Thursday, February 20, 2025

Klabu ya Simba imepangiwa kukutana na Al Masry Robo Fainali CAF Shirikisho

Klabu ya Simba imepangiwa kukutana na Al Masry Robo Fainali CAF Shirikisho


Klabu ya Simba imepangiwa kukutana na 🇾🇪Al Masry kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho Barani Afrika.

Mshindi kwenye mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Stellenbosch na Zamalek kwenye hatua ya nusu fainali.

Je, Mnyama atatoboa _____?

Mbunge Sillo ampongeza Samia kwa miradi ya Maendeleo



Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Daniel Sillo, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuleta miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Mhe. Sillo ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake katika Kata ya Mamire, ambako alisikiliza kero za wananchi na kueleza kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kuboresha huduma za kijamii na miundombinu.

Katika ziara hiyo, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mamire na kuahidi kuwa serikali itaendelea kukiboresha zaidi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya. 

Pia, ametembelea ujenzi wa ofisi ya Umoja wa Wanawake wa kata hiyo na kuahidi kutoa mifuko 20 ya saruji kusaidia kukamilisha mradi huo.

Mhe. Sillo ameeleza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 3 zimeshatolewa kwa miradi mbalimbali katika kata hiyo, ambapo kati ya hizo, bilioni 3 zimetengwa kwa ujenzi wa geti la kuingilia hifadhi ya Taifa ya Tarangire, jambo linalolenga kuboresha huduma kwa wananchi wa eneo hilo.

Mpaka sasa, Mhe. Sillo amefanya ziara katika kata zote 25 za jimbo hilo na vijiji 102, akisikiliza wananchi na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa ipasavyo kwa manufaa ya jamii.

WAJUMBE JUMUIYA YA WAZAZI SHINYANGA MJINI WAPONGEZA UJENZI WA MADARAJA CHIBE - OLD SHINYANGA, IBINZAMATA MAKABURINI

  • Mrindoko Asisitiza Rais Samia Ametekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa Vitendo
  • Jumbe Asema Wana Kila Sababu ya Kutamba na Rais Samia
  • ***
    Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wameeleza kuridhishwa na ujenzi wa miradi ya madaraja katika kata za Chibe na Ibinzamata, wakisema kuwa miradi hiyo ni kielelezo tosha cha namna fedha zinazotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zinavyosaidia kuboresha miundombinu ya barabara.

    Wakiwa katika kata za Chibe na Ibinzamata leo Februari 20,2020 ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutembelea kata zote za Jimbo la Shinyanga Mjini, Wajumbe hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko, wamesema uboreshaji wa miundombinu ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

    Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old Shinyanga

    "Tumeliona daraja linalounganisha Chibe na Old Shinyanga, ni zuri, limejengwa na mhandisi mahiri, linaunganisha kata ya Chibe na Old Shinyanga na maeneo mengine kama Mwawaza hadi. Daraja hili ni zuri na tunaenda kuifanyia kazi ombi la diwani kuwekewa taa kwenye daraja hili ili kuimarisha usalama kwa wanaopita nyakati za usiku," amesema Mrindoko.

    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini

    "Tumejionea pia ujenzi unaoendelea wa daraja la Ibinzamata Makaburini. Daraja hili linajengwa vizuri. Tunawapongeza viongozi wote mliofanikisha kujengwa kwa daraja hili ili kurahisisha usafiri, lakini pindi tatizo la msiba linapotokea, wananchi waweze kupita kwa urahisi kwenda kuwahifadhi ndugu zetu waliotangulia mbele za haki. Ujenzi unaendelea vizuri na lipo katika hatua za ukamilishaji," ameeleza Mrindoko.

    Mrindoko ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya barabara, elimu, maji, afya n.k.

    Fue Mrindoko 

    Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe, amesema ujenzi wa daraja kubwa la Chibe ni sehemu ya kazi nzuri zinazofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha miundombinu ya barabara inakuwa mizuri ili kuwezesha kukua kwa uchumi.

