Saturday, March 28, 2020

VISA VYA MAAMBUKIZI YA CORONA VIRUS VYAONGEZEKA UGANDA NA KENYA, WAWILI WAPONA.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

CHANZO:BBC SWAHILI

Kenya imethibitisha visa saba zaidi vya maambukizi ya ugonjwa wa coronavirus, huku Uganda ikiandikisha visa vingine vitano vya ugonjwa huo hatari.
Akizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Jumamosi, waziri wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amesema kwamba idadi hiyo inaongeza visa vya maambukizi nchini Kenya kufikia 38, huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki naye mwingine akipona maambukizi hayo.
Waziri Kagwe amesema kwamba kufikia sasa mji mkuu wa Nairobi unaongoza kwa maambukizi ya visa 28.
Amesema kwamba kati ya visa hivyo saba kuna Wakenya wanne raia wawili wa DR Congo na raia mmoja wa China.
Ameongezea kwamba idadi hiyo ni miongoni mwa watu 81 ambao walifanyiwa vipimo katika maabara tofauti nchini katika kipindi cha saa 24.
Maambukizi ya virusi vya corona yaongezeka kote duniani huku China yakipunguaHaki miliki ya picha
Image caption

Amesema wanne kati ya visa hivyo ni watu wenye historia ya kusafiri katika mataifa yenye idadi kubwa ya maambukizi huku mmoja akiripotiwa kusafiri hadi Mombasa nao wengine wawili wakiambukizwa na visa vya awali.
Vilevile waziri huyo alikuwa na habari njema pale aliposema kwamba wagonjwa wawili waliokuwa wakiugua virusi hivyo wamepona.
''Mgonjwa wetu wa kwanza na watatu wamepona virusi hivyo , watafanyiwa vipimo vingine katika kipindi cha saa 48 , tuna matumaini kwamba vipimo hivyo vya pili vitabaini kwamba wamepona kabisa ili kuruhusiwa kutoka katika vituo vyetu vya tiba'', alisema.

Nairobi inaongoza kwa maambukizi

Amesema kwamba visa vyote saba vinatoka katika kaunti ya Nairobi ikiwa ndio inayoongoza , ikifuatiwa na kilifi visa 6, Mombasa visa 2 huku kajiado na Kwale zikiwa na kisa kimoja kila moja.
Aidha waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kujitenga akisema mwanae na mpwa wake wametengwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
''Mimi mwenyewe nina mwanangu ambaye amewekwa karantini . Pia nina mpwa wangu ambaye amewekwa karantini . Tunachosisitiza ni kwamba wakati mtu anapowekwa katika karantini anajilinda yeye na maisha ya wengine'', alisema Kagwe bila kutoa maelezo zaidi.
Image caption

Nchini Uganda

Wakati huohuo Idadi ya watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda imeongezeka na kufikia 23 kutoka 18 baada ya watu wengine watano kukutwa na maambukizi siku ya Ijumaa.
Kati ya sampuli 227 zilizofanyiwa vipimo siku ya Ijumaa watu 222 hawakupatikana na virusi vya corona huku watu watano wakipatikana na ugonjwa huo, alisema Dkt. Jane Ruth Aceng katika chapisho lake la mutandao wa twitter.
''Waganda tafadhalini fuateni maelezo na mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivi. Tunaweza kuzuia maambukizi ya virusi hivi pamoja'', alisema afisa huyo.
Haki miliki ya picha
Hata hivyo Aceng hakutoa maelezo ya watu walioambukizwa.
Rais Museveni alisema kwamba kutokana na visa hivyo vipya huenda kukawa na umhimu wa kuchukua hatua kali zaidi ili kuzuia maambukizi kulingana na ujumbe wa twitter uliotumwa na katibu wake wa maswala ya habari bwana Don Wanyama .
Maafisa wa afya wanasema kwamba watu wote 14 waliothibitishwa hapo awali kuwa na virusi hivyo wanaendleea vyema katika hospitali ya Entebbe Grade B , Hospitali ya Mulago na hospitali kuu ya Adjumani.
Je utajilinda vipi?
jinsi ya kulinda dhidi ya virusi
Presentational white space

Presentational white space
Tumia kitambaa kuziba
Iwapo huna tishu tumia sehemu yako ya mkono
Jizuie kugusa macho yako , pua na mdomo iwapo hujaosha mikono
Jiepushe na watu ambao ni wagonjwa
Presentational white space

Je dalili ni zipi?

