Friday, January 29, 2021

Walimu Kenya wataka kupatiwa bunduki ili kujilinda dhidi ya wahalifu



Chama cha walimu nchini Kenya (KUPPET) kinaitaka serikali kutoa mafunzo ya usalama kwa walimu na kuwapa silaha wale wanaopelekwa kufundisha kwenye maeneo yaliyo ya hatari.


Kaimu Katibu Mkuu wa KUPPET Moses Nthurima amesema kuwapa walimu silaha si kuwa tu kutawaogopesha watu wanaowashambulia lakini pia kutawapa walimu hali ya kujiamini kufanya kazi katika mazingira ya hatari.



"Tunarudia ombi hilikwamba katika hali ya ukosefu wa usalama, lazima walimu wafundishwe na kupatiwa bunduki.''



''Huwezi kumkabili mtu mwenye bunduki kwa kutumia chaki. Tunapompeleka mwalimu katika maeneo ambayo usalama ni mbovu mwalimu ataishi kwa hofu kila wakati. Lakini ikiwa bunduki inaning'inia mgongoni hata majambazi watajua kuwa mwalimu ni eneo lisilofaa na watachukua sekunde kufikiri kabla ya kufanya makosa, "Alisema Bw. Nthurima.



Ombi hilo limekuja baada ya kutokea matukio ya kuuawa kwa walimu na watu wenye silaha katika maeneo ya Kaskazini-Mashariki na Pwani ya Kenya.

Rayvanny aachia Cover ya Album yake ya Kwanza

 


Staa wa muziki wa Bongo Fleva a.k.a CHUI Rayvanny ameachia Cover rasmi ya Album yake ya Kwanza Sound From Africa ambayo tayari maandalizi yake yamekamilika na huenda ikaachiwa Muda wowote kuanzia sasa

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny amepost cover ya albam hiyo na kuandika " My First Album in my Music career , Thanks God For this one πŸ™πŸ™πŸ™ #SoundFromAfrica 🎼πŸ₯πŸŽΌ

Nione comment Yako TUACHIE 

Msemaji wa serikali Dkt Abbas:Tanzania inazingatia tahadhari dhidi ya corona

 


Msemaji mkuu wa serikali nchini Tanzania Dkt. Hassan Abbas amesema Tanzania inazingatia miongozo yote ya tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona na hata wakati huu ambao dunia inapambana na wimbi la pili la maambukizi ya virusi hivyo.

Akihojiwa na kitoa cha redio cha EFM kilichopo jijini Dar es salam, Dkt. Abbas amesema "Sisi Tanzania msimamo wetu ni ule ule,tunafahamu tatizo lipo duniani na dunia inahangaika lakini cha kwanza watanzania waondoe hofu wizara ya afya ilishatoa miongozo, ile miongozo bado ipo haijawahi kufutwa kuna tahadhari za kuchukua hivi wewe kunawa mikono mpaka covid? Alihoji Dkt Abbas.


'' Tulikuwa tuna nawa sana shule baadaye tukaacha kwahiyo kuna zile tahadhari kama alivyosema juzi Mh Rais tuendelee kuzichukua lakini Tanzania tunaamini tumedhibiti haya maambukizi kwa njia zetu za kisayansi na kumshukuru Mwenyezi Mungu''.


''Unajua Tanzania watu wanasahau wanafikiri tulidharau sana huu ugonjwa tulichukua hatua zote dunia ilizokuwa inataka isipokuwa kujifungia ndani maana kuna watu wanatamani sana kufungiwa ndani sijui kuna nini huko ndani" Alisema Bw. Abbas.


Kauli hii inakuja siku moja baada ya shirika la Afya duniani WHO kupitia ofisi yao ya kanda ya Afrika kutoa taarifa ikizitaka mamlaka nchini kujiandaa kupokea chanjo ya corona kama mataifa mengine yanavyofanya na kuikumbusha Tanzania hayo ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa.


