Friday, July 26, 2019
Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa sisi ni Taifa huru - Rais Magufuli
Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema nchi imeudhihirishia ulimwengu kuwaTanzania ni Taifa huru na sio masikini.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa bwawa la kufua umeme la mto Rufiji.
"Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa sisi ni Taifa huru na sio masikini,mradi huu ulipigwa vita ndani na nje ya nchi tangu tulipoonesha nia ya kuujenga, kwakuwa nchi yetu huru na sio masikini tuliamua tuutekeleze kwa fedha zetu wenyewe," amesema Rais Magufuli.
"Mradi huu utazalisha umeme mwingi kuliko umeme wote uliozalishwa nchini tangu tumepata Uhuru, tutakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu, ujenzi wa uchumi wa viwanda kokote Duniani ni lazima uwe na uhakika wa umeme wa bei nafuu, mradi huu ni suluhisho."
Source
Joto Kali Lakumba Ulaya
Joto kali limeendelea kukumba miji kadhaa kaskazini magharibi mwa Ulaya huku viwango vya joto vikizidi kuongezeka na kuweka rekodi mpya nchini Uholanzi, Ubelgiji, Ujerumani na Ufaransa.
Hapo jana Ujerumani ilirekodi kiwango cha juu zaidi cha nyuzi joto 42.6 katika mji wa Lingen, kaskazini magharibi mwa jimbo la Saxony.
Katika mji mkuu wa Ufaransa Paris, viwango vya juu vilifikia nyuzijoto 42.6. Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo Meteo France imesema hicho ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa.
Baadhi ya miji ya Uholanzi na Ubelgiji pia imekumbwa na joto kali na maafisa katika nchi kadhaa wametoa tahadhari.
Hata hivyo viwango vya joto, vinatarajiwa kushuka leo Ijumaa na kesho

Thursday, July 25, 2019
MAKONDA APOKEA MIL 23 KUFADHILI MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60 WENYE UHITAJI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 25 amepokea zaidi ya Shilingi Milioni 23 kutoka kwa wadau ambao wameguswa na kampeni aliyoanzisha ya ufadhili wa matibabu ya upasuaji moyo kwa watoto 60 kutoka familia zenye hali duni.
Miongoni mwa Wadau waliomuunga Mkono Makonda ni Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe. Sylvester Koka ambaye amekabidhi hundi ya Shilingi milioni 10 kwa ajili ya matibabu ya watoto 5 huku Mkurugenzi wa Dorka Catering Bi. Dorothy Kansolele akichangia milioni 6 na mkurugenzi wa kampuni ya Abe Professional Sound Bw. Abraham Ngomko akichangia Milioni 6 kwaajili ya matibabu ya watoto 3.
Akipokea fedha hizo Makonda amezikabidhi kwa uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kueleza kuwa zitasaidia kugharamia zaidi ya Watoto10 kwenye upasuaji wa awamu ya pili.
Aidha Makonda amewashukuru wadau wote wanaondelea kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo inayolenga kuokoa maisha ya watoto ambao wangeweza kupoteza maisha kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Kwa upande wao wadau waliokabidhi fedha hizo wameeleza kuwa wataendelea kuunga mkono zoezi hilo kwa kuongeza fedha nyingine kwakuwa wanaamini kampeni aliyoanzisha Makonda ni njema na linapaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali ili kuokoa maisha ya watoto.
Friday, July 19, 2019
UMEONA PICHA WATU WAKIONEKANA VIJANA AU WAZEE MTANDAONI?? .....SENETA KAAGIZA APP YA 'FACEAPP' ICHUNGUZWE

Seneta mwandamizi wa jiji la New York nchini Marekani Chuck Schumer amewataka FBI kufanya uchunguzi kuhusu mtandao wa FaceApp ambao umekuwa ukitumika kubadili picha ya mtu kumuonyesha akiwa mzee au kijana.
Hatua ya Shumer imekuja siku moja baada ya app hiyo kutumiwa na watu maarufu duniani wakiwamo wanamichezo, wasanii na viongozi wa siasa.