Presentational white space
Hizi ndizo ishara za ugonjwa huu
Presentational white space

Nifanyeje iwapo sijisikii vyema?

Piga simu ili upate usaidizi
Presentational white space
Pia unaweza kushauriwa usalie nyumbani
Presentational white space

Unaweza kufanyiwa vipimo vya virusi

Rashford Awatoa Hofu Mashabiki wa United “Niko Fiti zaidi ya Mara 10” Wachezaji 8 wa West Ham Wawekwa Karantini kwa Kuonekana na Dalili za Corona

Mshambuliaji wa Manchester United Marcos Rashford awatoa hofu mashabiki wa United.

"Nipo fiti zaidi mara 10, Nipo katika nafasi nzuri zaidi, Nina furaha kuliko vile niliyokuwa nayo mwezi mmoja uliopita, mambo yanaonekana kuwa mazuri zaidi kwangu kutokana na jeraha nililokuwa nalo, Niko ndani nafanya mazoezi, nasoma vitabu na kuangalia movie"

Mbali na hilo imeaelezwa kuwa wachezaji nane (8) wa klabu ya West Ham kutoka nchini Uingereza wamewekwa karantini baada ya kuonekana na dalili za virusi vya Corona. Chanzo ( Karren Brady)

Yaelezwa kuwa wachezaji nane (8) wa klabu ya West Ham kutoka nchini Uingereza wamewekwa karantini baada ya kuonekana na dalili za virusi vya Corona. Chanzo ( Karren Brady)

VIDEO: Askari wawili wafariki kwa ajali ya gari wakiwa doria

Askari wawili wa wanyamapori ambao ni wafanyakazi wa hifadhi ya taifa ya mikumi wamefariki na mmoja kujeruhiwa wakati wakifanya doria katika hifadhi hiyo kwenye barabaraya morogoro iringa   baada ya gari walilokua wakitumia katika doria hiyo kupinduka.

TAZAMA FULL VIDEO CHINI..... USISAHAU KUSUBSCRIBE

Source

Chidi Benz Aomba Msamaha Watanzania Baada ya Kufanya Mzaa Kuhusu Ugonjwa wa Corona

Kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV inayoruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 usiku hadi 5:00 usiku, MwanaHipHop maarufu hapa nchini Chidi Benz, ameomba msamaha kwa wananchi juu ya kuleta utani kwenye janga la ugonjwa wa virusi vya Corona.

Chidi Benz ameomba msamaha huo baada ya kusambaa kwa video mitandaoni ikimuonyesha anazungumzia ugojwa huo kwa njia ya utani kupitia chombo kimoja cha habari kwa kusema

"Corona ni mafua ambayo yamekuwa ni mara mbili yake, watakaoathirika ni wale ambao mfumo wao wa pua utakua unashika vumbi kwa haraka ila kwa sisi Waafrika ukikamua mafua yanatoka kama keki Corona haipiti kokote" 

Aidha akiomba msamaha huo Chidi Benz ameeleza kuwa 

"Kuhusiana na Corona ni ugonjwa ulio serious mtu yoyote asiuletee utani, mimi naomba msamaha kwa kile nilichokifanya kuhusu Ugonjwa wa Corona, ile niliongea kama utani tu ili nisichanganye watu".

UPDATE YA MAAMBUKIZI YA CORONA TANZANIA

"Kwa kipindi cha masaa 24 tangu Machi 27, 2020 jumla ya sampuli 26 zimewasilishwa kwa vipimo katika Maabara Kuu ya Taifa Dar es Salaam na zote  zimethibitishwa na wataalamu wa maabara kuwa hazina  maambukizi (Negative), hivyo mpaka sasa nchi bado ina idadi ya watu 13 waliothibitika kuwa na maambukizi (Positive)."

