Sunday, March 16, 2025

Mzee Atapeliwa Akitaka Utajiri Kwa Mganga, Aachwa Makaburini Akiwa Uchi




Mzee Mussa Rashid ambaye ni Mkazi wa Tabora, ametapeliwa pesa Tsh. laki mbili, simu, kadi ya CCM na kadi ya NIDA, suti yake ya gharama kubwa na saa yake yenye thamani ya Tsh. milioni moja baada ya kusafiri hadi Sumbawanga Mkoani Rukwa akiufuata utajiri wa haraka kwa Mganga wa kienyeji ambaye ameishia kumtapeli na kumkimbia.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana March 14,2025, ambapo Mzee huyo (anayeonekana kwenye picha) aliwasili Sumbawanga March 13,2025 saa 4 usiku na kukutana na Mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea kisha baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa akiwa uchi wa mnyama kabla ya kutapeliwa na akatelekezwa hapo akiwa utupu hadi Wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.

Mzee huyo amesema "Nilipokutana na Mganga akaniambia chukua maji ya Tsh.500 nikachukua madogo mawili, tukaenda hadi makaburini, akaniambia chukua madongo ardhini tumefika akapaka lile kaburi yale madongo, akaniambia lala juu ya kaburi wakati huo nimeshavua nguo zote, akanimwagia dawa zake, akaniambia nenda pale ulipochukua mchanga na madongo nenda kaombe unachotaka pale, nikaenda kurudi sijamkuta, laki mbili imechukuliwa, simu imechukuliwa, saa ya gharama ya milioni moja imechukuliwa, kadi ya CCM na kadi ya NIDA vyote vimechukuliwa, suti yangu imechukuliwa"

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina huku akihimiza Wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea Waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu na kuwataka Watu waache kujidanganya kuwa Sumbawanga kuna utajiri… Polisi tayari wameanza kumtafuta Mganga huyo feki.

Source: Millard Ayo

Kamati yaridhishwa na Ujenzi wa Jengo la Jeshi la Zimamoto Manyara


Na John Walter -Babati 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) imefanya ziara mkoani Manyara kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Katika ziara hiyo, kamati ilitembelea na kukagua ujenzi wa jengo la ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, ambalo linaendelea kujengwa katika Kata ya Maisaka, eneo la Katani.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ameieleza kamati kuwa pato la mkoa huo, ambao unajikita katika sekta za kilimo, ufugaji na utalii, limeendelea kuimarika. 

Pia amebainisha kuwa hali ya ulinzi na usalama mkoani humo imeendelea kuimarika, huku changamoto kubwa ikiwa ni msongamano wa mahabusu kwenye magereza.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Paul Mbogo, amesema kamati imepokea changamoto zilizowasilishwa na kwamba zitafanyiwa kazi katika bajeti ijayo ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi.

Jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Manyara litakuwa na sakafu mbili na litajumuisha ofisi saba, zikiwemo ofisi za Kamanda wa Mkoa, Kamanda wa Wilaya, Mhasibu na Masijala. 

Pia, litakuwa na magari matatu yenye mitambo ya kisasa ya kuzima moto ili kuhakikisha huduma za uokoaji zinaboreshwa katika mkoa huo.

Kwa mujibu wa taarifa, gharama za ujenzi wa jengo hilo hadi kukamilika kwake ni shilingi milioni 600.6, na hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 48.2.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, amepongeza hatua ya ujenzi ilipofikia na kusisitiza kuwa kukamilika kwake kutarahisisha shughuli za uokoaji wakati wa majanga, hivyo kuokoa maisha na mali za wananchi.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga (CDF), amesema jengo hilo litakuwa na mifumo ya kisasa ya TEHAMA, na linatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2025.

Aidha, Masunga alibainisha kuwa kituo hicho ni sehemu ya miradi saba ya ujenzi wa vituo vikubwa vya zimamoto vinavyojengwa katika mikoa ambayo awali haikuwa na vituo vikubwa vya huduma hiyo. 

