Tuesday, October 27, 2020

Mawakala wa wagombea urais wa vyama 14 waapishwa


 Na. Lilian Shembilu – MAELEZO
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera amewaapisha mawakala wa vyama vya siasa 14 ambapo Chama cha ACT-Wazalendo hakina mwakilishi wa uwakala, hivyo kufanya idadi ya Vyama vya siasa vitakavyogombea nafasi ya urais tarehe 28 Oktoba 2020 kufikia 15.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt.Wilson Mahera amesema mawakala wa wagombea wa nafasi ya urais ni wawakilishi walioteuliwa na chama baada ya kupata ridhaa ya wagombea wao.

"Wakala wa kujumlisha kura ni mwakilishi aliyeteuliwa na Chama baada ya kupata ridhaa ya mgombea, kwahiyo mliopo humu ndani mmeteuliwa na vyama vyenu baada ya ridhaa ya mgombea, hongereni sana" amesema Dkt. Mahera.

Dkt. Mahera amewaeleza wajibu na majukumu ya mawakala kuwa ni kushuhudia ujumlishaji wa kura za urais, kulinda maslahi ya mgombea na wagombea kwa kuhakikisha sheria, taratibu na kanuni zinafuatwa wakati wa kujumlisha matokeo ya uchaguzi na kanuni hizo za sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 na kuzingatia pia katiba ya nchi, vilevile mawakala wana wajibu wa kusaini fomu ya matokeo ya uchaguzi.

"Si kuhesabu kura tu bali kufuata sheria na kanuni zote za wakala na ukienda ndivyo sivyo utawajibika kama sheria inavyosema" amesema Dkt. Mahera.

Akizungumza katika kikao hicho mwanasheria wa Serikali Bi.Rose Chilongozi aliwaasa mawakala wote kuhakikisha wanasimamia kiapo walichoapa na wajue kuwa wakivujisha siri ambazo hawakuambiwa wazitoe na kwamba zitatolewa na wahusika hilo ni kosa la jinai.


Sillo amalizia Kampeni kwa kumuombea Kura Dk. Magufuli kata ya Galapo


Na John Walter-Babati.

Wananchi wa Jimbo la Babati Vijijini wanamatarajio ya kutatuliwa kero ya miundombinu ya barabara na maji kutokana na ahadi ya mgombea ubunge wa jimbo hilo alipokuwa akiowaombea kura diwani wa kata ya Galapo Michael Naasi na Dk. John Magufuli mgombea Urais Ccm.

Akijinadi mbele ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara wa kufunga kampeni za Kunadi sera na ilani ya Chama Chama Mapinduzi  uliofanyika katika kijiji cha Galapo kata ya Galapo, Mgombea Ubunge Jimbo hilo anaesubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa Daniel Sillo,  alisema kuwa ilani ya Chama hicho imesheheni mambo mengi ikiwemo  miundombinu ya barabara, Elimu, Maji na Afya.

Alisema kuwa miundombinu ikiwa bora inasaidia kukuza uchumi wa wananchi kutokana na shughuli za kimaendeleo ambazo zinakuwa zinafanyika katika maeneo ya vijiji au miji ya kibiashara hasa usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali.

Amesema ilani ya Chama cha Mapinduzi  imeendelea kutekelezwa kwa vitendo ambapo katika jimbo la Babati Vijijini lenye vijiji 102, Vijiji 84 tayari vinawaka Umeme  na kubaki vijiji 18 pekee na kazi bado inaendelea ambapo lengo ni kufikisha umeme hadi kwenye vitongoji.

Sillo alisema kuwa jimbo hilo linakabiliwa na changamoto  ya maji  hivyo atahakikisha maeneo yote yenye changamoto hiyo na nyingine,  anatafuta njia ya kuzitatua.

Amewataka wananchi   kutochezea amani ya Nchi na Badala yake wawe Mabalozi Wazuri wa kutunza na kuenzi amani hiyo  kwa kumchagua tena  Dr. John Pombe Magufuli kuiongoza nchi ya Tanzania kwa miaka mingine Mitano.

Mgombea Udiwani kata ya Galapo Michael Naasi  ameahidi kushirikiana na Mbunge kuwasemea wananchi katika vikao vya Baraza la Madiwani ili changamoto zilizopo zitatuliwe.

