Tuesday, May 7, 2019

Jambo hili ni muhimu ili kuleta ushindani katika biashara unayoifanya

Miongoni mwa mambo yatakayokusaidia kuweza kusonga mbele husasani katika kipengele cha biashara ni kuweza kuwa bora katika biashara ambayo unaifanya.

kama leo ukienda sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri unajua hii inatoakana na nini, Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.

Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako. Pia usipende kufanya kile kitu ilimradi unafanya tu bali unatakiwa kujiuliza hivi ni kwa kwanini wateja wanakuja kwangu na hawaendi sehemu nyingine?
Mpaka kufika hapo hatuna la ziada, endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.

RC Makonda aeleza alivyolipiwa deni la zaidi ya mil 140 na mzee Mengi, amtaka kumbenea kulipa deni analodaiwa na Mengi (+ Video)

Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Mh. Paul Makonda ameeleza jinsi roho nzuri ya mzee mengi ilivyokuwa na kueleza jinsi alivyosaidiwa zaidi ya milioni ya 140 kulipa deni lake katika moja ya sherehe zake alizofanya na kuwaalika viongozi wa dini ya kikristo. akiongea wakati wa kuaga mwili wa Mengi katika ukumbi wa Karimujee jijini …

The post RC Makonda aeleza alivyolipiwa deni la zaidi ya mil 140 na mzee Mengi, amtaka kumbenea kulipa deni analodaiwa na Mengi (+ Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Picha : RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA BUNGE LA AFRIKA


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akimpokea Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika "Pan- African Parliament" yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini leo Mei 7,2019.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akimkaribisha ofisini Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete. 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang (katikati) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele. 
Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Roger Nkodo Dang akizungumza jambo wakati wa majadiliano hayo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa majadiliano yake na Viongozi wa Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu hali ya uchaguzi Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete ambaye anaongoza Timu ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019 akiongoza kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi huo nchini Afrika Kusini.
Kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu  nchini Afrika Kusini kati ya Viongozi wa Bunge la Afrika na  timu ya waangalizi ya Umoja wa Afrika inayoongozwa na Dkt. Jakaya Kikwete kikiendelea.
Waheshimiwa Mabalozi kutoka Kenya,Nigeria wa kiongozwa na Balozi Naimi Aziz wa kwanza kulia anayeiwakilisha Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika ambao wameambatana na Mheshimiwa Kikwete.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele (wa tatu kulia) akizungumza wakati wa kikao cha kujadili maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2019 nchini Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete  akitembelea ukumbi wa Bunge la Afrika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele akipiga picha ya kumbukumbu ofisini kwake na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete katika Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Jijini Johannesburg, Afrika Kusini. 

****
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete ametembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika "Pan- African Parliament" yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Dkt. Kikwete ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika wa Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019 amepokelewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele leo Jumanne Mei 7,2019.

Amelipongeza Bunge la Afrika kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kusimamia Demokrasia, Utawala na Masuala ya Ulinzi na Usalama barani Afrika.

"Mimi nilikuwa miongoni mwa Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao tulikutana kule Sirte Libya kuandaa kanuni za kuanzishwa kwa Bunge la Afrika,hivyo ninayo furaha kubwa kuona hatua kubwa ya maendeleo ya bunge,Nawapongeza sana Rais na Makamu wa Rais kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuendeleza bunge hili na Waafrika wote tunawatagemea",amesema Dkt. Kikwete

"Leo na timu yangu ya uangalizi ambao tupo hapa Afrika Kusini kwa ajili ya uangalizi wa Uchaguzi mkuu wa mwaka huu,na ninashukuru miongoni mwa timu yangu wabunge wa bunge la Afrika ni miongoni mwa wajumbe wangu,nawapongeza sana Bunge la Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika kusimamia demokrasia",ameongeza Dkt. Kikwete.

Kwa upande,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele amemshukuru na kumpongeza, Mheshimiwa Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa bara la Afrika kwenye nyanja za afya,elimu na demokrasia.