Ameeleza kuwa lengo ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuhakikisha kila mkoa unakuwa na kituo cha kisasa cha zimamoto na uokoaji.

Jeshi hilo kwa sasa lipo kwenye wilaya 25 na linaendelea na mpango wa kupanua huduma ili kuzifikia wilaya zote nchini. 

Mpango huo unakwenda sambamba na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya zimamoto na uokoaji ili kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo.

Kamati hiyo imeishukuru Serikali kwa kutenga fedha za umaliziaji wa vituo hivyo na imewataka makamanda wa mikoa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Saturday, March 15, 2025

Kijiji cha Sangaiwe Chaongoza Kitaifa kwa Ukusanyaji wa Mapato ya Utalii


Na John Walter -Babati 

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, amepongeza juhudi za Kijiji cha Sangaiwe katika uhifadhi wa mazingira, hatua iliyowafanya kuwa vinara wa kitaifa kwa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na utalii. 

Kaganda amesema kijiji hicho ni mfano wa kuigwa katika Mkoa wa Manyara na Tanzania kwa ujumla kwa mafanikio yake makubwa ya maendeleo.

Kijiji cha Sangaiwe, kilichopo katika Kata ya Mwada, kimepata mafanikio makubwa kutokana na uhifadhi wa wanyamapori. 

Kupitia mapato ya utalii, kijiji kimefanikiwa kuboresha miundombinu na kuinua hali ya maisha ya wakazi wake.

Kwa kutumia mapato hayo Kijiji kimejenga ofisi ya kisasa kwa shughuli za utawala, hatua iliyorahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi, Kila kitongoji sasa kina shule ya msingi, huku shule hizo zikiboreshwa kwa madarasa mazuri na walimu wanaolipwa vizuri kwa juhudi za kijiji.

Matokeo mazuri yameonekana kwenye sekta ya elimu, ambapo shule za msingi za kijiji zilishika nafasi ya kwanza na ya nne katika mtihani wa darasa la saba na la nne kwa ngazi ya mkoa mwaka 2024.

Kijiji kinapokea wageni 70-80 kwa siku, huku majirani zao wa Tarangire wakipokea zaidi ya 1,000 kwa siku.

Zahanati ya kisasa imejengwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 200, ikiwa na vifaa tiba na dawa, hatua iliyosifiwa na Mkuu wa Wilaya, Emmanuela Kaganda, kama hatua muhimu kwa afya za wananchi.

Kwa miaka mingi, wakazi wa Sangaiwe walikumbwa na changamoto ya tembo kuharibu mazao yao. 

Hili liliwasukuma kugeuza tatizo hilo kuwa fursa kwa kuingia makubaliano na wawekezaji wa sekta ya malazi ya wageni.

Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge (JUHIBU), Patricia Mosea, amesema kijiji kimeanzisha hifadhi za jamii zinazojumuisha vijiji 10 ili kunufaika na uwepo wa tembo badala ya kuwa wahanga wa uharibifu wa mazao.

Wakazi wa Sangaiwe wameonesha uvumilivu wa hali ya juu kwani, licha ya tembo kupita kwenye makazi yao kila siku, wamejifunza kuishi nao bila bughudha huku wakiruhusu wawekezaji kujenga hoteli kwa wageni wanaotembelea kijiji na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Kwa kipindi cha miaka miwili, Shilingi Bilioni 2.4 zimeelekezwa kwenye huduma za jamii kupitia mapato ya utalii.

Hata hivyo, kuna malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu sheria mpya ya mgao wa mapato. 

Awali, vijiji vilikuwa vinapata asilimia 60 ya mapato kutoka kwa wawekezaji, lakini sheria mpya inataka wapewe asilimia 20 pekee.

