Friday, February 26, 2021

NAIBU WAZIRI MARYPRISCA MAHUNDI : SERIKALI HAITAMVUMILIA MKANDARASI MZEMBE, TUTAMNYANG'ANYA MRADI


Serikali itawanyang'anya na haitowapa tena kazi ya kujenga miradi ya maji Wakandarasi wazembe walioshindwa kuitekeleza kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. 

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa tamko hilo Februari 25, 2021 wakati wa ziara yake kwenye mradi wa maji wa vijiji vya Buyagu, Kalangalala na Bototo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza. 

Tamko hilo amelitoa kufuatia taarifa ya utekelezaji na hali halisi aliyoishuhudia ya mradi huo ambapo alieleza kusikitishwa na Mkandarasi mzawa aliyekuwa akiutekeleza. 

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi, Meneja wa Wakala wa Maji vijijini (RUWASA) Sengerema, Mhandisi Cassian Wittike alisema ulikuwa ukitekelezwa na Mkandarasi mzawa Kampuni ya D4N Construction Limited ya Wilayani Kahama ambaye alishindwa kuukamilisha kwa mujibu wa mkataba wake. 

"Mradi huu ni miongoni mwa miradi tuliyorithi kutoka kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa mwaka 2019 na haukuwa umekamilika kutokana na uwezo mdogo wa mkandarasi," alieleza Wittike mbele ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi. 

Aidha Mhandisi Wittike alisema kwamba mradi ulianza kutekelezwa tangu Desemba 2013 na ulipaswa kukamilika Juni, 2014 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.7.

"Mkandarasi aliyepewa jukumu alishindwa na hivyo tuliuchukua na kuanza kutekelezwa na wataalam wa RUWASA Sengerema kuanzia mwaka 2019 na sasa hivi tupo kwenye majaribio na umeanza kutoa maji", alisema Mhandisi Wittike.

Kufuatia maelezo hayo na hali halisi ya mradi aliyoishuhudia, Naibu Waziri Mahundi alisisitiza kwamba Serikali haitamvumilia mkandarasi mzembe na badala yake atanyang'anywa mradi na atawekwa kwenye orodha ya wakandarasi ambao hawana sifa ya kukabidhiwa kutekeleza miradi ya maji kote nchini. 

"Mkandarasi atakayeshindwa kutekeleza mradi inavyopasa atanyang'anywa mara moja na hatapewa tena kazi nyingine, hapo ajue amejifuta na ameingia rasmi kwenye orodha ya wakandarasi wasiokuwa na sifa wala uwezo wa kujenga miradi ya maji nchini," alisisitiza Mhandisi Mahundi. 

Aliongeza kwamba hali ya uzembe wa baadhi ya wakandarasi hususani wazawa inamsikitisha Rais. Dkt. John Pombe Magufuli hasa ikizingatiwa kwamba dhamira yake ya kuwainua haileti tija iliyokusudiwa. 

"Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli anafarijika kuona wakandarasi wazawa wanapata kazi ya kujenga miradi lakini bahati mbaya baadhi yao kwa kukosa uzalendo wanamuangusha kwa kushindwa kutekeleza vyema miradi wanayokabidhiwa," alisema Naibu Waziri Mahundi. 

 Mahundi alisisitiza kwamba Serikali imeonya wakandarasi wote wenye tabia ya kutumia fedha wanazolipwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji  badala yake wanaipeleka kwenye masuala mengine yasiyohusiana na mradi. 

"Wakandarasi mnapaswa kutambua fedha mnayolipwa ni kwa ajili ya kujenga miradi na siyo kufanyia matumizi mengine sasa bahati mbaya huwa fedha hii mnaipeleka kwenye matumizi tofauti na hapa ni lazima mshindwe kutekeleza miradi kwa ubora uliokusudiwa," alisisitiza Naibu Waziri wa Maji.

Polisi kutofungua kesi za madai, ardhi

 


Jeshi la Polisi limesema kuanzia sasa hawatafungua kesi za migogoro ya ardhi na madai kufunguliwa kwenye vituo vya polisi bali jukumu hilo wataliacha kwa mahakama.