Kupitia barua aliyoiweka kwenye mtandao wa Twitter Julai 18, 2019 Schumer alisema kuwa app hiyo inamilikiwa na kampuni ya Urusi ambako ndiko yalipo makao makuu ya kampuni hiyo inachukua data za maelfu ya picha zinazotokana na utumiaji na kuwapo kwa hatari ya kudukuliwa habari zao.
Ikumbukwe kuwa vyombo vya habari vya Magharibi huhusisha chochote chenye historia ya kuwa cha Urusi huwa kinahusishwa na ujasusi.
Kufuatia barua ya Schumer kampuni ya Wireless Lab ambayo ndiyo wamiliki wa app hiyo wameshatoa ufafanuzi ikisema ingawa makao makuu ya app hiyo ni Urusi ila servers zinazotumika katika kupokea na kutengeneza picha mpya hazipo nchini Urusi.
Kampuni hiyo imenukuliwa na BBC ikisema kuwa wanachofanya ni kukusanya picha maalumu zilizotumwa kwa ajili ya kuzihariri.
Wednesday, July 17, 2019
Tanzania kuwasilisha Umoja wa Mataifa taarifa ya Mapitio ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akifuatilia ufunguzi wa mikutano ya Jukwaa la Juu la Kisiasa la Ngazi za Mawaziri chini ya Umoja wa Mataifa inayofanyika New York nchini Marekani. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. John Jingu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo.
Waziri Mpango anatarajiwa kuwasilisha kwa mara ya kwanza taarifa ya Tanzania ya Mapitio ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu.
Monday, July 15, 2019
WAZIRI WA KILIMO AANZA ZIARA MKOANI SHINYANGA...AKUTANA NA WAKULIMA NA WAMILIKI WA VIWANDA VYA PAMBA
Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga amefanya ziara mkoani Shinyanga kwa ajili ya kutatua changamoto ya zao la pamba kwa wakulima ikiwemo ununuaji wa zao hilo ili wakulima waweze kuuza na kupata fedha zao kwa wakati.
Hasunga ameanza ziara yake ya siku tatu mkoani hapa kuanzia leo Julai 15 na atakamilisha ziara hiyo Julai 17, 2019, ambapo ameanza kwa kutembelea wakulima wa zao la pamba, wamiliki wa viwanda wa zao hilo kwa ajili ya kuzungumza nao, na kuwatia moyo kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakikisha changamoto zilizokuwa zinawakabili hapo awali zinatatuliwa.
Amesema Serikali inatambua changamoto iliyokuwepo awali ya kusuasua ununuzi wa zao hilo pamoja na wakulima kukopwa fedha za mauzo ya zao hilo kupitia kwenye vyama vya msingi vya ushirika AMCOS, lakini kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa ambapo hadi kufikia Julai 30 mwaka huu wakulima wote watanunuliwa pamba yao pamoja na kulipwa fedha zao.
"Changamoto iliyojitokeza ni kuwepo kwa mgogoro kati ya nchi ya China na Marekani na kusababisha kushuka kwa dola, hali iliyopelekea bei ambayo tuliipanga ya mkulima kununuliwa pamba yake kwa shilingi 1,200 kuonekana kwa wafanyabiashara kutawatia hasara na hivyo kuacha kununua pamba,"amesema Hasunga.
"Lakini kwenye kikao ambacho tumekaa juzi na waziri mkuu Kasimu Majaliwa mkoani Tabora tumekubaliana kwamba kutokana na kushuka kwa dola, wafanyabiashara waendelee kununua pamba kwa bei hiyo ya 1,200, lakini dola ikiendelea kuwa chini basi serikali italipa fidia ya hasara ambayo wataipata, kuliko kushusha bei ya pamba ambayo itamuumiza mkulima," ameongeza.
Pia amesema kutokana na kusuasua kwa masoko ya nje, serikali imejipanga kufufua viwanda vya ndani ambavyo huwa vinatumia malighafi ya zao hilo la pamba ili kuondoa changamoto hiyo ya kusu sua kwa ununuzi wa zao la pamba.
Katika hatua nyingine amewataka wakulima wa zao la pamba kujikita kulima kilimo chenye tija ambacho kitawapatia mavuno mengi, kuliko kuendelea kulima kwa mazoea na hatimaye kupata mavuno kidogo ambayo yatawapatia fedha kidogo na kushindwa kukua kiuchumi.
Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Albert Msovela akisoma taarifa ya mkoa huo, amesema kwa msimu wa kilimo (2018-19) zao la Pamba mkoani humo limelimwa hekta 97,270 na kutarajia kuvuna Tani 48,435, na kubainisha changamoto iliyopo kuwa ni ukosefu wa fedha ya kununulia pamba kwenye Vyama vya Msingi vya Ushirika AMCOS.
Nao baadhi ya wakulima wa zao la Pamba,akiwemo Peter Samson kutoka kijiji cha Mwaweja wilayani Kishapu, ambao ni miongoni mwa wakulima ambao wamekwenda kuuza pamba yao kwenye kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini, wamesema wamekwenda kuuza pamba yao hapo kutokana na vyama vya msingi vya ushirika AMCOS kutokuwa na pesa ya kuwalipa na hivyo kuwa azimu kuingia gharama tena ya usafirishaji na kupongeza juhudi hizo za Serikali za kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika Uzogole Shinyanga mjini Kulwa Chagu, amekiri kutokuwa na pesa ya kuwalipa wakulima pale wanaponunua pamba yao, na hivyo kushindwa kuendelea na zoezi la ununuaji wa pamba hiyo, ambapo kwa sasa wakulima wanaiuza kwenye kiwanda cha Afrishan ambacho ndiyo mkombozi wao.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akizungumzia lengo la ziara yake mkoani Shinyanga kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia), kuwa ni kutatua changamoto zinazolikabili zao la Pamba likiwamo na suala la kusuasua kwa ununuzi wa zao hilo.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Awali Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Albert Msovela akisoma taarifa ya mkoa huo juu ya zao la pamba na kuelezea kuwepo na changamoto juu ya kusuasua kwa ununuaji wa zao hilo kwenye vyama vya Msingi vya Ushirika AMCOS kutokana na ukosefu wa fedha.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, akiipongeza Serikali kuitatua changamoto hiyo ya ununuaji wa zao la Pamba kwa wakulima.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akipongeza jitihada za Serikali za utatuzi wa changamoto hiyo ya zao la Pamba, na kuomba pia lifanyiwe kazi suala la kuzuia wafanyabishara wa zao la dengu kutoinunua kwa wakulima hadi AMCOS jambo ambalo litasababisha kutokea kama kwenye kilimo cha pamba, ambapo waziri alifuta agizo la kuzuiwa wafanyabishara hao kutonunua zao hilo moja kwa moja kwa mkulima.
Waziri wa Kilimo.Mhe. Japhet Hasunga akiwasili kwenye kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini ambacho kinanunua Pamba kutoka kwa wakulima licha ya wafanyabishara wengine kushindwa kuinunua Pamba hiyo kwa bei ya 1,200 mara baada ya kushuka kwa dola kwenye soko la nje kwa kuhofia ya kupata hasara.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (mwenye ushungi kichwani) pamoja na viongozi wengine wa mkoa huo, wakiangalia namna ununuaji wa Pamba unavyofanyika kwenye kiwanda hicho cha Afrishan kupitia vyama vya msingi vya ushirika AMCOS ambavyo na viwezeshwa fedha na kisha kuinunua kupitia kwao.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini Ally Habshy, akizungumza ambapo amesema kwa sasa wananunua pamba hiyo kwa mkulima kwa bei ya shilingi 1,200 kupitia fedha zao za ndani, ambapo benki zilisuasua kuwapatia fedha na kupongeza jitihada hizo za Serikali za kutatua changamoto hiyo ya ununuzi wa zao la Pamba pamoja na wao wafanyabiashara kuwa watakopeshwa fedha za ununuaji wa pamba.
Ununuaji wa zao la pamba ukiendelea nje ya kiwanda cha Afrishan Shinyanga mjini.

Wakulima wakiendelea kuleta Pamba yao kuuzwa kwenye kiwanda hicho cha Afrishan Shinyanga mjini ambapo wengine wanatoka Igunga na Mwanza kwa ajili ya kuuza Pamba yao na kupata fedha taslimu.
