Wednesday, April 28, 2021

Giggs Ashitakiwa Kuwanyanyasa Wanawake




MENEJA wa Klabu ya Wales, Ryan Joseph Gigs anashitakiwa makosa matatu ya unyanyasaji dhidi ya wanawake wawili. Anashutumiwa kwa kusababisha madhara ya mwili kwa mwamke aliye na umri wa miaka zaidi ya 30 na unyanyasaji wa kawaida dhidi ya mwanamke mwingine mwenye umri wa zaidi ya miaka 20 katika eneo la Salford, Novemba 2020.

 

Giggs (47), wa Worsley, pia anashitakiwa kwa kosa la kulazimisha au tabia ya kuthibiti. Amepewa dhamana ya kufika katika makakama za hakimu mkazi za Manchester na Salford, Aprili 28. Giggs alisema katika taarifa yake kwamba atakana mashitaka mahakamani.

 

"Ninaheshimu kabisa mchakato wa shetia na ninafahamu ukubwa wa madai," alisema.

"Ninasubiri kusafisa jina langu."

 

Polisi wa Manchester Police walisema maafisa wa polisi waliitwa saa nne na dkika tano za usiku tarehe 1 Novemba kutokana na taarifa za usumbufu zilizotokea katika eneo la Worsley.

 

Polisi walisema kuwa mwanamke mwenye miaka zaidi ya 30 alitibiwa majeraha madogo katika eneo la tukio. Giggs pi anashutumiwa kwa tabia ya kulazimisha na mienendo ya kudhibiti anayodaiwa kutekeleza katika miezi ya Disemba, 2017 na Novemba, 2020.

 

Shirikisho la Soka la Wales (FAW) limethibitisha meneja msaidizi Robert Page h atachukua usukani wa timu hiyo kuanzia msimu huu wa Championi Lig.

 

FAW lilisema kutakuwa na mkutano wa bodi ya klabu hiyo "kujadili suala hilo na athari yake kwa shirikisho na timu ya taifa ".

 

Katika taarifa yake, Bw Giggs alioneza kuwa: "Ningependa kumtakia Robert Page, makocha, wachezaji na mashabiki kila mafanikio katika michuano ya Eropa msimu huu."

 

Winga huyo wa zamani wa Manchester United ni mmoja wa wacheza waliotunukiwa tuzo zaidi nchini Uingereza baada ya miaka 24 ya mchezo wake katika Old Trafford na aliteuliwa kuwa OBE mwaka 2007 kabla ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC mwaka 2009.

 

Pia alishinda kofia 64 za mchazaji bora wa Wales kati ya mwak 1991 na 2007 na aliteuliwa kuwa meneja wa taifa wa Wales Januari,2018, ambapo aliongoza timu ya taifa hilo kufuzu michezo ya Ulaya 2020, ambayo iliahirishwa kwasababu ya Covid-19. Pia ni mmiliki mwenza wa timu ya Ligi ya daraja la pili ya Salford City.


Serikali Yasitisha Matumizi ya Vitamin C Kutibu COVID-19




WIZARA ya afya nchini Uganda imesitisha matumizi ya vitamin C katika kutibu virusi vya Covid-19 kutokana na matumizi mabaya ya wagonjwa.

 

Vitamni C ndiyo moja ya dawa zilizokuwa zinatumiwa kWa wagonjwa wa covid-19 nchini Uganda kwa sababu zinasaidia kuendeleza chembe hai nyeupe(White blood cell) kupambana kuondoa virusi.

 

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya afya wanaoshughulika na masuala ya utafiti, wanadai vidonge vya vitamn C vinapatikana kwa urahisi na hivyo watu hutumia kiholela kupita kiasi na kuleta madhara.

 

Daktari Misaki Wanyegera ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kupambana na virusi vya corona katika wizara ya afya nchini Uganda, amesema walichukua hatua ya kuondoa Vitamic C baada ya wagonjwa hospitalini kukutwa wakitumia hovyo vitamin hizo na kusababisha figo kushindwa kufanya kazi kutokana na matumizi mabaya.

 

Kulingana na ushauri wa madaktari, matumizi ya Vitamin C kwa mgonjwa wa mafua ni tembe 2 kila baada ya saa 8, lakini watu wanatumia mara tatu ya hizo. Mwezi Januari kulikuwa na ukosefu wa Vitamin C za Gramu 100 kote nchini humo kutokana na matumizi mabaya.


Kirusi Kipya cha Covid 19 ni Hatari Zaidi




SHIRIKA  la Afya duniania WHO limesema aina ya virusi vya corona ambavyo vinahofiwa kuchangia wimbi la visa vya maambukizi nchini India vimebainika katika mataifa mengine kadhaa duniani.

 

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kirusi aina ya B.1.617 vya Covid-19 ambavyo kwa mara ya kwanza viligundulika India, kwa rekodi za jana vilibainika katika mataifa mengine takribani 17.

 

Taarifa hiyo ilisema idadi kubwa ya visa vyake vya maambukizi vimetokea Uingereza, Marekani na Singapore.

