Wednesday, June 18, 2025

Bilioni 1.4 zatekeleza Miradi ya Maendeleo Kata ya Ufana 2020-2025.



Na John Walter- Babati

Diwani wa Kata ya Ufana, Mheshimiwa Bernard Bajuta amepongezwa kwa utekelezaji madhubuti wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miaka mitano, ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa na kuboresha maisha ya wananchi wa kata hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari Ndeki, Mheshimiwa Bajuta alieleza mafanikio yaliyopatikana, likiwemo suala la mawasiliano ya simu ambayo sasa yanapatikana tofauti na miaka ya nyuma ambapo kata hiyo haikuwa na huduma hizo muhimu. 

Alisema hali hiyo imerahisisha mawasiliano kati ya wananchi na taasisi mbalimbali, hivyo kuchochea maendeleo.

Katika jitihada za kuwawezesha wananchi kiuchumi, Bajuta alisema kuwa vikundi 15 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vimenufaika na mikopo ya Halmashauri  ambapo jumla ya shilingi milioni 67.5 zimetolewa kwa ajili ya shughuli za kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wa huduma za maji, Diwani huyo alisema mabomba chakavu yameanza kuondolewa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa uhakika. 

Alisema kuwa serikali imetenga shilingi milioni 18 kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Guse–Ufana, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa usafiri na usafirishaji wa mazao ya kilimo.

Akizungumzia suala la umeme, Bajuta alisema kuwa kila kijiji katika kata ya Ufana sasa kinapata huduma hiyo muhimu, huku vitongoji sita kati ya kumi vikitarajiwa kuunganishwa na umeme muda wowote kuanzia sasa.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mhe. John Noya, alisema kuwa mradi wa maji wa Madunga umefikia asilimia 90 ya ukamilishaji, na unatarajiwa kuhudumia wananchi wa tarafa ya Bashnet yenye kata sita za Nar, Ufana, Bashnet, Secheda, Madunga na Qameyu.

Madiwani wa kata za Secheda, Nar, Ufana na Madunga walimpongeza Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Daniel Sillo, wakisema kuwa kutokana na jitihada kubwa alizofanya katika kata zao, ataibuka mshindi kwa kura nyingi katika uchaguzi ujao. 

Diwani Bajuta aliongeza kuwa shilingi bilioni 1.4 zimetolewa na serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo, ikiwa ni matokeo ya ushawishi mkubwa alioufanya kwa niaba ya wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Dinamu, Joseph Mandoo, alieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika Jimbo la Babati Vijijini ni ushahidi kuwa Mbunge Sillo ni kiongozi makini, na wananchi hawapaswi kumkosa tena kwenye uchaguzi ujao.

Bajuta ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake mahiri uliopelekea mafanikio makubwa katika kata ya Ufana. 

Pia alimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, kwa sapoti yake ya karibu katika kuhakikisha maendeleo yanatimia.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Madiwani wa Viti Maalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, ambao walielezea kuridhishwa kwao na kasi ya maendeleo katika kata hiyo.

Thursday, June 5, 2025

TBS YASISITIZA UMUHIMU WA VIWANGO KATIKA MAONESHO YA BIASHARA TANGA


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi na wajasiriamali katika Maonesho ya 12 ya Biashara na Utalii yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwahako City Garden, mkoani Tanga.

Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bw. Abdul Ngozoma, ametoa wito kwa wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kupitia Shirika hilo.

Amesema kuwa kuthibitisha ubora wa bidhaa si tu ni hatua ya kuongeza ushindani wa bidhaa sokoni, bali pia inalenga kulinda afya ya walaji. 

Aidha, Bw. Ngozoma ameongeza kuwa huduma hiyo hutolewa bila malipo kwa wajasiriamali wadogo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za TBS kuwawezesha na kuwainua kiuchumi.

BASHUNGWA AHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUHAMASISHA AMANI NA USALAMA



Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ametoa wito kwa Waandishi wa habari kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwaelimisha na kuwakumbusha Watanzania juu ya umuhimu wa tunu ya amani na usalama, ambayo ni urithi kutoka kwa waasisi wa taifa letu, Tanzania.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika katika ukumbi wa JNICC – Dar es Salaam, leo tarehe 5 Juni, 2025.

