Thursday, December 27, 2018

Makosa yanayofanywa na wajasiriamali wengi

Wajasiriamali wengi wamekuwa wanafanaya makosa Fulani fualani yanayowafanya washindwe kusonga mbele katika sula la kupata mafanaikio. Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na;

Kupuuza maoni ya wateja
"Mteja ni mfalme"; je unalifahamu hili? Wajasiriamali wengi hupuuzia maoni ya wateja bila kujua kuwa maoni ya wateja ndiyo huwawezesha kujirekebisha na kuweza kuwapa wateja wao kile wanachokihitaji. Kosa hili lisiposhughulikiwa litakupotezea kiasi kikubwa cha wateja na kuleta matokeo mabaya kwenye biashara au mradi wako.

Kuacha fursa zipite
Wajasiriamali wengi hupenda kungojea mazingira yawe mazuri bila hata kujali fursa zinazopotea. Ni dhahiri kuwa hakuna mtu atakaye kutengenezea mazingira unayotaka; ukiona fursa itumie na mambo yatakaa vyema mbele ya safari. Inawezekana fursa unayoiona leo kesho isiwepo tena.

Kukataa ushauri wa kitaalamu
Kila kitu kizuri kinahitaji maarifa stahiki ili kiweze kutokea. Ni dhahiri kuwa wajasiriamali wengi wanafanya kosa la kupuuza ushauri wa kitaalamu katika kazi zao kwa kuona kuwa hauna nafasi. Kwa mfano kama unafuga kuku au unalima mazao fulani kwanini usimwite mtaalamu wa kilimo au mifugo ili akushauri? Ni dhahiri kuwa ukipata ushauri wa kitaalamu utakuwa mwenye tija zaidi.

Kutokwenda na soko linavyotaka
Mjasiriamali mzuri ni yule anayefahamu kuwa kwa sasa soko linataka nini. Ni lazima uweze kuepuka kosa la kutokutazama mahitaji ya soko, ili uhakikishe mauzo ya bidhaa au huduma yako hayaathiriki. Kwa mfano zamani watu walinunua zaidi kuku walio hai, lakini leo soko la kuku waliochinjwa ni kubwa pia; kwanini wewe bado unauza tu kuku walio hai? Ni dhahiri ukitazama mfano huu utaona jinsi kosa hili linavyowaathiri wajasiriamali wengi katika maeneo mbalimbali.

Kushindwa kubaini wateja lengwa
Ni lazima wewe kama mjasiriamali uwabaini wateja wako ili huduma au bidhaa yako iuzike. Kwa mfano umetengeneza dawa ya kuua mbu, kisha unaiuza mikoa ya baridi badala ya mikoa yenye joto (kwenye mbu wengi); ni dhahiri kuwa hutoweza kupata wateja wa bidhaa yako sawa sawa. Chukua hatua leo watafute na uwafuate wateja sahihi wa huduma au mradi unaoufanya.

Mbinu duni za masoko
Maswala ya masoko ni taaluma kamili ambayo watu hujifunza katika shule na vyuo mbalimbali. Hivyo ni muhimu wewe kama mjasiriamali kutokupuuzia taaluma hii kwani ndiyo itakayokuwezesha kubaini njia bora na sahihi za kuuza huduma au bidhaa yako. Hakikisha mbinu za masoko unazifahamu vyema tena zinaendana na soko husika la bidhaa yako. Hakikisha pia mbinu zako zinabadilika kulingana na mazingira na hali ya soko.

Maarifa sahihi ni msingi wa kufanya vitu kwa ubora. Ni dhahiri kuwa makosa mengi yaliyoelezwa hapa yanatokana na ukosefu wa maarifa stahiki ya ujasiriamali. Nakushauri ujifunze kila siku ili kupanua uwezo na uzoefu wako wa kiujasiriamali. Pia usisahau kuweka kwenye matendo yale yote unayojifunza.

Tuesday, December 25, 2018

Good News : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi ...Bonyeza HAPA SASA

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Monday, December 24, 2018

MBUNGE WA CHADEMA APATA AJALI YA GARI..KUNA TAARIFA YA VIFO



Mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kunti Yusuf Majala, amejeruhiwa vibaya baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali. Anaripoti Yusuph Katimba.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu, tarehe 24 Desemba, maeneo ya Kilema, katikati ya wilaya za Chemba na Kondoa.

Taarifa zilizothibitishwa na ofisa mmoja wa Bunge mjini Dodoma, ambaye hata hivyo, hakupenda kutajwa jina lake, zinaeleza kuwa katika ajali hiyo, watu wengine wanne wamefariki dunia.

Afisa huyo ambaye anasema siyo msemaji wa Bunge, anaeleza kuwa gari ambalo mbunge alikuwa akilitumia lilianguka baada ya kuchomoka tairi la mbele mkono wa kushoto wa dereva.

