Thursday, December 31, 2020

Mripuko katika uwanja wa ndege wa Yemen wauwa watu 26


Karibu watu ishirini na sita wameuwawa baada ya miripuko katika uwanja wa ndege wa Aden huko Yemen muda mchache baada ya maafisa wa serikali mpya ya Yemen kuwasili nchini humo.

 Duru za serikali na kimatibabu zimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa ingawa hakuna afisa yoyote wa serikali aliyeathirika zaidi ya watu hamsini wamejeruhiwa. 

Kipindi moshi ulipokuwa unafuka kutoka uwanja huo wa ndege huku watu wakikimbia kuwanusuru waliojeruhiwa, kulisikika mripuko wa pili. 

Ukanda wa video wa shirika la habari la AFP umeonyesha kile kilichoonekana kuwa kombora lililoulenga uwanja huo wa ndege. 

Baadhi ya maafisa wamewalaumu waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran kwa shambulizi hilo.

Mama Diamond Akata Mzizi wa FITINA, Amweka Zari Namba Moja Anaefaa Kuolewa na Mondi

 


Mama Dangote Bi Sandra azidi kumkubali Zari kuwa anafaa kuolewa na Mwanae Diamond... Mama Dangote kavunja ukimya na kuandika Ujumbe kuwa " HAKUNA MWINGINE" Yaani zari ndio Top Manyota

Vanessa Mdee avalishwa pete ya uchumba na Rotimi


Staa wa Tanzania aliyetangaza kuacha muziki Vanessa Mdee, amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Rotimi ambaye ni msanii wa filamu na mwanamuziki Rotimi ambao wanaishi wote kwa sasa nchini Marekani.

Kupitia 'videos clip' ambazo zimepostiwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha Rotimi akiwa amepiga magoti mbele ya Vanessa Mdee huku akimvalisha pete hiyo ya uchumba, kisha wakakumbatiana na kuanza ku-kiss.

Ikumbukwe tu mwanzoni mwa mwezi wa kumi mwaka 2020, Vanessa Mdee na Rotimi walishea picha mitandaoni zikiwaonyesha wamechorana 'tattoo' zenye majina yao kwenye miili yao.

Penzi la wawili hao lilianza Oktoba 2019, baada ya Vanessa Mdee kuachana na mkali wa RnB Bongo Juma Jux ambao walidumu kwa miaka 6.

Wednesday, December 30, 2020

Zifahamu Sifa Na Ubora Wa Simu Za TECNO Kwa Mwaka Huu Wa 2020


Mwaka 2020 karibia unafikia ukingoni, bila shaka mwaka huu umekuwa ni mwaka wa changamoto nyingi kwa duniani nzima, lakini pamoja na hayo mwaka 2020 ni mwaka ambao umefanya teknolojia kutumiwa na watu wengi sana duniani ikiwa pamoja na ujio wa bidhaa bora ambazo zimerahisha maisha ya wengi.


Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha sifa pamoja na ubora wa simu mpya za TECNO zilizotoka kwa mwaka 2020. Kama ulikuwa unafikiria kununua simu ya yoyote ya TECNO iliyotoka mwaka 2020 basi pengine list hii inaweza kusaidia kufanya manunuzi kulingana mahitaji yako.


TECNO Camon 16 Premier

Kama unatafuta simu ya TECNO yenye ubora karibia kila mahali TECNO Camon 16 Premier ni simu bora sana, simu hii inakuja na kamera bora huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 na nyingine zikiwa na Megapixel 8 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja ambazo ni low-light sensor. Kamera hizi zinakuja na teknolojia ya image stabilization ambayo inakusaidia kuchukua video za 4K zilizotulia zaidi. Mbali na hayo simu hii pia inao uwezo mkubwa wa kuchukua picha na video bora sana hata wakati wa usiku.

Kwa upande wa kamera ya mbele Camon 16 Premier inakuja na kamera mbili za selfie, kamera moja inakuja na Megapixel 48 ambayo ni wide sensor na nyingine ni Megapixel 8 ambayo hii ni ultrawide. Kamera hizi zote kwa pamoja zina kuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p.