Wakulima wakiendelea kuleta Pamba yao kuuzwa kwenye kiwanda hicho cha Afrishan Shinyanga mjini ambapo wengine wanatoka Igunga na Mwanza kwa ajili ya kuuza Pamba yao na kupata fedha taslimu.
Pamba ikiwa imemwagwa chini.
Wakulima wa zao la Pamba wakiwa kwenye kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini wakiuza Pamba yao, mara baada ya vyama vya msingi vya ushirika AMCOS kukosa fedha ya kuwanunulia pamba hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwataka wakulima hao wa Pamba kutoiweka Pamba chini ambapo inachafuka bali waiweke sehemu ambapo ni pasafi chini ya matulubai na kutoipotezea ubora wake.
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akiwataka wakulima, kuwa wavumilivu wakati Serikali ikilitatua tatizo la ununuzi wa zao hilo ambapo hadi kufikia Julai 30 fedha zitakuwa zimepatikana na Pamba yote ya mkulima itanunuliwa pamoja na kulipwa pesa zao zote.
Wakulima wa Pamba wakisikiliza ujumbe kutoka serikalini juu ya utatuzi wa changamoto hiyo ya ununuzi wa zao la Pamba kupitia kwenye vyama vya msingi vya ushirika AMCOS.
Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Mhe.Jasinta Mboneko mkono wa kulia akimkaribisha Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga alipowasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya ziara ya siku tatu ya kutatua changamoto ya zao la pamba.

Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akifurahia jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko mkono wa kulia.
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akifurahia jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko mkono wa kulia.
Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Yanga Yaleta Beki Spesho wa CAF
UONGOZI wa Yanga umekamilisha taratibu za usajili wa beki wa kushoto wa Rayon Sports ya Rwanda, Ericky Rutanga anayejiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo Ligi Kuu Bara maalum kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Awali, Yanga iliwahi kumfuata beki huyo na kuzungumza naye na kushindwa kufikia muafaka mzuri na kusalia Rayon huku Gadiel Michael aliyekuwa akicheza nafasi hiyo, naye akitimkia Simba.
Yanga mara baada ya kushindwana na beki huyo haraka ikakamilisha usajili wa beki wa Singida United, Muharami Salum maarufu kwa jina la Marcelo ambaye tayari yupo kambini mkoani Morogoro.
Yanga msimu ujao itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika 'Caf' ambapo itaanzia hatua ya awali iliyopangwa kuanza Agosti 9, mwaka huu na michuano hiyo itamalizika Mei 30, mwakani.
Hivyo basi kama itafanikiwa kushinda mechi za awali za mtoano na kutinga hatua ya makundi, basi itapewa nafasi ya kuongeza wachezaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Rutanga rasmi atajiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.
Habari zinasema kwamba beki huyo atajiunga na Yanga katika usajili huo kuchukua nafasi ya mchezaji wa kigeni, Klaus Kindoki aliyekataa kutolewa kwa mkopo huku akisubiria mkataba wake kumalizika kipindi hicho.
"Rutanga tayari amemalizana na Yanga kwa asilimia 70 na anajiunga nayo kwenye usajili wa ligi na atakuja kuchukua nafasi ya Kindoki ya wachezaji wa kigeni.
"Kama unavyofahamu nafasi za wachezaji wa kigeni tayari zimefikia kumi kama idadi ambao TFF wanaitaka, hivyo wakati Kindoki anaondoka baada ya mkataba wake wa miezi sita kumalizika na Rutanga atakuwa amekuja Yanga.
"Kikubwa uongozi unataka kuwa na mchezaji mwenye uzoefu na uwezo wa michuano ya kimataifa ambayo Yanga watashiriki, mwaka huu," alisema mtoa taarifa huyo.

Sunday, July 14, 2019
Wachezaji wa Yanga wazuiwa kuzungumza
Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amewazuia wachezaji wake kuzungumza chochote na waandishi wa habari.
Mwandila amewazuia wachezaji wake na badala yake amewataka waelekeze nguvu zao zote mazoezini kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Yanga inaendelea na mazoezi kujiandaa na tamasha la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika Uwanja wa Taifa August 4 2019.
Tamasha hilo litafanyika ambapo timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki na AS Vita

Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...