Wednesday, August 11, 2021
Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa
KATIBU MKUU CCM ATOA SIKU 14 KWA VIONGOZI WA WILAYA NA MIKOA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza viongozi wa chama hasa kupitia Kamati za Siasa katika ngazi za wilaya na mikoa ndani ya siku 14 wakamilishe kukagua miradi yote ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika maeneo yao na taarifa ya kilichojiri iwasilishwe ofisini kwake.
Sambamba na maagizo ya kuwataka kukagua miradi ya maendeleo, Chongolo pia amewaagiza kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani na amesisitiza kuwa chama kitafuatilia utekelezaji wa maagizo hayo.
Chongolo ametoa maagizo hayo tarehe 10 Agosti, 2021 mkoani Morogoro wakati akikagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), akiwa ameambatana na Wajumbe wa Sekreterieti ya Chama Taifa.
"Niwapongeze watu wa Morogoro kwani mmeweza kuonesha njia nami nimeamka nije hapa na sekretarieti yangu kujionea kama kinachofanyika hapa ni kile kilichoelekezwa katika ilani yetu ya uchaguzi na ndicho kinachoelezwa kila mara,"amesema Chongolo na kuongeza "Haya ni maagizo na maelekezo Kama tulivyopeana mara baada ya mkutano mkuu maalum kuwa wote tushuke chini kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo yetu ."
Amesema wao wanawajibu wa kuisimamia Serikali na utekelezaji wa Ilani kwani ni sisi ndio tutakaorudi kuwaeleza wananchi nini tumefanya.
Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa amesema anaishikuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa wakati kwa ajili ya kukamilisha mradi huo huku akifafanua mpaka sasa wamelipa hati 34 kati ya 35 huku hiyo moja ambayo inalipwa muda wowote kuanzia sasa.
RC Tabora ahimiz uwekezaji katika ufugaji nyuki
WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wamehimizwa kuwekeza katika ufugaji wa kisasa wa nyuki kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa asali
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati alikuwa akizindua Mabaraza ya Biashara ya Wilaya ya Kaliua na Urambo.
Asali ni mojawao wa bidhaa ambayo inaweza kuwaondoa wakazi katika umaskini na kuendelea kuutangaza Mkoa wa Tabora ndani na nje ya Nchi .
Balozi Dkt. Batilda alisema hivi sasa ufugaji wa nyuki katika Mkoa wa Tabora bado unatumia mizinga ya asili ambayo uzalishaji wake wa asali ni kidogo ambapo ni wa wastani wa kilo 9 kwa kila mzinga.
Alisema wakazi wa Tabora wakikubali kubadili teknolojia ya kizamamani na kutumia mizinga ya kisasa watapata wastani kilo 20 hadi 25 kwa mzinga mmoja.
Balozi Dkt. Batilda alisema hivi Mkoa huo unawastani wa mizinga laki nne ambapo kati ya hiyo 40,000 ndiyo ya kisasa.
Alisema Mkoa wa Tabora unatakiwa kutumia fursa iliyopo ya miti ya miombo kuongeza idadi ya mizinga ya kisasa kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa asali.
Balozi Dkt. Batilda alisema tayari uongozi wa Mkoa umeshafanya juhudi ya kukutana na TAWA ili kuomba kibali cha kuwaruhusu wafugaji wa nyuki kutumia mapori yao
Katika nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda amewataka wakulima kuendesha kilimo ambacho ni rafiki wa mazingira na uoto wa asili.
Alisema hatua itawezesha nyuki kuendelea kuwa na malighafi ambazo zinatumiwa katika utengenezaji wa asali.
Balozi Dkt. Batilda aliongeza kuwa sanjari na hilo ni vema Kila Halmashauri Mkoa huo ikaanzia zoezi la kuwa na mistu yake na elimu hiyo waipeleke hadi ngazi za familia.
Zifahamu faida za kula Strawberry
Kula matunda ni faida kubwa katika maisha yetu, na matunda yako mengi. Leo nakudokeza kidogo tu tunda moja linalojulikana kwa jina la 'strawberry'
Tunda la Strawberry lina umuhimu na faida nyingi sana katika mwili wa binadamu. Miongoni mwao ni faida za kiafy kama vile;-
1. Kuimarisha mifupa
2. Husaidia nguvu za kiume na muamko wa kufanya mapenzi. Hii ni kwa kuwa zina madini ya zink basi husaidia katika mfumo wa uzazi wa mwanaume.
