Monday, May 19, 2025

Wananchi Njombe waomba wigo wa miradi ya kusambaza umeme uongezwe.

Na mwandishi wetu -Njombe

Wananchi wa vitongoji mbalimbali vya  Mkoa wa Njombe wameiomba Serikali kuongeza wigo wa miradi ya kusambaza umeme ili iweze kutekelezwa katika vitongoji vyote.

Wakizungumza katika  nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara inayoendelea wakati wa kampeni ya kutoa elimu na kuhamasisha umma kuunganisha umeme katika Mkoa wa Njombe, wananchi hao wameiomba Serikali kuongeza  wigo wa miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji ili iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi na taasisi nyingi zilizopo katika maeneo yao.

Mikutano hiyo imefanyika katika vijiji vya Ibatu, Usetule, Manga, Kifumbe, Mtulingala, Mbugani na Nyamande, ambapo wananchi wa vitongoji vya Magomati, Mjimwema, Kidete, Mtanga, Ilongo, Kisaula, Matangini, Mvengi B na Nyamande A, wameiomba Serikali kuongeza miradi ya kusambaza umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa.

Aloyce Ng'angalila mkazi wa Kitongoji cha Magomati Kijiji Cha Usetule amesema, "nyumba zilizopitiwa na nguzo za umeme ni chache na ambazo hazijapitiwa na mradi huo wa umeme ni nyingi, naomba REA itusaidie kupata Umeme katika maeneo yaliyobaki".

Wakiongea katika mkutano uliofanyika katika Kijiji Cha Mtulingala, Christina Mdendemi na Anet Mtenga wamesema kuwa hawajaunganishiwa umeme katika biashara na makazi yao hivyo  wanatumia nishati ya umeme jua ambayo haikidhi mahitaji yao na kusababisha wafunge biashara mapema. 

Hivyo wameiomba Serikali kuongeza nguzo katika maeneo yao ili waweze kuunganisha umeme.

Nae, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ibatu amesema kuwa nyumba zaidi ya 30 hazijafikiwa na nguzo za umeme ikiwemo Ofisi ya Kijiji, hivyo anaomba Serikali kupeleka umeme katika taasisi hiyo na maeneo mengine ambayo hayajafikiwa.

Akijibu hoja za wananchi hao,  Meneja wa REA Mkoa wa Njombe, Mha. Marlon Bulugu ameeleza kuwa Serikali imeandaa mpango wa kusambaza umeme katika vitongoji vyote kwa kipindi cha miaka mitano na kuwa utekelezaji wake unafanyika kwa awamu.

Aidha, aliwataka wananchi ambao majengo yao yapo katika wigo Mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji (HEP 2A), ambao utekelezaji umeanza kuandaa majengo yao kwa ajili ya kuunganishiwa umeme kwa kufanya wiring na pia kutumia umeme kuanzisha shughuli za uzalishaji mali.

Picha mbalimbali Wananchi wa Njombe wakipewa elimu 

Saturday, May 17, 2025

SERIKALI INAFIKIRIA KUJA NA MPANGO WA UUZAJI WA SARAFU ZA DHAHABU KWA WANANCHI

▪️Lengo ni kuwaongezea Watanzania wigo wa uwekaji akiba na uwekezaji kupitia dhahabu

▪️Waziri Mavunde azitaka Taasisi za Fedha kuwawezesha watanzania kimtaji

▪️Afungua Tawi jipya la STANBIC GEITA

▪️Wachimbaji wadogo kukopa fedha isiyozidi 115,000,000 bila dhamana

▪️STANBIC kuja na riba ndogo ya mikopo kwa wachimbaji nchini

Geita

Ikiwa ni hatua ya kuwaongezea watanzania wigo wa uwekaji akiba na uwekezaji kupitia ununuzi wa dhahabu, Serikali ipo mbioni kuanzisha uuzaji wa Sarafu ya dhahabu nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17 Mei, 2025 na Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb) akiwa Mkoani Geita aliposhiriki katika uzinduzi wa tawi la benki ya Stanbic Geita.

"Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dkt. Samia S. Hassan amefanya makubwa katika sekta yetu ya madini, na ndiyo maana tumeweza kuchangia katika pato la Taifa kufikia asilimia 10.1 kwa mwaka 2024, mwaka mmoja kabla ya mwaka 2025 kama ilivyokuwa imeelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi na Mpango wa Maendeleo wa miaka 5.

Wizara kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzanania(BOT) tunajadiliana namna bora  ya uanzishwaji wa Sarafu za dhahabu(𝙜𝙤𝙡𝙙 𝙘𝙤𝙞𝙣𝙨) ili kuongeza umiliki wa dhahabu miongoni mwa wananchi, kuimarisha soko la ndani la dhahabu na mzunguko wa fedha ndani ya nchi yetu.

Hatua hiyo ya uanzishwaji wa uuzaji wa Sarafu ya dhahabu ni sehemu ya maboresho ya mpango wa ununuzi wa dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania ili kufikia malengo tarajiwa ya kuwa na ununuzi wa dhahabu endelevu na wenye tija nchini.

Nawapongeza Benki ya STANBIC kwa kusogeza huduma  rafiki ya kibenki kwa wananchi wa Geita hususani wadau wa madini na hivyo kuzitaka Benki nyingine kuiangalia sekta ya madini kwa upekee ili kuwezesha mitaji kwa watanzania ili washiriki katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini, kwani sekta hiyo ina utofauti mkubwa na sekta nyingine za uzalishaji nchini" Alisema Mavunde

Awali, akitoa maelezo kuhusu uanzishwaji wa Tawi hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic, Bw. Fredrick Maxi aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara na kubainisha kuwa Benki ya Stanbic kwa sasa ina matawi 15 nchini na inaendelea kufungua matawi mengine mengi kwenye maeneo ya uchimbaji ili kuwafikia wadau wengi zaidi kwenye sekta ya madini,na pia Benki inakuja na mpango maalum wa kutoa riba ndogo isiyo ya kibiashara kwa sekta ya madini ili kuchochea shughuli za madini nchini ambapo kwa sasa wachimbaji wadogo wanaweza kuchukua mikopo isiyozidi Tsh 115,000,000 bila kuwa na dhamana.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Martin Shigela aliishukuru benki ya Stanbic kwa kuleta Tawi Mkoani Geita na kusisitiza kwamba, ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwezesha sekta za uzalishaji zinazochochea ukuaji wa biashara na kuzifanya benki za biashara kuchangamkia fursa zinazoendelea kuibuka mkoani hapo na kuwataka wananchi wa Geita kuchangamkia huduma zitolewazo na taasisi hizo za fedha katika kujiimarisha kimtaji.   

ZAMECO YAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA HABARI DUNIANI

Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) imeadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani leo Mei 17, katika ukumbi wa RAHALEO STUDIO ambapo waandishi, wadau wa habari pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali zilishiriki.

Maadhimisho hayo yana lengo la kukuza na kuimarisha kada ya habari nchini na kusisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na Sheria mpya na rafiki yenye kusimamia mazingira salama kwa waandishi wa habari hasa kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Msemaji mkuu wa shughuli ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Wataalamu wa masuala ya Habari (ZAMECO) ndugu Salim Said Salim amesema ni jambo la kusikitisha na kutia unyonge kuona kuwa imechukua muda mrefu kupatikana kwa sheria bora ya habari ambapo sheria nyengine zinachukuwa muda mchache kufanyiwa marekebisho.

"Tunashuhudia sheria nyingi zikipitishwa katika Baraza la Wawakilishi, ila sheria ya habari imechukua zaidi ya miaka 20 hali inayoifanya tasnia habari kuwa kama watoto yatima ambao hatuna msaada kwa baba wala kwa mama'' ameelezea mwandishi huyo mkongwe, Salim Said.

