Saturday, May 29, 2021

Dulla Makabila afunga ndoa

 


Staa wa muziki wa singeli nchini, msanii Dulla Makabila siku ya Alhamisi, Mei 27, alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Bi. Rahma Waziri, maeneo ya Kawe Beach, Jijini Dar es salaam.

Harusi ya wawili hao ilirushwa Live kupitia BONA Tv ambapo pia walifanyiwa mahojiano na kituo hicho.

Rahma Waziri ambaye ndiye mke wa Dulla Makabila alielezea kwamba alimjua #Dulla miaka 8 iliyopita na uhusiano wao umekuwa wa kuachana na kurudiana mara nying hadi sasa walipoamua kuwa mke na mume.

Rahma alijitambulisha kuwa ni mhudumu wa afya (Nesi) ambaye anaishi na kufanya kazi Marekani na alirejea hapa nchini yapata siku tano zilizopita kwa ajili ya harusi hiyo.

Alipoulizwa ikiwa atamkubalia Dulla Makabila (mume wake) aoe mke wa pili, #Rahma alisema hilo halipo na tayari wameshajadili kuhusu hilo.

Dulla naye alisema watasikilizana na kupanga namna gani watakuwa wanatembeleana kabla ya kuamua pa kuishi kabisa kama ni Tanzania au Marekani.

Sanjali na hilo, Dulla Makabila alilalamika kuhusu wasanii ambao walikausha kutoa michango kwa ajli ya harusi yake, akisema kuwa ameshawatungia nyimbo na ataitoa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Dulla Makabila, wasanii hao hawakuamini kwamba anaoa kweli ila walidhania anachangisha tu pesa kwa sababu nyingine akisingizia ndoa.


Friday, May 28, 2021

MANGE amchana DIAMOND "Unataka FORBES wakuweke na umepanga, wanao wanavaa vitu vya China, huna hela"


MANGE amchana DIAMOND "Unataka FORBES wakuweke na umepanga, wanao wanavaa vitu vya China, huna hela"


Mangekimambi Ameandika haya:

Well deserved 👏👏👏. Kwa kuangalia ile listi , BET watawapa wanaigeria sababu wana ushawishi mkubwa ila kwa huu mwaka uliokwisha Diamond ana deserve kushinda hii tuzo and this is coming from a committed Diamond hater (me).


Alafu kuhusu Forbes mdogo angu kwa upande wa Africa sometimes wanaangalia na lifestyle.Wale wasanii waliowekwa juu ukiangalia tu social media zao unaona lifestyle wanaozoishi,musician wa Nigeria humkuti na gari ya Japan.Wako Nama-G-wagon,Ma Rollys Royce wako na Maserati mpaka wanaziimba(Girl hop in my Maserati) kutwa wako na designer things, mijengo yao ni ya balaa alafu sio ya kupanga.Sasa wewe mtu akiangalia insta yako tu lifestyle anaona kabisa huna hela ndefu.Wanawake zako hata siku moja sijawahi ona unawaingiza Chanel au LV kuwafanyia shopping,wanao wenyewe wakivaa Gucci basi ni Gucci za MunaLove, kweli watoto wa tajiri anaestahili kuwa kwenye list ya Forbes watavalishwa Gucci za China? Davido alikuwa anamfanyia shopping Chioma huko Gucci, Chanel na akamnunulia bonge la Porsche, wanawake dunia nzima walikuwa wanaona wivu lifestyle Davido aliyompa Chioma.Sasa wewe mdogo wangu ukihonga demu ni gari ya Japan, tena sio ya maana, tena used, miles zimezidi laki,tena sometimes unamtapeli hata hiyo gari ya Japan humpi kweli kama ulivyofanya kwa Tanasha. Sasa waangalie wale wanaigeria, akihonga demu gari ni gari kweli kila mtu anakaa chini. Sasa mdogo wangu wewe mwenyewe tu huna gari ya kufanya watu waumie vichwa kama gari wanazoendesha wenzio.Mpaka leo unavaaga raba za FILA wale kina WizKid hata umlipe dola laki havai FILA.

Kina Davido nyimbo zao tu wanaimba kitajiri, utaskia Gucci, Prada, Chanel. Wewe hudhubutu hata kutaja hizo kwenye nyimbo zako. Na unaogopa kutaja maana unajua hapo ni parefu, ndo unabakigi kusema 'Aga'.

Sisemi kwamba uchezee pesa zako au ujibane ili ufanye hayo niliyoyasema ila najaribu kuku explainia why Forbes wameku-diss.Na Forbes hata wakisema wafatilie wasafi FM and TV wanakuta mtu mwingine ndo mmiliki mkuu.