Anasema, "gari hili lilikuwa na watu 11 (kumi na moja), watoto saba na wakubwa wanne. Mhe. Kunti ana maumivu makali sana ya kiuno na shingo."

Anasema, kufuatia hali ya mbunge huyo kuwa mbaya, ofisi ya Spika, imeanza kufanya utaratibu wa haraka wa kuhakikisha mara atakapofikishwa kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, aweze kusafirishwa yeye na majeruhi wengine, kupelekwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi."

Hata hivyo, afisa huyo hakuweza kuwafahamu mara moja majina ya wale waliofariki dunia; na au kujeruhiwa. Bali, taarifa kutoka maofisa wa Chadema zinasema, baadhi yao waliofariki, sehemu kubwa watakuwa familia ya mbunge huyo.

Kwa mashuhuda, gari lililokuwa limembeba Kunti na ambalo limepata ajali, lilikuwa na namba za usajili, T 624 DPE. Lilikuwa likitokea Dodoma mjini kuelekea Kondoa.

Dereva wa gari hilo alikuwa ni Stephano Masawe, ambaye ni dereva wa Katibu wa Chadema, Kanda ya Kati.

Chanzo - Mwanahalisi online

Yanga Wakifikisha Nusu ya Mashabiki Tuliokua Nao Jana Najiuzulu Nafasi Yangu- Haji Manara

Yanga Wakifikisha Nusu ya Mashabiki Tuliokua Nao Jana Najiuzulu Nafasi Yangu- Haji Manara
Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara ameendelea na majigambo yake hasa kwa watani wake Yanga, ambapo amesema kuwa endapo watani zake wa jadi Yanga katika mchezo wake na Tukuyu Stars leo, wakifikisha nusu ya mashabiki waliohudhuria kwenye mchezo wao dhidi ya Nkana FC, yuko yatari kujiuzulua nafasie ya usemaji, ndani ya klabu.

Manara amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika kuwa Simba haiwezi kufananishwa na timu zingine Tanzania wakiwemo watani wake, Yanga.

"Yanga leo wanacheza na Tukuyu Stars, wakijaza asilimia kumi kama jana najiuzulu usemaji wa Simba, halafu yupo mswahili anaweza kuthubutu kunifananisha De la boss na wasemaji wengine?", ameandika Manara.

Yanga inacheza na Tukuyu stars katika dimba la taifa, jijini Dar es salaam katika michuano ya shirikisho (AFC), huku watani wao Simba wakiwa  wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15, wakiichapa Nkana FC ya Zambia.



Friday, December 21, 2018

SAED KUBENEA : SINA MPANGO WA KUHAMIA CCM..MAKONDA ATAONDOKA KWA AIBU

Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusema kuwa yeye na Mbunge wa Kibamba John Mnyika walitaka kujiunga na CCM, si kweli.

Kubenea amesema kuwa hawakuongea vile na Rais bali walikuwa wakizungumza mambo mengine, na Makonda amesema yale ili kuwafurahisha wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwepo kwenye hafla ile.

Kubenea amesema kuwa uchaguzi ujao watahakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo hadi serikali inayoongozwa na CCM ishangae.

"Nataka nimwambie tu RC Makonda kwamba katika uchaguzi unaokuja upinzani tutashinda zaidi kuliko ilivyo kawaida, na ataondoka kwa aibu", amesema Kubenea.

Kubenea ameongeza, "Nchi yetu inajenga matabaka, mtu akionekana anaikosoa serikali wanasema huyu mpinzani na siku hizi wametupatia jina jipya wanatuita mawakala wa mabeberu".

Kubenea amesema kuwa, wale wanaomuunga mkono Rais Magufuli wengi wao ndio wanaompinga kimya kimya wakishirikiana na wanachama wengine ndani ya chama ambao wanajiandaa kumpinga katika uchaguzi ujao.

Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kudai kuwa, amepokea maombi ya wanachama mbalimbali wanaotaka kujiunga na CCM, wakiwemo wabunge wawili wa CHADEMA, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wa Kibamba, John Mnyika, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Selander na barabara unganishi jijini Dar es salaam.

Thursday, December 20, 2018

“Sina Habari na Mambo Ya Ndoa”- Linah Sanga

Mwanamuziki wa Bongo fleva mrembo Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana mpango wa kuolewa na wala hawazi kuhusu mambo ya ndoa. Linah amefunguka kuwa maisha ya ndoa kwa sasa hayafikirii na badala yake anatamani kuona muziki wake unampa heshima kwanza. Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Linah alisema, licha ya wanawake wengi kutamani ndoa lakini kwake inekuwa tofauti na badala yake ameelekeza nguvu zaidi kwenye kazi zake. Mimi ukiniuliza mambo ya ndoa kwa sasa ni ngumu kueleza.. niulize muziki wangu unakwendaje au kuhusu mwanangu". Linah amezaa Mtoto mmoja na mwanaume ambaye alikuwa kwenye mahusiano naye ya muda mrefu aitwaye Shaban Mchomvu ambaye amezaa naye Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris.

