Monday, June 23, 2025

WARAGHIBISHI WAJENGEWA UWEZO KUCHOCHEA USAWA WA KIJINSIA

Na Deogratius Koyanga, Kondoa

Zaidi ya Waraghibishi 30 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa (DC) na Halmashauri ya Mji wa Kondoa (TC) wamepata mafunzo kabambe ya siku nne yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kuongoza mabadiliko katika jamii zao kwa mtazamo wa kijinsia. Mafunzo hayo yamefanyika katika Viwanja vya Riverside, Kondoa Mjini, yakiratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) kwa kushirikiana na The Aga Khan Foundation kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Ireland chini ya mradi wa Tuinuke Pamoja.

Katika mafunzo hayo, Waraghibishi wamefundishwa mbinu za kuibua na kuchambua changamoto zinazowakabili wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na makundi mengine yaliyo pembezoni kwa kutumia mbinu ya ABCD (Asset-Based Community Development) – inayowahimiza kutumia rasilimali zilizopo ndani ya jamii kutatua matatizo yao badala ya kusubiri misaada ya nje.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo, Ndg. Deogratius Temba, ambaye ni Mwezeshaji wa Kitaifa katika masuala ya kijinsia na maendeleo ya jamii, alisema mafunzo hayo yamelenga kuimarisha uwezo wa Waraghibishi katika kutoa elimu na kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu kwenye michakato ya maendeleo, hususan mchakato wa bajeti na mipango ya maendeleo ya jamii kwa mtazamo wa kijinsia.

"Kupitia mafunzo haya, Waraghibishi wameelewa kwa kina namna ya kushiriki katika mzunguko wa mchakato wa bajeti ya serikali za mitaa, kuanzia hatua ya uibuaji wa vipaumbele vya kijinsia kupitia mfumo wa O&OD, hadi kuwasilisha mapendekezo kwenye ngazi ya Halmashauri," alisema Ndg. Temba.

Aidha, washiriki walifundishwa jinsi ya kutumia nyenzo mbalimbali za serikali, ikiwemo sera na miongozo ya bajeti, ili kuhakikisha mahitaji ya wanawake na makundi mengine maalum yanazingatiwa katika mipango ya maendeleo.

Kwa upande wake, Bi. Fredina Saidi, mmoja wa wakufunzi wa warsha hiyo, alisema waraghibishi wamefundishwa kutumia mbinu shirikishi kama njia ya kuchambua changamoto na kushauri suluhisho linalojikita kwenye muktadha halisi wa jamii zao.

"Uraghibishi ni kama mwanga unaoangaza giza la changamoto za kijamii. Kupitia mafunzo haya, washiriki wataweza kuchochea majadiliano ya kina katika jamii zao, kufuatilia utekelezaji wa mipango na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika safari ya maendeleo," alisema Bi. Fredina.

Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka ambapo serikali za mitaa zinajiandaa kuanza mchakato wa kuandaa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26, hivyo kuwapa Waraghibishi nafasi muhimu ya kushiriki kikamilifu kwa niaba ya wananchi, hasa wanawake na makundi yaliyo pembezoni.

Mradi wa Tuinuke Pamoja umekuwa nguzo muhimu ya kuwawezesha wananchi wa ngazi ya jamii kuibua sauti zao, kushiriki kwenye maamuzi na kushinikiza uwajibikaji kwa viongozi, kwa lengo la kujenga jamii jumuishi na yenye usawa wa kijinsia.




CRDB YAWANOA MAWAKALA WAKE SHINYANGA KWA MAFUNZO YA HUDUMA BORA NA USALAMA WA MIAMALA


Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Benki ya CRDB imeendesha mafunzo maalum kwa Mawakala wake kutoka Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwaongezea uelewa na ufanisi katika utoaji wa huduma bora za kibenki kwa wananchi.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Juni 23,2025 katika Ukumbi wa Makindo Hotel, Mjini Shinyanga yakihusisha mada mbalimbali muhimu ikiwemo, Utoaji wa huduma bora kwa wateja, Huduma mbalimbali za kibenki, Udhibiti wa utakatishaji fedha na elimu ya ujasiriamali ili kukuza biashara za mawakala.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Bw. Jumanne Wambura Wagana, amewahimiza Mawakala hao kuwa mabalozi wa huduma bora na waaminifu kwa jamii, akisisitiza kuwa wao ni kiungo muhimu kati ya benki na wananchi waliopo katika maeneo ya vijijini na mijini.