"Sisi viongozi vijana tuna mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wako mkubwa kwenye masuala ya uongozi na siasa za kimataifa, binafsi nakushukuru sana kwa malezi yako  ambapo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nimeweza kufika hapa nilipo kiuongozi",amesema Mhe. Masele.

Aidha amemuahidi Mheshimiwa Kikwete kuwa Bunge la Afrika litatoa ushirikiano wote unaohitajika ili kuweza kutimiza majukumu yake katika uangalizi wa uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019.

Na Kadama Malunde - Johannesburg,Afrika Kusini

Naibu Waziri Mhe.kanyasu Apiga Marufuku Ukamataji Mchanga Pori La Akiba La Rungwa

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amepiga marufuku ukamataji wa  vifurushi vya mchanga unaodaiwa kuwa na madini ya dhahabu unaochimbwa na wachimbaji wadogo wadogo ndani ya Pori la Akiba la Rungwa wilayani Manyoni, mkoani Singida kinyume cha sheria na kuuagiza Uongozi wa Pori hilo kuhakikisha unaimarisha   ulinzi  katika maeneo yote yanayodaiwa kuwa na madini ndani ya pori hilo ili kuzuia Wachimbaji  kuingia na kuendesha shughuli ya uchimbaji wa mchanga kinyume cha sheria.

Marufuku hiyo imekuja kufuatia taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Maafisa Wanyamapori  ambao wamekuwa wakiwaruhusu Wachimbaji hao kuingia ndani ya Pori hilo nyakati za usiku  kwa ajili ya  kuchimba mchanga unaodaiwa kuwa una madini kwa makubaliano yaliyo nje ya utaratibu.

Akizungumza  na Watumishi wa geti la Doroto katika Pori hilo wilayani Manyoni mkoani Singida, Mhe.Kanyasu amesema kuwa tuhuma hizo za rushwa zitaisha tu pale watakapoimarisha ulinzi katika eneo hilo na sio kukamata vifurushi vya mchanga kwenye geti hilo.

 Ameuagiza Uongozi huo kuhakikisha  unakamata vifurushi wanavyohisi ndani yake kuna madini  na lazima Afisa Madini awepo ili kuhakikisha anataja thamani ya madini  pamoja na taratibu zinazotakiwa kufuatwa  ili kukidhi matakwa ya sheria ya utaifishaji wa mali iliyokamatwa.

 Baadhi ya Wachimbaji wadogo walionyang'anywa mchanga wao wamedai kwamba Maafisa hao wamekuwa wakikagua magari kwenye geti la kutokea la Doroto na pale wanapokamata vifurushi hivyo bila kujua mchanga huo una madini kiasi gani wamekuwa wakimruhusu mtuhumiwa aende zake bila kumueleza taratibu zozote zile jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Amesema kitendo hicho ni unyang'anyi na uonevu wa hali ya juu na ni kinyume cha sheria kwa sababu sheria ya utaifishaji wa mali iliyokamatwa inampa nafasi mtuhumiwa kujua thamani ya mali aliyokamatwa nayo  na ndipo taratibu za kesi kwenda mahakamani hufuata.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewaonya Maafisa Wanyamapori katika pori hilo kuacha tabia ya kuwaonesha wachimbaji hao mahali wanapohisi  kuwa kuna madini kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Amesema ni ngumu kwa Mwananchi yeyote kujua sehemu ambako kuna madini ndani ya Pori bila kudokezwa na wenyeji ambao ni Wahifadhi wa Pori hilo

Amesisitiza kuwa endapo uchimbaji huo wa madini ndani ya Hifadhi utaendelea kufanyika itakuwa ni ushahidi tosha kuwa Meneja wa Pori hilo kashindwa kazi.

Aidha, Mhe.Kanyasu amewataka kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Pori hilo ili kukomesha ujangili wanyamapori pamoja na ukataji miti ndani ya Pori hilo.

Kwa upande wake, Meneja wa Pori la Akiba la Rungwa, Patrick Kutondolana amekiri kuwa wamekuwa wakikamata mchanga huo kwa mashirikiano kati ya Kamati ya Ulinzi wa Wilaya hiyo ili kukomesha tabia hiyo ya uchimbaji mchanga ndani ya Hifadhi.

