Sunday, August 31, 2025
HIFADHI YA MPANGA-KIPENGERE YAKONGA NYOYO ZA WALIMBWENDE MISS UNIVERSE 2025
Tuesday, August 26, 2025
DOTTO BAHEMU AMEWAOMBA WANA - CCM KUVUNJA MAKUNDI NA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KUTAFUTA USHINDI WA KISHINDO


Wananchi waiomba Serikali kutengeneza mfumo mmoja ili wafanyabiashara walipe Kodi kulingana na uwezo wa biashara zao
Wananchi wameiomba Serikali Kupitia Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuhakikisha unatengeneza mfumo mmoja ambao utasaidia kwa kila mtanzania anayefanyabiashara kulipa kodi kwa kiwango cha uwezo wa biashara yake.
Hayo aliyasema katibu w Jumuiya ya wa wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Ismail Masuod wakati akizungumza katika semina ya wafanyabiashara ya Elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Tanga iliyofanyika katika ukumbi wa YDCP jijini Tanga
ambapo alisema kuwa elimu inasaidia wafanyabiashara kujua umuhimu wa kulipa kodi na sheria ya kodi.
Aidha alisema kuwa hiyo itasaidia mambo makubwa matatu kwanza ni kutengenza walipa kodi wapya,kwani kuwa na mpango maalum wa kutengeneza walipa kodi katika nchi kutakuwa walipo kodi wacheche.
Akizungumzia Daniel Ramadhani ambaye ni Kaimu meneja wa mkoa wa Tanga alisema lengo la Mafunzo hayo kwa wafanyabiashara ni kuwawezesha kujua sheria ya fedha kutokana mabadiliko ya sheria kwaajili ya maborehsoya kodi yanayotokea kila baada ya bunge la bajet ambapo Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imepanga kuwafikia makundi yote ambayo inatakiwa kulipa kodi.
Aliongeza kusema kuwa sheria iliuofanyiwa marekebisho ni pamoja na sheria ya ongezeko la kodi ya samani ambayo kutakuwa zuio la kodi ya samani ni mauzo ya biadhaa kwa maana ya asilimia tatu ya mauzo ya bidhaa na mauzo ya ya huduma kwa mfano banki na mitandao mengine.
Kwa upande Chama Siliwa Afisa Masidizi wa elimu na mawasiliano wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu alisema wametoa elimu kwa mlipa kodi kutokana mabadiliko ya sheria mpya ya ulipaji wa kodi hivyo tumeamua kuwapa elimu hiyo wazijue wanapoendelea kulipa kodi changamoto kuwa ya watu kutokulipa kodi ni pamoja na uelewa mdogo wa sheria.
Monday, August 25, 2025
WALICHOKIFANYA WANANCHI WA WILAYA YA MULEBA KWA WALIOTEULIWA KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MULEBA KASKAZINI NA KUSINI
Dkt. Oscar Kikoyo aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kusini akizungumza na wananchi baada ya kufika ofisi za Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Athumani Kahara( Aliyevaa Kanzu ) akiwa na wateuliwa wa nafasi ya Ubunge baada ya kufika ofisi za chama hicho.Thursday, August 14, 2025
KATAVI WAMPA HEKO RAIS SAMIA UMEME VIJIJINI
Wananchi wa Kijiji cha Mapili Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kubadili maisha yao kupitia mradi wa umeme uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Wametoa shukrani hizo kwa nyakati tofauti kijijini hapo Agosti 11, 2025 wakati wa kampeni maalum ya uhamasishaji wa matumizi ya umeme kwa ajili ya shughuli za kiuchumi inayotekelezwa na REA katika maeneo mbalimbali kote nchini.
"Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kabla ya kupata nishati hii ya umeme mazingira hayakuwa mazuri, usiku hatukuwa na mwanga sasa hivi tunaishi kwa amani na hata baadhi ya shughuli za kimaendeleo zinafanyika hadi muda wa usiku lakini pia tunapata habari kwa kutazama luninga muda wowote tunaotaka pia baadhi ya vijana wamepata ajira kupitia umeme," alisema Mwalimu Mstaafu, Mkazi wa Kijiji cha Mapili, Amos Katawa.
Mrisho Mussa Fundi Uchomeleaji katika Kijiji cha Mapili alisema kabla ya umeme kufika kijijini hapo walikuwa wakilazimika kufanya shughuli zao maeneo ya mjini ambapo ni mbali na kijijini hapo na hivyo kusababisha kupanda kwa gharama ya bidhaa walizokuwa wakizalisha pamoja na kutumia muda mrefu kukamilisha kazi.
"Tulikuwa tunalazimika kutengenezea mageti huko Inyonga na kisha tunasafirisha, hali hii ilikuwa ni usumbufu kwetu hadi kwa wateja wetu, lakini sasa mambo yote tunafanya hapa, hakuna haja tena ya kurudi mjini, nawasihi mafundi na wengine wenye fani zao wasipende kukimbilia mijini; Rais Samia ametuona, kila kitu hapa kijijini sasa hivi kinapatikana," alisema fundi Mussa.