"Kazi za Uwakala zinahitaji umakini na uaminifu. Tuendelee kuchukua tahadhari wakati wa kutoa huduma kwa sababu matukio ya wizi wa kutumia nguvu na utapeli mtandaoni yanaongezeka. Epukeni rushwa na vitendo vya utakatishaji fedha," amesema Wagana.

Aidha, amewashauri Mawakala kuimarisha usalama wa ofisi zao na kukata bima ya fedha ili kujikinga dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na biashara ya fedha au miamala.

Ameeleza kuwa, Benki ya CRDB inaendelea kuhakikisha  kuwa, huduma zake zinafika kwa wananchi wote kwa ufanisi na kwa kuzingatia usalama wa kifedha.

Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB Kanda – Kitengo cha Mawakala, Bw. Kidagaa Kubalunga, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa CRDB kuhakikisha kila wakala anatoa huduma bora kwa kuzingatia maadili ya kazi, maarifa ya kifedha na matumizi ya teknolojia.

"Tunataka kila CRDB Wakala awe na uelewa mpana kuhusu huduma za benki, udhibiti wa miamala yenye viashiria vya utakatishaji fedha na pia awe na uwezo wa kuwahudumia wateja kwa njia rafiki, salama na ya kisasa," amesema Kubalunga.

"Tunayatambua mafanikio makubwa yanayotokana na mtandao wa zaidi ya mawakala 25,000 nchini. Hawa ndiyo wanaosogeza huduma za kibenki hadi maeneo yasiyofikika na matawi ya benki," ameongeza.

WANAFUNZI VYUO VIKUU MWANZA WAJENGEWA UWEZO WA KUTAMBUA FURSA KUPITIA KONGAMANO LA IAESEC KWA UDHAMINI WA BARRICK

Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Mwanza anayeshughulikia Taaluma Prof. Hosea Rwegoshora, akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Mwanza kwenye kongamano la kuwajengea uwezo, kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi lililoandaliwa na AIESEC na kudhaminiwa na Barrick.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Mwanza anayeshughulikia Taaluma Prof. Hosea Rwegoshora, akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Mwanza kwenye kongamano la kuwajengea uwezo, kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi lililoandaliwa na AIESEC na kudhaminiwa na Barrick.
Afisa Raslimali Watu Mwandamizi wa Barrick North Mara, Emmanuel Msacky akiongea na wanafunzi wakati wa kongamano hilo
Wanafunzi wakifuatilia mada mbalimbali
Wanafunzi wakifuatilia mada mbalimbali
Wafanyakazi wa Barrick katika picha ya pamoja na meza kuu
Vijana wasomi nchini waliopo vyuoni wametakiwa kuongeza bidii, maarifa katika masomo yao na kuwa wabunifu ili kuweza kupenya kwenye soko la ajira kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo migodini sambamba na kuweza kujiajiri kwa kutumia taaluma zao pindi wamalizapo masomo sambamba na kuchangamkia fursa muhimu kwa mafanikio ya kitaaluma.


Ushauri huo umetolewa na , Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT),Profesa Hosea Rwegoshora, wakati wa kongamano la Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mkoani Mwanza lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji kwa vijana ya AIESEC Tanzania ambalo limedhaminiwa na Barrick nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ambalo limefanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino kilichopo jijini Mwanza.


Amesema kuwa hivi sasa tuko kwenye kipindi cha mapinduzi makubwa sayansi na teknolojia hivyo aliwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kuingia soko la ushindani wa ajira hapa nchini sambamba na kuibua fursa za kujiajiri.


Naye Afisa Raslimali Watu Mwandamizi kutoka Barrick North Mara, Emmanuel Msacky , wakati akieleza shughuli za kampuni na programu zake wezeshi kwa jamii kwa washiriki, alisema kampuni ya Barrick nchini ambayo inaendesha shughuli zake kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals, itaendelea kutafuta rasilimali watu kwa ajili ya kufanya kazi kwenye migodi yake ikiwemo vijana wanaohitimu kutoka kwenye vyuo vikuu mbalimbali na vya ufundi vya kati hapa nchini na lengo kubwa kuhakikisha inaendelea kuibua vipaji na kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira.