3. Husaidia kuponya majeraha kwa haraka
4. Hutunza ngozi ya mwili
5. Kupunguza madhara yatokanayo na presha ya kupanda na kushuka
6. Kwa wenye uzito mkubwa husaidia kupunguza uzito
7. Kuongeza kumbukumbu
8. Huzuia kuzaliana kwa bakteria na virus mwilini
Lakini pia Strawbery ina matumizi tofauti ikiwemo
1. Kuliwa kama matunda mengine
2. Kutia ladha katika vyakula mbali mbali
3. Kutengeneza marashi
4. Kutia nakshi katika baadhi ya vipodozi
Tuesday, August 10, 2021
POLISI WAMKAMATA YULE MHUNI "TELEZA' ANAYEDAIWA KUBAKA NA KUCHUKUA CHUPI ZA WANAWAKE ARUSHA

Corona; Wananchi wanavyoishi kwenye ‘mstari’ wa kifo Dar
Ummy Mwalimu ataka Wakurugenzi wa Halmashauri kushirikiana na Makatibu Tawala wasaidizi mikoa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu ameanza ziara ya kikazi leo mkoani Njombe ambapo pamoja na mambo mengine atakagua miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya ngazi ya msingi, sekta ya elimu na ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Akizungumza leo Agosti 10,2021 na Sekretarieti ya Mkoa huo, Waziri Ummy ameupongeza uongozi na watendaji kwa kuendelea kwa kasi, ari na jitihada katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo na kuongoza kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka 2021/2022.
Amesema Sekretarieti za Mikoa zina wajibu wa kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatimiza majukumu yao kikamilifu kwa kuwa wananchi wanahitaji kupatiwa maendeleo na maendeleo yanapatikana kwa Halmashauri imara.
Katika ziara hiyo, Waziri Ummy amesisitiza umuhimu wa viongozi wa sekretarieti za Mikoa nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani kwa kuwa ndio wasimamizi wakuu katika ngazi ya Halmashauri.
Aidha, amesema kuwa Makatibu Tawala wasaidizi wa Mikoa wana wajibu wa kuhakikisha wanachambua bajeti za halmashauri na kuangalia vipaumbele ambavyo vinasaidia katika kutatua kero za wananchi zikiwemo ununuzi wa madawati, ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa vituo vya afya na Hospitali za Wilaya na ujenzi wa miundombinu ya Barabara.
"Makatibu Tawala wasaidizi wa Mkoa wanawajibu wa kuhoji na kuchambua bajeti za Halmashauri kwa kina, kwa kuangala vipaumbele vitakavyosaidia kutatua kero za hasa katika masuala ya elimu, afya na miundombinu kwa ujumla. Ni kazi yenu kufanya kazi hiyo na sio ofisi ya Rais TAMISEMI, Ni wajibu wenu kusimamia matumizi ya Halmashauri kwa kuhakikisha fedha zinapelekwa katika kutatua kero za wananchi,"amesisitiza.
Katika hatua nyingine, Waziri Ummy amewaagiza Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotatua kero za wananchi.
Kabla ya kikao na Sekretarieti ya Mkoa, Waziri Ummy amekutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya na kukutana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM).
Tanzania Yasaini Mkataba Wa Uanzishwaji Wa Taasisi Ya Udhibiti Wa Dawa Ya Umoja Wa Afrika
Tanzania imesaini Mkataba wa uanzishwaji wa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency) na kuwa Nchi ya 22 kusaini Mkataba huo unaohusisha Nchi Wanachama.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini Mkataba huo katika Ofisi za Makao Makuu za Umoja wa Nchi huru za Afrika (AU) zilizopo Addis Ababa nchini Ethiopia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amesema lengo la Tanzania kusaini mkataba huo ni kuunganisha nguvu na jitihada za pamoja na nchi nyingine za Afrilka katika kupambana na dawa bandia na duni.
Ameongeza kuwa Taasisi hiyo ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (African Medicines Agency) kwa kifupi AMA itasaidia katika kuunganisha jitihada za taratibu za kuwianisha (harmonization) mifumo ya udhibiti wa dawa katika Jumuiya za kiuchumi za kikanda Barani Afrika akitolea mfano chanjo mbalimbali ikiwemo ya UVIKO 19.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bwana Adam Fimbo, amesema uwepo wa Taasisi ya AMA utawezesha kupatikana kwa soko la dawa nchini Tanzania kuendana na Mkataba wa Afrika wa maeneo huru ya kibiasahara pamoja na kuwezesha upatikanaji wa haraka wa dawa wakati wa dharura pamoja na majanga ambapo kwa sasa Tanzania ina takribani viwanda vipya 17 vya dawa vilivyopo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dkt. Monica Nsanzabaganwa, amesema kuwa Taasisi ya AMA ni muhimu hasa katika kuweka mifumo imara ili kuwezesha nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kutatua kwa pamoja changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta ya afya.
Taasisi ya Udhibiti wa Dawa ya Umoja wa Afrika (AMA) inatarajiwa kuanza rasmi kufanya kazi mwaka 2022 baada ya kusainiwa na jumla ya nchi 27 za Umoja wa Afrika ambapo mpaka sasa nchi 22 zimesaini ikiwemo Tanzania ambayo ilipaswa kusaini mkataba huo tangu Februari 2020 lakini kutokana na janga la UVIKO 19 zoezi hilo liliahirishwa.
Aliyekuwa Msajili wa Hazina akabidhi ofisi rasmi
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...