"Niendelee kuwaomba, muendelee kushirikiana na Serikali kwa kuwakumbusha Watanzania kuwa amani ni tunu ambayo waasisi wa taifa letu wametuachia, na ulinzi wa taifa letu ni jukumu la kila Mtanzania," amesema Bashungwa.

Bashungwa amesisitiza nafasi ya vyombo vya habari katika kufanya uandishi wa uchunguzi (investigative journalism), ili kuwaonesha Watanzania hali halisi ya mataifa yanavyopata shida kutokana na kukumbwa na migogoro iliyopelekea amani kutoweka.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kulinda nchi kwa uzalendo mkubwa, mshikamano na utulivu, na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.

Ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuviwezesha vyombo vya usalama, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi, kwa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarishwa.

Kadhalika, Bashungwa amesema Tanzania inaendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za SADC katika kupambana na uhalifu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema mkutano huo wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za SADC utajadili na kujipanga kwa pamoja kupambana na uhalifu mkubwa wa kupanga na unaovuka mipaka, ili kwa pamoja kuzuia matukio ya kihalifu katika nchi hizo.





Source

Madaktari bingwa wamtibu mzee aliyekuwa na tatizo la kuoza sehemu ya utumbo.


Na John Walter -Manyara 

Madaktari Bingwa wa Rais Samia wamefanikiwa kumfanyia upasuaji wa utumbo mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka (69) ambaye jina limehifadhiwa aliyeteseka na tatizo hilo kwa zaidi ya miazi sita.

Hali hiyo imebainika Juni 04, 2025  ambapo mwananchi huyo alifika Hospitalini hapo akiwa na maumivu makali na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo. 

Kwa mujibu wa Madaktari Bingwa hao walibaini sehemu ya utumbo mpana ikiwa imejikunja kwa nyuzi 720, hali iliyosababisha utumbo huo kujaa na kuharibika na kuonyesha dalili za utumbo kuoza.

"Aliletwa jana hapa tukamfanyia vipimo na tukabaini utumbo mpana ulikuwa umejifunga, tukamuandaa kwa ajili ya upasuaji, wakati wa upasuaji tumekuta utumbo umejikunja zaidi ya mara mbili, umejaa na kuoza ikabidi tukate sehemu ya utumbo uliooza na hadi sasa mgonjwa anaendelea vizuri" amesema Dkt Julius Mollel, Daktari Bingwa wa usauaji.

Hapo awali mgonjwa huyo, aligunduliwa kuwa na tatizo la tumbo (acute abdomen) takribani wiki mbili zilizopita na akaelekezwa kupata huduma ya kibingwa katika ngazi ya juu, hata hivyo, kutokana na changamoto za kifedha, hakuweza kufanikisha rufaa hiyo na hivyo kulazimika kurejea nyumbani.

Mara baada yakupata taarifa za ujio wa madaktari Bingwa mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam na vipimo vya picha vilivyobaini kujikunja kwa sehemu ya utumbo mpana kisha kufanyiwa upasuaji huo. 

Bi. Fatuma Hamis na Bi. Jamila Issa ambao ni wake wa mgonjwa huyo, pamoja na mtoto wake Ramadhan Mzamiru wametoa shukrani kwa Madaktari hao na kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha mpango huo wa madaktari bingwa kwani umeokoa maisha ya Mzee huyo.

"Kusema kweli hatukutegemea kama angeweza kuendelea vizuri hivi kwa hali aliyokuwa nayo awali, Tunashukuru sana Mama (Rais Samia Suluhu Hassan) kwa kututumia hawa madaktari tunamuombea Mungu azidi kumbariki katika uongozi wake" ameeleza Jamila Issa, Mke wa Mzee huyo.

"Hatuna cha kulipa zaidi ya kusema asante sana kwa madaktari hawa, kama siyo kambi hii ya Rais Samia, baba yetu huenda angepoteza maisha kutokana na changamoto ya kifedha tuliyonayo, huduma hii ni msaada mkubwa kwa sisi wa kipato cha chini," amesema mtoto wa Mzee huyo.

