Tuesday, December 17, 2024

Airtel Tanzania yazindua promosheni ya Airtel Santa Mizawadi Kuwazawadia wateja na mawakala


Airtel Tanzania inaanza msimu huu wa sikukuu na Airtel Santa Mizawadi promosheni maalum yakutoa shukrani na kuwazadia  wateja na mawakala wote wanaoendelea kutumia huduma za Airtel katika msimu wa sikukuu. Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.

Jinsi ya kushirikina kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, ikiw awewe ni Wakala wa Airtel unatakiwa tu kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa,  kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60#, au kwa kutumia 'My Airtel App'.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo iliyofanyika makao makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson Mmbando alieleza kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi ni inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel katika msimu wote huu wa sikukuu.

"Kupitia Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi tunasambaza upendo na kunogesha sikukuu kwa wateja na  mawakala wetu wetu ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yetu," alisema Mmbando.
Mmbando alisisitiza kuwa Airtel inaendelea kujidhatiti kutoa huduma za kipekee katika msimu wa sikukuu huku akidokeza kuwa kila muamala unaofanyika unatoa nafasi kwa wateja au mawakala kujishindia zawadi zitakazoboresha Maisha yao.

Kwa upande wake Meneja Huduma kwa Wateja Bi Celine Njuju "Airtel tunawadhamini sana wateja wetu, Tusingefika hapa tulipoleo bila ya wateja na mawakala wetu, Airtel Santa Mizawadi  ni promosheni kabambe kwa kuwa itanogesha balozi wetu, mtamuona Mr SANTA wetu akitembele  baadhi ya mitaa yetu kuhakikisha wateja na mawakala wanapata pia zawadi za papo kwa hapo, ikiwa utabahatika kukutana nae basi nakuahidi atanogesha msimu wako  wa sikukuu vizuri ufurahie wewe na  wapendwa wako."

"Kwa kumalizia, washindi wa Airtel Santa Mizawadi watapatikana kupitia Droo za zitakazochezwa kila wiki mara moja ambapo washindi  wote watapigiwa simu kupitia namba maalum ya Airtel 100" alisisitiza Bi Njuju

Kwa taarifa zaidi kuhusiana na promosheni hii, tunawahimiza wateja na mawakala wetu kutembelea tovuti ya Airtel au kuwasiliana na watoa huduma wetu wa Airtel kwa kupiga 100.

WANANCHI WACHOSHWA NA AHADI, WAAMUA KUCHONGA BARABARA WENYEWE KWA SOFI MHONGOLO

 

Wananchi wa mtaa wa Sofi kata ya Mhongolo wakichimba mtaro ili kupunguza maji yanayotuama katika eneo hilo yanayosababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya kata ya Mhongolo na kata ya Busoka Manispaa ya Kahama.


NA NEEMA NKUMBI -KAHAMA


Wakazi wa mtaa wa Sofi, Kata ya Mhongolo, Manispaa ya Kahama, wamechukua hatua ya kujitolea kufanya marekebisho ya barabara inayounganisha Sofi, Mhongolo na Busoka baada ya kukumbwa na changamoto ya mafuriko na ukosefu wa mawasiliano wakati wa masika.

TANZIA: Jaji John Tendwa Afariki Dunia



Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji John Tendwa amefariki dunia.

Taarifa za awali za kifo chake zimetolewa leo Desemba 17, 2024 na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Jaji Mutungi amesema wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa familia na wao kama ofisi ya Msajili watatoa taarifa rasmi.

Amesema Jaji Tendwa aliwahi kuhudumu kwenye ofisi hiyo hivyo muda mfupi kutoka sasa watatoa taarifa kamili.

REA kusambaza mitungi ya gesi Manyara kwa bei ya Ruzuku


Na John Walter -Manyara 

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetangaza mpango wa kusambaza mitungi 16,275 ya gesi ya ujazo wa kilo sita kwa kila mwananchi mkoani Manyara ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali ya awamu ya sita wa kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 ya watumiaji ifikapo mwaka 2034.  

