Tuesday, March 30, 2021

Faida za kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako




Biashara nyingi hutumia njia na mbinu mbalimbali kujitangaza ili kuongeza ufahamu wa biashara zao kwa wateja, kuongeza na kupanua solo la bidhaa zao lakini kubwa zaidi kukuza mapato ya biashara husika. Na moja ya njia hizo ni matumizi ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuitangaza biashara yako. 

Asilimia 90 ya wataalamu wa masoko wanakiri kuwa mitandao ya kijamii ina nguvu sana katika kutangaza biashara na imekuwa ikionesha matokeo chanya katika biashara zao. Baadhi ya mitandao ya kijamii inayotumika sana katika matangazo ya biashara ni kama Facebook, Instagram, Twitter, Blogs, youtube, linkedin, n.k 

Mitandao ya kijamii sasa imekuwa nguzo muhimu sana kama moja ya mikakati inayotumika ya kutangaza biashara na biashara zisizotumia  mitandao ya kijamii inakosa fursa muhimu na makini sana katika kupanua masoko ya biashara zao. 


Faida za kutumia  mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako; 

Inachangia kufahamika zaidi kwa biashara yako. 
Mitandao ya kijamii ni moja ya njia za kutangaza biashara yako kwa gharama nafuu zaidi na inauhakika wa kuwafikia wateja wengi zaidi, kwani asilimia kubwa ya watu wengi sasa hivi wanatumia muda mwingi sana  katika mitandao ya kijamii hivyo kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako kutakuongezea idadi ya wateja na watu wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara yako kwa ujumla. 

Inapanua wigo wa kupata wateja wapya tofauti na wale wanaokuzunguka 
Kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutangaza biashara yako  kunakuongezea wigo wa wateja wapya ambao ni vigumu kufahamu kuhusu biashara yako kwani wako mbali na eneo  la biashara husika lakini mitandao ya kijamii inakupatia nafasi ya watu wote watakao kutuna na tangazo la biashara yako kuifahamu na kushawishika kutumia  bidhaa zao na hivyo kugeuka wateja wa biashara yako. 

Inajenga uhusiano wa karibu na wateja wako. 
Kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara yako na wateja wako hii inasaidia kuweka ukaribu wa kusikiliza maoni, shida na kutafuta ufumbuzi kiurahisi wa kero za wateja wako kwani kwa urahisi kabisa wanaweza kuwasilisha maoni yao kupitia akaunti za biashara yako  za mitandao ya kijamii. 

Inaongeza imani na uaminifu wa watu kwenye biashara yako. 
Moja ya malengo ya kila biashara ni kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa bidhaa za biashara hiyo, hivyo mitandao ya kijamii kupitia ukaribu unaojengeka baina ya biashara na wateja wake na urahisi wa taarifa za biashara yako kumfikia mteja inapelekea kutengeneza wateja waaminifu na wakudumu wa biashara yako. 

Inasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako. 
Biashara nyingi hutumia fedha nyingi sana kwa ajili ya kujitangaza na hili huonekana. Pale ambapo njia zinazotumika kutangaza biashara husika zinakuwa ni ghali sana na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa biashara husika hivyo kupitia matumizi ya mitandao ya kijamii kama njia ya kujitangaza inapunguza gharama hizo za kujitangaza na kupelekea kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara husika na kuipatia biashara nafasi nzuri ya kifedha kuikuza zaidi. 

Inaongeza ufahamu wa kutosha dhidi ya soko husika na wateja wako 
Kupitia ukaribu unaojengekana wateja wako katika mitandao ya kijamii na kujibkujibu comments za wateja wako katika mitandao ya kijamii hii inapelekea biashara husika kupata taarifa za kutosha za soko husika na kuipa nafasi biashara kuwa na taarifa za kutosha za wateja wake na hii inasaidia biashara kufanya maamuzi na kuweka mikakati inayohitajika kwa wakti husika na solo husika. 

Hizo ni baadhi ya faida za kutumia mitandao ya kijamii  kuitangaza biashara yako na Kama bado hujaanza kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako ni vema ukaanza sasa kwani unapitwa na mengi ambayo biashara yako ingenufaika kwa kutumia mitandao ya kijamii. 

Bunge La Bajeti Kuanza Leo Jijini Dodoma....Tazama Ratiba Hapa

 Mkutano wa Tatu wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaanza leo  jijini Dodoma.


Pamoja na mambo.mengine, mkutano huo utajadili na kupitisha bajeti za wizara mbalimbali pamoja na bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Mkutano  huo unaanza katika kipindi hiki ambacho Taifa lipo kwenye siku 21 za maombolezo, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli.