Rais Magufuli ameweka wazi chanjo hazifai na kuwataka watanzania kusimama imara na kuwa waangalifu na mambo ya kuletewa huku akiendelea kusisitiza msimamo wake wakutojifungia ndani na kutaka watu kuchukua tahadhari ikiwemo kujifukiza na kumuomba Mungu.


Mapema mwanzoni mwa juma Kanisa Katoliki nchini humo kupitia baraza la maaskofu lilitoa ujumbe wa tahadhari kwa waumini wake na kukusitiza ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari kwani wao kama kanisa wameona iko haja ya kufanya hivyo.




Senzo Ataja Sababu ya Kumpa Ukocha Nizar

MSHAURI Mkuu wa Klabu ya Yanga kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko, Senzo Mazingisa amesema kuwa wameamua kuwaongeza vijana ndani ya timu ili kwenda na kasi ya soka la kisasa.

Yanga, juzi Januari 27 ilimtambulisha Nizar Khalifan kuwa kocha msaidizi akichukua mikoba ya Juma Mwambusi ambaye aliomba kujiweka kando kutokana na matatizo ya kiafya pamoja na Edem Mortotsi kuwa kocha wa viungo.


Nizar alikuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya African Lyon ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na pia aliwahi kucheza timu ya Mtibwa Sugar pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mazingisa alisema: "Tunahitaji kuongeza thamani ya ubora katika benchi ndiyo maana wote ni vijana na hata kocha mkuu wetu ni kijana ili kuendana na soka la kisasa.

"Aliongeza kuwa anaamini watu waliochaguliwa ni sahihi na watafanya kazi kwa ushirikiano kufanikisha malengo waliyojiwekea katika msimu huu."

Ninaona watu ambao wamechaguliwa ni watu wazuri, hivyo ni suala la kusubiri na kuona namna ambavyo tutaendelea kupambana," alisema Senzo.Yanga inashika nafasi ya kwanza katika ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza michezo 18.

Stori: Wilbert Molandi,Dar es Salaam


Source

MHUBIRI ALIYEJIGAMBA KUFUFUA WAFU SIKU YA ALHAMIS AKAMATWA



Mhubiri Onyebuchi Okocha kutoka Nigeria ambaye alidai kwamba angewafufua wafu siku ya Alhamisi, Januari 28, 2021, amekamatwa na maafisa wa polisi.

Onyebuchi Okocha ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Amafor alikamatwa siku ya Jumatano, Januari 2021, hii ni kwa mujibu wa taarifa za Anambra Broadcasting Servicen nchini humo.

Hata hivyo, nabii huyo ameomba msamaha ingawa serikali ya Anambra imesema itakabiliana naye kisheria kwa sababu anawapotosha wananchi.

Video zake kadhaa zimekuwa zikienezwa mitandaoni zikimuonyesha Nabii huyo akifanya miujiza kadhaa. 

Video ya hivi punde, ilimuonyesha mhubiri huyo akiwarushia noti wanaume waliokuwa uchi wakiwa ndani ya mto.

 Serikali ya Anambra ilighadhabishwa na video hiyo, maelfu ya wananchi wa Nigeria pia walitoa maoni tofauti wakikashifu vitendo vya mhubiri huyo. 

Mhubiri huyo amekuwa akionywa kwa mara kadhaa kuhusiana na vitendo vyake lakini inaonekana hajakuwa akitilia maanani, serikali ya Anambra imeapa kukabiliana naye kisheria.

Via Tuko News

Fahamu Kiundani Kuhusu Tatizo la Pumu




PUMU AU ASTHMA NI NINI
Pumu au asthma ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Ugonjwa huu wa pumu hufanya kuta za ndani ya njia ya hewa kuvimba na hivyo hupunguza kiasi cha hewa kinachoingia na kutoka katika mapafu.

Hali hii husababisha mgonjwa kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua pia kubanwa na kifua, kushindwa kupumua vizuri na kukohoa sana,, watu wenye pumu Mara nyingi hupata Dalili hizo wakati wa usiku na asubuhi sana.

