Monday, June 28, 2021
LISSU: Miezi 3 ya Samia kuna uhuru, watu wanapumua
Tanzania Kunufaika Soko Eneo Huru La Biashara Afrika
Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali ya Tanzania inategemea kunufaika na soko la bidhaa zake katika masoko ya nje baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa ushiriki katika Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA).
Akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTA) Mhe. Wamkele Mene, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kwa sasa Serikali ipo katika hatua za mwisho kusaini Mkataba wa AfCTA.
"Lengo la ziara ya Mhe. Mene hapa nchini pamoja na mambo mengine ni kukutana na viongozi na wadau wengine muhimu kujadiliana na masuala mbalimbali yanayohusu Mkataba wa AfCTA ikiwa ni pamoja na umuhimu wa Tanzania kuridhia Mkataba huo," Amesema Balozi Mulamula
Balozi Mulamula ameongeza kuwa, uanzishwaji wa AfCTA ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa ambapo pamoja na mambo mengine, utekelezaji wake unatarajiwa kuongeza wigo wa fursa nafuu za biashara nchini kwa kuwavutia wawekezaji na kuongeza mauzo hasa ya bidhaa za kilimo.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Sekretariati ya Eneuo Huru la Biashara Afrika (AfCTA) Mhe. Wamkele Mene ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano ambao imempatia tangu wakati wa uchaguzi hadi sasa na kuahidi kuwa utekelezaji wa Mkataba huo utanufaisha kila Nchi Mwanachama.
"……….Naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwani tangu ilipoingia Madarakani imetumia muda mfupi katika kushiriki kwa ukamilifu katika majadiliano ya kusaini mkataba huu na Tanzania imeshiriki vizuri sana kwenye majadiliano haya muhimu," Amesema Mhe. Wene
Ameongeza kuwa kwa sasa Eneo Huru la Biashara Afrika lina Nchi wanachama 38 ambazo zimekubaliana na Mkataba huo na kwamba kwa sasa Sekretariati hiyo inaendelea kuimarika katika kukuza biashara na sekta binafsi katika nchi wanachama wa AfCTA.
Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika umesainiwa na Nchi 54 kati ya nchi 55 za Umoja wa Afrika ikiwemo Tanzania. mkataba huo ulipata nguvu ya Kisheria Julai, 2019 baada ya nchi 28 kuridhia Mkataba huo. Mkataba wa AfCTA unahusisha maeneno ya ushirikiano katika bishara ya bidhaa, biashara ya huduma, uwekezaji, hakimiliki na ubunifu pamoja na Sera za ushindani.
Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula kongamano hili litakuwa mahsusi kuangalia masuala ya uswa wa jinsia kwa kizazi hiki na kizazi kijacho na kwamba wakuu wa Nchi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa watakuatana Ufaransa katika kongamano hilo kuanzia tarehe 30 Juni hadi 2 Julai 2021.
Balozi Mulamula ameongeza kuwa, Tanzania itashiriki katika kongamano hilo ambapo Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan atawakilishwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango
Uzinduzi wa Kongamano la Usawa wa Kijinsia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam umehudhuriwa na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Fredric Clavie pamoja na Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Bibi Hodan Addou.
TGNP YAJIVUNIA SIKU 100 ZA RAIS SAMIA... LIUNDI ASEMA ' ANA MWENDO WA TOFAUTI USAWA WA KIJINSIA'
Dc Busega aanza na kwa kusimamia ushuru wa ndani
Mkuu wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu Gabriel Zakaria amesema atahakikisha anasimamia makusanyo (ushuru) ndani ya Wilaya hiyo ikiwa ni moja kati ya vipaumbele vyake atakavyovitekeleza akiwa Wilayani hapo.
Mkuu huyo alisema hayo jana wakati wa kikao chake na wananchi wa kijiji cha Bukabile kata ya Nyashimo ,kilichofanyika katika viwanja vya standi Wilayani hapo.
Alisema bila kusimamia makusanyo ya ushuru,wilaya hiyo haiwezi kuwa na miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo ataanza na usimamizi madhubuti wa ushuru kwa kuunda kikosi kazi cha ufuatiliaji na ukusanyaji.
"Suala la ushuru( mapato) kwangu mimi ni kipaumbele cha kwanza na nitahakikisha tunakusanya zaidi ili asilimia 40 ya miradi iweze kubaki kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za jamii" alisema.
Aliongeza kuwa Wilaya ya Busega ina vyanzo vingi vya makusanyo na kwa kutumia vyanzo hivyo wataweza kukusanya fedha zaidi na wananchi watapata huduma za afya,miundombinu na elimu .
Aidha amewataka wananchi kulipa kodi wanazostahili na kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kwa pamoja waweze kuibadilisha wilaya hiyo na kwa Wilaya ya mfano.
Tanzania kuanzisha utalii wa lugha ya Kiswahili
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa inampango mkakati wa kuanzisha utalii wa lugha ya Kiswahili kwenye maeneo yote yenye kumbukumbu kama Butiama kwa lengo la kuwawezesha watalii kujifunza Kiswahili pamoja na kusimuliwa historia na kumbukumbu za waasisi wa Taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 28, 2021, na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Mary Masanja wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Esther Matiko, aliyehoji mpango wa serikali wa kuyaboresha maeneo aliyozaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ili pawe historical site kama ilivyo Afrika Kusini kwa Hayati Nelson Mandela.