Awali Mpango huo ulianza kwa kishirikisha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Magereza, na shule mbalimbali.

Mkurugenzi wa Teknolojia Jadidifu na Nishati Mbadala kutoka REA Mhandisi Advera Mwijage amesema mitungi hiyo 16,275 itasambazwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 284 kati ya jumla ya shilingi bilioni 8.6 zilizotengwa kitaifa kusambaza gesi kwa wananchi kwa bei ya ruzuku.

Mhandisi Advera amesema kwa mkoa wa Manyara mtungi mmoja wa ujazo wa kilo 6 utauzwa kwa bei ya shilingi 17,500 badala ya bei ya awali ya shilingi 35,000 kwa kila mtungi wa ujazo wa kilo sita. 

Amesema Kampuni ya Manjis imepewa jukumu la kusambaza mitungi hiyo kwa gharama ya Shilingi 35,000 kwa kila mtungi ambapo serikali italipa asilimia 50 ya bei hivyo mwananchi atanunua kwa bei ya ruzuku ya shilingi 17,500 kama ilivyodhamiria Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Advera pia ametangaza fursa ya mikopo ya masharti nafuu ya hadi shilingi milioni 120 kwa wanaotaka kufungua biashara ya vituo vya kuuzia mafuta maeneo ya vijijini kwa lengo la kusogeza nishati hiyo karibu na wananchi. 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, amepongeza jitihada hizo za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kutoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Manyara kuchangamkia fursa hiyo kutumia nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kuboresha afya na mazingira. 

Amesema mpango huo unalenga kuleta mabadiliko makubwa katika matumizi ya nishati safi nchini, huku ukihakikisha upatikanaji wa gesi kwa gharama nafuu kwa wananchi wa kawaida.

Ademola Lookman Mchezaji Bora wa Mwaka Afrika CAF Awards 2024


Mshambuliaji wa Atalanta na Timu ya Taifa ya Nigeria Ademola Lookman ameshinda tuzo ya Ballon d'Or mchezaji bora wa mwaka wa Afrika mwaka 2024 kwa upande wa wanaume.

#CAFAwards2024

WAMILIKI NA MAMENEJA WA SHULE NA VYUO VYA KATI WAPEWA MAFUNZO YA UENDESHAJI BORA


CHUO Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kwa kushirikiana na Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na vyuo vya kati visivyo vya Serikali (TAMONGSCO) wametoa Mafunzo kuhusu namna bora ya uendeshaji wa shule za Msingi , Sekondari na vyuo vya kati kwa Wamiliki na Mameneja wa shule na vyuo vya kati visivyo vya Kiserikali nchini

Mafunzo hayo yatawapa fursa kujifunza masuala mbalimbali hususan fedha, uongozi pamoja kuwasilisha maoni na mapendekezo kuhusu mabadiliko ya sheria ya elimu.

Akizungumza leo Desemba 16,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo hayo ya Siku mbili, Kaimu Naibu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba amesema mafunzo hayo yanakwenda kusaidia kuleta ufanisi na ubora mkubwa katika shule na vyuo vyao.

Amesema wataalamu ambao wanawapitisha kwenye mada mbalimbali ni wazoefu na watahakikisha washiriki kupata uelewa mkubwa na kwenda kuboresha maeneo yao .

"washiriki wote ninawasihi msikilize kwa makini mada zote ambazo zitawasilishwa, naamini mtapata uelewa mkubwa kwani wataalamu watakaowapitsha kwenye mada zilizoandaliwa ni wazoefu". Amesema Coretha.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo,  CPA Charles Albert amesema mafunzo hayo yatasaidia kuboresha mifumo yao ya malipo na matumizi sahihi ya fedha pamoja na mipango ya kibajeti na maendeleo endelevu ya shule zao.