TECNO Camin 16s
TECNO Camon 16s ni toleo lingine la simu mpya za Camon 16 mwaka 2020, toleo hili ni tofauti kidogo na toleo la Camon 16 Premier, kwani kwa bei nafuu zaidi utapata simu hii yenye kamera nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 48, kwa kutumia simu hii unaweza kuchukua video hadi za 1080p@30fps. Kwa mbele simu hii inakuja na kamera moja ya Megapixel 8 huku nayo ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.

TECNO Camon 15 Premier
Camon 15 Premier ni toleo jingine la simu za Camon, simu hii imetoka mapema mwaka 2020 na inakuja na sifa bora, Camon 15 Premier ni simu inakuja na RAM ya GB 6 pamoja na uhifadhi wa ndani wa GB 128 huku ikiwa na kamera kuu yenye uwezo wa Megapixel 64 na kamera ya selfie ikiwa na Megapixel 32.

TECNO Camon 15
Camon 15 ni toleo jingine la ambalo pia linakuja na sifa nzuri ikiwa pamoja na kamera kuu ya megapixel 48, pamoja na kamera ya nyuma ya selfie ya Megaixel 16. Kama unataka kuiliki simu ya Camon 15 yenye kamera nzuri basi unaweza kununua simu hii ya Camon 15.

TECNO Pouvoir 4
TECNO Pouvoir 4 ni simu nyingine bora kutoka kampuni ya TECNO iliyotoka mwaka 2020, simu hii ni bora hasa kama wewe unataka simu yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu, simu hii inakuja na battery kubwa ya 5000 amh, battery ambayo inaweza kudumu na chaji siku nzima kulingana na matumizi yako.

TECNO Pouvoir 4 Pro
TECNO Pouvoir 4 Pro ni toleo lingine ambalo linakuja na uwezo mkubwa wa battery lakini zaidi ya hapo simu hii pia inakuja na sifa nzuri kama uhifadhi wa ndani wa GB 128 pamoja na RAM ya GB 6. Kama unataka uwezo zaidi na simu yenye kudumu na chaji zaidi basi simu hii ya TECNO Pouvoir 4 Pro ni simu bora kwako.

TECNO Spark 5 Pro
TECNO Spark 5 Pro ni simu nyingine kutoka TECNO iliyotoka mwaka 2020, simu hii inakuja na kioo kikubwa cha Inch 6.6 ambacho kina resolution ya hadi 720 kwa 1600 pixels. Mbali ya kuwa simu hii inayo kioo kikubwa pia inakuja na battery bora yenye uwezo wa kudumu na chaji. Bila kusahau Spark 5 Pro inakuja na kamera nne, kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja na nyingine ikiwa ni QVGA.

TECNO Spark 5
TECNO Spark 5 ni toleo lingine la Spark 5 Pro, simu hii nayo ni moja kati ya simu ambayo inapatikana kwa bei nafuu zaidi huku ikiwa na kioo kikubwa kama cha Spark 5 Pro cha inch 6.6, pamoja na battery kubwa ya 5000 mAh. Pia simu hii inakuja na kamera nne kwa nyuma huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 16 na nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 na moja ya mwisho ikiwa ni QVGA. Simu hii pia ina uwezo wa resolution ya hadi 720 kwa 1600 pixels.

Tembelea https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/ kwa mengi zaidi kuhusiana na bidhaa za TECNO.




Iran yaitupia lawama Marekani

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Jawad Zarif ameilaumu Marekani kwa kusema,

"Utawala wa Washington unawajibika kwa vurugu zozote zinazoweza kutokea katika eneo hili,".

Kulingana na taarifa iliyoandikwa na kutolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Zarif alikuwa na mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar Muhammed bin Abdurrahman Al Thani na Waziri wa Mambo ya nje wa Armenia Ara Ayvazyan.

Zarif alijadili uhusiano wa nchi mbili na maendeleo ya kikanda na mwenzake wa Qatar.

Akiashiria kwamba nchi katika eneo zinapaswa kuchangia usalama na utulivu bila uingiliaji wa wageni, Zarif aliishutumu Marekani kwa kuchukua hatua "za tuhuma na uovu",

"Utawala wa Washington unawajibika kwa vurugu zozote zinazowezekana katika eneo hili," alisema.