Jeuri yako ya pesa bado haijaonekana, Ila jeuri ya kujisifia una pesa kwa mdomo ndo unayo mdogo wangu. Ila usivunjuke moyo, kwa standard za kibongo we ni tajiri, maana TZ ukiwa na VX tu au X6 we ni milionea.



Lamine Moro afunguka kuhusu sakata lake ndani ya Yanga

 


Kufuatia sakata lake la kudaiwa kufanya utovu wa nudhamu dhidi ya kocha Nasreddine Nabi, nahodha wa kikosi cha Yanga Lamine Moro ameibuka na kufungukia kuwa hausiki na tuhuma hizo.

Lamine wiki iliyopita aliondolewa kikosini kwenye kambi ya Yanga iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, kutokana na madai ya utovu wa nidhamu.

Akizungumzia kuhusu sakata hilo, Lamine amesema: "Mimi si mtovu wa nidhamu kama inavyoelezwa, kabla hatujasafiri kwenda Mtwara nilipata majeraja ambayo benchi la ufundi walilifahamu.

"Kocha aliuliza madaktari kwa nini sifanyi mazoezi, akaambiwa kuhusu majeraha yangu, lakini alisisitiza kwamba nilitakiwa kufanya mazoezi, nikamweleza kuhusu hali yangu lakini alionyesha kutoniamini, kiasi cha kupimwa kwa mara nyingine na ikathibitika kuwa nina majeraha, lakini baadaye nilirudishwa Dar."

CCM Yalaani alichokifanya Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa UWT mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige, baada ya kwenda kuvunja geti na kuingia kwenye makaburi ya familia mahali ambapo amezikwa Kuzula Madoda anayedaiwa kuwa mchumba wake.

Taarifa ya kulaani kitendo hicho imetolewa leo Mei 28, 2021, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, na kusema kuwa CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa Katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM," imeeleza taarifa hiyo.

Haya yote yanajiri baada ya video kusambaa mitandaoni zikimuonesha Mbunge huyo pamoja na watu wengine wakitumia nguvu kushiriki katika mazishi ya mfanyabishara huyo mkoani Arusha




Kampuni Nike Yamtema Neymar





KAMPUNI kubwa ya mavazi nchini Marekani Nike inasema iliacha kufanya kazi na mwanasoka wa Brazil Neymar kwa sababu "alikataa kushirikiana katika uchunguzi kwa nia njema " juu ya madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mfanyakazi.

 

Tukio hilo linalodaiwa lilitokea mnamo 2016 na liliripotiwa kwa Nike mnamo 2018. Nike alisema uchunguzi wake haukuwa wa kweli. Msemaji wa Neymar alisema alikataa unyanyasaji wa kijinsia na akajitenga na Nike mwaka jana kwa sababu za kibiashara.

 

"Neymar Jr atajitetea kwa nguvu dhidi ya mashambulio haya ya msingi ikiwa madai yoyote yatatolewa, ambayo hayakutokea hadi sasa," aliiambia gazeti la Wall Street Journal (WSJ), ambalo liliripoti habari hiyo kwanza.

 

Nike iliachana na Neymar mnamo Agosti 2020, na kumaliza moja ya mikataba yake ya udhamini wa hali ya juu. Kampuni hiyo haikutoa sababu ya kutengana naye wakati huo.



Katika taarifa yake Alhamisi, ilisema: "Haitakuwa sahihi kwa Nike kutoa taarifa ya mashtaka bila kuweza kutoa ushahidi wa kuunga mkono."

 

Lakini iliongeza: "Nike ilimaliza uhusiano wake na mchezaji huyo kwa sababu alikataa kushirikiana katika uchunguzi kwa nia njema kuhusu madai ya kumdhulumu mfanyakazi."

 

Nike alisema mfanyakazi huyo aliripoti madai hayo mnamo 2018 lakini mwanzoni alitaka kuepusha uchunguzi na kuiweka siri. Ilisema iliagiza uchunguzi huru juu ya suala hilo mwaka uliofuata, wakati alipoonyesha nia ya kuifuata.

 

Mtuhumiwa hajatajwa, Nike akisema: "Tunaendelea kuheshimu usiri wa mfanyakazi na pia tunatambua kuwa hii imekuwa hali ngumu kwake."

 

Neymar kwa sasa anachezea timu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain. Hapo awali alikanusha mashtaka ya ubakaji mnamo 2019, katika kesi ambayo mwishowe ilifutwa.

 

WAZIRI UMMY AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WANNE UBADHIRIFU UJENZI MACHINJIO MANISPAA YA SHINYANGA


 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu akiwa kwenye ujenzi wa mradi wa machinjio ya kisasa Shinyanga.