Diwani wa Kata ya Mwada, Michael Mombo, pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Sangaiwe, Mariani Mwanso, wamesema mabadiliko haya yanawavunja moyo wananchi na wanaomba serikali iendelee na mgao wa asilimia 60 ili maendeleo ya kijiji yaendelee kwa kasi.

Ujenzi wa shule, zahanati, na ofisi ya kijiji ni ushahidi wa jinsi uhifadhi unavyoweza kuinua maisha ya jamii. 

Licha ya changamoto ya tembo na mjadala wa mgao wa mapato, wananchi wa Sangaiwe wanaendelea kufanikisha maendeleo yao kwa kauli mbiu ya Kata ya Mwada "Maendeleo Kwanza, Mambo Mengine Baadaye."  "Tembo kwa Maendeleo."


Huu Hapa Msimamo wa Ligi Kuu Bara Baada ya Ushindi wa Simba Leo...


Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika alasiri ya leo kati ya Simba SC na Dodoma Jiji FC, Simba imeibuka na ushindi mkubwa wa mabao 6-0.



Ushindi huu umeleta mabadiliko makubwa kwenye msimamo wa ligi, huku Simba ikikaribia kuifikia Yanga SC ambayo bado inashikilia nafasi ya kwanza.

Kabla ya mchezo huu, Simba ilikuwa na pointi 54, huku Yanga ikiwa kileleni na pointi 58. Kwa ushindi huu, Simba imeongeza pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi 57, ikisalia nyuma ya Yanga kwa tofauti ya pointi moja pekee.

Mabadiliko haya yanaashiria ushindani mkali kati ya timu hizi mbili, ambazo zinawania ubingwa wa ligi msimu huu.

Kwa upande wa Dodoma Jiji, kipigo hiki kinawaweka katika nafasi ngumu zaidi, kwani wanazidi kupoteza alama muhimu katika mbio za kusalia kwenye ligi.

Timu hiyo italazimika kujipanga upya ili kuhakikisha inapata matokeo mazuri katika mechi zake zijazo.

Kwa mafanikio haya ya Simba, presha inaongezeka kwa Yanga kuhakikisha wanashinda michezo yao ijayo ili kusalia kileleni. Mashabiki wa soka Tanzania wanatarajia kuona ushindani mkali zaidi kadri msimu unavyoendelea.

Friday, March 14, 2025

Nchi Kumi Ambazo ni Vigumu kwa Mwanaume Kupata Mwanamke wa Kumuoa


Nchi Kumi Ambazo ni Vigumu kwa Mwanaume Kupata Mwanamke wa Kumuoa


Japokuwa inafahamika kwamba, katika jumla ya idadi ya watu bilioni 7. 5 waliopo dunia leo hii, idadi ya wanaume na wanawake inapishana kwa kiasi kidogo, zipo baadhi ya nchi ambazo wanaume ni wengi kuliko wanawake, kiasi kwamba inakuwa kazi ngumu kwelikweli kumpata mwanamke wa kuoa.

SWEDEN
Nchini Sweden, inaelezwa kwamba idadi ya wanaume, inazidi kwa 12,000 zaidi ya idadi ya wanawake waliopo na kundi kubwa ni la vijana. Idadi hii inatarajiwa kuongezeka zaidi kwa hiyo, wanaume wengi wanajikuta katika wakati mgumu wa kupata wachumba wa kuingia nao kwenye ndoa.

Sababu nyingine inatajwa kwamba ni ongezeko la wahamiaji kutoka kwenye nchi zenye vita ambao wanapata hifadhi kwenye nchi hiyo na baadaye kupewa uraia. Ongezeko la wahamiaji, limesababisha wananchi wengi wa Sweden wasiotaka shida, kuhamia kwenye nchi nyingine zisizo na idadi kubwa ya wahamiaji na wengi wanaoondoka, ni wasichana.

AFGHANISTAN
Kabla ya nchi ya Afghanstan kukumbwa na vita, ilikuwa ikisifika kwa kuwa na wanawake wengi warembo waliokuwa wakionekana kwa wingi mitaani, hasa katika Jiji la Kabul.