Monday, March 29, 2021

UVCCM walivyoomba radhi vijana na kuahidi ushirikiano kwa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan



Akiongea na wana habari jana jijini Dodoma Mwenyekiti UVCCM KHERI JAMES amesema haya:

"kama kuna jambo huko nyuma ambalo kwa maneno au vitendo litatumika kama rejea ya kuzuia dhamira ya Rais wetu sisi tunasema tunaomba radhi na tupo tayari kushirikiana na Rais wetu"

BABU AOA MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA KWA MAHARI YA NG'OMBE WAWILI


Katika tukio la kushangaza, mzee mwenye umri wa miaka 52 anadaiwa kumuoa mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Bugire iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Vyanzo vyetu vya uhakika kutoka Rorya vimeeleza hivi karibuni kuwa msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 ameolewa na mwanaume huyo mwaka jana (2020) akiwa darasa la sita.

"Ina maana Januari mwaka huu (2021) huyu mwanafunzi huyo angekuwa darasa la saba," kimeeleza chanzo chetu kutoka serikalini.

Taarifa zaidi zilizoifikia Mara Online News zinasema mwanaume huyo ametiwa mbaroni hivi karibuni na msichana huyo amerejeshwa kwa wanafamilia.

"Mzee aliyehusika kumuoa huyo mwanafunzi amekamatwa pamoja na mzazi wa msichana - aliyepokea ng'ombe wawili kama mahari wamekamatwa," kimesema chanzo chetu.

Taarifa hizo zinadai kuwa mwanafunzi huyo ameolewa kuwa mke wa tatu wa mwanaume huyo.

"Kwa sasa anahitaji msaada hata wa kisaikolojia," amesema ofisa wa serikali wilayani Rorya.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bugire, Jackson Nyangubo amezungumza na Mara Online News na kuthibitisha tukio la kuolewa kwa mwanafunzi wake huyo.

"Ni kweli huyo msichana ni mwanfunzi wa shule yangu na watuhumiwa [muoaji na mzazi] tayari wametiwa mbaroni," amesema Mwalimu Nyangubo.

Serikali yatangaza tahasusi ‘combinations’ mpya


Serikali imetangaza kuanza kwa tahasusi (Combination) mpya tano kwa ajili ya wanafunzi watakaoingia kidato cha tano mwaka 2021.

Lengo la kuongeza tahasusi hizo ni kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo leo Jumatatu Machi 29, 2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Tahasusi hizo ni  Physics, Mathematics, Computer Studies (PMC); Kiswahili, French ,Chinese  (KFC); Kiswahili, English, Chinese (KEC); Physical Education, Biology, Fine Art (PBF) na Physical Education, Geography, Economics (PGE).

Jafo amesema tahsusi ya PMC itatolewa katika shule ya sekondari ya  Dodoma ambayo itakuwa maalumu kwa wasichana ambapo kwa wavulana itakuwa sekondari ya wavulana ya Iyunga.

Amesema tahsusi ya  KFC na KEC itatolewa katika shule ya sekondari ya wasichana Morogoro na ya wavulana Usagara wakati PBF na PGE  itatolewa shule ya sekondari ya wasichana ya Makambako, shule ya sekondari ya wavulana Kibiti na sekondari ya Mpwapwa ambayo ni ya mchanganyiko.



Source

KAMPUNI YA UDALALI YA YONO AUCTION MART YASEMA INA IMANI KUBWA NA RAIS SAMIA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart' Scholastika  Kavela.
***

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart' Scholastika  Kavela amesema wana imani kubwa ya utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan na kuwataka Watanzania kumuunga mkono kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake wa kiti hicho Hayati Dk. John Magufuli.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kevala alisema   hana mashaka na utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mchapakazi wa kweli na kwamba yeye na kampuni yake wataendelea kusimama pamoja naye wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake.

"Kwanza kabisa tunampa pole kwa msiba wa mtangulizi wake sote tukiamini kuwa hayo yote ni mapenzi ya Mungu ...nasi tumepokea kwa masikitiko kama ilivyo kwa watanzania wote na ulimwengu kwa ujumla" alisema Kevela 

Alisema  watanzania kwa wanaamini chini ya uongozi wa Mama Samia Tanzania itazidi kupiga hatua za kimaendeleo huku akiwataka wasaidizi wake wa ngazi zote kumuunga mkono.

Alisema  endapo watendaji hao waliopo chini yake watatimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ni wazi watakuwa nguzo nzuri kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa hili.

Alisema nyota njema huonekana tangu asubuhi na kwamba hata utendaji wa kazi wa Rais ulionekana tangu akiwa na nyadhifa zingine ndani ya Serikali tofauti na hiyo ya ngazi ya juu aliyonayo hivi sasa.