"Ambao wamepata taarifa na hawakuweza kufika kwenye mafunzo haya wamekosa uelewa wa namna ya upangaji wa bajeti zao kwasababu nimeangalia wamiliki wengi wa shule walikuwa hawajui kupanga bajeti zao vizuri lakini pia walikuwa hawajui viwango gani ambavyo vinatakiwa vikatwe kodi hasa katika kodi ya ongezeko la thamani inayotokana na mishahara ya wafanyakazi". Amesema

Naye mmoja wa washiriki, Mkurugenzi wa shule ya Morelight ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa shule na vyuo vya kati visivyo vya Kiserikali (TAMONGSCO) Wilaya ya Ubungo, Gervas Njoele amesema wamefundishwa namna ya kuendesha taasisi zao hasa kimapato na matumizi.

"Kwenye biashara unapopata mafunzo na semina mbalimbali za namna hii, zinatusaidia kujua namna za kuziendesha hizi taasisi ambazo zipo kwenye jamii". Amesema Gervas.

Mkuu wa Idara ya Kozi fupi na Shauri za kitaalamu Chuo Kikuu Mzumbe Dkt Darlene Mutalemwa na Mratibu wa mafunzo ambaye pia ni Katibu Mkuu TAMONGSCO Bw. Youstor Ntungi wamesema Mafunzo hayo yanashirikisha Wamiliki na Mameneja zaidi ya themanini(80) kutoka Shule za Msingi, Sekondari na vyuo vya kati kutoka Tanzania.
Kaimu Naibu Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt.Coretha Komba akifungua mafunzo.
Mratibu wa Mafunzo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TAMONGSCO Bw. Youstor   Ntungi (kulia) akitambulisha washiriki kabla ya Mafunzo kuanza
Mtoa mada CPA . Charles Albert akiwasilisha mada

Monday, December 16, 2024

WAZIRI SILAA AAGIZA TTCL KUJIENDESHA KIBIASHARA

 

******
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb), ameiagiza Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuandaa mpango kazi utakaowezesha shirika hilo kujiendesha kibiashara.

Waziri Silaa ametoa maagizo hayo leo tarehe 16 Desemba, 2024 wakati akizindua Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa maagizo hayo yanakuja kufuatia maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 10 Desemba, 2024, Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar wakati wa hafla ya uapisho wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Naibu Makatibu Wakuu na Mabalozi kuhusu usimamizi wa shirika hilo kujiendesha kibiashara.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Bodi na menejimenti ya Shirika la TTCL, Waziri Silaa amesema, "Serikali ya Rais Dkt. Samia imewekeza fedha nyingi katika miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo mkongo wa taifa wa mawasiliano, minara ya mawasiliano, pamoja na kituo cha kuhifadhia data cha taifa (National Data Center).

"Nia ya Rais ni kuona uwekezaji huu mkubwa unaleta tija nchini." Amesema Waziri Silaa na kuongeza;

"Shirika hili likiendeshwa vyema lina uwezo wa kusaidia sekta nyingine, kwa sababu wizara yetu ni wezeshi katika mawasiliano, hivyo wizara nyingine na Taasisi zinaitegemea katika kukuza sekta zao za TEHAMA."

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL Bw. David Nchimbi amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumteua kuongoza bodi hiyo na kuahidi kusimamia shirika ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Bw. Nchimbi amemshukuru Waziri Silaa kwa utayari alioonesha na kuahidi kuwa bodi itatoa ushirikiano kwa wizara wakati wote itakapokuwa inatekeleza majukumu yake.






TUWAINUE WABUNIFU WAZAWA KUWANADI KIMATAIFA - DKT. BITEKO



Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa pamoja na jitihada za kuwainua wabunifu wawekezaji nchini, bado kuna umuhimu mkubwa wa kuwawezesha wabunifu wetu kukua zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 16, 2024 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la Uwekezaji wa Kampuni Bunifu (STARTUPs)

Amesema kuwa Tanzania imerekebisha mifumo mingi ili kuwezesha ubunifu na uwekezaji wa moja kwa moja nchini kuleta maendeleo, suala ambalo tumeona likifanikiwa na kwahiyo linahitaji kupaliliwa na kuungwa mkono kwa matokeo chanya.

