Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeanza kutoa huduma ya matibabu ya kuvunja mawe kwenye figo na mfumo wa mkojo kwa njia ya mawimbi mshituko kwa kitaalam Extracorporeal shock wave lithotripsy (ESWL).
Kuanzishwa kwa matibabu haya ni mwendelezo wa kutekeleza juhudi za Serikali za kuboresha huduma bobezi za kibingwa nchini ili kuongeza wigo wa huduma ambazo hapo awali zilikuwa hazipatikani hapa nchini kutokana na kutokuwepo kwa wataalamu, vifaa tiba au vyote viwili. Huduma hii inatolewa na wataalamu wazawa walioko Upanga na Mloganzila.
Huduma hii inafanywa kwa kutumia mashine ambayo inatoa mawimbi sauti yanayosafiri kupitia ngozi hadi kwenye figo sehemu yenye jiwe au mawe. Mawimbi hayo hugeuka kuwa nishati yenye uwezo wa kuvunja mawe kuwa madogo mithili ya mchanga ambapo yakishasagwa yanatoka kwa njia ya haja ndigo (kukojoa).
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa huduma hii mapema Juni mwaka huu jumla ya wagonjwa wanane wamenufaika na matibabu haya.
"Tumeanza kutoa huduma hii mapema Juni mwaka huu jumla ya wagonjwa wanane wameshanufaika na matibabu haya ambayo yameonesha matokeo mazuri, na hivi leo wagonjwa wawili wanaendelea kuhudumiwa hivyo kufikisha idadi ya wagonjwa 10 tangu ilipoanzishwa" amesema Prof. Museru.
Aidha Prof.Museru ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2019 jumla ya wagonjwa 1035 wenye mawe kwenye figo walionwa katika kliniki za wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila ambapo kati ya hao wagonjwa wapya walikuwa 425 wakati wagonjwa waliolazwa kutokana na tatizo hilo walikuwa 114.Pia katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2017 jumla ya wagonjwa 23 wenye matatizo ya mawe kwenye figo walipatiwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mfumo wa Mkojo MNH-Mloganzila Dkt. Hamis Isaka ametaja faida ya matibabu haya, kuwa hayahitaji mgonjwa kulazwa hospitalini kwani anaweza kutibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyo hiyo ili kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.
"Faida ya upasuaji huu ni kuwa mgonjwa anaweza kufanyiwa siku hiyo hiyo na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zake za kila siku pia uwepo wa huduma hii unaondoa ulazima wa upasuaji mkubwa kwa wagonjwa hawa" amesema Dkt. Isaka.
Dkt. Isaka ameongeza kuwa ziko sababu mbalimbali zinazosababisha ugonjwa huu kuwa ni uwepo wa madini kwa wingi katika mkojo, mfano madini aina ya calcium oxalate, citric acid na wakati mwingine inatokana na kutengeneza kiwango kidogo cha mkojo katika figo hasa kwa wale ambao hawanywi maji ya kutosha.
Vilevile maambukizi ya bakteria katika mfumo wa mkojo yanaweza kusababisha kupata ugonjwa wa mawe kwenye mfumo wa mkojo. Kwa kiasi kikubwa waathirika zaidi wa ugonjwa huu ni wenye umri kati ya miaka 40 mpaka 70.
Kwa upande wake mmoja wa mashuhuda ambaye amepatiwa huduma hii hospitalini hapa Bi. Mwajuma Mbangwi ameishukuru hospitali na kueleza kuwa kabla ya matibabu alikuwa akipata maumivu makali lakini kwa sasa afya yake imeimarika kabisa.
Hospitali itaendelea kushirikiana na nchi marafiki katika kufanikisha azma hii, tunatoa shukrani kwa African Future Foundation kupitia KOFIH ya Korea Kusini ambao tumeshirikiana kupitia mtandao (Zoom) kwa mgonjwa wa kwanza hatua ambayo imeleta matokeo mazuri katika kutoa tiba hii ya kibobezi.
Thursday, June 18, 2020
Bulembo "Unachukuaje Fomu ya URAIS Wakati Magufuli Hajamaliza Vipindi vyake Viwili?"
Aliyekuwa Mbunge wa kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amesema taratibu haziruhusu mwanachama mwingine kuchukua fomu ya kugombea Urais zaidi ya John Magufuli
Amefafanua, "Kwa mujibu wa sheria kama wewe ni mwana-CCM, Rais anatakiwa awe katika vipindi viwili sasa unatokea wapi kuchukua fomu? Unajadiliwa kikao gani?"
Bulembo amesema hataki kugombea (Ubunge) licha ya kwamba anajua atashinda na kwamba haiwezekani nyumba nzima wawe Wabunge
Ameongeza, "Nataka niondoke salama, mtoto wangu Halima yupo kwenye jimbo, mke wangu naye yupo kwenye jimbo anagombea Viti maalum, haiwezekani nyumba yote kuwa Wabunge haileti picha nzuri"
Aidha, amesema "Nimejifunza vingi tangu nimeteuliwa na Rais, wenzetu wanaoendelea kutafuta majimbo wanaendelea kugombea, juzi Rais alivyosema kwa herini kila Mtu ameshakwenda kwenye jimbo lake, bado nipo Dodoma napumzika, niko kwenye kustaafu, sina presha sina haraka ya kwenda popote"
Mahakama Yaipa Serikali Siku 7 Kesi Ya Tundu Lissu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambao wanataka mshtakiwa huyo akamatwe ili wajitoe udhamini.