Amesisitiza kuwa si kweli kuwa wamekuwa na ushirikiano na Wachimbaji hao kwa makubaliano ya kupata rushwa ni kwamba hiyo imekuwa njama ya kutaka kuwachafua kwa lengo la kuwakatisha nia.

Kutana na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na shariff Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Adam shariff  Mwenye UWEZO wakufanya dua mbali mbali  Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?

Wasilina na Adam shariff Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO   Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? . Adam shariff Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN  . Anatafsiri Ndoto. , KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na Biashara.


Mawasiliano: (+255 )715971688 au (+255  )756914036



VIDEO: Wakili anaedaiwa kupotea afikishwa mahakamani


Hakimu wa mahakama ya wilaya Mkoani Arusha Benard Nganga,na wenzake wanne wakiwemo mawakili wa serikali  wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka kumi na moja yakiwemo ya uhujumu wa uchumi na utakatishaji wa fedha.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu mfawidhi Niku Mwakatobe wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Mwendesha mashtaka wa serikali Javelin Rugailuza amewataja washtakiwa wengine ni Maneno Mbunda wakili wa shirika la hifadhi za Taifa (Tanapa),Fortunatus Mhalila na Tumaini Mdee wote ni mawakili wa serikali na mfanyabiashara Nelson Kangero.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI USIKOSE KU-SUBSCRIBE

Monday, May 6, 2019

Mkewe mwanamfalme Harry wa Uingereza ajifungua mtoto wa kiume

Mkewe mwanamfalme Harry wa Uingereza ajifungua mtoto wa kiume Mwanmfalme Harry amesema kuwa yeye na Meghan “wanafuraha iyokuwa na kifani” baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa. Amewashukuru wote waliyowapatia usaidizi kipindi cha ujauzitio wa mke wake. Amesema Meghan na mtoto wao wako katika ”hali nzurI Jinala toto halijatolewa. “Bado tunafikiaria jina tutakaliompatia,” Mwanamfalme Harry …

The post Mkewe mwanamfalme Harry wa Uingereza ajifungua mtoto wa kiume appeared first on Bongo5.com.


Source

Zifahamu dalili za hisia za usaliti kwa wanawake

Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mwenzi wako. Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au mfanyakazi mwenzio.

 Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine.

Kutoka kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana, unagundua kwamba huyu bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika mazungumzo yenu anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara katika kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita rafiki ingawa ni wa jinsia tofauti, si dhambi kuwa na rafiki  wa jinsia tofauti bali urafiki huo unapaswa kuwa na mipaka.

Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity , kwa tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako.

Wanawake ni viumbe wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.

Zifuatazo ni dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na rafiki uliyenaaye (jinsia tofauti) utakupelekea kuisaliti ndoa yako:-
1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibu na kutumia muda mwingi kuwa naye.

2. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo.

3. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi.


4. Unawasiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri.

5. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa.

6. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.

7. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.

Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki wa jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.

HII HAPA RATIBA YA KUPOKEA MWILI WA DR.MENGI KESHO


Ratiba ya kuupokea mwili wa Dr. Reginald Mengi, Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere imeelezwa kuwa itafanyika kesho, Jumatatu, saa 8:00 mchana.

Mwili wake utaletwa na ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kutokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Baada ya mwili kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa JNIA, utapitishwa maeneo ya Tazara, Buguruni, Ilala, Kigogo, Magomeni hadi Kinondoni.

Kutoka Kinondoni, mwili wake pia utapitishwa hadi katika maeneo ya Morocco, barabara ya Bagamoyo, Sayansi, Mwenge hadi katika hospitali ya Lugalo ambako mwili wa Dr. Reginald Mengi utahifadhiwa.

Ratiba hiyo itaendelea siku ya Jumanne ya Mei 7, 2019, ambapo mwili utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee, kwaajili ya watu wote kuuaga na kisha utarejeshwa nyumbani kwake. Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame ambako Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamis katika kanisa la Kisereni (KKKT).


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...