Friday, November 27, 2020

Hatma ya Halima Mdee na Wenzake Kujulikana Leo


 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo Ijumaa tarehe 27 Novemba 2020, kinafanya kikao maalum cha kamati kuu kuwajadili wanachama wake 19 wanaodaiwa kukisaliti kwa kukubali uteuzi wa ubunge viti maalumu.

Kikao hicho, kinafanyika jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

  Wanachama hao 19 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee wanajadiliwa baada ya tarehe 24 Novemba 2020 kwenda bungeni jijini Dodoma kuapishwa na Spika Job Ndugai.

Kutokana na tuhuma hizo za usaliti, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alitangaza kufanyika kwa kamati kuu leo Ijumaa na kuwataka kufika makao makuu ya Chadema, Kinondoni Dar es Salaam saa 2:00 asubuhi.


Wakenya waliokuwa wakielekea Dubai wakamatwa na satakabadhi gushi za corona


Maafisa wa uwanja wa ndege nchini Kenya wamewakamata wasafiri 21 ambao waliokuwa wakielekea mjini Dubai, katika Muungano wa falme za kiarabu (UAE), kwa kutumia vyeti gushi vya Covid-19.

Wasafiri waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Wasafiri hao wamekamatwa wakati wa msako wa vyeti hivyo uliokuwa ukifanyika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta katika mji mkuu, Nairobi.

Hii inakuja saa kadhaa baada ya UAE kupiga marufuku utoaji wa vibali vya kusafiria (visa) kwa wasafiri wanaotoka nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya.

Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa marufuku hiyo iliwekwa baada ya wasafiri kutoka Kenya kupatikana na vyetu gushi vya Covid-19 walippowasili katika taifa hilo la Ghuba.

Kenya imekuwa ikirekodi ongezeko la maambukizi ya Covid-19, huku jumla ya watu wenye maambukizi ikifikia 80,102 vikiwemo vifo vya watu 1,427.

Mawaziri SADC – Troika Wakutana Kwa Dharura Botswana

Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama wamekutana katika mkutano wa dharura na kujadili masuala ya siasa, ulinzi na usalama.

Mkutano huo umefanyika  mjini Gaborone, Botswana ambapo ulitanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ulioanza asubuhi na kumalizika mchana.

Kupitia mkutano huo, mawaziri wameweza kujadili masuala ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC na kupendekeza njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwenye siasa, ulinzi na usalama ndani ya ukanda wa SADC.

Pamoja na mambo mengine, Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama  inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama
.


Source

Yafahamu mambo ambayo mwanamke anayahitaji katika mahusiano ya kimapenzi



1. Anataka mume anayemjali na kujali kila anachokitaka. Sio tu mahitaji ya kimwili, bali pia ayatambue mahitaji yake ya kisaikolojia, upendo na kujali hisia zake.

2. Anataka mume anayemlinda na kumfanya ahisi kuwa yuko salama wakati wowote, kiasi kwamba hana hofu ya chochote kwa sababu anajua kwamba mumewe atamlinda na kumkinga na maudhi.

3. Mume anayehisi kwamba ameshikamana naye na kuridhika naye.

4. Mume anayeshiriki naye katika maongezi matamu yenye hisia tamu. mume anayempa maneno laini, sio maongezi makavu yasiyokuwa na hisia za kimahaba.

5. Anataka mume anayembusu kila anapoagana naye au anapokutana naye. Mke anapenda jambo zuri linalofanywa mara kwa mara hata kama ni dogo, kuliko jambo kubwa linalofanywa kwa kuchelewa au kwa muda mrefu. Busu unalompa kila siku kabla ya kwenda kazini ni bora kwake kuliko "outing" unayompa baada ya miezi sita.

6. Anataka mume anayeyaona yanayofanywa na mkewe kwa ajili yake, hata kama ni madogo. "Attention" ya mume kwa mke ni jambo muhimu mno. Anataka attention yako kwenye mavazi, kwenye chakula na hata mabadiliko madogo anayoyafanya kwenye chumba chenu....sio unakuta kitanda kimebadilishwa mkao unaanza kuponda

7. Mke anataka mume anayemkubali vile alivyo na kuchunga sana usalama wa hisia zake. Usalama wa hisia za mwanamke ni muhimu mno kuliko hata usalama wa uchumi wake. Haitakuwa na maana kama unamnunulia mavazi mazuri, lakini ukawa unaziumiza hisia zake.

8.mke anataka mume mwenye imani asiyetereka wala kuyumbishwa kwa maneno ya dada zake hata wazazi wake anayeweza kujisimamia ,sio kuperekeshwa

Ili kujifunza zaidi namna ya kutunza na kuimarisha mahusiano yako Pia usisahau kusikiliza sauti ya Mungu na kutenga Muda wa kuomba zaidi.