Bw. Msacky , aliwaeleza washiriki kuwa migodi inayomilikiwa na Barrick nchini ya North Mara na Bulyanhulu imekuwa ikitoa fursa kwa vijana wa vyuo vikuu kuomba ajira mara tu wanapomaliza masomo na wakiwa kazini wanapata nafasi ya kujengewa uwezo na kampuni pia kampuni inayo programu ya kutoa nafasi ya mafunzo kwa vitendo kwa Wanafunzi wanapokuwa bado wako vyuoni.


Semina za kuwanoa vijana wasomi vyuoni kupitia taasisi ya AIESEC kwa udhamini wa Barrick nchini mwaka huu tayari zimefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Arusha, Iringa na Zanzibar.

MDEMU AWATAKA WANAWAKE KUPENDANA, KUSHIKAMANA NA KUPEANA SAPOTI KATIKA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI

Na WMJJWM – Iringa

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu, ametoa wito kwa wanawake nchini kupendana, kushikamana, na kupeana taarifa kuhusu fursa zinazotolewa na serikali ili kujikwamua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika nyanja mbalimbali za kijamii na kisiasa, ikiwemo kugombea nafasi za uongozi.

Mdemu ametoa kauli hiyo Juni 22, 2025 wakati wa hotuba yake kwenye kongamano la kuelekea kilele cha Siku ya Wajane na Wagane Duniani, linalotarajiwa kufanyika Juni 23, 2025, mkoani Iringa.

Katika hotuba hiyo, amesisitiza umuhimu wa wanawake kuelimishana na kupeana taarifa kuhusu mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kama njia ya kuwawezesha kiuchumi.

"Kinamama tupendane, tuache chuki na wivu wa maendeleo. Tushikane mikono, tupeane fursa. Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametupatia mikopo na fursa nyingi kwa ajili ya kutuinua kiuchumi. Naomba tupeane habari na tushirikiane kuzifikia,  tuache kukwamishana," amesema Mdemu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Badru Abdunur, ametoa pongezi kwa uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kuandaa kongamano hilo muhimu ambalo limewakutanisha wajane na wagane ili kujadili changamoto na fursa zinazowahusu.

"Ni faraja yetu kukutana nanyi leo, na tumeweza kujifunza mambo kadhaa. Tuna matumaini kuwa mtayafanyia kazi mafunzo mliyopata ili yakawasaidie kukabiliana na changamoto na kukimbilia fursa mbalimbali. Serikali imeendelea kupokea na kutatua changamoto za makundi maalum, ikiwemo wajane na wagane," amesema Badru.

Aidha, Afisa Maendeleo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Saida Mgeni amewataka wanawake kuwa na nidhamu ya fedha na kujifunza tabia ya kujiwekea akiba, hata kama ni kidogo, ili waweze kujitegemea kiuchumi. Pia aliwasihi kusimamia kwa uadilifu mali walizoachiwa na wenza wao waliotangulia mbele za haki.

Baadhi ya wajane na wagane walioshiriki kongamano hilo waliishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuwaandalia siku maalum inayolenga kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.

Source

Sunday, June 22, 2025

MATI SUPER BRANDS YADHAMINI MASHINDANO YA WEST KILI TOUR CHALLENGE 2025

 



Na Ferdinand Shayo ,Kilimanjaro .

Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imedhamini mashindano ya West Kili Tour Challenge 2025 msimu wa 5 yanayojumuisha mbio za riadha,baiskeli na piki piki yaliyofanyika katikati ya Hifadhi ya shamba la Miti la West Kilimanjaro kwa lengo la kukuza utalii wa michezo na kuunga mkono juhudi za Rais Dr.Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya The Royal Tour.

Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo Brayson Mnene amesema wamekuwa wakidhamini mashindano hayo kwa miaka miwili mfululizo kwa lengo la kuunga mkono utalii wa michezo na shughuli za uhifadhi zinazofanywa kwa lengo la kutunza ekolojia ya Mlima Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Christopher Timbuka amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya utalii katika hifadhi ya shamba la miti la West Kilimanjaro lenye vivutio mbali mbali vya utalii ikiwemo wanyamapori,ndege na miti ya asili.