The post "Sina Habari na Mambo Ya Ndoa"- Linah Sanga appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Tuesday, December 18, 2018

Tambua umuhimu wa kuvaa soksi


Miguu ni sehemu mojawapo inayotoa jasho  sana hivvo ni vema kuiweka mikavu kuzuia ukuaji wa bacteria au fungus.Wakaka tunajua umuhimu wa soksi au tunavaa bila kujua na wengine hatuvai? Hii ni kwa wadada pia wanaovaa viatu kama raba au hata nyumbani. Ni vema sana kufahamu kwanini tunavaa soksi na mda mwingine soksi gani tuvae.

1.KUZUIA MAGONJWA YA NGOZI MIGUUNI.

Tumia sekunde tatu tu kuvaa soksi na ujikinge na maradhi haya ya fungus na bacteria, kama sio mpenzi was soksi nashauri ufikirie tena maamuzi yako ya kutovaa soksi.

2.EPUKA HARUFU MBAYA YA MIGUU
Image result for atletes foot
Kwa kweli hii ni kero kwako na wanaokuzunguka.Usipovaa soksi jasho lote la miguu litaenda kwenye viatu na ivo viatu kutoa harufu.Soksi hunyonya lile jasho na huzuia harufu iyo. Aya basi tushtuke aibu hii ya nini katika karne ya watanashati sisi.Tuvae soksi na kubadili kila siku.

3.LAINISHA NGOZI YA MIGUU YA YAKO

Nani hapendi miguu soft?? wadada kutwa kusugua miguu saloon.Simple ukirud nyumban kama sakafu ni ngumu vaa soksi zako nyepesi safi miguu iwe laini.Baadhi ya viatu pia vina surface ngumu kwa chini (wakaka) ukiweka soksi zako safi hamna maneno.

4.KUPUNGUZA MAUMIVU MIGUUNI

Hii hasa kwa watoto wadogo ..tuwazoeze mapema kuvaa soksi.Mtoto anatembea ndani Mara akanyage maji mara vitu vya ncha Kali....Pia kuna viatu ukivaa bila soksi lazima upate maumivu na kupata zile sugu nyeusi.

5.KUPATA JOTO NYAKATI ZA BARIDI 

Wale was mikoa iliyo na baridi kwa sasa naamini tuna soksi za kutosha za miguuni na mikono.Kama kuna sehemu inayongoza kutoa joto ni miguuni na mikononi.Basi vaa soksi ili kuzuia joto lisipotee.

6.MVUTO

Ili sio geni, mi mtu akivaa viatu bila soksi kwa kweli napunguza maksi za utanashati...wengine wanasema kuna viatu vya kutovaa soksi. .hakuna kitu kama icho kuna soksi ndogo ambazo hazionekani kwa juu zimejaa tele madukani tutafte.Ebu mtu kavaa kiatu chake safi akiweka na soksi safi inaonekana mvuto lazima uwepo....Nani hapendi kuvutia??basi sote tunapenda tuvae soksi


Siandiki mengi sana, soksi sio jambo geni, tubadilike tujijali,.Ok unavaa soksi Je?unavaa soksi pea moja mara ngapi, unafua na kukausha vizuri maana soksi mbichi ni janga jingine la uchafu na maradhi.Kitu kingine ujue aina ya soksi nyakati za joto usivae soksi ambazo  ni nzito sana vaa nyepesi, ambazo ni nzito vaa nyakati za baridi. Na soksi za watoto tununue ambazo hazibani sana.

Monday, December 17, 2018

Baada ya Jana Kuachwa na Ndege ya Air Tanzania...Leo Aipanda Ndege hiyo na Kuandika Yafuatayo


Fom #diamondplatnumz - Telling my Wifey we jus Ordered another 2 Airbus for Our AirTanzania Airline, so KQ Better be Ready and she was Like "Ooh Really?" i said Oooh Yes😋!!!...
(Nimemwambia Mke, Tumeagiza Ndege Zingine Airbus Mbili kwajili ya Shirika letu la Air Tanzania, Hivyo KQ zijiandae... akasema "Ooh kweli?" nikamwambia Pigia Mstari😋!!!).... Asante @airtanzania_atcl
leo Huduma Zimeboreka barabara!!!

Source

VIDEO: Tuliowanyanganya watakuwa wamechukia / naomba mniombee kwa Mola - Rais Magufuli


Rais Magufuli awataka Waislamu kuzitunza mali walizodhulumiwa ambazo zimerejeshwa.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA, PIA SUBSCRIBE 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...