"Rais alishajipambanua katika utawala ndani miaka mingi, ameshashika nafasi za juu katika Serikali ikiwemo ya Makamu wa Rais, Waziri katika Serikali ya awamu ya nne na hata Makamu  Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, uzoefu wake unamtosha kuliongoza Taifa hili", alisisitiza Kevela.

Alisema hatua ya yeye kuwa Rais wa Taifa hili kwa kiasi kikubwa kumeweza kuionyesha Dunia na ulimwengu mzima kuwa Tanzania ni nchi isiyokumbatia masuala ya mfumo dume unaotoa fursa kwa jinsia moja kushika nyadhifa ya juu ya uongozi. 

Alisema hatua hiyo pamoja na kupokelewa vyema na wananchi wote zaidi kumewaheshimisha wanawake nchini na dunia nzima na kumuona kama mfano kwao katika jitihada za kujiletea maendeleo.

"Tunamuombea kwa Mungu aweze kumpa ulinzi wa kutosha na afya njema wakati wote ili aweze kutekeleza ipasavyo majukumu ya  kututumikia wananchi wake", alisema  Kevela.

Alisema Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan  ipo katika mikono salama na zaidi akawaoamba wananchi kumuunga mkono kwa kuchapa kazi bila kuchoka ili kulisukuma mbele Taifa la Tanzania. 


CAF yatupilia mbali malalamiko ya Corona ya Al Merreikh dhidi ya Simba




Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetupilia mbali malalamiko ya klabu ya Al Merreikh kuhusu kufanyiwa hujuma na Simba SC juu ya vipimo vya Covid-19 kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wa kundi A, uliopigwa Machi 16, 2021 kwenye uwanja wa Mkapa.



Kabla ya mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliyopigwa uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wachezaji nane (8) wa Al Merrikh waligundulika na kuwa na viashiria vya Virusi vya Corona hali iliyopelekea kukkosa kucheza kwenye mechi hiyo dhidi ya wenyeji Simba SC.


Mwambusi Ashusha Presha ya Kocha Mpya Yanga





UONGOZI wa Yanga umesema kuwa uamuzi wa kumpa timu kocha wao Juma Mwambusi mpaka mwishoni mwa msimu, umepunguza presha kubwa waliyokuwa nayo katika mchakato wa kumtangaza kocha mpya atakayekuja kufundisha kikosi hicho.

 

Yanga ipo kwenye mchakato wa kumtangaza kocha mpya atakayekuja kuchukua nafasi ya kocha Mrundi, Cedric Kaze aliyetimuliwa Machi 7, mwaka huu, ambapo Mfaransa, Sebastian Migne anatajwa kuwa kwenye nafasi kubwa ya kutwaa mikoba hiyo.

 

Mpaka Ligi Kuu Bara inasimama kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa, Yanga imesalia kuwa vinara wa msimamo ambapo wamecheza mechi 23 na kukusanya pointi 50.Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alisema:

 

"Uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na kamati yake ya ufundi unaendelea na mchakato wa kufanya upembuzi wa wasifu (CV), za makocha ambao waliwasilisha maombi ya kazi kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa kocha wetu Cedric Kaze.



"Tunatarajia kuweka wazi jina la kocha mkuu hivi karibuni, lakini kabla ya kufikia maamuzi ya kumpa timu kocha Mwambusi, kama uongozi tulikuwa na presha kubwa sana ya kusaka kocha mpya ili kuziba nafasi ya Kaze.

 

"Lakini kwa sasa mchakato huo hauna presha kubwa kwa kuwa tuna imani kubwa na kocha Mwambusi, na ndiyo maana tumekubaliana kumpa timu mpaka mwishoni mwa msimu."

STORI: JOEL THOMAS,Dar es Salaam

 

Mjue Frank Lentini, Aliyezaliwa Akiwa na Miguu Mitatu

 


Frank Lentini alizaliwa Mei 1889 Nchini #Italia na alifariki Septemba 1966 akiwa Marekani. Aliishi maisha yake kama Mwanamaonesho akitumia umbo lake kama sehemu ya kazi hiyo


Frank ni moja kati ya Watoto waliotakiwa kuzaliwa pacha lakini pacha wake aliunganika naye kwa kile ambacho kisayansi kinaitwa 'Parasitic twin' ambapo alijikuta ameungana uti wa mgongo na pacha wake


Hali hiyo ilimfanya awe na miguu mitatu na sehemu mbili za siri, hali iliyoonesha kuwa pacha wake alikuwa Mwanaume. Alipozaliwa Wazazi wake walimuona ni laana na walimgawa kwa wengine waweze kumlea


Mbali na hali hiyo ambayo haikuwa kawaida, aliweza kuoa na kupata Watoto wanne

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...