Kwa upande wake Scholastica Kitwewe, Mkazi wa Kijiji cha Mapili alisema umeme umerahisisha maisha ya wanawake kijijini hapo kwani hapo awali walikuwa wakitumia muda mwingi kuandaa mahindi ya unga kwa kutwanga katika kinu lakini sasa mashine za kusaga na kukoboa nafaka zimefunguliwa kijijini hapo jambo ambalo linarahisisha shughuli zao za mapishi ya kila siku na kuwaokolea muda.
Kwa upande wake, Elasto Mwampaya maarufu kama Fundi Lam ambaye ni Fundi Seremala kijijini hapo alisema kuwa umeme umewezesha kukua kwa karakana yake ya useremala na kwamba hivi sasa anatengeneza fenicha zenye ubora na kuuza katika mikoa mbalimbali kote nchini jambo ambalo halikuwezekana hapo awali kabla ya kufikishiwa umeme.
Alisema umeme umemuwezesha kupanua wigo wa ajira na kwamba katika karakana yake ameajiri vijana wengi na pia anatoa mafunzo kwa vijana namna ya kutengeneza bidhaa kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyotumia umeme.
Akizungumza kuhusiana na umeme kijijini hapo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mapili Anthony Mwijuma, aliipongeza REA kwa kutekeleza mradi huo ambao alisema umekuwa ni neema kwa wananchi wake ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kufikiwa na umeme.
"Wananchi wa Mapili tunasema asante kwa Rais Samia kwani kupitia umeme vijana wamepata ajira, wengine wamebuni miradi na biashara ndogondogo za vinywaji, vifaa vya simu na wengine sasa hivi na mafundi wa kuchomelea hapahapa kijijini," alisema Mwijuma.
Akizungumza hali ya usambazaji umeme mkoani Katavi, Msimamizi wa miradi ya REA Mkoani humo, Mha. Gilbert Furia, alisema vijiji vyote vina umeme na kazi inayoendelea sasa ni kusambaza umeme katika vitongoji ambavyo havikufikiwa.
"Tunamshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ambayo imewezesha kufikisha umeme katika vijiji vyote 49 ndani ya Halmashauri za Mlele na Mpimbwe na sasa tunatekeleza mradi wa kusambaza umeme vitongojini; hadi sasa katika Hamashauri hizi vitongoji 176 kati ya vitongoji 251 vimefikiwa na mradi unaendelea wa kufikisha umeme kwenye vitongoji vilivyobaki," alisema Mha. Furia
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Mlele, Yahaya Mbulu aliipongeza REA kwa kukamilisha mradi wa kufikisha umeme vijijini na alisema kuwa amejionea namna ambavyo kazi ya kufikisha umeme vitongojini ikiendelea kutekelezwa kwa kasi.
"Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia REA; vijiji vyote vimefikiwa; wananchi wa Mlele tunasema asante kwa Serikali maana umeme umeleta fursa, Mlele ya jana sio ya leo, hatua imepigwa," alisisitiza Mbulu.
Sunday, August 10, 2025
Mama Manyara adaiwa kumuua mtoto wake kikatili kwa shoka.
Na John Walter Babati, Manyara
Wakazi wa Kitongoji cha Vituwey, Kijiji cha Ngoley, Kata ya Mwada wilayani Babati mkoani Manyara wameshtushwa na tukio la kikatili lililofanywa na mwanamke anayejulikana kwa jina la Mariam Mohamed, anayedaiwa kumuuua mtoto wake wa kumzaa wa kiume mwenye umri wa miaka 2.5 kwa kumtenganisha viungo vya mwili wake kwa kutumia shoka.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Vituwey, Jackson Mombo, amesema tukio hilo lililotokea majira ya saa nne asubuhi Agosti 8, 2025, limewaacha wananchi midomo wazi na kushindwa kuamini kilichotokea.
Ameongeza kuwa ni muhimu jamii kuwa karibu na mtu yeyote anayeonyesha dalili za mawazo mazito au matatizo ya afya ya akili ili kuepusha madhila kama hayo.
Mashuhuda wamesema kuwa baada ya mauaji hayo, Mariam alipiga yowe akisema "jamani nisaidieni, nimemuua mwanangu", hali iliyowafanya majirani kukimbilia nyumbani kwake ambapo walipofika, walimkuta akiwa hajakimbia, huku mwili wa mtoto ukiwa juu ya godoro wanalolalia.
Baadhi ya majirani wamesema hawaamini kuwa mama huyo amefanya kitendo hicho kwa akili timamu, wakidhani huenda alikuwa na tatizo la afya ya akili.
Baba mkwe wa Mariam, Kimweri Juru, ameeleza kuwa aliwahi kumpa onyo mara kadhaa kuhusiana na tabia ya unywaji wa pombe, lakini hakutaka kusikia, na kwamba matokeo haya yanaweza kuwa ni sehemu ya madhara ya tabia hiyo.