Katika mazungumzo yake ya simu na Waziri wa Mambo ya nje wa Armenia Ayvazyan, Zarif alisema kuwa kumalizika kwa vita huko Karabakh kuliunda msingi wa ushirikiano wa pande nyingi kati ya nchi za eneo hilo.

 

MWANAHARUSI AELEZA HALI YA UTAPIAMLO MKALI KWA WATOTO WILAYANI KISARAWE



Julieth Ngarabali , Kisarawe 
Mratibu wa lishe wilayani Kisarawe mkoani Pwani Mwanaharusi Issa amesema takwimu zinaonyesha kwamba watoto wenye umri wa miaka mitano wenye utapiamlo mkali katika Wilaya ya hiyo ni asilimia 0.7 huku wenye utapiamlo wa kadri ni asilimia 13.6.

Amesema kwa hali hiyo kundi hili pia linaingia kwenye uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya milipuko kama wazazi wasipokuwa makini kuanzia uandaaji wa lishe , hata mama anapotaka kunyonyesha basi ahakikishe ziwa lake safi.

"Jumla ya watoto chini ya miaka mitano waliofanyiwa tathmini ya hali ya lishe ni 43,757 , matokeo utapiamlo mkali ni watoto 315 sawa na asilimia 0.7 na kadiri ni 5,942 sawa na asilimia 13.6.",amesema Mwanaharusi.

Mwanaharusi amesema ili kupunguza tatizo la utapiamlo lililopo ,wataalamu wa afya wanatakiwa kumuelekeza mama jinsi ya kumpakata mtoto na kumweka kwenye titi ipasavyo mara baada ya kujifungua.

"Pia kumuelekeza mama aliyejifungua jinsi ya kukamua maziwa yake ili mtoto aweze kupatiwa pindi anapokua mbali na ahakikishe yapo kwenye usafi unaotakiwa kuepusha mlipuko wa magonjwa mengine ikiwemo kuhara",ameeleza.

Naye Meneja wa mradi wa Chakula na Lishe kutoka shirika lisilo la kiserikali la Feed The Children Silvia Imalike amesema takwimu za utafiti wa hali ya Kidemografia na afya uliofanyika mwaka 2015 zinaonesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 0 hadi miezi 6 nchini wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee.

"Hii inamanisha asilimia 41 ya watoto wenye umri huo hawanyonyeshwwi ipasavyo hivyo wapo kwenye hatari ya kupata utapiamlo na magonjwa yanayotokana na taratibu zisizofaa za ulishaji watoto", amesema Imalike.

Nyota wa Liverpool Mo Salah asababisha chuki na gumzo mitandaoni kwa kupiga picha na mti wa Krismasi


Nyota wa Liverpool azua gumzo lililotanda chuki miongoni mwa mashabiki wake mitandaoni baada ya kuweka picha zinazoonesha ujumbe wa kusherehekea krismasi.

Mashabiki wa mshabuliaji huyo wa Liverpool na Misri Mohamed Salah wameandika ujumbe wa chuki kuonesha kutofurahishwa na kitendo chake kama nyota wa Kiislamu kutuma ujumbe wa krismasi akiwa pamoja na familia yake.

Salah, 28, aliweka picha mtandaoni zinazomuonesha yeye na familia yake wakiwa wamevalia vizuri na kusimama mbele ya mti wa Krismasi, na kwenye ujumbe huo akaweka emoji 2, na hashtag Merry Christmas.

Ujumbe wa Salah kwenye mtandao wa Instagram umepata 'likes' zaidi ya millioni 2.3 huku ujumbe wake kwenye Twitter wenye picha hizo hizo ukiwa na 'likes' zaidi ya 300,000.

Lakini pia ujumbe huo wa Salah umesababisha hasira kwa baadhi ya wafuasi wake Waislamu ambao wamehoji kuwa nyota huyo wa Kiislamu haruhusiwi kusherekea sikukuu ya Krismasi.