"Nimewasikiliza wanakongamano na kupitia majadiliano haya ni wazi kwamba bado kuna namna ya kuboresha zaidi mifumo yetu ya usimamizi na utawala ili kuhakikisha Wabunifu wanapata nafasi nzuri zaidi." amesema na kuongeza kuwa, Tunatamani kuona Watanzania wanashiriki katika kukuza uchumi wa nchi yao na pengine kuazimwa katika nchi nyingine." amesema Dkt. Biteko
Amesema wapo baadhi ya Watanzania wanaofanya shughuli zao nje ya Nchi ambao wanaiwakilisha vema Tanzania kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia misingi iliyowekwa katika nchi hizo na hivyo kuwataka wabunifu wawekezaji kuiga mfano huo.

Aidha, Dkt. Biteko amesema kuwa Maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yako wazi na kwa nyakati mbalimbali amekuwa akijipambanua kuhusu uwezeshaji wa makundi mbalimbali wakiwemo wabunifu wawekezaji.

"kwa kutekeleza maono ya Rais, ni muhimu kuwasikiliza, kuwaamini na kufanyia kazi maoni na bunifu zao ili kuboresha mazingira yatakayo wawezesha kutekeleza Bunifu zao na kupata fursa ndani na nje ya Nchi".

Naye, Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo akimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Kitila Mkumbo amesema Serikali imekuwa ikizingatia suala la uwezeshaji kwa Wabunifu Wawekezaji ikiwa ni pamoja na kupokea maoni yao kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Nyongo ameongeza kuwa, Serikali imeboresha mazingira ya biashara kwa kupunguza gharama za biashara ili kuwawezesha wabunifu kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake, Waziri Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa amesema Wizara imeandaa mazingira ya kuwawezesha Wabunifu kufanya majaribio ya kazi zao kupitia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Amesema Serikali imejenga vituo vya ubunifu vinane (8) katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuwawezesha Wabunifu kujiandaa na hatimaye kupata ajira katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TSA, Zahoro Muhaj amemshukuru Rais Samia kwa maono yake ya kuwatambua na kuwawezesha wabunifu ili waweze kuchagiza maendeleo ya nchi.

" Tunaomba salam zetu zifikishwe kwa Mheshimiwa Rais, ambaye amekuwa akitubeba na kusafiri nasi katika nchi mbalimbali ili tupate uzoefu na kukua kama mtu kama mtu mmoja mmoja na baadae kama Taifa," amesema Muhaj.
Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Nelson Bonephace ameishukuru Serikali kwa jitihada za kuwawezesha wabunifu wawekezaji kukua.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2020 hadi sasa zaidi ya dola za kimarekani Milioni 49 zimetolewa ambazo zinatumika kujenga Kampasi mpya za Kagera, Zanzibar na Lindi.





FAINALI ZA CRDB BANK SUPA CUP 2024 ZAMALIZIKA KWA MAFANIKIO JIJINI ARUSHA



Jumamosi tarehe 14 Desemba 2024, jijini Arusha, Benki ya CRDB ilihitimisha fainali za CRDB Bank Supa Cup 2024, mashindano yaliyojumuisha michezo ya soka na netiboli, kwa timu zilizoundwa na wafanyakazi wa benki hiyo, yakiwa ni mashindano yenye mbwembwe na ushindani wa hali ya juu. Timu mbalimbali kutoka kanda tofauti za Tanzania zilishiriki katika fainali hizo ambazo zilileta burudani, mshikamano, na ushindani mkubwa.

Fainali hizo zilihudhuriwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Frank Mmbando, pamoja na viongozi mbalimbali wa Benki ya CRDB. Viongozi hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi wa CRDB Bank Congo, Jessica Nyachiro, Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo, Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Bruce Mwile, Afisa Mkuu wa Biashara, Boma Raballa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa.
Matokeo ya Soka

Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu, timu ya Ulipo Tupo FC kutoka Kanda ya Ziwa iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Boom Advance FC kutoka Kanda ya Kaskazini.