Maombi hayo namba 2/2020 yalikuja jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo upande wa Jamhuri uliomba kuongezewa muda wa kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliiomba mahakama iwaongezee muda ili waweze kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani kutokana na maombi yaliyowasilishwa na wadhamini hao.
Hakimu Simba alikubali maombi hayo na kuwapa upande wa Jamhuri muda ambapo wametakiwa ndani ya siku saba wawe wamewasilisha majibu hayo na maombi yatasikilizwa Julai 14.
"Kesi ya msingi namba 208 ya mwaka 2016 itatajwa Julai 14 mwaka huu ikisubiri maombi kusikilizwa na kutolewa uamuzi," alisema Hakimu Simba.
Februari mwaka huu, wadhamini wa Lissu kwa nyakati tofauti waliieleza mahakama kuwa wamewasilisha maombi mahakamani hapo kuomba itoe hati ya kukamatwa Lissu ili waweze kujitoa udhamini kutokana na mtuhumiwa huyo kutohudhuria katika kesi yake.
Wakili Wankyo alikiri kupokea maombi yaliyoambatanishwa na hati ya kiapo na kuomba mahakama iwape muda wa kutosha waweze kuyachambua.
"Tumepokea hati ya kiapo cha maombi ya wadhamini, tunaomba mahakama itupe muda wa kutosha ili tuweze kuchambua maombi hayo kwa sababu yana vitu vingi," alidai Wankyo.
Lissu na wenzake wanne katika kesi ya msingi, wanakabiliwa na mashtaka matano, ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.
Inadaiwa kati ya Januari 12 na 14, 2016 Dar es Salaam, washtakiwa Jabir Idrisa, Simon Mkina na Lissu waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho 'Machafuko yaja Zanzibar'.
Katika shtaka la pili, wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.
Mshtakiwa Ismail Mehboob ambaye ni mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, anadaiwa kuwa Januari 13, 2016 katika jengo la kampuni hiyo lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.
Ilidaiwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
Mto Wami: Mmiliki wa LORI Akata Tamaa na Kurudu DSM "Inaumwa Wameshindwa Kulitoa Lori Mtoni Namuachia Mungu"
Mto Wami: Mmiliki wa LORI Akata Tamaa na Kurudu DSM "Inaumwa Wameshindwa Kulitoa Lori Mtoni Namuachia Mungu"
Tazama Hapa VIDEO Akifunguka...kwa Kweli Inasikitisha:
Source
Serikali Kuwachukulia Hatua Kali Za Kisheria Wafanyabiashara Wa Mafuta Wanaoficha Nishati Hiyo
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa amezielekeza FCC, EWURA, WMA kufanya ukaguzi na kuwachukulia hatua wafanyabiashara na waagizaji wa mafuta wanaoficha bidhaa hiyo kwa lengo la kuyauza kwa bei ya juu yatakapoadimika au kupanda bei.
Waziri Bashungwa aliyasema Juni 17, 2020 jijini Dar es salaam katika kikao kazi na Watendaji wa Mamlaka za Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Vipimo (WMA), Mamlaka ya Bandari (TPA) pamoja na TRA kwa lengo la kufanya mapitio na marekebisho ya utaratibu wa kanuni ya bei elekezi ya mafuta kwa bidhaa za petroli zinazoingizwa nchini kupitia bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga, kwa nia ya kuwezesha manufaa ya punguzo la bei kuwafikia wananchi sa mikoa yote nchini kwa usawa.