Aidha ameziomba mamlaka husika kuhakikisha wanasimamia ukweli wakati wanapoahidi upatikanaji wa sheria ya habari kwani kufanya hivyo ni kuwavua waandishi wa habari katika janga zito la ufanyaji wa kazi za kuhabarisha umma kwa kutoa taarifa zilizo sahihi katika mazingira salama.

Akizungumza kwa niaba ya katibu mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mratibu wa (MCT, Zanzibar) Ziada Ahmed Kilobo amesema usalama wa wandishi wa habari ni suala la muhimu hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ambapo Serikali inajukumu la kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi ya kuhabarisha jamii kwa ufasaha na bila ya vitisho.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar ndugu Salum Ramadhan amesema changamoto ya habari ipo njiani kutatuliwa ili kuwawekea waandishi wa habari mazingira mazuri ya kazi, sambamba na sera ya habari ambayo itazinduliwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) Dkt Mzuri Issa amesema pamoja na waandishi kuwa na wajibu wa kuandika habari kwa weledi na kuzingatia maadili lakini nao wanayo haki ya kupata sheria ya habari inayotetea maslahi yao.

"Sote ni wataalamu na tunafanya kazi kwa kuzingatia hilo lakini lazima tupatiwe haki yetu ya kuwa na sheria nzuri ya habari, kufuatilia michakato ya sheria, kupewa ulinzi pamoja na kutopewa vitisho na kufanya kazi kwa usawa na ukweli.

Siku ya Uhuru wa Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 3 Mei ambapo kwa upande wa Zanzibar kauli mbiu inasema "Sheria nzuri ya Habari ni chachu ya uchaguzi ulio huru na wa haki".

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Utetezi
TAMWA ZNZ

Friday, May 16, 2025

MAELFU WAJITOKEZA MKUTANO WA HADHARA CHADEMA SHINYANGA MJINI, "NO REFORM, NO ELECTION" YAPAMBA MOTO

Na mwandishi wetu - Malunde 1 Blog.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) taifa John Mnyika katika ziara yake mkoani Shinyanga ameendeleza msimamo wa 'No reforms, No election' akiwataka wanashinyanga kulinda haki na utamaduni wa Chadema.

Amebainisha hayo leo Mei 16, 2025 katika mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika katika uwanja wa Jasko uliopo katika kata ya Ngokolo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, mkoani Shinyanga.

Mnyika amesema wako tayari kushiriki uchaguzi hata kesho endapo yatafanyika mabadiliko ya Katiba sambamba na tume huru ya uchaguzi.

Picha : MAHAFALI YA 44 YA WANACHUO WA HATUA YA TATU 2025 YAFANYIKA VETA SHINYANGA, KITINGA ATAKA WACHANGAMKIE MIKOPO ‘FEDHA ZIPO’

Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga yamefanyika leo ambapo jumla ya wahitimu 147, wanaume 82 na wanawake 65 ,wamehitimu Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Tatu (III) katika fani mbalimbali za Umeme (Electrical Installation), Bomba (Plumbing and Pipe Fitting), Ujenzi (Masonry and Bricklaying), Uhazili na TEHAMA (Secretarial and Computer Application) na Ufundi wa Mitambo Mikubwa (Heavy Duty Equipment Mechanics).

Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Ijumaa Mei 16,2025 alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.

Akizungumza, Kitinga amewataka wahitimu hao kujisajili katika vikundi ili kunufaika na mikopo ya halmashauri, akisisitiza kuwa fedha zipo kwa ajili yao.

"Wanafunzi wanaosoma chuo wapewe mafunzo ya namna ya kusajili vikundi na waunde vikundi ili kupata fedha za mikopo inayotolewa katika halmashauri. Pesa ipo Halmashauri! Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi, kazi ni kwenu kujiunga kwenye vikundi," amesema Kitinga.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga.