 

IGP Sirro azungumzia vurugu Zanzibar....Asisitiza viongozi kulinda amani


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka viongozi wa siasa, tume na wadau wengine wa siasa kutimiza wajibu wao katika kulinda amani ya nchi wakati huu wa uchaguzi.

"Tunatarajia kumpata rais mmoja atakayechaguliwa na wananchi hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake kudumisha amani iliyopo."- Amesema IGP Simon Siro leo Oktoba 27 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa za vikundi vya watu wanaotaka kufanya vurugu.

Ameongeza kuwa jeshi la Polisi limejiandaa kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa huku akiwasisitiza wapiga kura, kwenda kupiga kura bila woga nakuepuka vurugu katika vituo vya kupigia kura. 

Aidha,IGP  Sirro amesema kuna watu 42 waliokamatwa kisiwani Pemba wakidaiwa kuwashambulia polisi waliokuwa wakisambaza masanduku ya kura jana.

"Kama kule Zanzibar, wakati askari wanasambaza masanduku ya kupigia kura, kuna vijana walianza kurusha mawe na wameshulikiwa. Wapo karibu 42. Mpaka sasa hakuna kifo chochote," amesema IGP Sirro.




Source

“Pemba wakati tunasambaza masanduku ya kupigia kura Polisi walirushiwa mawe”

 


Mkuu wa Jeshi laPolisi nchini, IGP Simon Sirro ametoa wito kwa watanzania katika kipindi hiki chauchaguzi kujihadhari na mihemko isiyokuwa na tija inayoweza kuwaletea matatizo.


Akizungumza nawaandishi wa habari hii leo, Sirro amesema kila mtu anategemewa na familia yake, hivyo ni vyema kuepuka vurugu zinazoweka kuharibu amani iliyopo.


"Kama unajua hutopiga kura usiwe sehemu ya kuanzisha vurugu kwakuwa hapo jana usiku huko Pemba kipindi tunasambaza masanduku ya kupigia kura Polisi walirushiwa mawe hivyohatutarajii kujirudia" Sirro.


Amesema kunamaisha baada ya uchaguzi na kwamba ushindani wowote lazima mmoja ashindena hata kama aliyeshinda ni adui yako unatakiwa uvumilia

Faida ya Benki ya NMB yapanda kwa asilimia 76 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2020


Benki ya NMB imepata ongezeko la asilimia 76 la faida kabla ya kodi kwa kipindi kilichoishia Septemba 30, 2020. Kwa miaka mitano sasa, Tanzania imeshuhudia ukuaji imara wa uchumi uliowezeshwa na sera thabiti za kiuchumi

za Serikali ya awamu ya Tano.

Maendeleo haya ya kiuchumi, mazingira rafiki ya kibiashara, pamoja na utekelezaji mzuri wa mikakati ya benki ya NMB ni sababu kuu zilizopelekea ongezeko hili la faida katika robo ya tatu ya mwaka 2020.

Katika kipindi hiki faida kabla ya kodi ya Benki ya NMB imepanda kwa 76% kutoka Shilingi bilioni 118 katika robo ya tatu ya mwaka 2019 hadi shilingi bilioni 208 mwaka huu, wakati faida baada ya kodi ikipanda kutoka shilingi bilioni 82 hadi shilingi bilioni 145 ambayo ni sawa na ongezeko la 77%.

Pia katika kipindi hiki, mkakati wa Benki ya NMB wa kukuza vyanzo vya mapato umejidhihirisha kwa ongezeko la

mapato yatokanayo na uendeshaji kwa 14% kutoka bilioni 527 katika robo ya tatu mwaka 2019 hadi bilioni 600

katika robo ya tatu ya mwaka huu (2020).

Katika kipindi hiki pia programu za Benki za kudhibiti gharama za uendeshaji na matumizi ziliimarishwa na kusababisha uwiano mzuri wa gharama na mapato kwa 52%. Vile vile, Benki ya NMB kama mwezeshaji mkubwa wa maendeleo na uchumi nchini, imeweza kukuza rasilimali zake kwa 15% kutoka shilingi trilioni 6.1 kipindi kama hiki mwaka jana hadi trilioni 7 katika robo ya tatu ya mwaka 2020; hili limesababishwa na ongezeko la amana za wateja kwa 15% na ongezeko la mikopo kwa wateja la 16%.