Hata hivyo, tangu machafuko yaikumbe nchi hiyo, idadi ya wanawake imepungua sana, sababu kubwa ni kwamba wanawake wengi na watoto wameikimbia nchi kutokana na vita na kwenda kutafuta hifadhi katika nchi zenye usalama. Waliobaki ni wanaume wanaoendelea kupambana na machafuko ya mara kwa mara yanayoibuka na kupotea, matokeo yake imekuwa vigumu sana kupata mke wa kuoa.

NIGERIA
Nchini Nigeria, uwiano kati ya wanawake na wanaume, haupo sawa. Wanaume ni wengi kuliko wanawake na sababu kubwa, inatajwa kwamba wanawake wa Kinigeria, wamekuwa wakiikimbia nchi yao na kwenda kutafuta hifadhi kwenye mataifa mengine kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo kukimbia ndoa za utotoni, tohara za wanawake na hali ngumu ya kimaisha.

Hivi karibuni, serikali ya nchi hiyo ilieleza kuhusu tatizo la vijana wengi waliofikia umri wa kuoa, kukosa wanawake wa kuwaoa.

UGIRIKI
Kwa kipindi kirefu, nchi ya Ugiriki ilikuwa ikitumika kama kituo cha watu wanaotoka Ulaya, hasa katika nchi za Uingereza na Ufaransa kwenda kwenye mabara mengine. Kutokanana uzuri wa hali ya hewa ya Ugiriki pamoja na mandhari yake, wasafiri wengi wakawa wanavutiwa kuendelea kukaa kwenye nchi hiyo na baadaye, idadi ya wahamiaji kutoka kwenye mataifa makubwa ya Ulaya iliongezeka na wengi kati yao, walikuwa ni wanaume.

Hali imeendelea hivyo kwa miaka mingi na kusababisha idadi ya wanawake kutotosheleza idadi ya wanaume wanaozidi kuongezeka kila kukicha. Hivi sasa ni vigumu sana kupata mke wa kuoa nchini Ugiriki.

MISRI
Misri ni moja ya nchi yenye idadi kubwa ya watu  kwenye nchi za Kiarabu na barani Afrika. Kama zilivyo nchi nyingine za Kiarabu, wanawake wanatakiwa kufanya shughuli za nyumbani tu na kutoonekana hovyo mitaani.

Wengi wameitumia fursa hii kujiendelea kielimu wakiwa majumbani na wanawake wengi wa Misri, ni wasomi wenye digrii kadhaa, walizozipata kwa kujiendeleza wakiwa majumbani mwao na baadaye kwenda vyuo vikuu.


Hali hiyo imesababisha wanawake wengi wasomi, kuanza kutafuta ajira nje ya nchi, ambako wanawake wana uhuru zaidi na tayari wengi wameondoka na kwenda kufanya kazi mbalimbali kulingana na elimu zao, hali iliyosababisha wanaume wengi wapate kazi kwelikweli wanaposaka wanawake wa kuwaoa.

CHINA
China ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko wote duniani, lakini katika idadi ya watu wote nchini humo, wanaume wanawazidi wanawake kwa idadi ya watu milioni 40. Tofauti hii kubwa kati ya idadi ya wanawake na wanaume, imesababishwa na Wachina kuwa na kawaida ya kuchagua watoto, na mwanamke anapokuwa na ujauzito wa mtoto wa kike, hulazimishwa kutoa ujauzito huo kwani Wachina wengi wanaamini kwamba mtoto wa kiume ndiyo mwenye thamani katika jamii.

Hali hiyo imesababisha uhaba mkubwa wa wanawake mitaani, kiasi cha serikali kuingilia kati na sasa, vijana wa kiume kutoka China wanaruhusiwa kwenda kutafuta wanawake nchini Urusi, ambako kuna uhaba wa wanaume.