Uamuzi huo wa Jeshi la polisi unalenga kupunguza mrundikano wa mahabusu unaooyakabilia magereza mbalimbali hapa nchini Tanzania.


Uamuzi huo umetangazwa leo Ijumaa Februari 26, 2021 na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro ambaye amesema kwa kutumia njia hiyo wamefanikiwa kupunguza mrundikano wa wahalifu kwa asilimia 21.7.


Ameongeza kuwa njia nyingine ya kupunguza mrundikano wa mahabusu ni kuruhusu watuhumiwa kupewa dhamana kwa makosa  madogo madogo.


Amber Lulu ajitokeza hadhani kuonesha ujauzito wake kwa mara ya kwanza




Kwa mara ya kwanza msanii wa BongoFleva Amber Lulu amejitokeza hadharani kuonesha ujauzito wake kwenye 'Baby Shower' yake iliyofanyika maeneo ya Mikocheni ambayo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa kike.

Wakati yupo kwenye 'red carpet' anafanya mahojiano na waandishi wa habari, Amber Lulu amesema anafuraha sana kuelekea kuwa mama mpya mjini ila cha ajabu hamfahamu ni mwanaume gani aliyempa ujauzito huo

"Nijasikia vizuri kwa sababu naenda kuwa mama mpya mjini na kuna vitu vingi ambavyo vimebadilika na nahitaji kuvifanya, mimi mwenyewe baba wa mtoto simjui ila yupo na sio P Funk Majani, labda msubiri nikijifungua" amesema Amber Lulu


Mtoto huyu Mtanzania anayesoma chekechea awashangaza watu kwa uwezo wake wa Hesabu


Mtoto huyu Mtanzania anayesoma chekechea awashangaza watu kwa uwezo wake wa Hesabu

Hii ni video ambayo imekuwa viral sana mtandaoni inayomuonesha mtoto wa chekechea akijibu maswali magumu ya hesabu

VIDEO:

Thursday, February 25, 2021

KMC kushuka dimbani kesho michuano ya kombe la Shirikisho


Timu ya KMC kesho itakuwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho (ASFC)  dhidi ya Kurugenzi kutoka mkoani Simiyu mchezo utakaopigwa saa 16.00 jioni.

KMC FC inashuka Dimbani ikiwa imetoka kuifunga Timu ya Kagera Sugar magoli matatu kwa sifuri mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara na kwamba imejipanga kuhakikisha inaendeleza wimbi la ushindi katika mchezo huo.

Aidha katika mchezo huo, KMC inahitaji kupata ushindi kwa mara nyingine ambapo katika droo ya tatu ilishinda dhidi ya Lipuli magoli mawili kwa sifuri na kwamba imejipanga kuhakikisha inafanya vizuri katika mchezo huo wakesho wanapata matokeo mazuri ilikuendelea kujiimarisha kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kombe hilo.

 "Michuano hii ambayo tunashiriki ni sehemu ya malengo yetu ya kuhakikisha kwamba tunakwenda kuchukua kombe hilo kwasababu uwezo tunao, nia tunayo, na kikubwa katika mchezo wakesho tunaingia tukifahamu katika tunacheza na Timu ambayo inahitaji kupata ushindi hivyo tumejipanga vizuri.

Hata hivyo katika mchezo wa kesho pia utatumika kujiweka vizuri katika kuendelea kufanya vizuri kwa michezo ya ligi kuu ambapo KMC FC itakutana na Polis Tanzania Machi Nne katika uwanja wa Sheih Amri Abeid Jijini Arusha. 

Mwanasheria wa ROMA kumfungulia mashtaka BABA LEVO, Aahidi kumyoosha kwa sababu hii

 


Mwanasheria wa ROMA kumfungulia mashtaka BABA LEVO, Aahidi kumyoosha kwa sababu hii

VIDEO:

Shule 8 ikiwemo sekondari moja kunufaika na simenti ya naibu waziri mazingira.


Na Timothy Itembe Mara.

Shule za msingi 8 ikiwemo ya sekondari moja Mbogi za halmashauri ya wilaya Tarime mkoani Mara kunufaika na mifuko ya sementi iliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya makau wa Rais muungano na mazingira Mwita Mwikwabe Waita.