Fainali kubwa ya soka ilishuhudia timu ya iMbeju FC kutoka Kanda ya Pwani ikiibuka kidedea kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Al Barakah FC kutoka Kanda ya Magharibi. Ushindi huu umeifanya iMbeju FC kutwaa ubingwa wa CRDB Bank Supa Cup 2024.

Matokeo ya Netiboli

Kwa upande wa netiboli, nafasi ya tatu ilichukuliwa na Lipa Hapa Queens kutoka Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuwashinda Popote Inatiki Queens kutoka Kanda ya Kati kwa alama 50-45.

Fainali ya netiboli iliwaweka uso kwa uso iMbeju Queens kutoka Kanda ya Pwani na Ulipo Tupo Queens kutoka Kanda ya Ziwa. iMbeju Queens walifanikiwa kushinda kwa alama 45-39, na hivyo kutwaa ubingwa wa netiboli.

Zawadi na Tuzo

Mashindano haya yalihitimishwa kwa utoaji wa tuzo mbalimbali kwa washindi wa michezo yote, huku fedha taslimu, medali, na vikombe vikikabidhiwa kwa washindi kama ifuatavyo:
Soka

Mshindi wa Kwanza: iMbeju FC – TZS 13,000,000/=
Mshindi wa Pili: Al Barakah FC – TZS 9,000,000/=
Mshindi wa Tatu: Ulipo Tupo FC – TZS 6,000,000/=

Netiboli

Mshindi wa Kwanza: iMbeju Queens – TZS 9,000,000/=
Mshindi wa Pili: Ulipo Tupo Queens – TZS 6,000,000/=
Mshindi wa Tatu: Lipa Hapa Queens – TZS 4,000,000/=
Tuzo Binafsi za Soka


Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP): Godwin Edward Junye (iMbeju FC) – TZS 500,000/=
Mfungaji Bora: Abdallah Magoe (Ulipo Tupo FC) – TZS 500,000/=
Kipa Bora: Abbas Wadi Makame (iMbeju FC) – TZS 300,000/=
Mchezaji Bora wa Mechi ya Fainali: Stanislaus John Masaswe (iMbeju FC) – TZS 300,000/=

Tuzo Binafsi za Netiboli


Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP): Ikutungangisya Richard (Ulipo Tupo Queens) – TZS 500,000/=
Mfungaji Bora: Saada Ally Juma (Lipa Hapa Queens) – TZS 500,000/=
Mchezaji Bora wa Mechi ya Fainali: Tumaini Ndosi (iMbeju Queens) – TZS 300,000/=
Akizungumza katika fainali hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alisema kuwa benki hiyo imeweka mikakati na sera mbalimbali za kuongeza chachu kwa wafanyakazi wake, na michezo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuhakikisha wanajenga umoja, afya njema, na furaha miongoni mwao.

"Mashindano ya CRDB Bank Supa Cup ni zaidi ya michezo; ni jukwaa la mshikamano, mawasiliano, na afya bora kwa wafanyakazi wetu. Tunajivunia kuona mshindano haya yakiendelea kuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Benki yetu," alisema Nsekela.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa, alisisitiza umuhimu wa mashindano hayo katika kuongeza mshikamano miongoni mwa wafanyakazi. "Michezo huchangia kwa asilimia kubwa kuwaleta watu pamoja, na kupitia Supa Cup tumeweza kuona mshikamano wa kipekee kati ya wafanyakazi wetu kutoka kanda mbalimbali," alisema Rutasingwa.

Mashindano ya CRDB Bank Supa Cup 2024 yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa, huku timu ya iMbeju kutoka Kanda ya Pwani iking'ara kwa kushinda vikombe vyote vya soka na netiboli. Shangwe na matarajio yameanza kuandaliwa kwa mashindano ya mwaka 2025, huku wafanyakazi na mashabiki wakiisubiri kwa hamu kubwa msimu ujao wa burudani.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...