Wakati tukio linatokea, mume wa Mariam hakuwepo nyumbani kwani usiku alikuwa akilinda mazao shambani dhidi ya wanyama waharibifu.
Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio, kuchukua mwili wa marehemu na kumkamata Mariam kwa uchunguzi zaidi.
Tukio hili limeongeza hofu kwa wakazi wa Tarafa ya Mbugwe, kwani ni la pili ndani ya wiki moja, baada ya lile la kitongoji cha Mbugani, Kata ya Magugu, ambapo mwanaume alimuua jirani yake mbele ya watoto wake wawili wadogo kwa kumkatakata kwa panga.
Wakazi wanasema matukio haya ya mauaji miongoni mwa watu waliokuwa wakiheshimika na kuonekana wema, yanahitaji uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo chake na kuchukua hatua za kudhibiti hali hiyo.
Thursday, August 7, 2025
Vasco Mgimba aibuka mshindi kwenye kura za maoni Ludende
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Ludende wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Ndugu Vasco Weston Mgimba ameibuka mshindi wa kura za maoni za wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata hiyo kwa ajiri ya kupata ridhaa ya kuwa diwani.
Mgimba aliyekuwa akitetea nafasi hiyo ameibuka kidedea kwa kupata kura 382 akimshinda mpinzani wake Stephano Weston Luoga aliyepata kura 11 za wajumbe ikiwa katika kata hiyo ni wajumbe wawili pekee waliokuwa wakishindania nafasi hiyo.
Tuesday, July 29, 2025
Airtel Africa Yatangaza Matokeo Mazuri ya Robo ya Kwanza 2025
Airtel Africa imetangaza matokeo bora kwa robo ya kwanza iliyoishia Juni 30, 2025, ikionesha ongezeko la wateja wanaotumia huduma za intaneti na Airtel Money katika nchi mbalimbali za Afrika.
Afisa Mtendaji Mkuu, Sunil Taldar, amesisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya utekelezaji wa mkakati thabiti unaolenga kuboresha huduma kwa wateja na kuwekeza katika teknolojia mpya kama vile Airtel Spam Alert ili kuhakikisha usalama na kuimarisha imani ya mtandao.
"Tunaendelea kukuza ujumuishaji wa kifedha na kuunganisha jamii nyingi zaidi barani Afrika," amesema.
Airtel Africa imeshukuru wafanyakazi na wadau wote kwa mchango wao katika kuhakikisha ukuaji endelevu na huduma bora kwa wateja nchini Tanzania na kwingineko.
Sunday, July 27, 2025
RC Manyara awapiga marufuku viongozi kujilimbikizia mali
Na John Walter-Babati
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amepiga marufuku viongozi na watumishi wa umma mkoani humo kujilimbikizia mali ambazo wanashindwa kuziendeleza, akieleza kuwa hali hiyo inaziba fursa kwa wananchi wengine kupata maendeleo.
Sendiga alitoa agizo hilo Julai 24, 2025, wakati wa hafla ya kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa stendi ya mabasi, barabara za lami na mitaro katika stendi ya muda ya Makatanini, mjini Babati.
Amesema baadhi ya viongozi wamekuwa wakijipatia mali nyingi – zikiwemo vibanda – lakini wanashindwa kuviendeleza, hali inayokwamisha matumizi bora ya rasilimali zilizopo kwa manufaa ya jamii.
"Marufuku kujilimbikizia vibanda vitakavyojengwa katika stendi hii mpya. Kila mmoja apate kibanda kimoja ili kutoa nafasi kwa wengine, wale waliopo sasa kwenye stendi ya muda wapewe kipaumbele kwa gharama nafuu," alisisitiza.
Aidha, alibainisha kuwa kukamilika kwa stendi hiyo kutachangia kukuza uchumi wa wananchi wa Babati na kuondoa kero ya vumbi ambalo limekuwa likisababisha maradhi kwa watumiaji wa stendi hiyo kwa muda mrefu.
Kwa upande mwingine, Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza mkandarasi anayetekeleza mradi huo, kampuni ya Wesons Engineers, kuhakikisha hakuna visingizio vya kuchelewesha utekelezaji wa mradi huo na kwamba kazi ifanyike kwa ubora na ikamilike kwa wakati.
"Tunataka kuona thamani ya fedha kwenye kila senti, hakuna sababu ya kuchelewa au kutoa visingizio. Ujenzi uende kwa kasi na ubora unaotakiwa," alisema Sendiga.
Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi 15 kwa gharama ya shilingi bilioni 19.996, na unahusisha ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 4.7 pamoja na mitaro ya kupitisha maji yenye urefu wa kilomita 8.15.
Ujenzi wa stendi hiyo mpya unatarajiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa sekta ya usafirishaji mjini Babati na kuchochea biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati.
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...







.jpg)







.jpg)
.jpg)