Ugonjwa huu huwaathiri watu wa Rika zote ingawaje Mara nyingi huanza utotoni hivyo huwaathiri Zaidi watoto, inasadikika kuwa takribani watoto MILION Sita nchini na watu wazima takriban 255,000 Duniani wanaugua ugonjwa huu.

Ugonjwa huu wa pumu ni mpana sana kwasababu Kuna aina nyingi za pumu kutokana na visababishi vake

AINA ZA PUMU

1. PUMU YA UTOTONI (CHILD_ONSET ASTHMA)

Hii ni aina ya pumu inayotokea baada ya mtoto kuwa Kwenye Vizio kama vile VUMBI LA WADUDU KAMA MENDE, MANYOYA YA WANYAMA KAMA PAKA, MBWA PIA KUTUMIA BABY WIPES ZENYE HARUFU (PERFUME).

Pumu hii hutokea kwa kuwa mwili wa mtoto hutengeneza Kinga ya mwili (ANTIBODIES) zinazosababisha pumu.

Ugonjwa wa pumu ni sugu sana kwa watoto wanaozaliwa na uzito mdogo wenye asili ya kiafrika pia pumu ya utotoni huwaathiri Zaidi watoto wa kiume Zaidi.

(2)PUMU YA UKUBWANI (ADULT_ONSET ASTHMA)

Pumu hii huanza baada ya kufika miaka 20, pumu hii huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume na pia haitokei sana kama pumu ya utotoni, Vizio kama vile perfume /cream zenye harufu kali /sabuni nk ndio husababisha pumu hii kwa asilmia kubwa.

(3)PUMU ITOKANAYO NA MAZOEZI (EXERCISE INDUCED ASTHMA)

Pumu hii huwatokea Zaidi wanaofanya mazoezi, ikiwa utakohoa na kukosa pumzi wakati wa mazoezi au baada ya mazoezi kuna uwezekano wa wewe kuwa na pumu ambayo inasababishwa na mazoezi pia hata kama sio mwana mazoezi kukimbia kwa kasi angalau dk 10 Kunaweza kusababisha kukosa pumzi kwa muda mrefu na kuonyesha kwamba una pumu

(4)PUMU ITOKANAYO NA KUKOHOA SANA (COUGH INDUCED ASTHMA

Hii ni aina ya pumu ambayo ni ngumu sana na kuumiza vichwa vya madaktar kuigundua kwasababu katika pumu hii inawezekana isitokee hata Dalili zingine Zaidi ya kukohoa kitu ambacho madaktari wanalazimka kuchunguza sababu nyingine za kukohoa sana na kuhakiksha sio zinasababishwa na kukohoa huko.

(5)PUMU YA USIKU (NOCTURNAL ASTHMA)

Pumu hii hutokea Kati ya saa Sita usiku na saa mbili asubuh, pumu hii huamshwa na vumbi la wadudu rangi ya nyumba, na harufu ya gesi pia Mara nyingi wagonjwa wa pumu hii hushtuka usingizini wakati wa usiku wa manane baada ya kukosa pumzi.

(6)PUMU KALI ISIYOKUBALI DAWA (SEVERE ASTHMA)

Wakati wagonjwa wengi wanapata unafuu baada ya kupata steroid wachache hawapati unafuu na hvyo kuhitaj matibabu makubwa zaid.

(7)PUMU YA NGOZI (ECZEMA /ATOPIC DERMATITIS)

Huenda utashangaa kwamba kuna pumu ya ngozi na ipoje sasa majibu yako yote yamepata majibu, naomba ufahamu kwamba neno ECZEMA ambalo ni neno la kigiriki na linamaanisha KUTUTUMUKA SEHEMU YA NNJE YA NGOZI hali ambayo huonekana pale mtu anapopata maradhi haya.