Upasuaji huo umefanywa na Daktari bingwa wa Upasuaji Dkt. Julius Mollel, Daktari Bingwa wa dawa za usingizi na ganzi tiba salama Dkt.Anna Dohho, Muuguzi bingwa wa Upasuaji Emelda Obara pamoja na timu nyingine ya madaktari wa hospitali hiyo.

Huduma za kibingwa katika mkoa wa Manyara zinaendelea kutolewa katika Hospitali za Halmashauri za mkoa huo hadi Juni 07, 2025 katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hospitali ya Wilaya ya Kiteto (Kibaya), Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mjini, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati Vijijini, Hospitali za Halmashauri ya Mbulu na Mbulu Mjini, Hospitali ya Wilaya ya Simanjiro.

KINGBET YAZINDUA KAMPENI YAKE YA "CHA KUKALIA" KUWASAIDIA WANAOCHEZA AVIATOR

KAMPUNI ya Kubashiri ya Kingbet imezindua rasmi kampeni yake ya CHA KUKALIA ambayo inalenga kuwasaidia wateja wanaocheza mchezo maarufu wa Aviator kujichotea Mkwanja wa maana kila usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 5, 2025 jijini Dar es Salaam amesema kampeni hiyo imeanza leo na itafika tamati Desemba mwaka 2025 ambapo itachukua miezi sita.

Amesema kuanzia saa moja hadi saa nne usiku kila siku, wachezaji wa Aviator watakuwa na nafasi ya kupiga mkwanja maradufu si tu kutoka kwenye ushindi wa kawaida wa kindege, bali pia kutokana na maokoto ya kampeni hiyo.

"Mezani, kuna mgao wa hadi TZS 500,000,000! YES huu ni mwaka wa neema kwa watumiaji wa Kingbet". Amesema

Amesema kingbet itagawanya mgao huo kwa washindi zaidi ya 3,000 watakaokidhi vigezo kwa kucheza Aviator mara nyingi zaidi kati ya saa 1 hadi saa 4 usiku.

"Washindi watalipwa papo hapo, hakuna kusubiri mpaka asubuhi, Tukisema tunakupa CHA KULALIA, tunamaanisha hautalala mpaka upate ushindi". Amesema

Aidha amesema Kingbet imetengeneza fursa hiyo kwa kuelewa mapenzi ya wachezaji wake kwa mchezo huo, na sasa imeamua kuugeuza kuwa tobo la mshiko kwa kila mchezaji.

Kwa upande wake Balozi wa Kampuni hiyo, mchekeshaji wa Majukwaa, Neila Manga amesema mgao wa hadi Sh. 500,000,000 uliowekwa ni bonge la shavu kila mtu ana nafasi ya kupata na kila mmoja atapata CHA KULALIA.

"Na ili kuhakikisha kila mmoja anapata, tumerahisisha namna ya kushiriki na kushinda kumerahisishwa sana yaani ukirusha Kindege cha Aviator kuanzia saa moja usiku hadi saa nne usiku basi unajiweka katika nafasi ya kusepa na mgao wa mpaka Sh. 500,000,000". Amesema

MWENGE WA UHURU KUZINDUA, KUWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI 13 YA RUWASA YENYE THAMANI YA BILIONI 16.713

 

Na Hadija Bagasha- Tanga

JUMLA ya Miradi 13 katika Sekta ya Maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 16.713  inatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Mkoani Tanga na itakayohudumia wananchi zaidi ya 85,017 hatua inayotajwa kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu ili kufuata huduma hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari Juni 5 mwaka huu,  Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari Lugongo alisema kwamba miradi hiyo itanufaisha wananchi 85,017 ambao wanapata huduma ya maji safi na salama na kuondokana na adha ambazo walikuwa wanazipata awali.

