Tuesday, July 14, 2020

MTOTO WA MUUZA KAHAWA 'HASSAN FATIU' ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI


Wakili  Hassan Athuman Fatiu maarufu 'Mtoto wa Muuza Kahawa' akionesha fomu ya Kuomba Kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. 

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Hassan Athuman Fatiu ambaye ni Wakili na Mkulima wa mpunga, mkazi wa kata ya Kitangili amesema endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga kipaumbele chake kikubwa ni Ilani ya Uchaguzi ya CCM na vipaumbele binafsi vitakavyofikishwa katika ofisi ya mbunge. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Source

BANDORA MILAMBO AJITOSA KINYANG'ANYIRO CHA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI


Mfanyabiashara Bandora Salum Milambo mkazi wa Ngokolo Manispaa ya Shinyanga akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuchukua katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumanne Julai 14,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

MUSA NGANGALA AJITOSA KUWANIA UBUNGE SHINYANGA MJINI

Musa Jonas Ngangala akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
*****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Musa Jonas Ngangala amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Musa Jonas amewasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumanne Julai 14,2020 majira ya saa tatu na kuchukua fomu ya kuomba  kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Musa Jonas Ngangala ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Imalilo kata ya Kitangili katika Manispaa ya Shinyanga mwenye Elimu ya Shahada ya Mipango Miji na Maendeleo amesema endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini atahakikisha anasimamia na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

"Nimechukua fomu ili kuomba ridhaa chama changu kinipatie nafasi ya kwenda kuwatumikia wananchi,naamini chama changu kikinipitisha kugombea Ubunge nitakuwa mwakilishi mzuri wa wananchi katika kutatua kero za wananchi na kutekeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi",amesema Ngangala.
Musa Jonas Ngangala akinawa mikono baada ya kuwasili katika ofisi cha CCM wilaya ya Shinyanga Mjini kuchukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

EPL: Obafemi ainyima Manchester United fursa ya kuingia 4-bora




MSHAMBULIAJI Michael Obafemi, 20, alitokea benchi katika kipindi cha pili na kufungia Southampton bao la kusawazisha kunako dakika ya 96 katika sare ya 2-2 dhidi ya Manchester United.
Matokeo hayo yaliyosajiliwa na The Saints uwanjani Old Trafford yaliwanyima Man-United fursa ya kupaa hadi nafasi ya tatu kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa alama 61 na hivyo kuweka hai matumaini ya kukamilisha kampeni za msimu huu ndani ya mduara wa nne-bora.
Man-United kwa sasa wanashikilia nafasi ya tano kwa pointi 59 sawa na Leicester City wanaoorodheshwa mbele yao kutokana na wingi wa mabao.
Ilivyo, matumaini ya Man-United ya kufuzu kwa kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao, yanategemezwa kwa matokeo yatakayosajiliwa na Chelsea na Leicester katika mechi zao tatu za mwisho. Kujikwaa kwa Chelsea na kuteleza kwa Leicester katika mchuano wowote kati ya hiyo mitatu kutawapa Man-United uhakika wa kuwa miongoni mwa washiriki wa kivumbi cha UEFA mnamo 2020-21.
Licha ya kuchezea ugenini, Southampton walianza mechi kwa matao ya juu na wakajiweka kifua mbele kupitia kwa Stuart Armstrong aliyechuma nafuu kutokana na masihara ya Paul Pogba na kutikisa nyavu katika dakika ya 12.
Bao hilo la The Saints liliamsha hasira za Man-United waliosawazisha kupitia kwa Marcus Rashford kunako dakika ya 20 kabla ya Anthony Martial kufunga la pili dakika tatu baadaye.
Ilikuwa hadi mwishoni mwa kipindi cha pili, sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mechi ambapo Obafemi alijaza kimiani mpira wa ikabu uliochanjwa na Jan Bednarek na kuhakikisha kwamba wanaoondoka ugenini na alama moja kikapuni.
Ilitarajiwa kwamba kichapo cha 3-0 ambacho Chelsea walipokezwa na Sheffield United uwanjani Bramall Lane mnamo Julai 11 na kile cha 4-1 ambacho Bournemouth waliwapa Leicester City siku hiyo hiyo ugani Vitality, kingekuwa kiini cha hamasa ya Man-United hiyo iliyowakutanisha na The Saints.
Hata hivyo, kikubwa zaidi ambacho bado kinawaaminisha Man-United kuwa watakamilisha kampeni za EPL msimu huu miongoni mwa vikosi vinne vya kwanza, ni uzito wa vibarua vilivyopo mbele ya Chelsea na Leicester.
Baada ya kuvaana na Norwich City leo Julai 14 uwanjani Stamford Bridge, Chelsea watakuwa na mtihani mgumu dhidi ya Liverpool na Wolves katika michuano yao miwili ya mwisho. Mechi hizi za mwisho zitapigwa baada ya Chelsea kupimana ubabe na Man-United katika nusu-fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley mnamo Julai 19.
Leicester nao wana kibarua kikali cha kuwazidi maarifa Sheffield United uwanjani King Power kabla ya kuwaendea Tottenham kisha kupimana ubabe na Man-United katika mechi yao ya mwisho wa msimu huu ugani King Power.
Kwa upande wao, Man-United wanatarajiwa kuwa na mteremko mkubwa dhidi ya Crystal Palace na West Ham United kabla ya kufunga msimu dhidi ya Leicester waliotawazwa mabingwa wa EPL mnamo 2015-16.