MAREKANI
Yawezekana ukashangazwa na kusikia kwamba nchini Marekani nako kuna uhaba mkubwa wa wanawake. Ukweli ni kwamba, katika baadhi ya majimbo, idadi ya wanawake ni ndogo kuliko wanaume.

Kwa mfano, katika majiji ya Los Angeles na Las Vegas, idadi ya wanawake ni ndogo kuliko wanaume kwa wastani wa wanaume 157 kwa wanawake 151, hali inayofanya iwe vigumu kupata wasichana wazuri wa kuoa.

INDIA
India ni miongoni mwa nchi zenye watu wengi zaidi duniani na inatarajiwa kwamba ifikapo 2024, itaizidi China. Licha ya idadi hiyo kubwa ya watu, India ina uhaba mkubwa wa wanawake kutokana na mila potofu ya nchi hiyo kwamba watoto wa kiume wana umuhimu sana kuliko wa kike wakiamini kwamba wana msaada mkubwa sana katika familia pale wanapofikia umri wa kujitegemea.

Wanaume wanawazidi wanawake kwa idadi ya watu milioni 37, hali inayofanya iwe vigumu sana kupata mke wa kuoa.

FALME ZA KIARABU
Katika kipindi cha karne ya 20 falme za kiarabu zilikuwa na idadi ya watu 40,000 tu, Kati ya hao wanawake wakiwa ni 22,000.Hata hivyo ugunduzi wa  mafuta umesababisha nchi hiyo ibadilike haraka na wahamiaji wengi kutoka nchi mbalimbali,wengi wakiwa ni wanaume ambao wamejazana nchini humo,kutafuta maisha.

Hali hiyo imesababisha kuwe na uhaba mkubwa wa wanawake jambo linalowapa shida wanaume wanapofikia umri wa kuoa.


QATAR
Nchi ya Qatar ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa wa mafuta lakini kijiografia ina eneo dogo na wananchi wazawa wachache. Hata hivyo kutokana na utajiri wa mafuta imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo, hali ambayo imesababisha wahamiaji wengi kukimbilia na kutafuta maisha.

Matokeo yake wanaume wamekuwa wengi kwa wastani wa 3:1, katika kila watu wa 4 wa 3 ni wanaume na mmoja ni mwanamke na kuifanya kuwa nchi yenye wanawake wachache zaidi duniani.

JKT yatoa onyo kali kwa wanaoghushi Vyeti vya Uhitimu wa Mafunzo ya JKT

 



Jeshi la Kujenga Taifa JKT limewaonya vijana au watu wanaojihusisha na utengenezaji wa vyeti feki vya uhitimu wa mafunzo yanayotolewa na JKT ili kuweza kupata nafasi kwenye kampuni na taasisi zinazohitaji vijana waliopitia mafunzo hayo

Hayo yamebainishwa leo Marchi 13, 2025 wilayani Chamwino Mkoani Dodoma na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Kanali Juma Mrai wakati akitoa taarifa ya uwepo wa vyeti vya kughushi vya vijana waliohitimu mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na wale wa kujitolea.

Amesema JKT imeamua kutoa onyo hilo baada ya kubaini uwepo wa baadhi ya vijana wanatumia vyeti feki kwenda kuomba kazi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kwenye taasisi na kampuni mbalimbali kitu ambacho ni kinyume na sheria.

"JKT tuko tayari kutoa ushirikiano kwa kampuni au taasisi yoyote inayotaka kufanya uhakiki wa watu waliotumia vyeti vya JKT kama moja ya kigezo cha kupata ajira, katika taasisi na kampuni hizo,"amesema Kanali Juma Mrai.

Amesema JKT wameanza msako mkali kuwabaini wanaojihusisha na vitendo hivyo na akisisitiza kuwa watakaowabaini watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa wanaamini kuna stationari zinazojihusisha na vitendo hivyo na kuzitaka kuacha mara moja.