Alisema kila Halmashauri itakuwa na mradi na miradi 6 ya uzinduzi,miradi 5 ya uwekeji mawe ya msingi katika miradi hiyo itakayozinduliwa itajumuisha vijiji 12 lakini kuwahudumia watu 28000 na karibia asilimia 1 ya wakazi wa mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba pia kuna miradi ya uzinduzi katika Jiji la Tanga kupitia Tanga Uwasa ambapo kutazinduliwa mita za malipo kabla na ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu ya viongozi wa chama na serikali ili kuhakikisha maji yanatumika kwenye viwango lakini yanatumika wananchi waweze kulipia kulingana na uwezo wao.

Aidha alisema kutakuwa na uzinduzi kwenye Jiji la Tanga ya Mita za malipo kabla 4,000 zitazinduliwa na mwenge pamoja  na kuwepo na miradi mengine ya uzinduzi kwenye wilaya za Handeni ,Lushoto ,Mkinga na mwengine utakuwa ni mradi wa uwekaji mawe ya msingi.

Alisema katika wilaya ya Pangani kwenye Jimbo la Waziri wa Maji kutakuwa na mradi wa uwekeji jiwe la msingi mradi wa maji Mkwaja ili uweze kukamilika kwa kipindi kifupi kijacho na katika miradi wanayoweka uzinduzi ni Kwedizinga wilaya ya Handeni Vijiji,Mgombezi Korogwe Mjini  na hapo wamejenga visima 900 vya Rais Samia Suluhu.

Aidha alisema kati ya visima hivyo ambavyo ni mradi maalumu wa kutatua changamoto ya maji kwenye maeneo yasiyokuwa na maji wilaya ya Korogwe watakuwa na mradi wa uzinduzi na wilaya ya Muheza watakuwa na mradi wa visima 900 watakwenda kuweka jiwe la msingi lakni watu wameshaanza kupata huduma ya maji ikiwemo wilaya ya Mkinga wanazindua mradi wa maji Gombero na wilaya ya Tanga ambazo  ni Mita za Luku za Maji na wilaya ya Lushoto ni mradi wa Funta –Wanga

Meneja huyo alisema pia kuna mirdi mitano ya uwekaji wa mawe ya msingi kwenye eneo la Kwamaligwa wilaya ya Kilindi ambao utahudumia vijiji saba na mradi wa Maji kwamahizi ambao utahudumia eneo la Handeni Mjini.

Alieleza pia Mwenge huo utatembelea mradi wa ukarabati miundombinu ya maji Lushoto Mjini ambao utaboresha huduma kwa wakazi zaidi 23,000 na uwekeji jiwe la msingi mradi wa maji Mkwaja na Visima 900 wa Rais kwa wilaya ya Muheza ambapo miradi hiyo yote inakwenda kuwahudumia wakazi wa Tanga asilimia 3 hivyo wanategemea miradi hiyo itakapokamilika itasaidia kuboresha asilimia 3.3 ya wakazi wa Tanga wakati ile asilimia 1 ya miradi itakayozindua nayo inakuwa imeshakamilika.

"Nimpongeze Rais Dkt Samia Suluhu kwa utekelezaji wa miradi hii pamoja na Mkuu wa Mkoa kwa kuendelea kutuongoza vema katika mkoa wetu pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huu Rajab Abdurhaman"  alisema

Mwenge wa uhuru unatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga Juni 6 mwaka huu na kukimbizwa katika maeneo mbalimbali kwenye Mkoa huo.

WAZEE WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUBORESHA HUDUMA KWA USTAWI WAO


Na WMJJWM-Dodoma

Wazee wameshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri katika utoaji wa huduma za Afya kwa wazee na masuala mengine ya Ustawi wao.

Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha Wazee Tanzania (CCWWT) Tadey Mchena alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu Juni 04, 2025 jijini Dodoma.

Mchena amesema katika kipindi cha miaka minne (4) ya Uongozi wa Rais Samia huduma zinazotolewa kwa Wazee zimeboreshwa hasa utoaji wa vitambulisho vya Bima kwa Wazee ili kupata huduma bora.