Benki yetu pia imepata mafanikio makubwa katika eneo la ukopeshaji kwa kupunguza tengo la mikopo chechefu

kwa asilimia 22 ukilinganisha na kipindi husika mwaka 2019. Kwa matokeo haya ya utekelezaji kwa kipindi hiki, Benki ya NMB imeendelea kuimarisha mtaji wake juu ya kiwango kilichowekwa kisheria na Benki Kuu ya Tanzania cha asilimia 12.5.

Hiki ni kiashiria muhimu sana kuthibitisha afya ya Benki ya NMB kuendelea na biashara yake kwa miaka mingi ijayo. Akitangaza matokeo ya robo ya tatu ya mwaka 2020 ya Benki hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema kuwa matokeo haya yamesababishwa na kukua kwa haraka kwa uchumi wa Tanzania, sera

wezeshi na mwendelezo wa ukuaji wa pato la taifa kwa miaka ya hivi karibuni kama ilivyodhihirishwa kwa nchi

yetu kuingia kwenye uchumi wa kati mwezi Julai mwaka 2020. Haya yote yamesababisha sekta ya kibenki kufanya

vizuri, ikiwemo Benki ya NMB.

Bi. Zaipuna alisema kuwa "utendaji mzuri wa kifedha wa Benki ya NMB mwaka wote wa 2020 ni kielelezo kizuri

cha ufanisi wa utekelezaji wa mikakati ya Benki, ubora wa wafanyakazi wetu na imani ya wateja wetu kuendelea kutumia huduma zetu za kibenki. Tunaendelea kuwashukuru wateja wetu, wanahisa wote na wafanyakazi wetu wote kwa matokeo haya chanya".

Ni katika muktadha huo, wiki iliyopita, benki ya NMB ilipata tuzo ya Benki Salama zaidi Tanzania kwa mwaka 2020

itolewayo na jarida la kimataifa la Global Finance la New York, nchini Marekani. Ushindi huu umepatikana miezi

kadhaa tangu jarida la Euromoney la London liitangaze Benki ya NMB kuwa Benki Bora Tanzania kwa miaka nane

mfululizo.

Billnass Afunguka Ukweli Mchungu "Nandy Anaingiza Hela zaidi Yangu"

 


Billnass aanika wazi kwamba Nandy anaingiza pesa nyingi zaidi yake. Kwenye mahojiano na kipindi cha Leo Tena Clouds FM, Nenga amesema Nandy anapata shoo nyingi na pia ana miradi mingi zaidi yake.


Akijibu swali la nani kati yao anaingiza fedha zaidi, Billnass alijibu kuwa ni Nandy lakini akaenda mbali na kufafanua kuwa yeye ndio mwenye fedha nyingi zaidi ya Nandy kutokana na matumizi ya mchumba wake huyo.

 

"Nandy anaingiza pesa zaidi yangu, anapata shoo nyingi na ana miradi mingi. Lakini mwisho wa siku tukiwa tunafanya tathimini za nani ana pesa nyingi kwenye akaunti, mimi ndio nakuwa juu," amesema billnass na kuongeza

 

"Hiyo inatokana na kuwa Nandy ana matumizi mengi kuliko mimi, kwa hiyo huingiza pesa nyingi lakini pia hutumia pesa nyingi zaidi." alimaliza Billnass ambaye safari hii ameshirikishwa na Nandy kwenye 'Do Me' wimbo wao mpya unaofanya vizuri kwa sasa.

Sifa ya Tanzania Duniani ni Umoja na Mshikamano – Rais Magufuli


Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha tunu ya umoja na mshikamano iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili na kamwe wasikubali kuibomoa iwe kwa dini au kabila.

Akizungumza jana (Jumatatu, Oktoba 26, 2020) wilayani Chamwino mkoani Dodoma, wakati  akizindua msikiti wa Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Rais Magufuli alisema kuwa  msikiti huo utumike kuwaweka pamoja kama ndugu, pia ukawe fundisho kwa wana Chamwino na watanzania katika kuwa wamoja na kutambua kuwa wana wajibu wa kumtanguliza Mungu katika  maisha yote.

"Msikiti huu ukatoe mafunzo yatakayojenga umoja wa watanzania, ukaguse na mioyo yao ya kutekeleza maandiko matakatifu yaliyopo kwenye Quran na yakajenge umoja ndani ya watanzania wote," alisisitiza.