''Katika kipindi cha mapambano ya Covid-19, moja ya fursa tulizozipata kama nchi ambayo pia tulipata maambukizi ni kushuka kwa bei ya mafuta, na sisi kwa sababu tunaingiza mafuta kutoka nje ya nchi, kushuka kwa bei ya mafuta duniani sisi tumenufaika lakini pamoja na kunufaika huku kwa kushuka kwa bei ya mafuta kuna baadhi ya mikoa bado bei ipo juu"
Aidha, Bashungwa ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wote ambao bado wana tabia za kuficha bidhaa mbalimbali pindi zinaposhuka bei au kuadimika kwa lengo la kujipatia kipato kikubwa, ameielekeza taasisi ya Tume ya Ushindani na Ewura kufanya msako mkali kama ulifanywa kwenye sukari ili kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaoendeleza tabia hizo
"Wafanyabiashara tunajua bei ambazo wananunulia mafuta na kipindi cha COVID-19, mfanyabiashara yoyote ambaye amenunua mafuta kwa bei ya punguzo lakini punguzo hilo halijaenda moja kwa moja kwa mlaji kwa maana ya mwananchi maeneo yote nchini ambayo wafanyabiashara hawa wanaingiza mafuta na kusambaza, tutatumia taasisi zetu ya Tume ya Ushindani na Ewura kuhakikisha kote nchini tunafatilia na kama kuna mfanyabiashara yoyote wa mafuta ambaye ana hodhi mafuta ili kupata faida tutatumia sheria kumchukukulia hatua kali kama tulivyofanya kwenye sukari,"
Waziri Bashungwa amesisitiza kuwa kuwa mapendekezo ya wataalamu katika kikao kazi hicho yatapelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini baada ya kukamilika leo hii ili kumshauri kuhusu namna ya kuweka uwiano sawa wa bei elekezi kwa bidhaa husika, huku akisisitiza kuwa wafanyabiashara watakaobainika kukiuka taratibu za leseni walizopatiwa na EWURA na wanaokiuka kanuni, sheria na taratibu za Ushindani watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwamo kunyang'anywa leseni za kufanya biashara ya bidhaa za petrol
Awali, Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kuwa "Mafuta yanayouzwa nchini yanapokelewa kupitia bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara. Katika kukokotoa bei ya mafuta, mikoa ya Kaskazinini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) hupangiwa bei zao kulingana na gharama ya mafuta yanayopokelewa kupitia bandari ya Tanga. Mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma) hupangiwa bei kulingana na gharamaya mafuta yanayopokelewa kupitia bandari ya Mtwara. Mikoa mingine yote hupangiwa bei zao kulingana na gharama ya mafuta yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es salaam.
Sambamba na hayo Mhandisi Godfrey amesoma mapendekezo ambayo yataleta mabadiliko ya kanuni za kukokotoa bei za mafuta ambayo ni;
Kuweka usawa wa premium kwa bandari zote na hivyo kuwa na bei za mafuta zenye ushindani na watumiaji wa mafuta kununua kwa bei ambayo ina usawa, kuweka kanuni za kubadilisha gharama za mafuta kila mwezi kulingana na mabadiliko ya soko la dunia, kuendelea kuwepo kwa nafasi ya ushiriki wa kampuni za wazawa katika zabuni za BPS.
NEW VIDEO: Ibra Jack Ametuletea Hii ya Walevi Inaitwa Bapa
Music produced by ibra jacko, directed by eddy
Huu ni wimbo umeandaliwa na #Ibrajacko unaoelezea juu ya athari za pombe kupitiliza katika maisha ya mwanadamu na hasara anazopokea endapo ataiweka katika harakati zake hivyo yapi yanapaswa kuzingatia muhimu zaidi #Bapa
Muingizaji wa Vichekesho Dorah Alilia PENZI la Harmonize "Nampenda Harmonize Lakini Hanielewi"
Ni Maneno ya Mwigizaji Dorah Kuhusu Swala Zima la Kumtaka Kimapenzi Harmonize Hikiwa na Yeye Teyari Anampenzi Wake SarahTz.
"Ni siku nyingi nimesema nampenda sana Harmonize kimapenzi lakini hanielewi kabisa sijui kwa vile ana mtu wake anayempenda"
Una Nini Cha Kuishauri Dorah Kulingana na Kile Alicho Kisema Kwa Harmonize? Tuambie Hapa Tafadhali.
Huu hapa Msimamo wa ligi kuu bara
MSIMAMO wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi ya jana kati ya JKT Tanzania na Yanga upo namna hii
Wednesday, June 17, 2020
TAKUKURU Yatahadharisha Rushwa Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020....Yasema Atakayebainika Na Rushwa Ataonja Jiwe La Joto La Sheria.
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU,Brigedia Jenerali John Mbungo amewatahadharisha wanasiasa wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Udiwani na Ubunge kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kampeni za uchaguzi kwani atakayebainika ataonja joto la jiwe.
Brigedia Jenerali Mbungo ametoa rai hiyo hii Juni 17,2020 Ofisini kwake Makao Makuu ya TAKUKURU Jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.
Amebainisha kuwa ni vyema sasa kwa wagombea na watia nia ambao wanatarajia kuwania nafasi hizo mblimbali za uongozi kujitathmini kwa kina na kuona kama wanafaa kuwa Viongozi na kama hawafai ni bora waache kuliko kuingia na kuanza kuwarubuni Wapiga kura kwa kuwapa hongo ya vitu mbalimbali ikiwemo fedha pamoja na Chakula ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi Mkuu Taasisi yake imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitaka nafasi za uongozi jambo ambalo ni kinyume na Sheria za Uchaguzi.
Pia amewaonya wananchi kuacha kujiingiza katika vitendo vya rushwa kwakudhani kuwa mchakato huo wa uchaguzi ni wa mavuno kwao kwa kujipatia chochote kwa njia ya rushwa.
Mkurugenzi huyo wa TAKUKURU ametaja madhara ya rushwa ni pamoja na kudumaza demokrasia,kuwa na viongozi wasiowajibika.
Uchaguzi Mkuu wa Madiwani na Wabunge unatarajiwa kufanyika Oktoba25 Mwaka huu.
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...











