambana na ugaidi na ushirikiano wa kibiashara. Mpango wa upanuzi wa barabara inayohusisha miji mikubwa ya Kenya, Mombasa na Nairobi pia ilijadiliwa.

BINTI AJIFUNGUA MAPACHA NDANI YA BESENI MWANZA


Winfrida Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Mwagala, Kata ya Ukiriguru wilayani ya Misungwi jijini Mwanza amejifungua watoto pacha kwenye beseni akiwa wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya baada ya kukosa huduma.

Tukio hilo limetokea jana Agosti 27,2018 saa 1:00 asubuhi hospitalini hapo.

Akizungumza na Mwananchi hospitalini hapo mama mzazi wa Winfrida, Flora Lugwisha amesema alimfikisha mwanaye katika hospitali hiyo saa 9:00 usiku baada ya kupewa rufaa kutoka zahanati ya kijiji cha Mwagala.

"Tulifikia mapokezi na usiku huo tulianza kusumbuliwa na wauguzi mara nendeni wodini, tulipofika wodini nikawaeleza nesi tatizo la mtoto wangu anaumwa tumbo chini ya kitovu, akaniambia ana kazi, nikampeleka kitandani mtoto alianza kulalamika uchungu wakati huo tayari saa 12:00 asubuhi," amesema.

"Nilirudi kwa nesi, akanieleza ana kazi na kunielekeza kwenda wodi ya watoto nikamtafute nesi mwingine lakini niliwakosa, nikarudi mtoto akanieleza anataka kujisaidia haja kubwa nikamweleza nesi akasema unanisumbua nikampelekea beseni wakati anataka kujisaidia akatoka mtoto wa kwanza baadaye akatoka mwingine saa 1:10 asubuhi," ameongeza.

Katika maelezo ya Flora anasema watu waliokuwamo wodini walianza kulalamika na miongoni mwao walitokea wanawake sita wakambeba mmoja akabeba beseni na kumpeleka chumba cha kujifungulia.

"Nesi alipoona hivyo ndipo alishtuka akaanza kuniomba wembe nikamwambia sina lakini badaye wembe ulipatikana akaanza kuwakatia," amesema Flora.

Mary Bujukano ni mmoja wa mashuhuda waliotoa msaada wa kumbeba mzazi ambapo amesema "mama yake (Winfrida) alipata taabu sana kutafuta huduma na kujikuta mzazi anajifungulia kwenye beseni. Kweli tulimsaidia kumbeba na kumpeleka chumba cha kujifungulia wakati tayari amejifungua watoto pacha."

Kabula Malemi mkazi wa kijiji cha Mwambola ambaye naye amempeleka mjamzito hospitalini hapo amesema huduma zao zinasikitisha kwani manesi hawahudumii wagonjwa kama inavyotakiwa.

Kwa upande wake, mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo, Dk Zabron Masatu amethibitisha kuwapo tukio hilo huku akidai kuwa wakati tukio linatokea wodi ya wazazi alikuwapo muuguzi mmoja na kwamba aliposikia kelele aliingia wodini akamkuta tayari amejifungua.

Hata hivyo, Dk Masatu amesema wanafanya uchunguzi zaidi na endapo ikithibitika ni uzembe wa muuguzi atachukuliwa hatua zaidi.

Kuhusu afya za pacha hao, Dk Masatu amesema pacha mmoja, Dotto amezaliwa utumbo wake ukiwa nje hivyo wamepewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando.


Na Twalad Salum, Mwananchi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...