"Serikali ina mpango wa kuanzisha utalii wa Kiswahili kwenye maeneo hayo yenye kumbukumbu ili mtalii anapofika katika maeneo hayo ajifunze lugha ya Kiswahili, lakini pia atasimuliwa historia na kumbukumbu ya waasisi wetu walikuwaje na walifanya nini na ukizingatia Mwalimu Nyerere alikuwa ni Muasisi wa kuboresha lugha yetu hii," amejibu Naibu Waziri Mh. Mary Masanja.
MANGE KIMAMBI amshauri HARMONIZE ‘Mashabiki wako karibia wote ni wa ALIKIBA, usishindane naye’
MANGE KIMAMBI amshauri HARMONIZE 'Mashabiki wako karibia wote ni wa ALIKIBA, usishindane naye'
Mdogo angu upande wa mama huyu….Fans wako karibia wote ni fans wa Kiba sasa jaribu usiwe unashindana nae unakuwa una kosa support. Kama mi dadako Kiba angekuwa hayuko hewani sasa hivi ningesimana na wewe tuwashinde wale 🤣🤣🤣 ila sasa ona hata nyimbo yako nimeposti ili nikupe hii meseji. Yani the only way na wewe ungeshine kipimdi hiki ilibidi fans wa Kiba wamwache Kiba waje kwako kitu ambacho ni kigumu.Inabidi uwe very strategic kwenye ku-release kazi zako. Hapa marekani wasaniii hawaachii kazi hovyo wanatumia akili kubwa mnoooooo katika kuachia ngoma. Timing ya kuachia kazi is almost as important as uzuri wa nyimbo. Kwa mfano Rihanna aachie ngoma kali hutokaaa usikue after 2 days Beyonce nae anaachia ngoma. The problem ni kwamba wote wanataka Ngoma zao ziwe#1 kwenye billboard charts sasa mkiachia wote same time lazma mmoja awe 2. Na wasanii wakubwa kutokuwa #1 ni big deal mnoo. So inabidi uachie kazi muda ambao hakuna hit kubwaaaa ili uwe namba 1. Hata kama only for 1 week ila angalau uiguse number 1.Ona hata Jide kaachia ngoma kali ila watu kama hatujaiona sababu tupo busy na watu wawili. Jide angetulia akaachia ngoma baada ya wiki 3 hivi ange hit kinoma noma. Ila muda hakuuchagua vizuri. Timing is crucial.Alafu huku wasaniii wanatangaza hadharani tarehe gani ataachia ngoma. Kwahiyo kila mtu anakuwa anasubiria. Drake hawezi kutangaza anaachia ngoma tarehe flani alafu Chris Brown akamvizia ile kaachia tu na yeye kesho akaachia. Mmoja wao ana risk kuwa namba 2 kwenye billboard charts. Mara chache mnoooooooo msaniii mkubwa anaachia ngoma by surprise. Na hata akichia kwa surprise ana hakikisha hakuna ngoma iliyoshika attention za watu.Kuna kazi ngumu sana inabidi ifanyike ya kuua team Dai na Team Kiba hizi team zinauwa wasaniii wengine. Inabidi tusapoti wasanii woteNa hiyo Kazi inabidi ianzie kwetu sisi vigagula. Ila na wasanii nao wapeane muda wakuachia kazi ili wote wapate attention kubwa, wasigawe mashabiki kwa wote kuachia kazi same time.
Majina ya waliopitishwa kugombea TFF kuwekwa hadharani leo
MCHAKATO wa uchaguzi kwa sasa bado unaendelea ambapo leo majina ya waliopenya hatua ya kugombea nafasi ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) inatarajiwa kuwa hadharani
Kwa mujibu wa kalenda ya matukio ya uchaguzi wa TFF Juni 25-27 ni siku za kufanya usaili wa wagombea ambao walipita kwenye mchujo wa awali na zoezi hilo lilifanywa na Kamati ya Uchaguzi na wagombea wenyewe.
Jana Juni 27 ilikuwa siku ya mwisho kukamilisha mchakato huo na leo Juni 28 itakuwa ni siku ya kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usaili na itafanywa na Kamati ya Uchaguzi TFF.
Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 8 ikiwa chini ya Kimoni Kibamba ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi.
Kwa upande wa nafasi ya Urais ni wagombea watatu walipitishwa kwenye mchujo wa awali ambao ni Evans G Mgeusa, Hawa Mniga na Wallace Karia ambaye anatetea kiti chake. Huku kwa upande wa wajumbe wakiwa ni 17 katika kanda 6.
Makamu Mwenyekiti wa Uchaguzi wa TFF, Benjamin Kalume alisema kuwa watasimamia haki katika uchaguzi huo kwa mujibu wa kanuni.
Source
Burna Boy Ashinda Tuzo Ya BET 2021 katika kipengele cha Best International Act
Msanii Burna Boy kutokea nchini Nigeria leo Juni 28, 2021 amefanikiwa kushinda tuzo ya BET kupitia kipengele cha BEST INTERNATIONAL ACT 2021.
Ushindi wa msanii huyo kutoka Nigeria, unamfanya awabwage washindani wake waliokuwa wakichuna katika kipengele hicho akiwemo Diamond Platnumz na Wizkid kutoka nchini Nigeria.
Wengine waliokuwa katika kipengele hicho ni Aya Nakamura (Ufaransa),Emicida (Brazili), Headie One (Marekani) Young T & Bugsey (Marekani) na Youssoupha (Ufaransa)
MSANII BURNA BOY KUTOKA NIGERIA ASHINDA TUZO YA BET 2021.. DIAMOND PLATNUMZ AKOSA

Source
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...