    "Daraja la Chibe ni kubwa na zuri. Haya ni mambo mazuri yanayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan. Mama Samia ametekeleza Ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 100. Ameonesha maendeleo ya kiuchumi kwa vitendo, nasi hatuna zawadi ya kumpa zaidi ya kumpatia kura za kutosha kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2025 kwa sababu tayari Chama kimempitisha kuwa mgombea Urais kupitia CCM pamoja na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi ili waweze kutuletea maendeleo zaidi," amesema Jumbe.

     Mhandisi James Jumbe 

    "Tunazo sababu nyingi za kutamba na Mama Samia, tunazo sababu lukuki za kumuunga mkono Rais Samia kwa mambo makubwa na mazito aliyoyafanya katika taifa hili. Amefanya mabadiliko makubwa katika Mahusiano ya Kimataifa, ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, umeme na kuimarisha Demokrasia katika nchi ambapo hata vyama vya upinzani vinafanya mikutano yake kwa amani," ameongeza Jumbe.

    Jumbe ametumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwakaribisha waliopo katika vyama vya upinzani na wasio na chama kujiunga CCM kwani ni chama imara chenye ni ya dhatiya kuwaletea maendeleo wananchi.

    "Mwaka 2020 Shinyanga tulikuwa wa pili katika kukipigia kura kwa Kishindo Chama Cha Mapinduzi, mwaka huu 2025 tunataka tushike nafasi ya kwanza. Nafasi ya Urais tayari tuna mgombea Mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, nafasi za Udiwani na Ubunge wagombea watapatikana kwa mujibu wa taratibu za Chama," ameongeza Jumbe.

    Diwani wa kata ya Chibe, Mhe. John Kisandu, amesema ujenzi wa daraja la Chibe – Old Shinyanga lenye urefu wa mita 45 lililopo katika Mto Mkubwa, linalojumuisha barabara, kalvati na daraja likigharimu jumla ya shilingi Milioni 475, umekamilika na lipo katika matazamio huku akiomba taa ziwekwe katika eneo hilo ili kuimarisha usalama wapitaji kwani linatumiwa na watu kutoka maeneo mengi, ikiwemo kutoka Mkoani Tabora.

    Diwani wa kata ya Chibe, Mhe. John Kisandu, akielezea kuhusu ujenzi wa daraja la Chibe – Old Shinyanga

    "Daraja hili limerahisisha mawasiliano kati ya kata ya Chibe na Old Shinyanga, kwa sababu hapa palikuwa hapapitiki wakati wa masika kutokana na kuwepo kwa mto mkubwa. Usalama sasa upo na mapato ya Halmashauri yameongezeka kutokana na kwamba sasa wafanyabiashara wengi wanaokwenda katika Mnada wa Old Shinyanga na Tinde wanapita katika daraja hili," ameeleza Kisandu.

    Naye Diwani wa kata ya Ibinzamata, Mhe. Ezekiel Sabo, amesema ujenzi wa Daraja la Ibinzamata Makaburini linasaidia kurahisisha kufika katika eneo la Makaburini na maeneo ya jirani kwani eneo hilo lilikuwa halipitiki wakati wa masika baada ya daraja la awali kuvunjika.

    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini inaendelea na ziara ya kutembelea kata za Jimbo la Shinyanga Mjini, lengo kuu ni kuzungumza na wanachama na viongozi wa CCM, kufanya tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuangalia hali ya uhai wa chama, na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo hayo.

