Friday, September 18, 2020

RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI WA UJENZI WA BARABARA YA TEGETA NYUKI KUKAMILISHA UJEZI IFIKAPO MWEZI OKTOBA, "AKIKAIDI PATACHIMBIKA"


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge
Na Azmala Said - Dar es salaam 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Aboubakar Kunenge ametoa mwezi mmoja kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa barabaara ya Tegeta Nyuki yenye urefu wa Kilometa 1.06 kuhakikisha anakamilisha kwa wakati  na kueleza kuwa endapo atashindwa kutekeleza agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

RC Kunenge ametoa maagizo hayo wakati Wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo amesema mkandarasi huyo wa Kampuni ya CMG Construction amekuwa akisuasua kumaliza mradi licha ya kuongezewa muda ambapo amewaelekeza TARURA kumsimamia ipasavyo Mkandarasi huyo.

Aidha RC Kunenge pia ametembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa Stand Mpya ya kisasa Mbezi Louis ambayo ujenzi wake umefika 80% na inagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 56 ambapo ameonyesha kuridhishwa na hatua ya ujenzi ilipofikia.

Akiwa kwenye ukaguzi wa Barabara ya Madale - Wazo yenye urefu wa Km 6 inayogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 9.9, Kunenge amefurahishwa na juhudi za mkandarasi huyo huku akieleza kuwa barabara hiyo ikikamilika itakuwa "shortcut" nzuri ya kutoka Mbezi kupitia Madale hadi Wazo.

Katika ziara hiyo Kunenge pia ametembelea ujenzi wa Daraja la Ulongoni A lililopo Kata ya Gongolamboto ambalo ujenzi wake unagharimu Shilingi Bilioni 4.3 na Ujenzi wa Daraja la Ulongoni B ambapo amewahimiza wakandarasi kuongeza juhudi ili ujenzi ukamilike ndani ya Muda uliopangwa ili kupunguza kero walizokuwa wakizipata wananchi.

Thursday, September 17, 2020

NKULILA AZINDUA RASMI KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM NDEMBEZI..AOMBA APEWE MITANO TENA

Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  akiwaomba wananchi wa kata hiyo wamchague tena kuwa diwani wa kata ya Ndembezi. 

Na Suzy Butondo - Shinyanga
Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  amewaomba wananchi wa kata hiyo wamchague ili aweze kuzimalizia changamoto zilizopo ikiwemo kujenga soko la Kisasa na barabara za kata hiyo.

Nkulila ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani iliyofanyika katika kata hiyo na kuhudhuriwa na wanachama wa CCM na wananchi wa kata hiyo.

"Nawaomba sana  wananchi wangu tarehe 28 mwezi wa kumi mnichague Mimi katika kuwakilisha kata, mmchague Patrobas Katambi katika kuwakilisha jimbo pia mchagueni Rais wetu John Pombe Magufuli katika kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi mzee wa kuleta maendeleo kwa nchi yetu", amesema Nkulila.

Nkulila amesema kauli mbiu yake ni kuwasaidia wanyonge na kusimamia wafanyabiashara wote waweze kutendewa haki akisaidiana na mbunge wake Katambi pamoja na Rais Magufuli.

Baadhi ya wananchi wanaoishi kata ya Ndembezi, Jenifer Mahona na Shija Masanja wamesema wanamjua Nkulila ni mchapa kazi, hivyo hawana hofu na yeye watampigia kura na wanaamini atashinda kwani kazi zake zinajiekeza, na maendeleo aliyoyafanya yanaonekana.

"Sisi hatuna shaka na mgombea wetu udiwani kwani ni mchapa kazi mzuri na akisimamia hoja ya maendeleo inatendeka na anapenda haki si mtu wa kupindisha pindisha", amesema Masanja.

Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  akiwaomba wananchi wa kata hiyo wamchague tena kuwa diwani wa kata ya Ndembezi. Picha zote na Suzy Butondo
Mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga David Nkulila  akiwaomba wananchi wa kata hiyo wamchague tena kuwa diwani wa kata ya Ndembezi. 







Wednesday, September 16, 2020

Picha : TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKUTANA NA WATOA HUDUMA YA HABARI MITANDAONI 'BLOGGERS'... 'YASISITIZA UMAKINI MTANDAONI'



Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.