Ugonjwa huu huchangia asilmia 40 ya maradhi yote ya ngozi kwa ufup huu ugonjwa huwapata Zaidi watoto na tatzo hil limekua likiumiza vichwa vya madaktar na wanasayansi wengi kutokana na kwamba haijajulkana sababu maalum, ugonjwa huu ni wa muda mrefu nikimaanisha kwamba mtu huweza kukaa na ugonjwa huu kwa muda mrefu ingawa si muda wote mwil huonyesha dalil za ugonjwa huu

CHANZO CHA UGONJWA WA PUMU

Visababishi vya pumu havijulkani waziwazi ila vitu vinavyochangia pumu ni vizio mfano Moshi wa sigara, bangi, gesi, perfume, kuwa na msongo wa mawazo, kuogea maji ya moto kila wakati, kutokupaka mafuta, kukaa kwenye vumbi, kuvaa mavazi yasiyo ya pamba,

DALILI ZA PUMU

NOTED :sio watu wote wenye Dalili hizi wanapumu na sio wote wenye pumu Wana

Dalili HIZI

1. Kukohoa~kikohozi huwa kikali wakati wa usiku na asubuhi

2. Kutoa sauti kama mluzi wakati wa kuongea

3. Kubanwa na kifua hasa nyakati za jioni na asubuhi sana

3. Kupungukiwa pumzi

4. Sehemu ya ngozi iliyoathiriwa huwa inatutumka

5. Maeneo yenye atharikubwa yanavimba na kuwa na joto Muwasho wa ngozi huwa mkali wakati wa jioni na usku


Nafasi za Ajira , Jiunge na Group Hili la TELEGRAM Usaidiwe Kutafuta Ajira Bonyeza HAPA Kujiunga


MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA PUMU

Matibabu ya ugonjwa kwa hospital yapo ya aina mbili moja ni Ile ya dharura ili kutoa tu msaada, dawa hii ni zile zinazosaidia kutanua njia ya hewa ambazo zimesinyaa (Bronchopdilators) pia husaidia kulainisha misuli ya njia za hewa iliyosinyaa, aina ya pili ya matibabu ni kutumia dawa za steroid za kuvuta (inhaled corticosteroids)

Ila kwa kawaida matibabu haya huwa chanzo cha matatizo mengine kutokana na kwamba dawa hizo ni za kemikal hivyo huwa si nzur kwani hazimalizi tatizo Zinampa mtu unafuu tu, pamoja na hayo ugonjwa huu unaweza kuzuilika kwa kuepuka kutumia vitu vyenye mzio ambavyo ni PERFUME, SABUNI ZENYE HARUFU KALI, RANGI ZA NYUMBA, KUACHA KUVUTA SIGARA NA BANGI, ACHA KUNYWA POMBE, EPUKA KUVUTA VUMBI LA WANYAMA, NA EPUKA KUKAA MAZINGIRA YENYE UNYEVU.

Ganoderma capsules imetengenezwa kwa viungo vya Spora ganoderma, Cordyceps Sinensis Mycelium, Radix Ginseng


Mambo Nane yatayomfanya mwenza wako aongeze malavidavu


Miongoni mwa vitu ambavyo vitamfanya mwenza wako awwze kuongeza upendo kwako ni pamoja na  mambo yafutayo

 1. Jiatahidi kumpongeza hasa pale afanyapo vizuri.

 2. Mkumbushe siku yake kuzaliwa.

 3. Mpeleke mazingira ambayo hajawahi kwenda.

 4. Muandie ujumbe ufupi wa mandishi mara kwa mara.

 5. Mpe muda wa kufanya mambo yanayomuhusu.

 6. Mfanyie shopping kila unapoweza.

 7.  Kumbuka majina ya rafiki zake na ndugu zake.

 8. Mwambie maneno ya kimahusiano mara kwa mara.


Source

JPM amtumia salamu mbunge mwenye viwanda Zimbabwe






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, amemuagiza mbunge wa jimbo la Kahama Mjini, Jumanne Mashimba, kuhakikisha anajenga kiwanda cha kuongeza thamani ya mchele jimboni kwake, hali itakayosaidia kuokoa soko la mpunga na kukuza kipato cha wakulima wa mkoa huo.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 28, 2021, Kahama mkoani Shinyanga, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa huo na ndipo ilipobainika changamoto ya wakulima kukosa soko la mchele hali iliyopelekea wengine kushindwa hata kununua viatu na madaftari ya watoto wao.