Na Mwandishi wa  Malunde 1 blog

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi wiki mbili watumishi Wanne wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupisha uchunguzi tuhuma za ubadhirifu ujenzi wa machinjio ya mifugo ya kisasa.

Watumishi waliosimamishwa kazi ni Mchumi Gwakisa Mwakyeba, Mkuu wa idara ya Mifugo Tito Kagize, Mhandisi wa ujenzi Kassim Thadei, pamoja na Mkuu wa Idara ya manunuzi Godfrey Mwangairo.

Waziri Ummy akizungumza leo kwenye ujenzi wa mradi wa machinjio hiyo ya mifugo ya kisasa, mara baada ya kupewa taarifa na Mkurugenzi wa Manispaa  ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi na kuonekana kuna ubadhirifu wa fedha, ndipo akaamua kuwasimamisha kazi watumishi hao ili kupisha uchunguzi.

Alisema Taarifa za mradi huo anazo kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuwa kuna ubadhirifu wa fedha kwenye machinjio hiyo, hivyo anashangaa watu ambao waliohusika kutochukuliwa hatua.

"Mkurugenzi wewe ni mteule wa Rais hivyo sitakugusa kwenye suala hili, saizi yangu ni hawa watumishi, hivyo kuanzia sasa nawasimamisha kazi wiki mbili ili kupisha uchunguzi juu ya ubadhirifu wa ujenzi wa machinjio hii ya kisasa," alisema Mwalimu.

"Kuna watumishi wengine najua wameshahamishwa hapa Shinyanga, hivyo naagiza waletwe hapa ili kujibu tuhuma za  ubadhirifu wa ujenzi wa machinjio hii ya mifugo ya kisasa, pamoja na Wakandarasi wachukuliwe hatua,"aliongeza.

Aidha alisema gharama za ujenzi wa machinjio hiyo anazifahamu ni Sh. bilioni 5.7 na zimeshatumika bilioni 5.1 na kuhoji juu ya Sh. milioni 600 mahali zilipo, huku mradi huo ukiwa bado haujakamilika na kutakiwa tena kuongezwa Sh. Milioni 172 kutoka kwenye mapato ya ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Godfrey Mwangulumbi, akitoa taarifa ya ujenzi wa machinjio hiyo, alisema gharama za mradi huo awali ilikuwa ni Sh. bilioni 5.9, lakini zikapungua hadi Sh. bilioni 5.5 na zimeshatumika Bilio 5.1 huku akibainisha fedha Milioni 600 zipo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati, alisema suala la watumishi hao atalifanyia kazi na watatoa taarifa ndani ya wiki mbili ambazo zimetolewa.

List Ya Wasanii Waliotajwa Kuwania Tuzo za BET 2021




TUZO za BET 2021 zinazotoa heshima kwa wasanii mbalimbali Wamarekani wenye asili ya Afrika na Wamarekani wengine wenye asili za pembeni (Black Entertainment Television – BET).

Usiku wa kuamki leo Mei 28, 2019 wametoa orodha ya wasanii wanaowania tuzo hizo na washindi watatangazwa Jumapili ya Juni 27, 2021.



Album of the year:

After Hours – The Weeknd
Blame It on Baby – DaBaby
Good News – Megan Thee Stallion
Heaux Tales – Jazmine Sullivan
King's Disease – Nas
Ungodly Hour – Chloe X Halle

 

Best female R&B / pop artist:

Beyoncé
H.E.R.
Jazmine Sullivan
Jhené Aiko
Summer Walker
SZA

 

Best male R&B / pop artist:

6lack
Anderson .Paak
Chris Brown
Giveon
Tank
The Weeknd

 

Best female hip hop artist:

Cardi B
Coi Leray
Doja Cat
Megan Thee Stallion
Latto
Saweetie

 

Best male hip hop artist:

DaBaby
Drake
J. Cole
Jack Harlow
Lil Baby
Pop Smoke

 

Best new artist:

Coi Leray
Flo Milli
Giveon
Jack Harlow
Latto
Pooh Shiesty

 

Best collaboration:

Cardi B featuring Megan Thee Stallion – "WAP"
DaBaby featuring Roddy Ricch – "Rockstar"
DJ Khaled featuring Drake – "Popstar"
Jack Harlow featuring DaBaby, Tory Lanez & Lil Wayne – "Whats Poppin (Remix)"
Megan Thee Stallion featuring DaBaby – "Cry Baby"
Pop Smoke featuring Lil Baby & DaBaby – "For the Night"

 

Best group:

21 Savage & Metro Boomin
Chloe X Halle
Chris Brown & Young Thug
City Girls
Migos
Silk Sonic

 

Dr. Bobby Jones best gospel/inspirational award:

Bebe Winans – "In Jesus Name"
CeCe Winans – "Never Lost"
H.E.R. – "Hold Us Together"
Kirk Franklin – "Strong God"
Marvin Sapp – "Thank You for It All"
Tamela Mann – "Touch From You"

 

BET HER award:

Alicia Keys featuring Khalid – "So Done"
Brandy featuring Chance the Rapper – "Baby Mama"
Bri Steves – "Anti Queen"
Chloe X Halle – "Baby Girl"
Ciara featuring Ester Dean – "Rooted"
SZA – "Good Days"

 

Viewer's choice award:

Cardi B featuring Megan Thee Stallion – "WAP"
Chris Brown & Young Thug – "Go Crazy"
DaBaby featuring Roddy Ricch – "Rockstar"
DJ Khaled featuring Drake – "Popstar"
Drake featuring Lil Durk – "Laugh Now Cry Later"
Lil Baby – "The Bigger Picture"
Megan Thee Stallion featuring Beyoncé – "Savage (Remix)"
Silk Sonic – "Leave the Door Open"

 

Video of the year:

Cardi B – "Up"
Cardi B featuring Megan Thee Stallion – "WAP"
Chloe X Halle – "Do It"
Chris Brown & Young Thug – "Go Crazy"
Drake featuring Lil Durk – "Laugh Now Cry Later"
Silk Sonic – "Leave the Door Open"

 

Video director of the year:

Benny Boom
Bruno Mars & Florent Déchard
Cole Bennett
Colin Tilley
Dave Meyers
Hype Williams

 

Best international act:

Aya Nakamura (France)
Burna Boy (Nigeria)
Diamond Platnumz (Tanzania)
Emicida (Brazil)
Headie One (Uk)
Wizkid (Nigeria)
Young T & Bugsey (Uk)
Youssoupha (France)

 

Best movie:

Coming 2 America
Judas and the Black Messiah
Ma Rainey's Black Bottom
One Night in Miami
Soul
The United States Vs. Billie Holiday

 

Best actress:

Andra Day
Angela Bassett
Issa Rae
Jurnee Smollett
Viola Davis
Zendaya

 

Best actor:

Aldis Hodge
Chadwick Boseman
Damson Idris
Daniel Kaluuya
Eddie Murphy
Lakeith Stanfield

 

Youngstars award:

Alex R. Hibbert
Ethan Hutchison
Lonnie Chavis
Marsai Martin
Michael Epps
Storm Reid

 

Sportswoman of the year award:

A'ja Wilson
Candace Parker
Claressa Shields
Naomi Osaka
Serena Williams
Skylar Diggins-Smith

 

Sportsman of the year award:

Kyrie Irving
Lebron James
Patrick Mahomes
Russell Westbrook
Russell Wilson
Stephen Curry


SHINDANO LA MISS KAHAMA 2021 KUFANYIKA JUNE 6...WAREMBO 12 KUCHUANA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners , Peter Frank Alex akizungumzia kuhusu maandalizi ya Shindano la Miss Kahama 2021. Kushoto ni Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata.

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shindano la Urembo kutafuta mlimbwende wa Kahama 'Miss Kahama 2021' yanatarajia kufanika June 6,2021 katika ukumbi wa African Lounge Mjini Kahama yakishirikisha warembo 12 huku Msanii Mr. Blue akinogesha mashindano hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Mei 28,2021, Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners ambao ni waandaaji wa Shindano la Urembo la Miss Kahama, Peter Frank Alex amesema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika.

Amesema shindano la Miss Kahama litafanyika June 6, 2021 African Lounge. Washiriki wapo 12 ambao ni mabinti warembo kutoka Kahama ambao sasa wapo kambini wanaendelea na mazoezi.

"Maandalizi ya shindano la Miss Kahama ni makubwa hivyo wananchi wategemee mambo makubwa siku hiyo kuanzia saa moja usiku. Tiketi zinaendelea kutolewa maeneo mbalimbali ikiwemo Huheso FM kwa Zakazi, BSL College, African Lounge na tunasambaza mtaa kwa mtaa na siku ya shindano tiketi zitapatikana getini",amesema.

"Sisi kama waandaaji wa Miss Kahama tumekaa na Waandaaji Wakuu wa Miss Tanzania na tumepewa taratibu na vigezo mbalimbali hivyo. zile sintofahamu ambazo zilikuwa zinaendelea mtandaoni tumeshazirekebisha hivyo Shindano la Miss Kahama lipo kama kawaida tarehe 6 Mwezi wa Sita",ameongeza Alex.