****

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutana na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni 'Online Content Service Providers' nchini Tanzania kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 28,2020.

Mkutano huo umefanyika leo Jumanne Septemba 15,2020 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .

Akifungua Mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles amesema Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ni wadau muhimu katika mchakato wa uchaguzi ndiyo maana wameamua kukutana nao ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uchaguzi ili waweze kuandika habari kwa usahihi na kulinda amani ya nchi.

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi tunavipongeza vyombo vya habari mtandaoni kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkitupatia.Tunathamini mchango wenu na tutaendelea kushirikiana nanyi ili kujenga nchi yetu. Tumewaita ili kuwajengea uelewa kuhusu mkachato wa uchaguzi,tunaamini kuwa mna nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu taratibu mbalimbali za uchaguzi",amesema Dkt. Charles.

Aidha amewataka waandishi wa habari kuvipa nafasi sawa vyama vyote vya siasa na kuepuka kuandika habari zenye kuhamasisha vurugu na kusababisha uvunjivu wa amani.

"Kipindi cha Kampeni za uchaguzi huwa kuna joto la uchaguzi ambapo joto la kuvunja amani nalo huongezeka. Naomba tulinde amani ya nchi yetu kwa kuepuka kuandika habari zenye kuleta chuki",amesema.

Katika hatua nyingine alivitaka vyama vya siasa kufuata maadili ya uchaguzi na sheria za nchi na kuhakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu huku akivikumbusha vyombo vya habari kuepuka kuandika kauli na matamshi ya kuvunja amani.

"Kuanzia sasa tutachukua hatua kali kwa viongozi wanaotoa matamshi ya kuvunja amani. Hata wewe mwandishi wa habari ukiandika habari zenye kuunga mkono matamshi hayo nawe utakuwa unavunja amani",ameongeza Dkt. Charles.

Dkt. Charles ametumia fursa hiyo kuviomba vyombo vya habari kuelimisha jamii kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza sera za wagombea na kupiga kura Oktoba 28,2020 ili kupata viongozi wanaowataka watakaowaletea maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari, amesema.

"Vyombo vya Habari mitandaoni vina nguvu kubwa katika masuala ya siasa hivyo ni muhimu watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha mnatumia vyanzo sahihi vya habari ili habari Mnazoziandika ziwe sahihi,Habari zitoke kwenye vyanzo sahihi ili habari ziwe sahihi".


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati akifungua Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari akizungumza mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati wa Mkutano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),uliofanyika leo katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Mpigakura, Giveness Aswile akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (hawapo pichani),wakati wa Mkutano huo kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni,uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.
"Vyombo vya Habari mitandaoni vina nguvu kubwa katika masuala ya siasa hivyo ni muhimu watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha mnatumia vyanzo sahihi vya habari ili habari Mnazoziandika ziwe sahihi,Habari zitoke kwenye vyanzo sahihi ili habari ziwe sahihi", alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma, ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh Asina Omari.


Baaadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri

Kushoto ni Mkurugenzi wa Kahama Tv Online, Shija Felician na Mkurugenzi wa Malunde Media, Kadama Malunde wakiwa kwenye Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni

Sehemu ye Meza kuu 
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo.


Monday, September 7, 2020

ESTHER BULAYA TISHIO BUNDA…SHUHUDIA HAPA MKUTANO WAKE JIONI HII

  Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Ubunge jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 

Na Helena Magabe  -Bunda
Mgombea Ubunge jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameendelea na Kampeni zake za Uchaguzi ambapo leo Jumatatu Septemba 7,2020  amefanya Mkutano eneo la Stendi ya Zamani Bunda Mjini  huku mkutano wake ukihudhuriwa na maelfu ya wananchi waliofika kusikiliza sera zake.

Akizungumza katika mkutano huo Mgombea huyo wa Ubunge jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya amesema hatawaangusha wana Bunda endapo watamuongeza miaka mingine mitano huku akisisitiza kuwa wana Bunda wanataka Mwakilishi wa Wananchi sio wa Serikali.