Membe Akataa Kufananishwa Na Lowassa "Nachokifanya Kinaitaji Mwanaume Kama Mimi"


Aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya nje na mwananchama wa chama cha Mapinduzi (CCM) Bernard Membe amekataa kitendo cha kufananishwa na aliyekwa Waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa kutokana na kitendo chake cha kuhamia upinzani na kugombea urais.

Membe amesema hayo kwenye mahojiano kupitia televisheni mtandao inayoendeshwa na mwandishi mkongwe Jenerali Ulimwengu alipoulizwa juu ya mfanano wa anachokifanya na alichokifanya Lowassa kwenye uchaguzi wa 2015.

"Edward Lowassa hawezi kuwa kufuli la maendeleo ya siasa nchini hatuwezi kujipima kwa kipimo chake,historia ni kujalibu na kujifunza mimi nina mikakati yangu na yeye alikuwa na mikakati yake, ninachokifanya kinahitaji mwanaume kama mimi kutetea haki za wanyonge na hata mazingira ya kipindi kile na hiki ni tofauti"

Ikumbukwe kuwa Bernard Membe amekuwa kihusishwq na kujiunga na vyama kadhaa za siasa ili kugombea urais kwenye uchaguzi ujao jambo ambako lilifanywa na waziri huyo mkuu wa zamani kwenye uchaguzi wa 2015.

Dokii Aeleza Sakata la Harmonize Kumsaidia Mavoko



Baada ya maswali kuwa mengi kuhusiana na ukimya wa muda mrefu wa msanii Rich Mavoko, EATV & EA Radio Digital imepiga stori na Dada wa msanii huyo Dokii na amenyoosha maelezo kuhusu ukimya wa Mavoko na kusaidiwa na Harmonize.

Kuhusu ukimya wa msanii Rich Mavoko Dokii ameeleza kuwa "Hata kama haonekani wamuache atulie, kama kuna tatizo wao watamsaidia nini, waache wakisikia tatizo kuhusu Mavoko ndiyo waniulize ila kwa sasa kila kitu kipo sawa, waache wawe na shauku ya kumuona hadi pale atakapotoka kuna vitu vizuri vinakuja".