Kanali Mrai amesema JKT inatoa nafasi kwa vijana kujiunga na mafunzo hayo kila mwaka kwa vijana wa kitanzania wenye sifa ili wamalizapo mafunzo ya JKT waweze kupata cheti cha kihitimu mafunzo ya JKT kihalali.

Katika hatua nyingine amewatahadhalisha wananchi kutotapeliwa kupitia jumbe mbalimbali zinazotumwa kwenye simu za mkononi za kuombwa pesa ili wapatiwe nafasi za kujiunga na jeshi hilo na kuongeza kuwa nafasi za mafunzo hayo zitatolewa kwa njia ya mtandao na vyombo vya Habari pekee.

 

Thursday, March 13, 2025

UVCCM KAGERA YAIPA TANO KAULI MBIU MPYA YA CCM "KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE"

 

Na Lydia Lugakila - Kagera

KAMATI ya utekelezaji umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Kagera kupitia kwa Wenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani amekishukuru kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuja na kauli mbiu ya Kazi na Utu Tunasonga Mbele kwa mwaka 2025-2030.

Faris ametoa pongezi hizo katika kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya ya Kyerwa mkoani kagera katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo ikiwa ni ziara ya siku 16 kutoa elimu ya uraia juu ya kupiga kura kutafuta wapiga kura wapya vijana.

Amewapongeza wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa walioketi Machi 10 mwaka huu kwa kupitisha kauli mbiu mpya ambayo itatumika 2025 -2030 ikiwa ni kauli mbiu mpya ambayo italeta maendeleo makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujmla hivyo vijana wanapaswa kuiishi na kuiweka katika mioyo yao.

Kupitia vikao mikutano mkusanyiko wa kampeni ya siku 16 mkoani Kagera elimu ya uraia kwa vijana wa CCM inaendelea kutolewa  kuhakikisha wanashiriki uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika mwaka huu.

"Tunatoa elimu ya uraia kwa vijana hatubagui vijana wa rika zote ambao wamefikisha umri wa kujiandikisha kuhakisha wanajiandikisha na kupiga kura mwaka huu kwa sababu utamaduni wa vijana wengi hawapigi kura wanaongelea vijiweni ,tunaamini hii kampeini italeta mabadiliko makubwa kwa vijana sambamba na kuwaasa vijana kuchukua fomu za kugombea udiwani na ubunge ili waweze kutimiza ndoto zao," amesema.

Saturday, March 8, 2025

Eddo Kumwembe 'Mechi Inahairishwa Kwa Sababu za Kibwegebwege Sana'




Mchambuzi ngulinwa Michezo nchini Tanzania Eddo Kumwembe kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ✍🏿

"Tunawadharau sana wateja wetu.....mashabiki. Huwa wanatoka mbali sana. Wengine wengi wanatoka mikoani wanajichanga sana kuja katika hizi game. Football is about passion na soka letu linabebwa na passion zao. Kwanini tunawaacha Wakenya katika mpira kwa sasa ni kwa sasa ni kwa sababu ya passion za hawa jamaa....halafu game inaahirishwa kwa sababu za kibwegebwege tu. Imagine coaster inageuka inarudi Kahama bila fans kutazama mechi.....kisa? Kutunishiana misuli.
That's why we love ENGLISH PREMIER LEAGUE".

Source

Bodi ya Ligi Yahairisha Michezo wa Yanga na Simba....


Kamati ya Usimamizi na Uendesha ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza rasmi kuahirisha mchezo wa Ligi Kuu namba 184 kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC uliyopangwa kuchezwa leo saa 1:15 usiku.

Bodi imefanya maamuzi hayo baada ya kupokea taarifa ya awali ya Ofisa Usalama wa Mchezo ambayo imeanisha matukio kadhaa yaliyopekea Simba SC kushtaki kwa TFF na Bodi ya Ligi kutokana na kushindwa kufanya mazoezi.

Bodi ya Ligi imesema mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusiana na sababu zilizosababisha mchezo huo kutochezwa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...