Moja ya jumbe zilizojibu ule wa Salah umeandikwa:

"Kama Muislamu hatustahili kusherehekea au hata kupongeza dini zingine wakati wanasherehe zao''.

Shabiki mwingine akamjibu:

"Hii ndio sababu [Nyota wa Arsenal na Misri] Mohammed Elneny ndio mfalme wa Misri na sio wewe" 

Wengine walioghadhabishwa na hatua ya Mo Salah ni kama ifuatavyo:

TECNO Kuwazawadia Wateja Wa Camon 16 Na Spark 5Pro Nchi 55 Ya TV


TECNO inaendelea kuwapa furaha wateja wake hii ni baada ya kukabidhi zawadi kwa Bwana Ramadhani Salim aliyejishindia mashine yakufulia, Jacquline Kaseja vocha ya manunuzi yenye thamani ya sh.500,000 na mshindi wa TECNO Spark 5pro Zee la Vyeti aliyepatikana kupitia challenge ya iliyofanyika twitter. 


Zawadi bado zipo nyingi na TECNO inawakumbusha wateja wake kutembelea maduka yote ya simu ili kuendelea kufurahiya zawadi mbalimbali kutoka TECNO kama vile rice cooker, blender, cattle na gift package pindi ununua apo simu yoyote ya TECNO lakini pia endapo ukinunua camon 16 na Spark 5 pro moja kwa moja utaingizwa katika droo kubwa na washindi kuondoka na Smart TV ya nchi 55, droo hii kubwa itachezeshwa live trh 15/1/2021 kupitia @tecnomobiletanzania.

TECNO camon 16 na Spark 5pro ni matoleo mapya kwa kampuni hii nah ii imepelekea simu hizi kuwa muonekano wenye kuvutia na uimara katika utumiaji. Camon 16 ni simu yenye kamera kali kuzidi simu zote za TECNO nyuma ikiwa na MP 48 na selfie ni MP 16, ukubwa wa memory ni 128GB+4GB RAM na battery lenye kudumu na chaji wa muda mrefu la mAh 5000.


Spark 5 pro ni simu yenye kioo kipana cha nch 6.6, Spark 5pro inakupa nafasi ya kuchukua picha kwa ukubwa zaidi kutoka na kuwa na wigo mpana wa kioo vilevile ina MP16 nyuma na selfie MP 8, memory kubwa GB 64+GB 3 RAM na battery lenye kudumu na chaji kwa muda mrefu mAh5000.


Tembelea https://www.tecno-mobile.com/tz/home/#/ 


 




MO Dewji atoa ya moyoni “sitamvumilia anenivunjia heshima”



Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema mwaka 2021 hatowavumilia wale wote wanaotoa lugha za matusi na kumvunjia heshima.
MO ametoa onyo hilo jana kupitia ujumbe wake mrefu wa kufunga mwaka 2020 aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Azimio langu kwa mwaka ujao humu mtandaoni ni kutovumilia wale wenye lugha za matusi na kunivunjia heshima mimi binafsi, nitalazimika, japo kwa shingo upande na moyo mzito sana, kuwa-block, ku-report na ikibidi, kuchukua hatua za kisheria. Naamini kutumia lugha ya matusi na kudhalilisha dhidi ya mtu katika hadhara si ustaarabu wetu Watanzania, si maadili ya dini zetu na si uungwana pia" MO dewji

"Sote tuna maisha nje ya mtandaoni. Wengi wetu ni wazazi, tunao pia wazazi, wategemezi na watu wengine muhimu kwetu ambao tunawaheshimu, wanatuheshimu na wana matarajio juu yetu, haipendezi kuwakwaza na kuwaumiza hao wanaotuthamini na kutuheshimu kwa figisu za maisha yetu ya mtandaoni" MO Dewji 

"Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza mtandaoni katika mwaka huu unaoishia. Nami nimesamehe wale wote ambao walinikwanza kwa namna moja au nyingine," MO

Kuhusu Klabu ya Simba, Mo amesema; "Tunapomaliza mwaka, nawashukuru wote humu mtandaoni kwa kunikosoa, kunijenga na kunishauri mengi mimi binafsi na klabu yetu ya


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...