Ameeleza kuwa wameandaa zawadi na fursa mbalimbali kwa washiriki wa shindano la Miss Kahama ambazo zitawasaidia katika maisha yao huku akiwaomba wakazi wa Kahama na maeneo ya jirani kujitokeza kushuhudia shindano hilo.

Kwa upande wake Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata amesema mwaandaaji wa shindano la Miss Kahama amekamilisha taratibu zote hivyo ana Baraka zote za kuendesha shindano hilo June 6, 2021.

"Waandaji wa shindano la Miss Kahama wameshakamilisha taratibu zote zilizokuwa zinatakiwa hivyo Mkurugenzi wa Br.Black Social Partners ,Peter Frank Alex ni mtu rasmi kwa ajili ya kuandaa shindano hilo Kahama kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya watoto wa kike pamoja na vipaji vingine ndani ya Kahama",amesema Mwata.

"Mwenzetu ameweza kuandaa maandalizi ya Miss Kahama. Kwa hiyo mimi kama Mwakilishi wa Miss Tanzania Organisation napenda kuwataarifu kuwa tumemruhusu Mkurugenzi wa Br.Black Social Partners ,Peter Frank Alex kufanya shindano la Miss Kahama kama chini ya Miss wilaya na utaratibu mwingine utafuata wa kuandaa Miss Mkoa na Kanda kama alivyoelekezwa",amesema.

Amesema Taasisi ya Miss Tanzania inamchukulia Mkurugenzi wa Br.Black Social Partners ,Peter Frank Alex kama mdau anayeandaa kwa watoto kwa ajili ya kuonesha vipaji vyao katika jamii na kutumia kutangaza utalii na uwekezaji.
Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata akizungumzia shindano la Miss Kahama 2021. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners , Peter Frank Alex ambaye ni Mwandaaji wa Shindano la Miss Kahama 2021.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners , Peter Frank Alex akizungumzia kuhusu maandalizi ya Shindano la Miss Kahama 2021.Kushoto ni Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

RC MALIMA AWATUMIA SALAMU WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU, WANAOPITISHA DAWA ZA KULEVYA AWAAMBIA WASIJARIBU

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari



MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amewatumia salamu mawakala wa wahamiaji haramu ambao wanatumia mkoa huo kuwapitisha na wale wanaopitisha dawa za kulevya kwamba wasijaribu kufanya hivyo maana watakachokutana nacho kitakuwa historia kwao.

RC Malima aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga ambapo alisema mkoa huo hautakuwa dezo ya kupitisha wahamiaji haramu na kama kuna watu wanadhani anatania wafanye hivyo waone watakumbana na jambo gani.

Alisema kwamba mkoa huo hautakuwa sehemu ya watu kupitisha mauzauza yao na wasijaribu kutokana na kwamba wamejipanga vilivyo kuhakikisha vitendo vya namna hiyo havifanyika kwenye mkoa huo huku akitoa onyo kwa wanaodhani wanaweza kujaribu.

"Ndani ya wiki mbili wahamiaji haramu wameongezeka naomba wasiufanye mkoa wa Tanga kuwa ni dezo ya wao kupitia na niwaambie kwamba Tanga hautakuwa mkoa wa kupitisha mauzauza yao na hata wale ambao wanafikiria kwamba wanaweza kupitisha dawa za kulevya wasijaribu zari kwani tumejipanga kuwashughulikia"Alisema

Alisema wahamiaji haramu hao wanapitia mkoa wa Tanga kwenda mikoa ya Pwani ,Dar,Bagamoyo kwa hiyo aliwataka waandishi wa habari kufikisha salama kwa wananchi kwa wale wanaojua wazi kwamba watu wanao wanashirikiana kwenye kusafirisha binadamu wanaowatoa mkinga wanawasafarisha usiku kwa usiku.

"Hao watu ambao wanao wanashiriikiana kusafrisha binadamu wanawatoa wilaya ya Mkinga kuwasafirisha usiku kwa usiku  wengine wanapita Korogwe wanatoka Kilindi wanachana Korogwe hadi Handeni wanapitia Mkata wanaingia Pwani wengine wanatokea Mvomero pia eneo la Gairo hilo ni tatizo kubwa na hawawezi kufanikiwa kama hawana watu ambao wana shirikishiana nao"Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka waandishi wa habari mkoa wa Tanga wafikishe ujumbe kwamba wale wanaotumika kuwasafirisha huenda dhambi ya kusafirisha ni kubwa sana kuliko kusafirishwa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...