Mgombea Ubunge jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa kwenye msafara

Friday, September 4, 2020

Namibia kufundisha mbwa kugundua virusi vya corona



Chuo Kukuu cha Namibia kitengo cha dawa ya mifugo kinawafundisha mbwa kubaini virusi vya corona kwa kunusa.

Mpango wa nchi hiyo ni kuwapelea nbwa hao katikaviwanja vya ndegena vituo vya mpakani, kwa mujibu wa mtandao wa The Namibian.


Mbwa wamethibitishwa kuwa na uwezo wa kubaini virusi vya corona kwa aslimia 95, mhadiri wa somo la tiba ya wanyama Alma Raath anasema.


Mradi huo ulianzishwa miezi miezi miwili iliyopita, inarsema taarifa ya mtandao huo wa The Namibian, lakini haujataja ni lini mbwa hao watakuwa tayari kufanya kazi.


Mtandao wa The Namibian unasema nchi hiyo itakuwa ya kwanza kutumia mbwa kubaini virusi vya corona.

WAGOMBEA MULEBA KUSINI WAJINOA VIKALI


Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo baada ya kupokea Ilani ya UchaguzI ya chama hicho kutoka kwa Mwenyekiti wa Mkoa Costancia Buhiye na kuhaidi kuinadi kwa wananchi.
 ***
Na Ashura Jumapili,Muleba
Wagombea wa Jimbo la Muleba Kusini katika nafasi ya Ubunge na Madiwani wameanza kunoa makali kupitia mikutano tofauti ya awali kabla ya uzinduzi rasmi wa kampeni utakaofanyika kesho siku ya Jumamosi Septemba 6,2020.

Mgombea Ubunge kupitia CCM Dr.  Oscar Kikoyo kwa nyakati tofauti ameshiriki mikutano iliyomkutanisha na wagombea wengine wa Ubunge na Udiwani kabla ya uzinduzi rasmi utakaofanyika katika uwanja wa Zimbihire mjini Muleba.

Katika uzinduzi wa kampeini ngazi ya Mkoa Dr. Kikoyo alihaidi kuinadi ilani ya CCM inayotoa mwelekeo wa ongezeko la miradi ya maendeleo na kutoa ufumbuzi wa changamoto zilizobaki katika awamu ya kwanza ya uongozi wa miaka mitano wa Rais John Magufuli.

Akiwa katika Kata ya Nshamba Dr. Kikoyo aliahidi kushirkiana na diwani wa Kata hiyo na wadau wengine kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la uhaba wa maji na kuinua elimu hasa ujenzi wa shule za kidato cha tano na sita katka Jimbo hilo.

Mkutano huo pamoja na viongozi mbalimbali pia unatarajiwa kupambwa na wasanii kutoka ndani na nje ya Wlaya ya Muleba ambapo wagombea udiwani wote wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo.
Mgombea Ubunge wa Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo akihutubia wananchi wa Kata ya Nshamba eneo la Muznga na kuwahaidi kasi ya maendeleo.
Baadhi ya wanachama na mashabiki wa CCM katika mkutano wa kampeni Kata ya Nshamba Jimbo la Muleba Kusini.
Mgombea Udiwani Kata ya Nshamba Gosbert Masilingi akijinadi kwa wananchi wa Kata hiyo kuomba achaguliwe tena kutekeleza ilani ya chama chake.
Mgombea Udiwani kata ya Kibanga Edson Issaya akinadi ilani ya CCM na mgombea wa chama hicho katika Kata ya Nshamba Gosbert Masilingi.
Mgombea Ubunge Muleba Kusini Dr Oscar Kikoyo akijadili jambo na baadhi ya wananchi baada ya mkutano katika eneo la Muzinga Kata ya Nshamba.
Mjumbe wa NEC kutoka Mkoa wa Kagera Wilbroad Mutabuzi akitoa nasaha kwa wagombea waliopita kwenye uteuzi wa vikao vya chama kunadi mafanikio ya awamu iliyopita na ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Mazinga iliyoko kwenye Ziwa Victoria Edson Alex akiwa tayari kusaka kura zake na wagombea wengine baada ya kukabidhiwa ilani na vitendea kazi vingine.
Mgombea udiwani kata ya Kishanda Helmes Mushumbusi akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika Kata ya Nshamba
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...