Akikabidhi mifuko hiyo katika shule mbalimbali kwa nyakati tofauti Waitara alisema kuwa kufanya hivyo ni kuhakikisha shule zinajengwa na kukamilika ili kuondolea wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakifuata masomo.


"Shule zinapokuwa karibu zinasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakutembea kufuata  masomo shule za mbali ikiwemo kupunguza mimba mashuleni kwa watoto wa kike"alisema Waitara.


Waitara aliongeza kusema kuwa kipindi cha uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais wake John Pombe Magufuli serikali imedhamiria kuwafikishia wananchi huduma karibu na kuwaondolea adha za mda mrefu kama vileAfya,Elimu,Maji na miundombinu ya barabara.


Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime vijijini,Simion Kiles aliwatupia lawama viongozi waliokuwa wakiuongoza halmashaurri hiyo kwa maana ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kuwa hawakufanya maendeleo pindi waliposhika halmashauri na kuiongoza.


Kiles aliongeza kusema madiwani pamoja na Mbunge wa Tarime vijijini wanapata wakati mgumu wakiulizwa mswala ya miradi iliyokwama kutekelezeka na wananchi kuendelea kuteseka pindi wapaokuwa wanahitaji huduma.


Akitoa mfano mbele ya Mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri na mkurugenzi Apoll Tindwa alisema kuwa kipindi kilichopita halmashauri ilikuwa inaongozwa na CHADEMA lakini miradi mingi imekwama kutekelezeka na wananchi wanaendelea kuteseka na kulaumu viongozi kama vile shule ya Magoto ambayo amechangia ujenzi wa darasa moja kwa nguvu zake mwenyewe.


Kwa upande wake diwani viti maalumu Tarafa Inchage,Rhobi Mwita Nyaihita alisema kuwa Mbunge kutoa mifuko ndani ya shule ya msingi Kihero iliyopo kata ya Nyarero kutasaidia kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo taklibani kilomita tano wakifuata masomo shule ya msingi Nyarero.


Nyaihita alitumia nafasi hiyo kushukuru serikali ya awamu ya tano na kuwataka wanajamii kwa ujumla kuunga juhudi za maendeleo serikali bila kutumia nguvu.


Akipokea mifuko na kukabidhi kwa shule husika mkuu wa wilaya Tarime Mtemi Msafiri alisema kuwa serikali imedhamiria kupunguza changamoto zilizopo kwa wananchi na milango iko wazi kwa yeyoye mwenye shida kufika Ofisini kwake ili kutekelezewa.


Msafiri aliongezakusema wananchi kwa ujumla wake wanatakiwa kuunga juhudi za maendeleo ndani ya maeneo yao bila kusukumwa na kuwa Chama cha mapinduzi kimejipanga kuoindoa kero kwa wananchi.


Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule ya msingi Kihero iliyopo kata ya Nyarero iliyopata mifuku ya sementi 60,Shule ya sekondari Mbogi mifuko 40,shule ya msingi kimusi mifuko 60 na Nyamiri shule ya msingi mifuko 60 nyingine ni shule ya msingi Iteremia mifuko 80,shule ya msingi Kewerumbe mifuko 80 na  shule ya msingi Keisaka mifuko 40

Picha : SERIKALI YASAINI MKATABA WA MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWENDA TINDE NA SHELUI...WAZIRI AWESO AONYA WATAKAOCHEZEA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja  Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakitia Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetia saini mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Shelui wilaya ya Iramba mkoani Singida utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi 12 ukigharimu Jumla ya shilingi Bilioni 24.4.

Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde na kushuhudiwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso na wananchi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga na Singida.

Mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga na Naibu Meneja  Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui,bwana Murali Mohan.

Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema mradi huo unaotarajiwa kutatua kero ya maji katika Miji ya Tinde na Shelui unatekelezwa kwa fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India kupitia Exim Bank India.

"Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kusukuma maji katika mji wa Tyeme kata ya Shelui,kulaza bomba kuu (Transmission main) lenye ukubwa kati ya milimita 400 na 300 kutoka bomba kuu kijiji cha Chembeli hadi Tinde lenye urefu wa kilomita 20.93 na bomba la ukubwa wa milimita 50 kwenye tanki la Didia lenye urefu wa kilomita 1.5",amesema Mhandisi Sanga.