 

Kwa namna inavyotambulishwa aina hiyo ya virusi inaonesha kuwa ni hatari zaidi kuliko ile ya awali ikioneshwa kuwa na uwezo wa kuwa na kasi ya maambukizo au kuweza kukwepa kinga za chanjo.

 

Mlipuko wa maambukizi wa India kwa rekodi za jana pekee umesababisha visa vipya 350,000, hali inayosababisha rekodi mpya ya maambukizo duniani kufikia watu milioni 147.7 na vifo zaidi ya milioni 3.1.


Rosa Ree Akiri Kulizwa na Mapenzi






RAPA mkali wa kike Bongo, Rosary Robert 'Rosa Ree' amekiri kulia kwa ajili ya mapenzi.

 

Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Ree anasema kuwa, sababu ya yeye kulia ni kitendo cha kuwa na mpenzi aliyekuwa akimsaliti wakati yeye alikuwa akimuamini kinoma hivyo hakuweza kuamini alichofanyiwa.

 

"Mapenzi yanauma asikwambie mtu, mimi nilishawahi kulia kwa ajili ya mpenzi wangu ambaye alini-chit (kusaliti). Nilikuwa nikimuamini sana," anasema Ree.



JAMAA AKUBALI KUMUOA ALIYEKUWA KAHABA NA KUZAA WATOTO 10 WA BABA TOFAUTI


Jaribu kuweka taswira ya picha ya siku ya harusi yako kila kitu kimeandaliwa lakini una wasiwasi kwa sababu haujawahi kukutana na mwanaume ambaye anataka kukuoa.

Kando na hali hiyo kuonekana nadhimu, hii ni hadithi ya Janet, ambaye alikutana na mume wake Jackson siku Spesheli ya harusi yao. 

Akizungumza kwenye mahojiano na Afrimax, Janet alisema mume wake ambaye alikuwa anaishi Marekani, alimjua baada ya video yake kusambaa akisimulia namna alivyoacha ukahaba na kuokoka.

Alisema video hiyo ilimfanya kudhalilishwa hususan baada ya kuchapishwa bila ruhusa yake lakini ilimvutia mwanaume mmoja ambaye aliguswa na ushuhuda wake. 

"Aliona ushuhuda wangu na aliguswa. Alihisi kwamba tunatakiwa kuishi pamoja milele," alisema.

 Alitafuta nambari zake za simu akiwa Marekani na baada ya kuzipata alimpgia na kuanza urafiki na kisha wakaishia kuwa wapenzi kisha mipango ya harusi ilianza akiwa bado ughaibuni 

Walikuwa wakizungumza kila siku na wakati mapenzi yao yalikolea na kuwa dhabiti, alimposa kupitia simu na kisha punde si punde mipango ya harusi ilianza.

 Jamaa huyo hakubabaishwa na ukweli kuwa mama huyo ana watoto 10 ambao aliwazaa akiwa kahaba.

 Badala ya kubabaishwa na maisha yake ya zamani, alichagua kumuoa mwanamke ambaye alikuwa anajaribu kuishi maisha mapya. 

Janet alisema alikumbana na pingamizi kutoka kwa kanisa lake kwa kumuona kama mwenye dhambi kubwa zaidi kufanya harusi lakini alikumbatiwa na kanisa lingine ambalo liliidhinisha ndoa yake Disemba 2020.

Siku ya harusi hiyo, ndege ya bwana harusi ilitua na kukutana na mke wake kwa mara ya kwanza na kisha wawili hao walibadilishana viapo vya ndoa. Baada ya kubadilishana viapo vya ndoa, wapenzi hao walikaa pamoja kwa wiki kadhaa kabla ya mwanamume huyo kurejea Marekani na kuanza mipango ya Janet kuhamia nchini humo.


Tuesday, April 27, 2021

Hali ya Mzee King Kikii Bado ni Tete “Nisaidieni”




GLOBAL TV imemtembelea msanii Mkongwe wa muziki wa dansi nchini aliyetamba zaidi na kibao chake cha 'KITAMBAA CHEUPE', Mzee King Kiki, ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maradhi ambayo yamemsababishia kukaa nyumbani na kushindwa kuendelea na kazi zake.

 

NGULI huyo amekumbwa na maradhi ya uti wa mgongo.

Unaweza kumchangia fedha kwa ajili ya matibabu kupitia nambari hii

( 0713 50 50 62 au 0757 50 50 62 – JINA COSTANSIA KALANDA)


JSC yampendekeza Martha Koome kuwa Jaji mkuu nchini Kenya

 


Koome ana uzoefu wa miaka 33 katika tasnia ya sheriana pia amewahi kuhudumu kamamtetezi wa haki za binadamu

Tume ya huduma kwa idara ya mahakama JSC imempendekeza jaji Martha Koome kuwa Jaji mkuu ajaye nchini Kenya ili kuichukua nafasi ya David Maraga aliyestaafu .

Kaimu mwenyekiti wa tume hiyo Olive Mugenda ametangaza kwamba uamuzi huo umeafikiwa na makamishna wote wa tume hiyo .Koome ana uzoefu wa miaka 33 katika tasnia ya sheria na pia amewahi kuhudumu kama mtetezi wa haki za binadamu . Iwapo rais Uhuru Kenyatta ataidhinisha uteuzi huo Koome atakuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama Jaji mkuu nchini Kenya .