Mkuu wa Hifadhi ya West Kilimanjaro Robert Faida ameyataka makampuni mbali mbali kuunga mkono mashindano hayo yanayolenga kutangaza utalii na fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta hiyo .

Kwa Upande wake Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godifrey Mzava amewapongeza Waandaaji wa mashindano hayo pamoja na wadhamini kwa kushiriki kwenye tukio hilo kubwa lililowakutanisha mamia ya wananchi na wadau wa utalii







FCC YATOA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA DODOMA KUELEKEA MAADHIMISHO YA KITAIFA SIKU YA UDHIBITI BIDHAA BANDIA



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Salvator Chuwa,akizungumza wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Salvator Chuwa,akizungumza wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma Bw.Gilbert Chuwa,akizungumza wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Tume ya ushindani kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.




Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia iliyoandaliwa na Tume ya ushindani kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia iliyoandaliwa na Tume ya ushindani kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia iliyoandaliwa na Tume ya ushindani kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia iliyoandaliwa na Tume ya ushindani kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.


Afisa ufuatiliaji Bidhaa Bandia kutoka Tume ya ushindani Frank Chondo,akiwasilisha mada wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.


Katibu Mtendaji Jumuiya ya wafanyabiashara Bw.Alexander Mallya,akizungumza wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia iliyoandaliwa na Tume ya ushindani kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.


Wafanyabiashara mbalimbali Mkoa wa Dodoma wakichangia mada wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia iliyoandaliwa na Tume ya ushindani kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.

Meneja wa Utekelezaji wa Sheria Kurugenzi ya Kudhibiti Bidhaa Bandia kutoka FCC, Hildagalda Kataraiya,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wafanyabiashara wakati wa semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Duniani yanayotarajia kufanyika Juni 25,mwaka huu jijini Dodoma.



Na Alex Sonna,Dodoma

TUME ya Ushindani (FCC) imeendesha semina maalum kwa wafanyabiashara mkoani Dodoma yenye lengo la kuwaelimisha kuhusu madhara ya bidhaa bandia na namna ya kuzitambua ili kulinda afya za wananchi na haki za watumiaji.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Salvator Chuwa, amesema kuwa wamefika mkoani hapa kushiriki tukio muhimu la Maadhimisho ya Siku ya Kudhibiti Bidhaa bandia, yakilenga kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu athari za bidhaa hizo kwa uchumi na maisha ya watu.

"Tumeamua kutumia jukwaa hili kuelimisha wafanyabiashara kuhusu wajibu wao katika kutambua na kuepuka bidhaa bandia. Bidhaa hizi sio tu kwamba zinadhoofisha ushindani wa haki bali pia zinahatarisha maisha ya walaji," amesema Chuwa.


Aidha Chuwa amebainisha kuwa bidhaa bandia zimekuwa changamoto kubwa nchini na zimechangia kuharibu sifa za bidhaa halali zinazozalishwa na wazalishaji wa ndani, jambo linalokatisha tamaa wawekezaji.


Kwa upande wake Meneja wa Utekelezaji wa Sheria Kurugenzi ya Kudhibiti Bidhaa Bandia kutoka FCC, Hildagalda Kataraiya,amesema kuwa moja ya majukumu yao makuu ni kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia sokoni zinazingatia viwango na ubora unaotakiwa kisheria.


"Tunaendelea kufanya doria na ukaguzi wa mara kwa mara katika masoko na maduka ili kuhakikisha hakuna bidhaa haramu au bandia zinazosambazwa. Tunawasisitiza wafanyabiashara kuwa sehemu ya suluhisho kwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka," amesema Kataraiya.


Tume ya Ushindani imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha soko la bidhaa nchini linakuwa na ushindani wa haki, huku akisisitiza ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wananchi ili kudhibiti tatizo hilo kwa ufanisi.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma Bw.Gilbert Chuwa,ameipongeza FCC kwa jitihada hizo na kuomba elimu hiyo iendelee kutolewa kwa maeneo mengine nchini, hasa vijijini ambako watumiaji wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusu bidhaa bandia.


Hata hivyo ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua kuwa jukumu la kupambana na bidhaa bandia ni la pamoja, na kwamba utoaji taarifa mapema kuhusu bidhaa zenye mashaka unaweza kusaidia kuokoa maisha na mali.

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...