Aidha, amewataka wazazi na walezi kuendelea kupeleka watoto wao VETA ili wapate ujuzi, akibainisha kuwa hakuna kozi za wanaume au wanawake pekee, kwani fursa zinatolewa kwa usawa kwa wote.

Kitinga amewahimiza wahitimu na vijana kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani, huku akiwataka kuwakataa wale wanaohubiri siasa za chuki na mgawanyiko.

"Nchi hii ni tulivu chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tuilinde amani yetu, tusikubali kugawanywa kwa misingi ya kisiasa," amesisitiza.

VETA Yazidi Kuandaa Nguvu Kazi Yenye Ujuzi

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Mwl. Abraham Richard Mbughuni, amesema kuwa chuo hicho kimeendelea kutekeleza dira, dhima na malengo ya mamlaka hiyo kila mwaka. 

Tangu kuanzishwa kwake, chuo kimeweza kudahili na kutoa wahitimu wengi wa kozi za muda mrefu, ambao wamejiajiri, wameajiri wenzao au wameajiriwa kwenye taasisi mbalimbali za umma na binafsi.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Mwl. Abraham Richard Mbughuni.

"Kufuatia maagizo ya serikali, VETA Shinyanga kimefanikiwa kusajili mafundi wapatao 1,553 waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi katika mkoa wa Shinyanga. Lengo ni kuwatambua rasmi, kuwafanyia tathmini na kuwapatia vyeti," amesema Mwl. Mbughuni.

Aidha, ametumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha VETA, akisema taasisi hiyo ni msingi wa mageuzi ya uchumi kupitia ujuzi.

Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye, akisoma taarifa kuhusu mafunzo katika chuo hicho, amesema kwa sasa chuo kina jumla ya wanafunzi 575 wa kozi ndefu—wavulana 378 na wasichana 197. Kwa upande wa kozi fupi, wanafunzi waliodahiliwa kuanzia Januari 2024 hadi leo ni 887.

Akitaja mafanikio, amesema kuwa wahitimu wengi wamefanikiwa kupata ajira au kuanzisha biashara binafsi.

Hata hivyo, changamoto kadhaa zinaendelea kukikabili chuo, zikiwemo: Ukosefu wa kituo maalum cha afya kwa ajili ya wanachuo, Uchakavu u wa vifaa vya TEHAMA (kompyuta na mitambo), Uharibifu wa uzio wa chuo na ukosefu wa usafiri wa uhakika kwa jumuia ya chuo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga yaliyofanyika leo Mei 16,2025- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Mwl. Abraham Richard Mbughuni akizungumza kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Mwl. Abraham Richard Mbughuni akizungumza kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye, akisoma taarifa kuhusu mafunzo katika chuo hicho kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Msajili wa VETA Shinyanga, Rashid Hamis Ntahigiye, akisoma taarifa kuhusu mafunzo katika chuo hicho kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Wahitimu wakisoma risala kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Wahitihimu wakiingia ukumbini kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Wahitihimu wakicheza wakati wa Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Kambi ya Nyani wakitoa burudani kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

MC Manyama akizungumza kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Sehemu ya wahitimu wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga

Sehemu ya wazazi na wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Sehemu ya wahitimu wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Wafanyakazi wa VETA wakifuatilia matukio kwenye Mahafali ya 44 ya Wanachuo wa Hatua ya Tatu katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Shinyanga
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiendelea na zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya Ukataji Madini Vito katika Chuo cha VETA Shinyanga.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya ubunifu, ushonaji na teknolojia ya nguo
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya ubunifu, ushonaji na teknolojia ya nguo
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya umeme
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika Karakana ya umeme
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika moja ya majengo yaliyojengwa na wanachuo cha VETA Shinyanga
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akiwa katika chumba kinachotoa Fani ya saluni
na urembo

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...