Source

Kenya yaanza kutekeleza amri ya kutotoka nje wakati wa usiku ili Kukabiliana na Corona

Amri ya kutotoka nje nchini Kenya kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri ilianza kutekelezwa majira ya saa moja jana huku wafanyakazi wa huduma muhimu pekee wakiruhusiwa kuwa nje usiku.

Jana majira ya saa kumi na mbili Wakenya wengi mjini Nairobi walionekana wakiharakisha kuelekea nyumbani hatua iliyosababisha msongamano mkubwa katika barabara kadhaa huku wale waliokuwa wakitumia usafiri wa umma wakionekana kusubiri katika vituo vya magari hayo licha ya muda kuyoyoma.

Magari machache ya abiria mashuhuri kwa jina la 'Matatu' nchini Kenya yaliyokuwepo yalitumia fursa hiyo kujitengezea fedha baada ya kuongeza nauli huku baadhi yao yakikiuka agizo jipya la kupunguza idadi ya abiria ndani ya magari hayo ili kuwaepusha maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya Hillary Mutyambai alionya jana kwamba wale watakaopatikana nje ya nyumba zao baada ya saa moja usiku watakabiliwa iwezekanavyo.

Hata hivyo mjini Mombasa na Eldoret mpango huo ulianza kwa mkosi baada ya maafisa wa polisi kukabiliana na wakaazi saa mbili kabla ya amri hiyo kuanza kutekelezwa.

Credit:Parstoday

Dr Mwaka Hataki Mchezo Kabisa..Aachia Ushahidi wa PICHA Kwamba Analala Kitanda Kimoja na Wake zake Wawili

Dr Mwaka Mtabibu wa magonjwa ya Wanawake Tanzania akiwa na wake wake wawili katika kitanda kimoja, Siku si nyingi Dr Mwaka na wakeze hao wawili alikaririwa akisema yeye na wake zake wanalala kitanda kimoja kitu ambacho kilileta ngumzo mitandaoni

Pichani ni Dr Mwaka ameamua kuvujisha picha kumaanisha alichokuwa anakisema kina ukweli

Friday, March 27, 2020

MKE NA MUME WATIWA MBARONI KWA KUSAMBAZA UONGO KUHUSU CORONA NDANI YA DALADALA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watu wawili ambao ni mume na mke kwa tuhuma na kueneza taarifa za uongo kwa wananchi kuhusu ugonjwa COVID-19(Corona) na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Akizungumza leo  Machi 27 mwaka 2020 ,Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema watu hao wamekamatwa Machi 20 mwaka huu saa saba mchana  wakiwa kwenye daladala aina ya Toyota DCM namba T 119 DKS iliyokuwa ikitokea Muhimbili.

"Tunawashikilia watuhumiwa wawili Boniphace Mwita na Mkewe Rosemary wakazi wa Tabata,DSM kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu corona wakiwa kwenye daladala ambapo walianza kupotosha, kukejeli na kutania kwa kusema Serikali inapotosha Wananchi kwamba kuna corona"-Amesema Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa kutokana na kejeli na uzushi wa watu hao abiria waliokuwepo ndani ya daladala hiyo walikasirishwa na kuchukua hatua za kuwaweka chini ya ulinzi na  kuitaka daladala hiyo ipelekwe Kituo cha Polisi na sasa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya hatua inayofuata ya kuwapeleka mahakamani.

"Baada ya Mwita na Mkewe kusema Serikali inapotosha kuhusu corona na haina fedha ndio maana imefunga shule na vyuo kwa kisingizio cha corona, abiria ktk daladala iliwakera wakawaweka chini ya ulinzi wakamuamuru Dereva apeleke gari Polisi, tunao, tutawapeleka Mahakamani"-Mambosasa

Amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi limeshachukua maelezo ya watuhumiwa hao na jarada tayari wameshapeleka kwa Wakili wa Serikali kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Mke na Mume Watiwa Mbaroni Kwa Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu Corona

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...