"Tunamshukuru sana Mhe Rais wa Jamhuri wa Muungano Kwa kujali na kuthamini Wazee mara kadhaa wa kadha amewatuma wasaidizi tuseme tu ametubeba Wazee katika masuala yanayotuhusu hasa katika huduma za Afya katika maneno tulipo", amesisitiza Mchena.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. John Jingu amesema Serikali kupitia Wizara inathamini wazee na itaendelea kuwapatia huduma stahiki katika maneno mbalimbali kwa sababu ni hazina ya Taifa.

"Niwashukuru wazee kwa kuja kuzungumza na Wizara yenu na niwaahidi mapendekezo na maoni yamepokelewa na yatafanyiwa kazi ili kustawisha maisha ya wazee nchini kote", amesisitiza Dkt. Jingu.

Aidha Dkt Jingu amewapatia miongozo na vitini mbalimbali vinavyohusu ustawi wa wazee, haki zao pamoja na kuwaomba kusoma ili waweze kuwaelimisha wazee ndani ya chama na nje ya chama chao.

MBELLAS HEAVENLY CAKES - KARIBU FURAHIE KEKI BORA KWA BEI RAFIKI

🌟 MBELLAS HEAVENLY CAKES 🌟
Classic Cakes for All Occasions 🎂✨

Unatafuta keki nzuri, tamu na ya kipekee kwa tukio lako?
Mbellas Heavenly Cakes ndio jibu lako! Tunatengeneza keki za kiwango cha juu kwa matukio yote:

🎉 Siku za Kuzaliwa
💍 Harusi
💝 Zawadi za Wapendanao
🎄 Sikukuu na Sherehe
👶 Baby Shower & Welcome Home
🎓 Graduation na zaidi!

🍰 Keki zetu ni:
✔️ Zenye ladha ya kipekee
✔️ Muonekano wa kuvutia
✔️ Ubunifu wa kisasa
✔️ Zinapatikana dukani kwetu na kwa oda maalum kulingana na tukio lako

📍 Tunapatikana Kahama Mjini Kahama - Shinyanga
📞 Wasiliana nasi leo:
📲 0753 998 330
📲 0654 717 970
📸 Instagram: @mbellas_hevenly_cakes

🔖 Karibu sasa ufurahie keki bora kwa bei rafiki!
📅 Tunapokea oda kila siku — book mapema!



Wednesday, June 4, 2025

Tuinuke Pamoja – Midahalo ya Kijamii Kuelekea Usawa wa Kijinsia


Na John Walter -Dodoma

Katika jitihada za kujenga jamii yenye usawa na haki kwa wote, mradi wa Tuinuke Pamoja unaotekelezwa na TGNP kwa kushirikiana na Aga Khan Foundation na kufadhiliwa na Ubalozi wa Ireland, umeendelea kuleta mwamko na majadiliano ya kina kupitia midahalo ya kijamii inayofanyika katika kata za Kidoka (Chemba), Keikei na Suruke (Kondoa).

Midahalo hii inalenga kuchambua kwa kina vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa usawa wa kijinsia katika jamii na kutafuta suluhu endelevu kwa changamoto zinazojitokeza. Kwa kuzingatia umuhimu wa ushirikishwaji, midahalo inawahusisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa kijamii na wa dini, wazee wa mila, wazee maarufu, vikundi vya kijamii pamoja na watu wenye ulemavu.

Katika midahalo hiyo, washiriki wamekuwa wakieleza uzoefu wao kuhusu masuala ya kijinsia, mila na desturi zinazokwamisha maendeleo ya wanawake na wasichana, pamoja na mapendekezo ya jinsi jamii inaweza kuondokana na mifumo kandamizi. Kupitia mchakato huu shirikishi, jamii inahimizwa kufikiria upya mitazamo na mienendo inayozuia maendeleo jumuishi.

Mradi huu umeweka mkazo mkubwa katika kushirikisha sauti za watu walioko pembezoni mwa maendeleo, kwa kutambua kuwa hakuna usawa wa kijinsia unaoweza kufikiwa bila ushiriki wa makundi yote ya jamii.

Kwa pamoja, tunaamini kuwa "Tukiinuka pamoja, tunaweza kujenga jamii yenye usawa kwa wote."

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...