    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga

    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
    Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old Shinyanga
    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza katika daraja la Ibinzamata Makaburini
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza katika daraja la Ibinzamata Makaburini
    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini
    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini
    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini
    Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini wakiondoka katika daraja la Ibinzamata Makaburini
    Ujenzi wa daraja la Ibinzamata Makaburini ukiendelea
    Ujenzi wa daraja la Ibinzamata Makaburini ukiendelea
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Chibe
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Chibe
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Chibe
    Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Chibe
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM

    WAZIRI JAFO AKABIDHI MAGARI MATANO KWA WAKALA WA VIPIMO


    Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) amekabidhi magari matano kwa taasisi ya Wakala wa Vipimo ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za uhakiki na ukaguzi wa vipimo bidhaa zilizofungashwa kwa haraka na kwa wakati kwa Wananchi ambao ndio watumiaji wa vipimo na bidhaa kila siku.

    Kadhalika, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameelekeza magari hayo yakatumike katika kaguzi mbalimbali za bidhaa zilizofungashwa kwa kuhakikisha vipimo vinakuwa sahihi katika bidhaa za nondo na mabati kwa kusimamia usahihi wa vipimo ili mnunuzi wa mwisho aweze kupata bidhaa inayoendana na thamani ya fedha anayolipa.

    "Wananchi wananunua nondo kiasi kwamba hata majengo yao yanakuwa hatarini kwakuwa wazalishaji wanasema wanazalisha nondo za mm 16 lakini zinakuwa chini ya vipimo hivyo, sasa niagize wazalishaji wote wa nondo kuzalisha nondo zenye ubora na zenye vipimo sahihi halikadhalika kwa wazalishaji wa mabati." Amesema Waziri Jafo.

    Waziri Jafo ameielekeza wakala wa Vipimo kuendelea kufanya kaguzi za kushtukiza kwenye viwanda vya uzalishaji wa bidhaa za nondo na mabati ili kuhakikisha bidhaa zinazofika kwenye masoko zinakuwa na vipimo sahihi kwa lengo la kuwalinda wanunuzi wa bidhaa hizo ili kuepukana na uchezewaji wa vipimo.

    Bw. Alban Kihulla Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo amemshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara kwa kuja kukabidhi magari matano ambayo yatasaidia kufika katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma za usimamizi na ukaguzi wa vipimo.

    "Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara katika mwaka huu wa fedha 2024/25 Wakala ilipanga kununua magari saba lakini mpaka sasa tumepokea magari matano ambayo umetukabidhi siku ya leo na magari mengine mawili yatafika hivi karibuni na gharama ya magari hayo matano ni Bil. 1,004,739,000."

    Bw. Alban amesema Wakala wa Vipimo itaendelea kutoa huduma za usimamizi wa vipimo kwa wakati kwa lengo la kuwalinda watumiaji wa huduma hizo na kaguzi mbalimbali za kushtukiza zitaendelea kufanyika ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia kwenye masoko zinakuwa na vipimo sahihi na adhabu kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na. 340 kwa wazalishaji watakaobainika kuchezea vipimo.

    Timu zilizoingihatua ya 16 bora UEFA Champions League.


    Timu zilizoingihatua ya 16 bora UEFA Champions League.

     Timu zilizoingihatua ya 16 bora UEFA Champions League.

    🏴󠁧󠁢 Liverpool FC

    🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Arsenal FC

    🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Aston Villa

    🇪🇸 Barcelona

    🇪🇸 Atletico Madrid

    🇪🇸 Real Madrid CF

    🇩🇪 Bayer Leverkusen

    🇩🇪 Bayern Munich

    🇩🇪 Dortmund

    🇫🇷 LOSC Lille

    🇫🇷 Paris Saint Germain

    🇳🇱 Feyenoord

    🇳🇱 PSV Eindhoven

    🇮🇹 Inter Milan

    🇵🇹 SL Benfica

    🇧🇪 Club Brugge

    Droo ni Ijumaa hii

    Wednesday, February 19, 2025

    Sinta Shangaa Mchezaji Huyu Akitua Jangwani au Msimbazi Dirisha Lijalo la Usajili...