"Mbunge Kishimba anzisha kiwanda hapa cha kufanya 'packaging' ya mchele, hakuna sababu ya kujenga kiwanda Zimbabwe wakati hapa Kahama wanahitaji viwanda, nikija hapa nataka unioneshe kiwanda nitakachokuja kukifungua ambacho umekijenga hapa kwa sababu wewe ni mfanyabiashara na ni mbunge wa hapa", ameagiza Rais Magufuli.



Mbali na hayo Rais Dkt. Magufuli pia ameipandisha hadhi wilaya ya Kahama na kuipa hadhi ya kuitwa Manispaa.

Thursday, January 28, 2021

WADAU WA HABARI KANDA YA ZIWA WAAHIDI KUENDELEA KUFANYA KAZI NA VYOMBO VYA HABARI

Wadau wa Habari wa Kanda ya Ziwa wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na vyombo vya Habari Nchini  ili kuifikia jamii na kuihabarisha juu ya shughuli wanazofanya.

Hayo yamesemwa kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliondaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) kuelekea tukio la hafla ya usiku ya Waandishi wa habari na wadau wa Habari iliyopangwa kufanyika Februari 1 mwaka huu.

Mwakilishi wa NHIF  Paul Bulolo alisema kuwa, Vyombo vya Habari na Waandishi wa habari wamekuwa na mchango mkubwa kwa kuwa daraja la kufikisha taarifa kwa jamii zinazofanywa na NHIF juu huduma za afya.

Naye Mkurugenzi wa shirika la EMEDO Editrudith  Lukanga amesema kuwa, Waandishi wa Habari wana nafasi kubwa ya kufikisha taarifa kwa jamii na hivyo kuwaomba waandishi kupitia klabu ya Mwanza kushirikiana na EMEDO ili kujua programu zinazowagusa wanawake na vijana zinavyotekelezwa.

Kuwa upande wake, Mkurugenzi wa Yuhoma Education Limited Bwana Yussuf Yuhoma amesema kuwa, vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa hasa kwenye kuemimisha, kuhabarisha na kuburudisha hivyo amesema wataendelea kufanya kazi na waandishi wa habari.

Bwana Makwaya Makani kutoka kampuni ya Jambo alisema  kuwa, kampuni yao inatambua mchango wa vyombo vya habari na hata wao wana mpango wa kufungua kituo cha redio kitakachoitwa Jambo FM ili kuchangia maendeleo ya Taifa na  kufanya kazi na klabu ya Waandishi ya Mwanza kwa ukaribu.

Mwakilishi wa kampuni ya bia ya TBL Diamond Mawai alisema kuwa,wao walianza zamani kufanya kazi na waandishi wa habari hivyo anatambua umuhimu wao na wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha.

Bwana Kalebe   Luteli mwakilishi toka Hospitali ya Bugando ameweka wazi kwamba  kwenye sekta ya afya Bugando imefanya mambo makubwa kupitia ushirikishwaji wa waandishi wa habari hivyo wataendelea kufanya kazi kwa karibu na waandishi.

Naye Mwenyekiti wa MPC bwana Edwin Soko alisema kuwa, wadau wa habari wasiviogope vyombo vya habari kwani waandishi wa habari sio maadui wa wadau wa habari bali ni marafiki zao.

Soko aliongeza kuwa, kukiwepo ushirikiano baina ya wadau wa habari na vyombo vya habari basi ni rahisi wananchi kupata maendeleo.

Usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari utafanyika Februari 1 kwenye Hotel ya Gold Crest Mwanza.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...