Aliongeza "ishara hii mliyoionyesha leo ni ya kipekee duniani kote, upendo huu na umoja huu ni wa maajabu sana, tuendelee kushikamana"

Aidha, Rais Magufuli aliwakumbusha watanzania kwenda kupiga kura  Oktoba 28 mwaka  huu kulingana na utashi wa mioyo yao kwa kuchangua viongozi watakaoweka mbele maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charls Mbuge alisema kuwa msikiti huo wenye ofisi ya Mufti umejengwa kwa gharama ya shilingi  milioni 319.28 umekamilika kwa asilimia 100.

"Endapo msikiti huu ungejengwa na mkandarasi basi ungetumia shilingi  milioni 439.43, na umekamilika kwa asilimia 100 na tumeujenga kwa mwezi mmoja na siku 28 tu."

Aidha, Meja Jenerali Mbuge, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuifanya JKT kuwa karibu na wananchi na kuahidi  kuendelea kutekeleza maagizo pamoja na majukumu  yao kwa ufanisi.

Naye Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi alimshukuru Rais Magufuli kwa kuwajengea msikiti wenye hadhi na sambamba na uamuzi wake wa kurudisha mali za waislamu zilizopotea.

"Umekuwa kiongozi  mwenye kipaji cha kupenda viongozi wa dini na mwenye kumtanguliza Mungu katika Kila jambo. Vitabu vya Mungu  vinasema anayefanyia wema mlipeni na kama hamna cha kumlipa muombeeni."

Aidha, Mufti Zuberi alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kujitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu, huku wakiendelea kuliombea taifa hata baada ya Uchanguzi Mkuu kumalizika.

Itakumbukwa kuwa Agosti 23, 2020, Rais Magufuli aliendesha  harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti  wa Chamwino katika  misa takatifu  ya uzinduzi wa  Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Immaculata   Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, ambapo shilingi millioni 25.6  zilipatikana.



Source

Mchunguzi wa UN asema Belarus lazima ikome kuwatesa watu wake


Mchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa haki za binaadamu kuhusu Belarus Anais Marin ameitaka serikali ya nchi hiyo kukoma kuwakandamiza watu wake, akisema karibu watu 20,000 walikamatawa Agosti na Septemba na mamia wameripotiwa kupigwa, kutishwa, kuteswa au kunyanyaswa kizuizini. 

Marin amenukuu duru kutoka Wizara ya Mambo ya ndani na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa takwimu hizo na kusema wafungwa wengi wamejikuta wakikabiliwa na mashitaka ya kiutawala au uhalifu, akitaja zaidi ya kesi 400 za uhalifu dhidi ya waandamanaji tangu uchaguzi uliopingwa wa Agosti 9. 

Ombi la afisa huyo wa Umoja wa Mataifa limesisitizwa katika taarifa iliyowasilishwa kwa kamati hiyo kutoka kwa nchi 52 za Ulaya na Umoja wa Ulaya. 

Pia zimetoa wito wa kusitishwa mashambulizi dhidi ya waandamanaji wa amani, unyanyasaji kwa wale walioko kwenye vuguvugu la kudai demokrasia, kuwatisha viongozi wa upinzani, wanahabari, watetezi wa haki za binaadamu na waandamanaji.

Polisi Kaskazini Pemba lalazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi


Mchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa haki za binaadamu kuhusu Belarus Anais Marin ameitaka serikali ya nchi hiyo kukoma kuwakandamiza watu wake, akisema karibu watu 20,000 walikamatawa Agosti na Septemba na mamia wameripotiwa kupigwa, kutishwa, kuteswa au kunyanyaswa kizuizini. 

Marin amenukuu duru kutoka Wizara ya Mambo ya ndani na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa takwimu hizo na kusema wafungwa wengi wamejikuta wakikabiliwa na mashitaka ya kiutawala au uhalifu, akitaja zaidi ya kesi 400 za uhalifu dhidi ya waandamanaji tangu uchaguzi uliopingwa wa Agosti 9. 

Ombi la afisa huyo wa Umoja wa Mataifa limesisitizwa katika taarifa iliyowasilishwa kwa kamati hiyo kutoka kwa nchi 52 za Ulaya na Umoja wa Ulaya. 

Pia zimetoa wito wa kusitishwa mashambulizi dhidi ya waandamanaji wa amani, unyanyasaji kwa wale walioko kwenye vuguvugu la kudai demokrasia, kuwatisha viongozi wa upinzani, wanahabari, watetezi wa haki za binaadamu na waandamanaji.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...