Dereva Taxi Arudisha Milioni 800 kwa Abiria

 


Kuna hii ambayo imetokea Uturuki ambapo Dereva teksi huko Istanbul, amemrudishia abiria aliyesahau Euro 300,000 (zaidi ya Sh milioni 800 za Kitanzania) alizokuwa amezisahau katika gari lake.


Dereva teksi huyo, Olgaç alimpakia abiria huyo wa kigeni kutoka uwanja wa ndege wa Istanbul na kumpeleka hotelini.


Wakati akiondoka ndipo alipoona begi katika kiti cha nyuma na kugundua kuwa lilisahauliwa na abiria yule, Dereva Olgaç akaona kuwa kulikuwa na hela katika begi hilo.


Aliamua kupiga simu kwenye hoteli aliyomuacha abiria yule akawasiliana naye na kumpelekea begi lililokuwa na Euro 300,000.


Ni nadra sana kuona dereva mwaminifu kama huyo, hasa katika Jiji kubwa kama Istanbul, watu wengi wameshangazwa na kufurahishwa na jambo hilo.

Simulizi Mfungwa Aliyempora Askari Bunduki ‘SMG’





NJOMBE: Ni ujasiri ulioje? Kijana, Isaack Kawogo (24) ambaye alikuwa mfungwa, amefanya tukio lililowaacha wengi midomo wazi la kumpora Askari Magereza silaha aina ya SMG (SubMachine Gun) mkoani Iringa, kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi baada ya kumjeruhi kaka yake, Andres Kawogo (61), UWAZI lina simulizi hii ya kutisha.

 

Kawogo alikuwa akimtuhumu ndugu yake huyo kuuza mashamba ya nyumbani kwao na kushindwa kumtoa gerezani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Hamis Issah aliliambia UWAZI kuwa, tukio hilo la kupora silaha hiyo lilijiri Novemba 20, mwaka huu huko maeneo ya Chaugingi mjini Njombe.

 

Kamanda Issah alisema kuwa, Kawongo aliiba silaha na kuitumia kufanya uhalifu ambapo alifanya matukio kadhaa huko mkoani Iringa ikiwemo kumshambulia Askari kwa panga, hali iliyosababisha wafungwa wengine kutoroka. "Hii ni silaha ambayo Askari Magereza wanaitumia katika ulinzi wa wafungwa hao, sasa huyu kwa kuwa ni mhalifu, akawa anaitumia katika kufanya uhalifu," alisema Kamanda Issah.

 

Alisema kuwa, silaha hiyo ilikuwa na risasi kumi, lakini mpaka inachukuliwa mikononi kwa Kawogo, ilikuwa imebakiwa na risasi mbili pekee huku risasi nane zikitumika kufanya ualifu maeneo tofauti ikiwemo tukio hilo lililotokea mkoani Njombe la kumjeruhi kaka yake.

 

Alisema kuwa, licha ya juhudi kufanyika za kutaka kuokoa maisha ya Kawogo ili alieleze Jeshi la Polisi namna alivyoondoka na silaha, lakini ilishindikana kwa kuwa umauti ulimfika wakati akinyang'anywa silaha hiyo.



"Ukimnyang'anya askari silaha, namna pekee ya kuipata hiyo silaha ni kwa kutumia silaha hivyo wanapaswa kuwa makini," Kamanda Issah.

 

Kwa mujibu wa watu waliozungumzia tukio hilo ambalo limekuwa gumzo katika Mikoa ya Njombe na Iringa, si jambo la kawaida kutokea na kwamba ni hatari mno.

 

"Si jambo la kawaida kutokea, ila kuna uzembe fulani utakuwa umefanywa na askari, haiwezekeni askari aporwe silaha, tena SMG akiwa ameishikilia, hii ni hatari sana," alisema Emmanuel Sanga, mkazi wa mjini Njome.

 

Tukio kama hilo liliwahi kutokea mkoani Arusha ambapo mahabusu mmoja alimpora silaha aina ya SMG mmoja wa Askari Polisi katika Mahakama Kuu jijini Arusha na kutokomea nayo mtaani, jambo lililozua taharuki kubwa, kabla ya kusakwa na kunyang'anywa kisha sheria kuchukua mkondo wake.


Thursday, November 26, 2020

TACAIDS yakanusha taarifa iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa wafadhili wamejitoa kununua dawa za ukimwi


TACAIDS yakanusha taarifa iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa wafadhili wamejitoa kununua dawa za ukimwi
Muungwana Blog · Muungwana 





Balozi wa Tanzania aitembelea kambi ya Simba nchini Nigeria




Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Benson Bana ametembelea kambi ya Simba jijini Abuja na kupewa jezi ya Simba itakayotumika Kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Simba Novemba 29 itamenyana na Plateau United mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika

Kiongozi huyo amesema kuwa ana imani ya kuona timu ya Simba ikipata matokeo chanya Kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo kabla ya ule wa marudio utakaochezwa Dar.

 


Serikali Yakanusha Taarifa Iliyoenea Kwenye Mitandao Ya Kijamii Kuwa Wafadhili Wamejitoa Kununua Dawa Za Ukimwi



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...