"Shughuli nyingine ni kulaza bomba kuu lenye ukubwa wa kati ya milimita 350 na 200 kutoka bomba kuu linalokwenda Igunga katika kijiji cha Ipumbulya hadi Mgeta, Shelui lenye urefu wa kilomita 70.5,kujenga matanki ya kuhifadhia maji,ukaratabati wa matanki na kujenga vituo vya kuchotea maji",amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji , Jumaa Aweso amesema ujenzi wa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe alilotoa Januari 29,2021 alipopita Tinde na Shelui ambapo alitaka wananchi wa maeneo hayo wapewe huduma ya Maji kutoka Ziwa Victoria.

"Hili ni Jambo kubwa sana na tunamshukuru Mhe. Rais Magufuli. Nimuombe Mkandarasi anayejenga mradi huu kuhakikisha anafanya kazi kwa kuzingatia mkataba wa mradi na kuhakikisha anamaliza ndani ya miezi 12. Niwaambie tu kuwa hatutaongeza muda",amesema Aweso.

"Mkandarasi hakikisha unamaliza ujenzi kwa wakati kwa kuzingatia mkataba na fedha zitumike kama ilivyopangwa na ikiwezekana chenji ibaki",ameongeza.

Aidha amesema hatamvumilia mtu yeyote atakayethubutu kuhujumu mradi huo akiwataka wananchi kushirikiana na mkandarasi

 "Huu ni mradi wangu wa kwanza kusainiwa nikiwepo, Msichezee huu mradi, ukishiba chezea kitambi chako au kidevu chako. Mimi ni Waziri Kijana atakayezingua tutazinguana. Ninachotaka wananchi wapate maji safi na salama kwa gharama nafuu", amesisitiza Aweso.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko alimuomba Waziri wa Maji kuingiza kwenye bajeti za mradi kata za Nsalala, Usule na Bukene kwani zimerukwa katika mradi huo  ambapo Waziri Aweso alisema kata ya Nsalala pia itanufaika katika mradi huo wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tinde na Kiomboi.

Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuzipongeza mamlaka za maji SHUWASA na KASHWASA kwa kazi nzuri wanazofanya katika huduma za maji kwenye wilaya ya Shinyanga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Emmanuel Ruhahula amesema mradi huo wa maji utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha ya maji katika mji wa Shelui.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack amewataka wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo wa maji na kuhakikisha wanashiriki katika ujenzi wa mradi ili kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Magufuli kutatua changamoto ya maji katika mji wa Tinde akiomba pia kata zilizosahaulika ziingizwe kwenye mradi na kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa maji katika kata ya Mwakitolyo.

Nao wananchi wa Tinde akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal wamesema kukamilika kwa mradi wa maji katika mji wa Tinde kutachochea maendeleo ya Tinde kwani yalisimama kutokana na changamoto ya maji.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. 

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja  Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakitia Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Kiomboi imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. 
Utiaji saini ukiendelea
utiaji saini ukiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja  Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakionesha nyaraka baada ya kutia Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja  Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui ,bwana Murali Mohan wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) na Naibu Meneja  Mkuu wa Kampuni ya Megha Engineering and Infrastructures Ltd katika Miji ya Tinde na Shelui, bwana Murali Mohan wakionesha mikataba baada ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui imefanyika leo Alhamisi Februari 25,2021 katika Mji wa Tinde. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakifuatilia Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Dk. Christina Mnzava akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Mhe. Albert Msovela  akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Mkuu wa wilaya ya Iramba, Mhe. Emmanuel Ruhahula akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela akizungumza wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Kulia ni Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal akiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum (katikati mwenye suti) akicheza ngoma ya Mabulo ya Jeshi kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji wakiwa  kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Viongozi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui 
Viongozi wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Awali Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akiwasalimia wakazi wa Tinde kushuhudia Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso baada ya kufanyika kwa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia) baada ya kufanyika kwa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Miji ya Tinde na Shelui.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...