Source

Makampuni yasiyolipa waajiri kutangazwa hadharani


Na Maridhia Ngemela, MWANZA

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, sera na Ajira, Patrobas Katambi.

 ,amewataka  waajiri kuwathamini wafanyakazi kwani wao ndo hufanya kazi na kuinua uchumi wa taasisi husika  hivyo ni vyema kuona thamani ya mwajiri na kumpatia sitahiku zake kwa wakati.

Ameongeza kuwa,wananchi kutambua,walioshikilia uchumi wa nchi ni wafanyabiashara wa kati kushuka chini,ndio maana serikali imeamua kuwawezesha,hivyo vijana,kina mama na baba wafanye kazi na sio kusubiri ajira ambazo upatikanaji wake umekuwa ni watabu.

Katambi alisema hayo jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na waajiri ,chama cha wafanyakazi pamoja wakala wa usalama afya  na mahali pa kazi ( Osha)  katika  maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahala pa kazi Duniani ambayo yalianza Aprili 26 mwaka huu hadi Aprili 28/2021 ambayo ndio itakuwa siku ya kilele,

"Waajiri wapo wanaowanyima haki wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi,natoa rai andapo wakibainika sisi tutawashughulikia,hivyo wale wote walioyo na madai walioumizwa na wanasumbuliwa na waajiri kupata haki yake wafike wizarani tutatatua madhira hayo,"alisema Katambi.

Katika maazimisho hayo zaidi ya wajasiliamali 600 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa walipatiwa mafunzo ya usalama,Afya mahala pakazi kwa kipindi cha wiki mbili,ambayo yamegharimiwa na serikali maana wananchi ili afanye kazi anategemea afya na usalama ikiwa ni kuleta mafanikio ndani ya familia na Taifa kwa ujumla

 Naye mkurugenzi mtendaji wa OSHA Khadija Mwenda,alisema, adha kubwa wanayokutana nayo katika usimamizi wa sheria ni uelewa mdogo wa kukabiliana na athari kazini kumepelekea matatizo,hivyo wananchi watambue mtaji wao ni usalama na afya,hivyo akipata madhara hawezi kujikomboa kiuchumi kutokana na maumivu au kilema alichokipata kutokana na mazingira ya kazi

Aidha mwenda alisema bado kunachangamoto katika mfumo  ya kuwalinda wafanyakazi mpaka sasa ni asilia 40 tu ndio kubwa wako salama mahala la kazi.

Kwa upande wake wakili mwandamizi  chama cha waajiri Tanzania Mercy Sevya amesema waajiri  wawaelimishe  kuhusiana  na namna ya kuishi salama na kutoa mfumo samala kwaajili ya wafanyakazi  mahala pa kazi .

AWESO ATOA SIKU 10 MRADI WA MAJI MWAKITOLYO SHINYANGA UKAMILIKE

 

Waziri wa Maji Jumaa Aweso (mwenye shati la bluu katikati) akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Ukaguzi ukiendelea.


Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga huku akitoa siku 10 mradi huo uwe umekamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Amesema kati ya miradi ya maji 177 ambayo ni kero hapa nchini, mmoja wapo ni mradi huo wa Mwakitolyo hivyo kuagiza hadi ifikapo Mei 5 mwaka huu ndani ya siku 10 zijazo, uwe tayari umeshakamilika.

"Mradi huu wa maji Mwakitolyo nina historia nao, ni kati ya miradi ya maji kichefuchefu hapa chini, hivyo naagiza hadi ifikapo Mei 5 uwe tayari umeshakamilika"

"Nakumbuka nilikuja hapa miaka ya nyuma mradi hiu ulikuwa ni changamoto nikaupa jina kichefu chefu kwa sababu haiwezekani zitokea fedha Bilioni 1.4 lakini mwananchi hana maji "Alisema

Waziri Aweso alisema mradi huo ni miongoni mwa 177 ambayo waliianisha ambayo ilikuwa inachafua wizara na maelekezo yalikuwa ni kuhakikisha miradi kichefu chefu yote inakwamuliwa na kati ya miradi 177 miradi 85 wameikamilisha ikiwemo huo wa Mwakitolyo .

Alisema hivi sasa hapo hakuna kisingizio kwa sababu fedha zimekwisha kutolea milioni 400 na mabomba yameshajengwa hivyo ndani ya Mei 10 mwaka huu wananchi wanakwenda kupata huduma ya maji.

"Hapa visingizio hakuna tena tutakwenda kugombana kwa hali ninavyoiona mambo ni mzuri kubwa ninaloliona pamoja na wananchi wa mwakitolyo kupata maji lakini na mwakitolyo maeneo ya jirani inakuwa kwa kasi sana kwa hiyo tutafute eneo la mlima tutengeneze tenki la lita laki tano"Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa, ambao ndiyo watekelezaji wa mradi kwa kushirikiana na (RUWASA),alimhakikishia Waziri Aweso kuwa utakamilika ndani ya siku hizo 10.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...