    Sinto Shangaa dirisha lijalo nikamuona akiwaniwa na timu kubwa kama ataendelea na mwendelezo bora kwenye ligi katika michezo iliyosalia

    Seleman Salim Rashid 'Bwenzi' kwenye mechi tatu mfululizo za ligi kuu Tanzania tangu atue Kengold, amefunga mabao matatu ndani ya dakika 189.

    Vs Tabora
    Vs Yanga
    Vs Fountain Gate

    Sio kwa bahati mbaya anauwezo mzuri mguuni, nguvu,ufundi wa kuchezea mpira, uhakika wa kulenga lango na kufunga lakini pia ubora wa kupiga mipira iliyokufa (Faulo,kona,free-kick)

    Rejea magoli yake akiwa Champions
    Vs Biashara akiwa Mbeya kwanza,
    Vs FGA akiwa na Tma n.k

    Huyu amewahi kucheza ligi kuu akiwa na Namungo mrejeeni vizuri mtanielewa.

    Kwenye ligi kwa sasa analingana nao Mishamo Daudi Michael na Herbert Charles Lukindo ambapo Mishamo amecheza mechi 16, dakika 1323 na Lukindo mechi 15, dakika 943.

    Selema Salim Rashid amejiunga na Kengold Januari 2025 akitokea Mbeya Kwanza ya championship.

    Hali ya Papa Francis Sio Nzuri, Vatican Yaanza Maandalizi ya Mazishi




    Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88, anaendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Gemelli jijini Rome baada ya kugunduliwa na nimonia kali. Ripoti zinadai kuwa walinzi wa Uswisi wanaolinda Vatican wameanza mazoezi ya maandalizi ya mazishi yake, jambo linalozua taharuki kwa waumini wa kabisa katoliki.

    Kwa mujibu wa #Vatican, Papa Francis anasumbuliwa na maambukizi ya kupumua yanayojumuisha pumu, na madaktari wamemwekea mpango wa matibabu kwa kutumia antibiotiki. Pamoja na ugonjwa huu, hali yake inaangaliwa kwa umakini zaidi kutokana na historia yake ya kiafya, kwani aliwahi kuondolewa sehemu ya mapafu yake alipokuwa kijana.

    Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Papa zinadai kuwa amewahi kusema, "Huenda safari hii nisimudu," jambo linaloashiria utayari wake wa kukabiliana na hatima yake. Hata hivyo, bado anapata lishe, anasoma magazeti, na anaendelea na kazi zake akiwa hospitalini.

    Waumini wengi wameanza safari kuelekea hospitalini humo kumuombea kiongozi wao mkubwa wa kiroho, huku ulimwengu ukifuatilia kwa makini maendeleo ya afya yake.

    Mfahamu Mrembo Aliyeonakana na Diamond na Kuzua Gumzo Mtandaoni, Wabongo Wajaa Kwenye Page yake

    Mfahamu mrembo aliyeonakana na Diamond na kuzua gumzo mtandaoni, Wabongo wajaa kwenye page yake


    Tumuonee Huruma Zuchu, Makosa Kafanya Diamond ila Anayeshambuliwa Zuchu....



    Eti wadau nielewesheni hapa kwanini mara nyingi makosa akiyafanya @diamondplatnumz huyu binti(@officialzuchu) ndiye anaeshambuliwa sana...? au kosa lake kubwa ni kuwa na mahusiano na Diamond na pengine baadhi yenu hamjaridhika?

    Bado nawaza @officialzuchu amewatengenezaje hawa maadui ambao wanashangilia na kumdhihaki mara kwa mara Diamond anapoonekana kuharibu mambo? ebu nipeni majibu.

    Yote kwa yote @wcb_wasafi kama record label nadhani mna wajibu wa kuhakikisha huyu binti afya yake ya akili inakua sawa hizi dhihaka zinazoendelea mitandaoni dhidi yake sidhani kama anastahili wakati yeye ndiye victim,she's young,talented & blessed na tunamtegemea katika kuikuza industry ya muziki wa Afrika mashariki.

    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...