Aidha akizungumzia suala la Harmonize kutaka kumsaidia Rich Mavoko kupitia post aliyoweka katika mtandao wa Instagram siku kadhaa zilizopita, Dokii amesema "Ilikuwa ni jambo zuri kama limetoka moyoni mwake, ulikuwa ni ujumbe mzuri na niliufurahia kwa sababu anajua anachofanya, Harmonize hajafanya jambo baya".

Sunday, July 12, 2020

HOTELI MPYA YA KISASA 'SHY PARK HOTEL' KUFUNGULIWA RASMI AGOSTI,2020 SHINYANGA MJINI...NAFASI ZA KAZI ZATANGAZWA

Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 2020;  Mkurugenzi wa SHY PARK HOTEL anawatangazia nafasi za kazi wale wote waliosomea na wenye uzoefu wa Masuala ya Usimamizi wa Hoteli.

SHY PARK HOTEL IKO WAPI?
SHY PARK HOTEL inapatikana Lubaga Mjini Shinyanga karibu na Ikulu pembezoni mwa Barabara ya Old Shinyanga.

HUDUMA ZINAZOPATIKANA SHY PARK HOTEL
Shy Park Hotel inatoa huduma za malazi 'vyumba vya kulala' ,vyakula ikiwemo nyama choma, vinywaji, kumbi za sherehe/harusi na mikutano, Swimming pool kwa watoto na watu wazima, michezo mbalimbali ya watoto, Sauna, Massage, Gym, Car wash, Car Parking n.k

NAFASI ZA KAZI
Shy Park Hotel inakaribisha maombi ya kazi kwa waliosomea masuala ya Usimamizi wa Hoteli 'Hotel Management na wenye uzoefu wa kutoa huduma tajwa hapo juu.

SIFA ZA WAOMBAJI WA KAZI
Sifa za muombaji awe na umri wa miaka kuanzia 20, awe na taaluma ya Usimamizi wa Hoteli 'Hotel Management' au mwenye uzoefu wa usimamizi wa hoteli. Watume maombi wakiambatanisha na barua ya udhamini iliyopitishwa na serikali ya mtaa.

KUTUMA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe ofisini, Fika SHY PARK HOTEL
Au kupitia  Email info@shypark.co.tz  au Whatsapp namba 0759096494
Kwa Mawasiliano zaidi piga simu namba 0621288344 

Mwisho wa kutuma maombi ni Julai 17,2020 saa sita mchana, usaili 'Interview' itafanyika Julai 18,2020

Karibu SHY PARK HOTEL
Picha mbalimbali muonekano wa majengo ya Shy Spark Hotel iliyopo Mjini Shinyanga.


Muonekano wa vitanda
Muonekano sehemu ya Sauna

Kanuni bora za ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili)....Soma Hapa Uwe Tajiri

Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. 

Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi.

 Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. 

Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.

2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.

3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.

4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.

5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.

6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.

7.Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.


Magonjwa na kinga kwa kuku wote

1.Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.

2.Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

3.Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.

4.Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

5.Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.

6.Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.


Chakula cha ziada
1.Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.

2.Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).

3.Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.

4.Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.

5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng'ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.

6Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.

Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.

2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.

2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.

3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.

4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.

5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.

Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.

3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wiki 2 toka kutagwa.

4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.

5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti

Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.

Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasiende mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.

Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.

2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba

3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;

Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.

2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja

3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.

4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.

5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.

6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.

7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.

8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.


Saturday, July 11, 2020

MAGUFULI AMCHAGUA SAMIA SULUHU KUWA MGOMBEA MWENZA URAIS TANZANIA


Samia Suluhu Hassan
Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli amemchagua Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM.

Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano alichofanya kazi na Mama Samia kama makamu wa Rais amejifunza mengi na ameamua kuendelea naye katika awamu ya pili.

''Katika kipindi nilichofanya kazi na Mama Samia nimejifunza mambo mengi sana na kupitia yeye nawahikikishia nitakuwa mtetezi mzuri wa wanawake. Nimekuwa nikimtuma popote hakatai kama na nyie kina Mama mkitumwa hamkatai'', amesema.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...